Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Ref:http://www.oikoumene.org/en/who-are-we.html

Tanzania kama nchi haiwezi kujiunga na World Council of Churches. Kama jina lake linavyosema, shirikisho hili ni kwa makanisa tu.Tanzania inawakilishwa katika jumuia hii kupitia makanisa yake ya Anglikana, Kilutheri na Moravian ambayo ni wanachama. WCC haifanani na OIC ambayo inalenga kuwaunganisha waislamu kupitia nchi wanazoishi. Askofu Dr. Owdenburg Moses Mdegella wa Kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania ni member wa Central Committee ya WCC.


Kwa wale wanaosema kuwa kila mtu anaweza kuajiriwa OIC bila kuangalia dini, angalia tangazo la kazi lililo live:



ref:http://www.oic-oci.org/oicnew/page_detail.asp?p_id=48

Hata kama nchi yako ni mwanachama ili kupata kazi ya maana katika OIC ni lazima uwe muislamu. Na kama umeoa, mke wako lazima awe muislamu. Kama ni mkristu au dini nyingine hautapata nafasi ya uongozi.

Kusema tena kuwa kinaongozwa na watu wasio wakali katika masuala ya dini si kweli! Katibu Mkuu wa sasa hivi ni Professor Ekmeleddin Ihsanoglu kutoka Turkey ambaye awali alikuwa akiongoza the Research Centre for Islamic History, Culture and Arts huko Istanbul.

OIC haijifichi kuwa ni shirika la kidini. Ni kujidanganya kusema vinginevyo. Ukiangalia hata kamati zake zimeundwa kulinda maslahi ya waislamu.

Kwangu mimi hili si tatizo. Tatizo ni kukataa kulizungumzia hata kama limeingizwa kisanii.

So what?
Wao wako wazi na jina lao linaonyesha hivyo. Tatizo letu Watanzania kuwa hili ni jumuiya ya Kiislamu au kuwa ni Jumuiya ya Kidini? Kama tatizo ni jumuiya ya Kiislamu basi na Tanzania ina Waislamu hivyo inawahusu Waislamu wa Tanzania na kama tatizo OIC ni jumuiya ya kidini basi tatizo liko wapi mbona Wananchi wa Tanzania wana dini hivyo wanahaki kujiunga na jumiya za kidini kama tunavyojiunga na jumuiya nyengine kwa magurupu yetu ndani ya jamii.
HILI SUALA LA UPANDE MMOJA FAIDA YAKE LAZIMA IKUBALIKE NA UPANDE MWENGINE HALITOTUPELEKA MBALI TUTAVUTANA BURE.
 
So what?
Wao wako wazi na jina lao linaonyesha hivyo. Tatizo letu Watanzania kuwa hili ni jumuiya ya Kiislamu au kuwa ni Jumuiya ya Kidini? Kama tatizo ni jumuiya ya Kiislamu basi na Tanzania ina Waislamu hivyo inawahusu Waislamu wa Tanzania na kama tatizo OIC ni jumuiya ya kidini basi tatizo liko wapi mbona Wananchi wa Tanzania wana dini hivyo wanahaki kujiunga na jumiya za kidini kama tunavyojiunga na jumuiya nyengine kwa magurupu yetu ndani ya jamii.
HILI SUALA LA UPANDE MMOJA FAIDA YAKE LAZIMA IKUBALIKE NA UPANDE MWENGINE HALITOTUPELEKA MBALI TUTAVUTANA BURE.

Ngekewa! Ni waislamu wenzako ndio wanaodai kuwa OIC si shirika la kidini! Hili kwangu mimi naona ni kosa maana ukweli utakuja kujulikana tu. Msimamo kama wako ndiyo unaotakiwa. Ikubalike kuwa Tanzania itajiunga kwa faida ya wananchi wake ambao ni waislamu. Sioni kwa nini waislamu wakatiliwe nafasi hii ili mradi hao wengine hawadhuriki kwa aina yeyote.
 
Uamuzi kama huu ni lazima uwe na majority support. Kwani tusipokuwa wanachama tunakosa nini? Tafuteni katiba ya hii organisation (IOC) imwagwe hapa jamvini tutoe mchango na media iipate ifanye mass awareness. Binafsi na usomi wangu sina details za hiki kitu, je majority ya watanzania itakuwaje? Tusiwe na haraka jameni. Thanks.
 
Huyo anayeona mimi napinga UISLAMU huyo ndio Mdini mkubwa.

