Mag3,
Poor Mkandara, no wonder you dare compare Vatican and OIC. After this I rest my case because all along I believed I was reasoning with an enlightened individual - what a shame!!
...
Duh, mkuu yamekuwa hayo tena?.. haya mimi ndio kabuntas lakini pamoja na yote sina jazba..na hakika sielewi nani kati yetu mchovu..!
Tatizo lako mkuu husomi maelezo ya watu vizuri na umakini. Kwanza ilikuwa Sultan ni lazima awe na elimu ya dini! nimekufahamisha vizuri bila kukushusha mshipa.. haya umerudi na jingine.. yote poa mkuu mimi sina nomaaaa nitakufahamisha bado sijachoka..!
Mkuu kabla ya chombo chochote nchini kujiunga na jumuiya hizi Organisation za kidunia ni lazima serikali yetu ikubali watu hawa kuingia ama sisi kujiunga kisha ktk kujiunga huko ndiko vyombo vinavyoshughulika na chombo mama vinaundwa ama vilivyokuwepo vilivyopeleka maombi..Hizo churches zote zilizojiunga na World council of Churches ni baada ya serikali yetu kukubali hawa jamaa waingie nchini na kuweka kambi zao na ndio maana kuna nchi ambazo pamoja na kuwepo madhehebu hayo hayo hazina ushirikiano na World conncil of Churches. Kuna nchi Umoja huo haukubaliki na serikali yao sio swala la matakwa ya madhehebu ya makanisa..
Je, unaweza kunambia kwa nini kuna nchi ambazo bado hawajajiunga hali ni dhehebu sawa na hilo la Tanzania?..sidhani utasema labda hawajataka...
Nitarudia kusema kwamba kila Organisation inayotaka kuweka mguu wake nchini ni LAZIMA ipate baraka za serikali na muhimu kwa sababu nyingi ikiwa ni pamoja na national security laa sivyo kama ingekuwa ni swala la dini kuamua basi bila shaka Tanzania au niseme Zanzibar wangekuwa wanachama wa Alqaeda..Sii ndivyo mnavyozungwaa! Kulingana na fikra zenu maswala la kujiunga na jumuiya hizi ni maswala ya jumuiya husika, serikali haiwezi kuhusishwa au sio, basi kama ingekuwa rahisi hivyo nchi ingekuwa haikaliki..nasema hivi check tena na Utawala wa nchi ujue (katiba) sheria zake inalenga wapi na nini mapana ya uhuru huo.
Kisha mkuu sikufananisha Vatican na OIC hata kidogo haya maneno unayatunga wewe nilichoandika mimi ni ktk kuonyesha tofauti kati ya
Vatican na Saudia, sio
Vatican na OIC kulingana na hoja ya Rev. Kishoka, ni tofauti ambazo unaweza pia kuziona kati ya World council of Churches na OIC.
Nimetumia muda mwingi kuwaonyesha OIC ni chombo cha aina gani tofauti na vyombo nyenu vinavyoongozwa na makanisa ama dini moja kwa moja na mkuu wa dini ama dhehebu ana mkono ndani ya chombo hicho hali Saudia na OIC ni vyombo vinavyoongozwa na watu wasiokuwa na wadhifa ktk dini ya kiislaam na nikatoa mfano wa Uongozi wa Queen..
Yote hii ni ktk kuwaingiza chumbani mpate kuona kitanda kiko wapi na choo kiko wapi ndani ya jumuiya za kiislaam.
Leo hii unaweza kabisa kumwondoa Sultan King Abdullah wa Saudia na hata kupinduliwa na watu wa kawaida kabisa lakini huwezi kufanya hivyo Vatican. Kiongozi wa OIC anaweza kuondolewa na watu nje ya Utawala wa dini lakini huwezi kufanya hivyo ktk vyombo vya kikristu kama World Council of Churches na ndio maana nikasema nyie Wakristu kusema kweli mmejipanga vizuri ktk uongozi wa dini yenu tofauti na waislaam ambao hakuna chombo cha kidini wala mkubwa isipokuwa ktk sehemu za Ibada...Ktl maswala ya jumuiya we are disorganised ile mbaya, Mkinielewa vitu navyojaribu kusisitizia basi bila shaka mnaweza kabisa kupima mengine.
Mimi sina pingamizi na jambo lolote linalohusiana na Ukristu maadam lina kheri ndani yake iwe kwa sisi wote ama wakristu na halijengi chuki baina yetu..
Je Tanzania sio member wa YMCA na YWCA na lini mliwahusisha waislaam kuhusiana na kujiunga kwenu..ni sehemu nyigni sana naweza kuzitasema lakini kama mlivyo mttaka kunieleza kazi ya vombo hivyo vya kwenu ktk kuendeleza Ukristu lakini nyi tena hamtaki kusikia chombo cha waislaam hata kama kitasaidia watu wote maadam kimebeba neno Uislaam..
kwaherini na nakutakieni majadiliano mema maanake mada hii imefikia mahala ambapo sintapenda kuendelea ila Mwenyezi Mungu mkubwa atawapeni mwanga..
Shukran zangu za dhati kwa Mwanakijiji, Rev. Kishoka, Yournnameismine, Fundi mchundo na wengine ambao tumejadiliana kwa hali tulivu wakati wote..Na nawaomba sana samahani kwa kutumia maneo nkama NYIE.. jambo ambalo sikupenda kabisa kulitumia na wala sii ustaarabu ama lugha nzuri.
Nilikuwepo!