Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Naamini kuwa kilichochangia sisi watu wa bara kutokuwa na migongano ya kidini au ya kikabila ni kuwa toka awali juhudi zilifanywa kutuchanganya bila kuangalia dini zetu au kabila letu. Tumekuwa pamoja, tumesoma pamoja , tumefungwa pamoja na tumezikana pamoja bila kuambiwa huyu kwa sababu tu ya imani yake ni tofauti na wewe. Kwa hali hiyo tumejuana na kushibana kiasi ambapo wale wa kizazi changu ni vigumu kumchukia yule ambaye si wa dini yako maana utakuta marafiki zako na ndugu zako wengi wanatoka dini hiyo. Leo hii tumeanza kusoma kila mmoja kivyake kuanzia chekechea hadi chuo kikuu. Na hili la kutuambia kuwa wenzetu watakuwa wanahukumiwa tofauti na wengine kutazidisha ufa ulioanza kujitokeza katika jamii yetu. Tunakanyaga kwenye utelezi na tusipoangalia tutaishia kubaya.
 
Mie sijasoma maelezo yote juu kuhusu maana ya mahakama ya kadhi nini..kama wanakusudia kuhukumu Kiisilam yani kwa dini ya kiisilam hadi sasa hata hao ambao ni nchi za kiisilam bado hawajaweza..ikiwa miongoni mwake ni saudia..ukiacha nchi za kiarabu tu ambazo sio za kiisilam..sasa sisi tanzania bado kabisaaa

Unaongea tu au unajua?
Kafuatilie tena huko Saudia!
 
Bubu yaani kwanini tujipalie mkaa eti tusubili yakisha tukuta ndo tukimbilie katiba?

We simply say No to Kadhi period. Hasa hasa kwamba kodi zetu wote zilipie taasisi ya wachache?? No No a big Nooooo!!

As long wewe sio muislamu basi hutolipa kodi na mahakama ya kadhi HAIKUHUSU!
 
Nijuavyo mimi, ikiwa mahakama ya kadhi itaanzishwa muislam atakayebadili dini hukumu yake ni kali. Hiyo inapingana tena na katiba inayosema mtu ana haki ya kuabudu didni anayotaka. Those are the complications that come with kadhi courts
 
Bongo,Siku zote CCM imekuwa ikitawala kiujanja-ujanja kwa kutumia shida na ujinga wertu Watanzania ili wapate ridhaa ya kutawala na hii ni hatari kubwa. Ishara ya hatari hii ni hii Waislamu kudai mahakama ya Kadhi (pamoja na hoja nzuri za Mwkjj kuhusu hoja hii). Ukiangalia kwa undani CCM wametumia shauku (shida) ya kundi mojawapo lenye ushawishi kwenye jamii ili kupata kura za kuendelea kutawala.

Nathubutu kusema iwapo Mahakama hii itakuwepo tutashuhidia kuparanganyika kwa Taifa letu kutakosababishwa na ujanja-ujanja huu wa CCM maana Mahakama ikianzishwa tu lazima makundi mengine yenye ushawishi mkubwa katika nchi hii (Wakristo) nao watadaisheria za Kanisa zitambuliwe Kikatiba na kutumika na kwa hila hizo hizo za CCM kutaka kuendelea kutawala basi watakubali (hawatakuwa na sababu ya kukataa wakati wamekubali kutambua Mahakama na mamlaka ya Kadhi)na hivyo tutashuhudia Taifa letu likiongozwa na sheria tatu tofauti zinazopingana. Mfano, Kanisa haliruhusu talaka wakati Sheria za Kiislamu zinatambua na Serikali hutambua; je, itakuwaje pale ambapo mtu na mke wake au mumewe kila mmoja anataka ifuatwe sheria tofauti kuhusu talaka katika shauri lake? Sijui Makarasinga na Wahindu nao wakitaka sheria za dini zao zitumike itakuwaje.

Hili litapelekea mwishowe kila dini iwe na eneo lake la kujitawala ambapo sheria zake ndiyo zinatambuliwa na kutumika kama vile Islamic territory, Christian territory na Government/Secular territory.

Nathubutu kusema kuwa kama Serikali ya CCM iko makini na haitaki kuliingiza taifa kwenye madhara Mahakama ya kadhi haitakuwapo na ikiwepo basi Sheria za kanisa nazo itapaswa zitumike, what a contardiction! Sulal la Mtikila (ingawa watu wanamwona kuwa ni kama Chizi katika suala la Mahakama ya Kadhi) ni ishara tu ya mambo yatakavyokuwa pindi Mahakama ya kadhi itaanzishwa.

