Mpaka Kieleweke
JF-Expert Member
- Feb 27, 2007
- 4,132
- 1,582
Hivi siku rais akiwa Mkristo na mahakama hii ikiwa imeanzishwa atakuwa na udhu wa kumteua kadhi mkuu?Imani hapo inasemaje?
hahaha kusilimisha itakuwa ngumu vatican nayo itakuwa haijalala ati.
kama nia ni kushinda uchaguzi Zanzibar inabidi wachambue kwa kina unaweza kupata hela nyingi kutoka uarabuni, na kushinda zanzibar !BARA je?wakristo nao watataka kuwaondoa katika uchaguzi ili waweze kuvunja mkataba wa kujiunga na IOC, then Kitakachofuata ni kuvunjika kwa Amani, TUNAHITAJI HEKIMA ZAIDI KULIKO KUNG'ANG'ANIA NI NANI KAJIUNGA NA NIFAIDA GANI KAPATA,
Serikali ya Tanzania haina dini ........period......... !!
yeyote anayezumgumzia udini ndani ya seriakli ikiwemo IOC hana tofauti na anayedai Zanzibar ni Sovereign State........
Bernard Membe anataka kugombea Urais na anataka cheap popularity toka kwa Waislam kama alivyowahi kufanya Mzee mmoja ambaye Mwalimu alimfutilia mbali pamoja na kusilimu kwake. This is my take ......be careful with politicians.......
IOC haina masharti kwamba ukijiunga basi nchi yako iwe ya kidini
Nchi ambazo zinaona zinapata manufaa kujiunga kwenye hio IOC kwanini zisijiunge?
Ni kama Waislam wanapokua open minded na wanapowapeleka watoto wao kwenye shule za st
Wanawapeleka watoto wao sio kwamba wanataka kuwabadilisha dini bali wanafuata ubora wa shule.
Mimi kama Darwin sijui manufaa ya IOC ila kama kuna wanaojua wanifahamishe.
Na kama IOC ina manufaa kwa watanzania kwanini iwe dhambi Tanzania kujiunga kwenye IOC.
Au mnataka kuniambia kwamba hospitali Agha khan inawasaidia waislam tu?
Au KCMC inawasaidia wakiristo tu.
Kama walivyosema wenyewe kwenye web-site yao, OIC ni chombo kinachowaunganisha waislamu. Kipo kulinda maslahi ya waislamu. Sasa kwa nini tuone ugumu kusema hili? Watu hawapingi kwa sababu kiongozi wake ni muislamu au makao yake makuu yako kwenye nchi ya kiislamu. La hasha. Ni identity yake kama chombo cha waislamu ndiyo inayowatia uoga.
Cha kujiuliza, ni jee, kuna ubaya wa chombo cha kiislamu kutetea maslahi ya waislamu? Na je, kuna ubaya gani kwa nchi yetu yenye waislamu wengi tu, kujiunga na chombo ambacho kitaangalia na kutetea maslahi yake? Je hawa waislamu wetu wangeweza kupata uwakilishi katika chombo hicho kupitia namna nyingine? Ukweli ni kuwa, hamna, hiki chombo kinaunganisha nchi na si vinginevyo. Kama jumuia ya madola. Kama Umoja wa Mataifa. Bakwata na hata EAMWS ingekuwepo isingeweza kujiunga. Zanzibar haiwezi. Mji wa Pangani hauwezi. Ni nchi tuu ndiyo inayoweza.Kama tunawakubali hao waislamu kuwa sehemu ya jamii yetu kwa nini tukatae ku'facilitate' wao kuweza kupata neema? Tukiona kuwepo kwetu huko kuna wadhuru wasio waislamu si tutaweza kujitoa? Ni kama vile Tanzania kujiunga na FIFA wakati si raia wake wote wanaopenda au kucheza mpira! Au shirikisho la Netball wa dunia. Tatizo liko wapi? Kwa vile hakuna chombo kama hicho kwa wakristu, si sababu ya kukataa kujiunga. Kama OIC wana ajenda nyingine zaidi ya kuwasaidia wenye dini wenzao basi iwekwe wazi.
hahaha kusilimisha itakuwa ngumu vatican nayo itakuwa haijalala ati.
kama nia ni kushinda uchaguzi Zanzibar inabidi wachambue kwa kina unaweza kupata hela nyingi kutoka uarabuni, na kushinda zanzibar !BARA je?wakristo nao watataka kuwaondoa katika uchaguzi ili waweze kuvunja mkataba wa kujiunga na IOC, then Kitakachofuata ni kuvunjika kwa Amani, TUNAHITAJI HEKIMA ZAIDI KULIKO KUNG'ANG'ANIA NI NANI KAJIUNGA NA NIFAIDA GANI KAPATA,
Serikali ya Tanzania haina dini ........period......... !!
yeyote anayezumgumzia udini ndani ya seriakli ikiwemo IOC hana tofauti na anayedai Zanzibar ni Sovereign State........
Bernard Membe anataka kugombea Urais na anataka cheap popularity toka kwa Waislam kama alivyowahi kufanya Mzee mmoja ambaye Mwalimu alimfutilia mbali pamoja na kusilimu kwake. This is my take ......be careful with politicians.......