Mimi hapa msimamo wangu ni uleule napinga serikali kujihusisha na mambo ya kidini maana inavunja katiba yake yenyewe.Nieleweke vizuri siwapingi waislaamu ila napinga kwa namna yoyote ile Serikali kujihusisha na mambo ya dini.Katiba imeweka mambo wazi na kinagaubaga ya kwamba Msuala ya IBAADA na kueneza DINI ni jukumu la mtu mhusika.

Huyo anayekuja na habari nyepesi nyepesi kwamba napinga DINI fulani na sio WAISLAMU ni wanasiasa ndiyo nakubali ni wanasiasa.
Mimi ndio hao wanasiasa nawapinga kwa nguvu zote kuingiza dini ktk katiba isiyo tambua dini.

Kwa tuliyekua pamoja tangu mwanzo nilishangaa suala la KIROHO yani IBAADA kukabidhiwa kwa KAIZAR yani wanasiasa.

Pia nitawashangaa viongozi wa kiislamu kama hii kitu inapushiwa na wana siasa Wao wakiwachaa tu wandelee kutumia UISLAMU ili kujipatia madaraka ,nitashangaa sana tena na tena.
Kama hii kitu ni yawana siasa basi viongozi wa dini husika waibuke na wakemee vikali wanasiasa hawa ya kwamba mambo ya KIROHO kumkabidhi KAIZAR ni kinyume na maadili ya MUNGU.

Narudia tena mimi napingana na serikali kujiingiza na mambo ya dini hata kama ingekua wanajiunga na dini ya kikristu, kihindu ama walugaluga.
 

OIC is Organization of Islamic Countries. Period. Tanzania is now ISLAMIC COUNTRY/NATION.

Wherefore, the members of OIC are Islamic Nations, which are knowingly and willingly have decided to be biased to their citizens, by joining such an organization without the will and consent of the people.

The malicious, unethical, and unmerital decision made by Tanzania GOV is evil to Tanzanians and can not be tolerated by joining a defacto organization.

Furthermore, Tanzania comprises of many beliefs and ethics and can not be ignored by few FISADI politicians, inter-alia, they can not compare Tanzania with countries "Mr. Politician" compared us with. We are better than them in many ways, you name it by your self.

It is more than evil to assume that every Tanzanian is a Zombie the way these unintegrity politicians are doing to the people and citizens of Tanzania.

In the interim, the GOV must cease and desist from joining such a defacto organization without the will of the people.

Their reason of joining OIC is ipso facto, defacto, and lacks judicial merits.

 

They think every body is a ZOMBIE. It is shame and sad to have such leaders.

 
REV nakubaliana nawe na hoja zako nyingi kuwa Tanzania si nchi ya kidini lakini sifikiri kuingia jumuiya ya kidini ni kuvunja katiba,

Mtiririko wa matokeo hapa kwetu umenifunza jambo moja. Wengi wetu hukimbilia Katiba kwa lile tusilolipenda na tuko tayari kuikana na kuiponda Katiba hiyo hiyo kwa yale tunayoyajengea hoja. Pengine hapa utakubaliana nami kuwa tabia hii ni double Standard. Tumekuwa wa mbele kudai kubadilishwa Katiba kwa yale nyoyo zetu tunayapenda na kudai kuwa Katiba inataka marekebisho.
Aidha nafikiri msingi wa kuundwa Katiba ni kuuweka utaratibu unaokubalika na wengi. Tunapodai jambo lipigiwe kura tuna maana kupata idadi ya wanaounga mkono au kwa maana nyengine wale wanaoona kuwa jambo husika litawanufaisha.
Sioni sababu ya kudharau Waislamu kwa wingi wao na kudai jambo fulani ambalo litawanufaisha. Rev, unaposema kuwa mgawanyo wakidini ni sawa na hapo hapo ukabeza matakwa ya nusu hiyo kwa madai kuwa halina ridhaa sasa ridhaa ni ipi hapa? Ile ya nusu inayotaka au nusu isiyotaka ? Hivyo kati yetu na dini zetu kama tungekuwa na uhuru wa kuamuwa tunayotaka kidini nani hataki Tanzania iishi kidini yake? Kwa muda wote tumekuwa tukiishi kwa kustahamiliana na kuona kuwa mwenzangu akifaidika basi nami nitafaidika kwa jengine. Tunaishi kwa give and take na tunaishi kwa Amani.
Tatizo la watu wawili linakuja zaidi kwa mmoja kumkatalia mwenziwe asifaidike na kitu ambacho yule mwengine hana faida nacho wala hakina madhara nae.
Pengine Rev ungeonyesha madhara ambayo wataipata sehemu ya pili nafikiri Waislamu nao wangekuwa tayari kutilia maanani uhusiano wa kindugu na kuzuiya kuuvunja kwa kujiunga na OIC. Suala la kusema Katiba nafikiri halina hoja thabiti kwani ni Katiba hiyohiyo tunataka ifanyiwe marekebisho na hata hivyo nafikiri hakuna kipengele kinachokaza Tanzania kujiunga na Jumuiya kama ya OIC.