Serikali ya CCM itabidi ituambie kwa nini iwakubalie Waislamu kutumia sheria za kidini katika masuala yao na kutukatalia sisi Wakristo kutumia sheria zetu!

maswali yako ni straight forward. Kama umeoa mbele ya kadhi basi utahukumiwa na kadhi! Na mkikubaliana kisheria za nchi msikimbilie kwa kadhi baada ya matatizo yenu!....... Jst like that simple
 
Nijuavyo mimi, ikiwa mahakama ya kadhi itaanzishwa muislam atakayebadili dini hukumu yake ni kali. Hiyo inapingana tena na katiba inayosema mtu ana haki ya kuabudu didni anayotaka. Those are the complications that come with kadhi courts

Jee kama wakieka limitations?...... Think inside and outside!......
 
Tatizo hutaki kuangalia ukweli kwamba kuna "slippery slope" hapo mbele, hii ya Mahakama ya kadhi itakuwa kama mvua itayoongeza huo uterezi. Mch Mtikila katoa "preview" tu ya nini kinachoweza kutokea kama mahakama hizi zikiruhusiwa. Sijasikia kwamba Waislam wa Zanzibar ni waislam sana kuzidi wale wa bara ati kwasababu tu wao wana mahakama ya kadhi. Kuna issue mingi sana za maana ndani ya uislam hapo bongo na nchi nzima kwa ujumla, na hii ya kadhi courts sidhani kama itajenga chochote cha maana zaidi ya kugawa watu. Kwanza nani kafanya-research kujua kwamba majority ya waislam wa bara wanataka hizi mahakama?? au ndio "udikteta" wa Bakwata!!? nani ana data kwamba waislam walim-vote kikwete ati miongoni mwa mengine ni kuahidi mahakama za kadhi kwa waislam?? Je hii si kwamba, watu wanataka kumweka Raisi na chama chake kwenye loose loose situation, wakti wakijua kwamba licha issue hii ni feasible lakini ni very diversive, kwa ajili ya political gains?.....baadae iwe raisi mbaya kwasababu kawapa waislam mahakama na wengine waseme mbaya kwasababu hakutimiza ahadi zake, na wengine waseme sisi mbona katubagua!!!!..........mwisho wa siku inakuwa chaos ya kisheria on top ya matatizo lundo ambayo tayari yanatukabili bila ahueni yoyote kwenye forecast. Ladies and gentlemen JUST SAY NO!!!!!.

I really dont see any point you are trying to make.
You know what you should do, jst ask how it will work! it will help you to understand!
 
Hapa HAKUNA MAHAKAMA YA KADHI wala nini
Mimi na mke wangu tuko dini tofauti, mmoja kati yetu ni Islam na mwingine Mkristo, sasa tukitofautiana tutasuluhishwa na mahakama gani?
 
I strongly oppose this....hii kitu mahakama ya kadhi ni selfishness tuu ya hardcore wingnut wachache wapenda udini na wanajua wakifanikiwa hili ndio mwanzo wa kupenyeza agenda zao na tunajua dini zote zinataka kuwa na influence/power kwenye utawala wowote ule,haya mambo ya dini sheria za kiislam kaeni nazo huko misikitini na waumini wenu,mnataka kutumia sheria za kiislam then jela mtatumia za nani mkitaka kuwafunga wakosaji? na vipi mtawapiga mawe wazinzi hadharani na kuwakata mikono wezi huku wengine tukiangalia,na dont waste ur time & being deluded this will never happen labda sheikh Ponda asiyejua kusoma wala kuandika awe Raisi.
 
Fikira duni kama hizi ndio tatizo na sio mahakama ya kadhi ama ubalozi wa Vatican

TanzaniaNjema,huenda huna background nzuri kidogo,si kosa lako.

Binafsi napiga kwa nguvu zote mahakama ya kadhi,haina lengo la kuendeleza ibada,zaidi sana ni kukuza influence ya uislamu na falme za kiarabu hapa Tanzania.

Narudia tena,waislamu si wa kuwaamini hata kidogo,kwani moja ya marais wetu alidiriki kuweka mkakati wa kuibadilisha nchi hii,kuwa "The United Islamic Republic of Tanzania",njama iliyokosa uhai pale wasomi wetu walipoishtukia na kuiweka jamvini.

Kwa wenye vichwa vigumu,mtakumbuka tukio la staili yake ya kufukuzwa kwa wanafunzi wote pale chuo kikuu miaka ile wazee wenu tunasoma pale.

Wasomi walishtukia deal zima,so mkuu wa nchi akaamua kutufukuza wote kwa sababu ya kupandikiza.

Acheni ujinga na ushabiki juu ya kadhi na ushamba wa kunyenyekea tamaduni za watu zitawatokeeni puani,eboooooooooo.
 