Mifano yako inahusu vitu vidogo visivyoweza kulinganishwa na nchi, wala haviwezi kufananishwa au kulinganishwa. Tusiwe biased, wakati tunakataa kufungua ubalozi wa Israel ndo wakati tunaotaka kujiunga na OIC!
Nauliza tena je tuanzishe Pettition ya Tanzania kujiunga na World Council of Churches?
FM usihadae watu, nani aliitaka Bakwata?..Mwalim ndie source ya Bakwata, na hadi leo inalindwa na Serikali...Waislam walikuwa na chombo chao, EAMWS, Nyerere akaivunja, na akapandikiza racism...
Mahakama ya kadhi ..haiamui kesi ulizozitaja hapo juu, uliza uambiwe!!!
Waulize wanasheria wako hapo Mliman au ktk vigenge vyao wakuambie kuwa sheria za Kiislam(Allah revealed laws) zilivyokuwa makini kuliko man made laws... leo akija Mchundo inafaa kesho akija Ben haifai...
Comrade Mkandara,
Nimekupata vizuri, labda hukunielewa au hujui msimamo wangu uko wapi katika jambo hili.
Nauliza maswali ya msingi kwa kuwa hoja imekuwa ni lazima Tanzania ijiunge na OIC ili kulinda maslahi ya Waislamu. Sasa OIC ni ushirika wa Nchi za Kiislamu. Swali linakuja, je Tanzania ni nchi ya Kiislamu? majibu yanakuja Msumbiji na Uganda ni Wanachama lakini si kujibu kama Tanzania ni nchi ya Kiislamu au laa.
Ndipo nikauliza kuna shida gani basi kwa Tanzania kujiunga na World Council of Churches?
Swali si kuzuia Waislamu kama jumuiya kujiunga na kunufaika na OIC, suala ni ukingiza Tanzania kama nchi ambayo hakuna majority religion kuwa mwanachama wa Jumuia ya Nchi za Kiislamu!
Ndio maana nilipoleta mfano wa Marekani, Pakistani, Canada na India nilisema kama ni misaada, basi hata yao ina walakini kwa kuwa kuna umasikini.
Sasa umezungumzia jumuiya ya Watanzania Kanada, minnesota kuna jumuiya ya Watanzania Umoja society, kuna wanachama Wakenya, Waganda hata kutoka Rwanda. Hawa wameingia kwa utashi binafsi kwa kuwa jumuiya ni za mtu mmoja mmoja.
Kujiunga OIC ambayo lengo lake kuu ni umoja wa Kidini huku Tanzania si nchi iliyofungamana na dini na mgawanyo wa raia kidini ni sawa, huku ni kujitakia matatizo maana hakuna ridhaa ya wananchi.
Kama alivyosema mtoa haja mmoja mapema, hatuwezi kujifananisha na Msumbiji au Uganda kwa kuwa hatufahamu katiba zao au taratibu walizofuata wao kujinga na OIC.
Ubaya wa huu mjadala ni jinsi ulivyoletwa na kushinikizwa kwetu na Wanasiasa.
Inaelekea wazi kuwa kauli hizi za harakaharaka hazijafikiriwa na ni juhudi za kuhalalisha mambo fulani ya kisiasa kama nilivyosema hapo awali kuwa Kikwete anakuwa compromised na ku-succumb to blackmail ili fukuto la Muungano litulie.
Kama jinsi tatizo hili la kujiunga OIC lilitokea 1993 pamoja na Membe kudai kuwa Zanzibar na Diria walijiingiza kinyemela, bado kwa Tanzania kujiunga OIC kutaleta vurugu na kutokuelewana.
I wish we could sit down and resolve the Muungano issue first as a nation and then let other things like OIC and Kadhi fall in place after reconciliation and new constitution with Union or without union!
Ni kweli unachosema na hasa mawazo yako ndiyo yenye lengo la kibaguzi. Kinacholetwa hapa ni maoni na kila mtu ana maoni yake. Kwa nini maoni yasiyoendana na yako uone ni ya kibaguzi?
Hoja kwamba hata Nigeria ni mwanachama siyo hoja hata kidogo kwani ungeweza kusema pia kuwa mbona Kenya, Afrika Kusini au DRC siyo wanachama. Kwangu mimi swali ni kwa nini sisi kama Tanzania tunataka kujiunga na OIC. Kitu ambacho naweza kuhoji ni kwamba Tanzania imesaini The Universal Declaration of Human Rights wakati OIC hailitambui kwa vile siyo 'consistent with Sharia Law'.
Ila OIC inatambua The Cairo Declaration of Human Rights in Islam na Article 24 inasema: "All the rights and freedoms stipulated in this Declaration are subject to the Islamic Shari'ah" wakati Article 25 inasema: "The Islamic Shari'ah is the only source of reference for the explanation or clarification of any of the articles of this Declaration."
Swali langu ni kwamba kwetu sisi kuwa wanachama wa OIC ina maana kwamba na sisi pia tunazikubali hizi articles zilizotajwa hapo juu au tutaendelea na zile za Universal Declaration of Human Rights?
Na pili, tunajiunga kwa mambo yapi hasa? Haya yote yangewekwa wazi isije huko mbele tukaanza kuingizwa kwenye mikataba itakayoanza kuleta machafuko nchini.
Tatu, hakutakuwa conflict of interests hasa kwa vitu ambavyo ni 'fundamentals'? Naomba machango wenu.