Ngekewa,

Ukinisoma kwa makini, sijasema waislamu wa Tanzania wasijiunge na OIC, ndio maana nimeuliza kwa nini Bakwata au chombo kikuu cha Jumuiya ya Kiislamu Tanzania isiingie OIC? Nilipoleta mfano wa WCC, nilitaka kupanua wigo wa mawazo. Najaufika kuwa WCC ni makanisa na si nchi zinazoingia humo ndani.

Ninachojaribu kubainisha ni kuwa Tanzania kujiunga OIC kama Nchi si sahihi, kwa kuwa OIC inatamka wazi kuwa ni Umoja wa Nchi za Kiislamu.

Ni sawa na leo Tanzania ikitaka kuingia EU, je ni nci ya Ulaya? nalo ni kosa kuingia EU kwa kuwa Tanzania si nchi ya EU!

Mfano wa uwiano, nimeutoa kwa kuwa kuna kauli za kusema kuwa dini fulani ina watu wengi Tanzania wakati dini kuu tatu, Usilamu, Ukristo na nyinginezo including wapagani ni mgawanyiko karibu sawa!

Sas kama tutaingiza Tanzania kama nchi katika Umoja wa Nchi za Kidini fulani, bila ridhaa ya wale ambao hawaamini hiyo dini, je hamuoni ni wepesi wa kuleta mtafuruku?
 

About OIC
The Organization of the Islamic Conference (OIC) has membership of 57 Islamic States spread over four continents. The Organization is the collective voice of the Muslim and Islam world and ensuring to safeguard and protect the interests of the Muslim and Islam world in the spirit of Allah by promoting international peace and harmony among various people of the world through Islamic Allah and Sharia Law.

The Organization was established upon a decision of the historical summit which took place in Rabat, Kingdom of Morocco on 12th Rajab 1389 Hijra (25 September 1969) as a result of criminal arson of Al-Aqsa Mosque in occupied Jerusalem.

In 1970 the first ever meeting of Islamic Conference of Foreign Minister (ICFM) was held in Jeddah which decided to establish a permanent secretariat in Jeddah headed by the organization’s secretary general. Prof Ekmeleddin Ihsanoglu is the 9th Secretary General who assumed the office in January 2005 after being elected by the 31st ICFM.

[media]http://www.oic-oci.org/oicnew/is11/english/Charter-en.pdf[/media]

AFFILIATED INSTITUTIONS

DEFINITION
Membership to these institutions is optional and open to institutions and organs of OIC Member States. Their budgets are independent of the budget of the Secretariat General and those of subsidiary and specialized organs. They were established under the auspices of the Islamic Conference of Heads of State and Government or the Islamic Conference of Foreign Ministers. Affiliated institutions may be granted observer status by virtue of a resolution of the Islamic Conference of Foreign Ministers. They may obtain voluntary assistance from the subsidiary and specialized organs as well as from Member States.
1. Islamic Chamber of Commerce and Industry (ICCI)
2. Organization of Islamic Capitals and Cities (OICC)
3. Islamic Solidarity Sports Federation (ISSF)
4. Islamic Committee of the International Crescent (ICIC)
5. World Federation of Arabo-Islamic International Schools (WFAIIS)
6. Organization of the Islamic Shipowners Association (OISA)
7. Islamic Conference Youth Forum for Dialogue and Cooperation (ICYF-DC)
8. International Union of Muslim Scouts (IUMS)
9. Federation of Consultants from Islamic Countries (FCIC)
10. Islamic World Academy of Sciences (IAS)
11. General Council for Islamic Banks and Financial Institutions (GCIBFI)
12. Federation of Contractors from Islamic Countries (FOCIC)



 
Wanabodi,
Ningependa nifahamishwe kitu kimoja hapa..tena ningependa sana Fundi Mchundo unijibu...
Hii OIC kama ni ya kidini inaongozwa na waislaam wa kanisa (dhehebu)gani?.. maanake kila kitu cha kidini kinatokana na kanisa ama kiongozi wa dini hiyo....Kama kuna kiongozi wa dini naomba jina lake na tutazame nafasi yake ktk dini ama dhehebu lake..Hapa ndipo tunaweza kabisa kuihusisha OIC na dini....
Nini nafasi ya OIC ktk dini ya kiislaam na imeandikwa wapi ama imeanzishwa na nani?

Kifupi ndugu zangu nilisema toka mwanzoni kwamba mada hii ni moja kati ya mada zenye upofu wa kuona mbali kwa sababu watu mnatumia sana imani na tofauti zenu za kidini kujadili kitu kisicho kuwa na madhara...

Sasa kwa wakristu ambao wanapinga nawaomba mutazame mfano huu wa Waislaam kisha mjue nilikuwa na maana gani toka mwanzo kifupi natoa hitimisho la mawazo yangu kuhusiana na kuijiunga na OIC...
Kuna ufinyu fulani ama utumwa wa kimawazo ambao waislaam wengi wameambukumbatia...Ni mfano mzuri sana kulingana na hoja hii pomoja na kwamba nimewapa ile ya kwanza ya waarabu kukataa isaada ya Red cross simply because of the Emblem..

Sasa mtazame ujinga mwingine wa sisi Waislaam ambao pia nasema tunatumia imani za rangi yetu kupinga vitu ambavyo hata havina uhusiano na mafundisho ya dini..

Ikitokea serikali ya Zanzibar ikaagiza nyama ya ng'ombe toka Israel hata kama mwenye kiwanda cha nyama hiyo ni Muislaam basi bila shaka itapigwa marufuku ama kupigwa vita isiuzwe Zanzibar au kwa waislaam ... sababu kubwa - ni hiyo nembo ya Made in Israel.. lakini kama nyama hiyo hiyo itakuwa na chapa ya made in Dubai, basi bila shaka itapokelewa bila hata kuuliza Uhalali wake na utasifiwa kwa utamu wake....mmmhnnnn! - Hapa wakuu hamuoni kitu cha ajabu hata kidogo?...

Nacho jaribu kusema hapa ni kwamba hoja zenu zote zinatokana na hilo jina la OIC na laukama kama ingeitwa jina jingine tofauti bila kuweka hilo neno Waislaam hata kama washiriki ni wale wale bila shaka msingeweka mashaka kabisa na ingepita labda mngeua sababu nyingine mtakapo ona waarabu..yaani bado rangi hiyo ya waarabu ndio tatizo kubwa...

Western World, hasa Wayahudi wamekwisha wasoma Waislaam na hasa waarabu...Wanapotaka kuingia nchi za kiarabu ama hizo zinazojiita za kiislaam huingia na gear kubwa kuwa mali inatoka nchi nje ya Uyahudi, mathlan Egypt, US, UK au Morocco..Na waislaam huzipokea hata bila kusita lakini siku wakisikia tu ni mali ya Myahudi utaona ktk magazeti...Ipigwe marufuku wakati wameshakula miaka kibao.
Hivi sasa watu wengi wanashindwa kuelewa kwa nini mashirika makubwa ya Marekani yana outsource shughuli zake ama kununua zaidi mashirika ya nje kuuza mali ambazo zinatengenezwa Marekani... Moja ya sababu kubwa ni pamoja na hizo zakutumia jina la nchi nyingine..Mfano wa mwisho ni hayo mashirika ya uchimbaji madini yaliyopo Tanzania, karibu yote yanamilikiwa na Wamarekani lakini kwa sababu marekani imesha haribu jina lake ktk maswala ya madini na dunia inawaamini zaidi Wa Canada kuwa watu wa haki basi tender zinapatikaa kirahisi..wazee wnavuka border na tunapigwa mchanga wa macho!...Wakuu hii ndio Globalization...
Karibuni, hakuna adui wala mchawi ikiwa mambo yako yatanyooka!..
Bush kenda fungua Olympic China..haikuingia akilini mwa kila Mmarekani.

Rev. Kishoka.
Mkuu tatizo la Bakwata kutoweza kujiunga na OIC ni kwa sababu inaendeshwa na serikali na haiwezi kujiunga na OIC bila baraka za serikali..kama nakumbuka vizuri hoja ya Zanzibar kujiunga na OIC ilitokana na vyombo vya kiislaam ambavyo haviwezi kujiunga tu kiholela na Foreign Organisation... Kwa hiyo hata ile jumuiya wa Wanawake Wakristu wa Tanzania walipotaka kujiunga na World Union of Catholic Organisation's (WUWO) ambayo inatambuliwa na UN walikuwa na baraka za serikali. Tanzania ni mwanachama pamoja na kwamba representative wa wanawake hao ni umoja huo wa wanawake wa Kikatoliki...Mkuu hiki chombo kinatambulika hadi UN....lakini hiyo OIC.... thubutu hapo Bongo tu imekuwa nomaa!

Kwaherini, MaaSalaam
 
Wanabodi,
Ningependa nifahamishwe kitu kimoja hapa..tena ningependa sana Fundi Mchundo unijibu...
Hii OIC kama ni ya kidini inaongozwa na waislaam wa kanisa (dhehebu)gani?.. maanake kila kitu cha kidini kinatokana na kanisa ama kiongozi wa dini hiyo....Kama kuna kiongozi wa dini naomba jina lake na tutazame nafasi yake ktk dini ama dhehebu lake..Hapa ndipo tunaweza kabisa kuihusisha OIC na dini....
Nini nafasi ya OIC ktk dini ya kiislaam na imeandikwa wapi ama imeanzishwa na nani?...........................

Kwaherini, MaaSalaam

Mkandara,

Samahani kama nitakuwa nimekosea lakini nikikumbuka kwa mbali moja ya malengo waliyopeana kwenye mkutano wao moja wa OIC uliofamyika Afrika Magharibi kwenye miaka ya tisini lilikuwa na maneno yaliyofanana na haya;

Kuimarisha Uislamu kwa kuanzisha mikakati ya kuhakikisha waislamu kwenye nchi husika hawakubali kuongozwa na makafiri.

Kama kuna ukweli wowote kwenye hili basi hii jumuiya haitufai hata kidogo na ni hatari kwa nchi yetu isiyofungamana na dini yoyote.
 
Wanabodi,
Ningependa nifahamishwe kitu kimoja hapa..tena ningependa sana Fundi Mchundo unijibu...
Hii OIC kama ni ya kidini inaongozwa na waislaam wa kanisa (dhehebu)gani?.. maanake kila kitu cha kidini kinatokana na kanisa ama kiongozi wa dini hiyo....Kama kuna kiongozi wa dini naomba jina lake na tutazame nafasi yake ktk dini ama dhehebu lake..Hapa ndipo tunaweza kabisa kuihusisha OIC na dini....
Nini nafasi ya OIC ktk dini ya kiislaam na imeandikwa wapi ama imeanzishwa na nani?

Mkandara, unanipotezea wakati. Nimekuwekea website ya hao wakina OIC. Nimekuonyesha mahali inaposema lengo lao ni wa kuwaunganisha waislamu. Nimekupatia jina la Katibu Mkuu wake, ambaye ni Profesa wa kituruki aliyekuwa awali mkuu wa research centre ya historia ya uislamu. Nimekuwekea tangazo la kazi linaloisha septemba mwaka huu, ambamo mwombaji ni lazima awe muislamu na kama ameoa, mke wake nae awe muislamu. Sasa unataka nikuambie nini kipya ili ukubali kuwa lengo la hiki chombo ni waislamu na sio watu wa dini nyingine? Kwa mtazamo wangu hicho ndicho kinachokifanya kuwa ni chombo cha kidini. Mimi mkristu sina nafasi ndani yake. Unataka nikuonyeshe kwenye uislamu kimetajwa wapi. Niambie wapi kwenye uislamu kumetajwa usunni, ushia, ubohora, uismailia, udruze n.k. Mbona wote hawa wanajiita waislamu? Leo utakataa kuwa the World Council of Churches ni cha kidini ati kwa sababu hakijatajwa kwenye biblia? Au the World Vision? Au the Salvation Army? Nenda kafanye tunavyofanya wengine, google hiyo OIC, na utajua yote hayo unayotaka kujua. Nilishakwambia, hauni'convince' na arguments zako. Naona hazina uzito kwa hiyo tukubaliane kutofautiana. Mimi sioni tatizo la OIC kwa maana sioni litaniingiliaje uhuru wangu kama mkristu raia wa nchi yangu. Naiona kama FIFA. Ila hiyo Mahakama ya Kadhi naiona ina hatari sana kwangu mimi kama raia mkristu na kwa nchi yangu. Ndiyo maana naipinga kwa nguvu zangu zote.
Enough said. Tuna waboa wengine.
 
Mifano yako inahusu vitu vidogo visivyoweza kulinganishwa na nchi, wala haviwezi kufananishwa au kulinganishwa. Tusiwe biased, wakati tunakataa kufungua ubalozi wa Israel ndo wakati tunaotaka kujiunga na OIC!

So if Israel is the promised land for most of us believers of both Christianity and Islam and the fact is the historical records show that we Christians, Muslims and so are the Jews are from the same Patriach, why would we denounce those of the faith that support Judaism and Jewish community?

If you look at the core foundation of OIC is the temple in Jerusalem as stated on this quote from OIC website
The Organization was established upon a decision of the historical summit which took place in Rabat, Kingdom of Morocco on 12th Rajab 1389 Hijra (25 September 1969) as a result of criminal arson of Al-Aqsa Mosque in occupied Jerusalem.
so, if the Christians are in support of Israel state and demand that Tanzania opens an embassy in Tel Aviv how will this sit with the Moslim community in Tanzania?
 
Fundi Mchundo,
Mkuu unajua wewe una ubishi usiokuwa na maana hata kidogo..bahati nzuri umesema mwenyewe kuwa Ukristu wako ndio unakuendesha ktk hoja zako tofauti na mimi nayetazama vitu kama vilivyo..Nimekuuliza maswali madogo sana...Wewe umekuja na vitu ambavyo hata haviingi akilini.. Umefikia hata kutaja World Vision na sijui Salvation Army.. sasa wewe mjuzi wa ku google nenda katazame jinsi vyombo hivi vilivyoanzishwa..kisha nionyeshe usawa wa vyombo hivi na hicho cha OIC..
Unauliza swali ambalo jibu unalo mwenyewe na hakuna mahala nimesema vyombo hivyo havina uhusiano wa moja kwa moja na makanisa ama dini..na hakuna mtu asiyeelewa.
Haya basi ktk kumtaja huyo Katibu mkuu wa OIC umetafuta kijisehemu kinachomhusisha yeye na Uislaam ili upate kuipamba hoja yako, sasa narudi nyuma tena nakuomba nambie hicho chuo ambacho yeye alikuwa mkuu wa research ya historia ya kiislaam na kwa muda gani!...
Kisha habari ya employment, mkuu hapa unazidi kupotea kabisa..Hivi kweli kwa akili yako chombo ambacho kimeundwa ili kusaidia waislaam ktk nchi zilizojiandikisha uanachama tena katk nafasi kubwa kama ile ulitegemea wangetangaza vipi?..nitarudia mifano yangu ya siku zote.. Kuwa mweusi haina maana wewe ni Mwafrika...Uislaam unakuja kwa rangi nyingi kama vile Afrika na huwezi kuwakilisha Afrika kama wewe sii mkazi wa Afrika, hii ni logic hata sisi kesho tunaweza kabisa kusema huwezi kugombea Ubunge wa wilaya fulani kama wewe sii mkazi wa pale... mfumo huu hauna maana mbaya kama unavyojaribu kuviweka. Bara na Zanzibar tunazo sheria ambazo zinawalenga Wazanzibar tu ktk chaguzi zetu lakini haina maana Bara tunatengwa isipokuwa ni ktk uwakilishi wa jumuiya unayokuhusu..
Wewe nambie chombo chochote kile kinachohusiana na jamii fulani kimetangaza nafasi kama hiyo tofauti maanake unapotoa hoja ni muhimu kuonyesha mapungufu ama tofauti fulani..

Bado unashindwa kuelewa kwamba malengo ni watu waislaam kama vile Umoja wa wanawake nchini una malengo ya kusaidia wanawake hivyo huwezi kutangaza nafasi kubwa kama hiyo kisha ati mwakilishi wa UWT huko UN awe mwanamme..
Chombo kama Sullivan hivi kweli kwa fikra zako unafikiria wanaweza kumweka mzungu ktk position kama hiyo?..Je, hivi kweli Sullivan wanahusiana vipi na movement za watu weusi kama vile Black Power. Sasa unachojaribu kusema hapa ni sawa na mwarabu wa Tunisia aje leo akwambie anafahamu vizuri kuwa Sullivan ni black movement!..sijui mwenzangu utajaribu vipi kumfahamisha..
Zaidi ya hapo je, sio kati yetu sisi wenyewe weusi tunakipiga vita kuwa hawa ni matapeli?..hata hao OIC wamepata malalamiko mengi sana yanayohusiana na huduma zao kwa sababu hiki ni chombo kinachojiendesha nje ya misingi ya dini. na ndio maana nilikuuliza swali langu la kwanza ambalo ulishindwa kulijibu isipokuwa kutafuta wahusika kama mnavyofanya kila siku ktk kutazama baraza la Mawaziri nchini, wabunge na kadhalika...
Mkuu OIC haina tofauti yoyote ile na vyombo vingine ambavyo vimeundwa na watu kutoa misaada wakati huo huo wanavuta zao..
Mimi nachozungumza nakifahamu hata kinavyofanya kazi wewe unafanya ku google kwa hiyo ni vigumu kukufahamisha hasa ukiwa umeubeba ukristu ktk majadiliano kama haya..

Mkuu wangu ktk mjadala wa dini niliwahi kuingia na kuwapasha kidogo kuwa tatizo lenu nyote ni kwamba siku zote ubishi wetu unatazama chupa ya soda kuweza kujenga hoja badala ya kile kilichomo ndani ya chupa hiyo..kwenu nyie Cocacola sii Cola ikiwa haipo ktk chupa ya Coca, Na kwa mswahili hasa nyie hata kama ukimimina soda yote ktk glass ukamuuliza mtu cocacola ipo wapi basi atakuonyesha chupa iliyo tupu...

Mkuu hapa unanionyesha chupa iliyo tupu - sioni hoja kabisa!

Nafikiri nimejieleza vya kutosha na kama bado hujaelewa basi mkuu ndio hivyo tumeshakuwa wanachama, na Tanzania ni wanachama wa Umoja wa wanawake Wakatoliki duniani ambacho kinatambuliwa na UN na hakuna Muislaam anayepiga kelele kwani hilo ni jambo zuri sana kwa kina mama wa Kikatoliki, hainidhuru mimi hata kidogo.
 
Nafikiri inabidi tusome charter ya OIC kabla ya kuendelea na huu mjadala.


Charter of the​
Organisation of the Islamic Conference​
 ا   ا ا 
In the name of Allah, the most Compassionate, the most Merciful​
We the Member States of the Organisation of the Islamic
Conference, determined:​
to acknowledge the Conference of Kings, Heads of State and Government of
the Member States convened in Rabat from 9 to 12 Rajab, 1389 H,
corresponding to 22 to 25 September 1969, as well as the Conference of
Foreign Ministers held in Jeddah from 14 to 18 Muharram 1392 H
corresponding to 29 February to 4 March 1972;
to be guided by the noble Islamic values of unity and fraternity, and affirming
the essentiality of promoting and consolidating the unity and solidarity among
the Member States in securing their common interests at the international
arena;
to adhere our commitment to the principles of the United Nations Charter, the
present Charter and International Law;
to preserve and promote the lofty Islamic values of peace, compassion,
tolerance, equality, justice and human dignity;
to endeavour to work for revitalizing Islam’s pioneering role in the world
while ensuring sustainable development, progress and prosperity for the
peoples of Member States;
to enhance and strengthen the bond of unity and solidarity among the Muslim
peoples and Member States;
to respect, safeguard and defend the national sovereignty, independence and
territorial integrity of all Member States;
to contribute to international peace and security, understanding and dialogue
among civilizations, cultures and religions and promote and encourage
friendly relations and good neighbourliness, mutual respect and cooperation;
to promote human rights and fundamental freedoms, good governance, rule of
law, democracy and accountability in Member States in accordance with their
constitutional and legal systems;​
to promote confidence and encourage friendly relations, mutual respect and
cooperation between Member States and other States;
to foster noble Islamic values concerning moderation, tolerance, respect for
diversity, preservation of Islamic symbols and common heritage and to defend
the universality of Islamic religion;
to advance the acquisition and popularization of knowledge in consonance
with the lofty ideals of Islam to achieve intellectual excellence;
to promote cooperation among Member States to achieve sustained socioeconomic
development for effective integration in the global economy, in
conformity with the principles of partnership and equality;
to preserve and promote all aspects related to environment for present and
future generations;
to respect the right of self-determination and non-interference in the domestic
affairs and to respect sovereignty, independence and territorial integrity of
each Member State;​
to support the struggle of the Palestinian people, who are presently under
foreign occupation, and to empower them to attain their inalienable rights,
including the right to self-determination, and to establish their sovereign state
with Al-Quds Al-Sharif as its capital, while safeguarding its historic and
Islamic character, and the holy places therein;
to safeguard and promote the rights of women and their participation in all
spheres of life, in accordance with the laws and legislation of Member States;
to create conducive conditions for sound upbringing of Muslim children and
youth, and to inculcate in them Islamic values through education for
strengthening their cultural, social, moral and ethical ideals;
to assist Muslim minorities and communities outside the Member States to
preserve their dignity​
, cultural and religious identity;

 

Attachments

Rev. Kishoka,
Mkuu wangu hivi hata wewe una tu underestimate waislaam kiasi hicho?... mkuu Tanzania ina Ubalozi Vatican na hakuna muislaam anayepiga kelele iweje nyie leo mnaanza kufikiria kuwa Waislaam hivi ama vile wakati mnayafanya yote bila kusikia tukihema?..
Waislaam waipinga Israel kwa jinsi wanavyo wa treat Wapalestina.. Waislaam waliipinga South Afrika ilipokuwa ikiendesha Apartheid hivi kuna asilima ngapi ya waislaam huko south kiasi kwamba mfikirie jinsi mnavyofikiria.
Mkuu ni haki ya watu inayozungumziwa hapa na sio jina la dini, haya mengine mkuu ndio ktk maelezo yangu yaliyotangulia kuwa wapo waislaam wanaopinga vitu kwa sura yake lakini kimsingi dini hii inatazama mabaya hata kama yalifanywa na mwarabu.
Hapa anayepinga OIC ni nyie na mifano inaweza kuzidi kila nitakapo kutajia uhusiano wetu na nchi za kiislaam.. Iran mojawapo.

Mkuu wangu ukisoma Charter ya IMF utaona ina maelezo mengi sana sawa ama yanafanana na hawa jamaa lakini haina maana kabisa kuwa IMF ni chombo cha nchi maskini kwa sababu tu walengwa ni nchi maskini!..Kwa taarifa tu OIC ina watu wake hadi Marekani..
 
Mkandara
Nimezielewa jitihada zako za kuiondoa hpja hii katika mwonekano wa kidini. Lakini nikuulize swali:- Kwanini waislam wanapenda kujiunga na OIC? Ukisoma malengo ya OIC ni kuimarisha ulimwengu wa kiislam (to strengthen muslim world) Hii inamaana gani?

Unaona namna waislam wanavyowachukia wayahudi ambao wakristo wanaamini kuwa ni taifa teule ambalo mungu alisema ukiwalaani utalaaniwa wewe na ukiwabariki utabarikiwa! Kwa maneno haya utaona kwamba Wakristo hawawezi kukubali kuliingiza taifa katika umoja wenye lengo la kuilaani nchi yetu.
 
Mkuu Nziku,
Umeniuliza kwa nini waislaam wanataka kujiunga na OIC... mkubwa ni ktk kutafuta maendeleo, kujiunga ni hiari yetu na ndio maana tunajadiliana hapa kama wewe una care kuhusiana na hali za waislaam nchini basi sidhani swala ni udini...
Waislaam siku zote hawana chombo kama wenzetu Wakristu ambacho kimeweza kujengea shule, hospital na kadhalika duniani pote. Hivyo baadhi wasomi walikaa na kupata idea ya kuanzisha chombo hiki ambacho kwa imani yangu wanavuta kishenzi toka kwa hao Masultan..
Sisi wahitaji na hatuna umoja kama wenu kwa hiyo chombo kama hiki kama kitaweza kusaidia jumuiya hi ya waislaam sioni ubaya wake hata kidogo na kama tukija fahamu kuwa ni matapeli basi tunaweza kujiengua, lakini kama wataweza kuwasaidia waislaam sioni kwa nini watu mnaweka kauzibe hali nyote mnawatakia mema waislaam ambao kila siku mnawasema wajikusanye wafanye vitu..Hoja ya msingi ktk mazungumzo yetu ingekuwa kuwachambua hawa OIC zaidi ya kutazama wanalenga kuwasaidia kina nani...
Kwa udogo wetu waislaam tunayataka maendeleo hayo kama mlivyokuwa nayo na uzuri tuna stick ktk sehemu ambazo wapo waislaam. Hatuna nguvu kama yenu ambayo mnaweza hata kwenda Afghanstan na kuweka kambi nyuma ya majeshi ya Marekani, au NATO bila ridhaa ya wananchi wa hapo..

Swala la Israel mkuu nafikiri lipeleke kwenye dini maanake hapa halifai hata kidogo na wala halihusiani na OIC..Kama wewe unaamini kuwa Wayahudi ni Taifa teule basi wewe na imani yako lakini mimi naamini kabisa Myahudi aliyetajwa ktk biblia ni yule aliyefuata agano la Kale sio kabila au society fulani kwani Hebrew wote hawakuwa Wayahudi pamoja na kwamba Wayahudi wote mwanzo walikuwa Hebrews.. ambao hawakuwa wazungu. Na biblia inaposema wayahudi waliasi ina maana wale waliokuwa wakiamini na kuabudu Mungu sio kila Mhebrew.
Kwa hiyo hata wewe ungeweza kuwa Myahudi kwa maana ya Imani isipokuwa hawa jamaa zetu wamekuja na mkaango mpya ktk mapishi ya Uyahudi kuwa ni kabila..Kwa maana hiyo hata watukuu wa Moses leo hii kama wapo hawawezi ku qualify kama wayahudi kwa sababu Moses alioa mke toka Misri...
Sasa wewe nambie kitukuu cha Moses aliyewaokoa hebrews toka Egypt leo hii hana sauti wala kudai kuwa yeye ni Myahudi kweli hii inaingia akilini?... hata hivyo sintajadili tena kuhusiana na dini turudi kwenye issue yenyewe.
 
Back
Top Bottom