I strongly oppose this....hii kitu mahakama ya kadhi ni selfishness tuu ya hardcore wingnut wachache wapenda udini na wanajua wakifanikiwa hili ndio mwanzo wa kupenyeza agenda zao na tunajua dini zote zinataka kuwa na influence/power kwenye utawala wowote ule,haya mambo ya dini sheria za kiislam kaeni nazo huko misikitini na waumini wenu,mnataka kutumia sheria za kiislam then jela mtatumia za nani mkitaka kuwafunga wakosaji? na vipi mtawapiga mawe wazinzi hadharani na kuwakata mikono wezi huku wengine tukiangalia,na dont waste ur time & being deluded this will never happen labda sheikh Ponda asiyejua kusoma wala kuandika awe Raisi.

Haya ni matusi na maneno yasiyo na maana.
Lakini ukija kwenye UTANZANIA upande mwengine bado unawavulia,hizo choko choko ulizoandika humo huzioni kuna wenzio wengi wameandika maneneo kama hayo still bado wanawavumilia hivi wakijibu si tutafika pabaya?
Achana na fikra potofu,kama kuna jambo la maana mnaweza kusema ni UBORA WAISILAMU WAANZISHE HIYO MAHAKAMA KWA PESA ZAO NA WAENDELEE KUABUDU NA SIO KUWAFANYA WAISILAMU NI WAJINGA NA SI WASOMI KAMA NYINYI.
Lakini on the other hand,inaweza kuwa si makosa yako labda wa yule aliyepotosha HISTORIA ya nchi hii lakini nadhani hujachelewa its just a matter of time kabla ya ukweli ha\uja\wa\ wazi.
 
Dr Khamis
Ni kweli MUNGU amerahisisha mambo ila binadamu tunajaribu kuyafanya magumu,

Haya ni maoni yangu si kila jambo liliondikwa ktk vitabu vitakatifu lazima litekelezeke lilivyo ,linategemeana kwanza na mazingira na wakati.

Naomba msamaha kwayeyote nitayemuudhi kwa mfano huu na swali hili.

Je Waislamu UGAIBUNI ina maana hawali nyama ya aina yoyote ?? maana kama ni kuku ,ng'ombe zinachinjwa kwa machine ,tena mashine hiyohiyo inamkatakata nguruwe pia.Hakuna cha uelekeo wala nini kuku anatupwa mashine inafanya kazi.Mmeshasikia wanagoma kula nyama??

Vitu vyote vinategemea mazingira na wakati na kwa mazingira yetu TZ hiyo kadhi inatakiwa iwe taasisi ndani ya BAKWATA.

Sawa umesema vizuri na swali lako pia nizuri waisilamu walio wengi na hasa wanojua dini yao walau kidogo,mara nyingi wakiwa katika nchi hizo hula mahara palipo andikwa HARARI FOOD tu mimi nikiwa mmoja wapo hata tukiwa huko UCHINA kwenye makorokoro na uchafu wa kila aina.

Hilo la nililo la mwisho jibu lake nihi.

KWANZA BAKWATA SIO CHOMBO CHA WAISILAMU ILA CHA KISILAMU KILICHO UNDWA NA SERIKALI YA TZ MWAKA 1964 BAADA YA KUFUTA EAST AFRICA MUSLIM SOCIAL WALFARE SOCIATY NA NYERERE AKAUNDA HIYO BAKWATA NA KUMTEUA MUFTI WA KWANZA.MISHAHARA NA MARUPURUPU YA VIONGOZI W A CHOMBO HIKO YANALIPWA NA SERIKALI TOKA TANGU.
NDIO MAANA WAISILAMU WANATAKA KUWEPO NA HIYO KADHI COURT KWA NIA YA KUA NA CHOMBO MBADARA WA BAKWATA KUWASIRISHA WAISILAMU NA SIO SERIKARI NA MASLAI YAKE KWA WAISLAM.
 
[/COLOR][/SIZE]

umejibu vyema
Sasa inabidi tuangalie mtazamo na maudhuhi.
Je kama mimi na mke wangu wote tupo waisilamu tukakosana mke wangu akanishitaki kwa kadhi na mimi nikakataa ni kasema hii kesi nitaikubali tu kama ikiwa kwenye mahakama za public je kadhi atanifanya nini?

Na je Kadhi ikinihuku nikaikataa hukumu kwa makusudi kadhi itanifanya nini?

Na je kadhi ikinihukumu harafu mimi nikasema sio mwislamu je kadhi itafanya nini?

Naomba majibu ya maswali hayo ili tujadili zaidi.
 
Tatizo kubwa ambalo baadhi ya watu wanalo kuhusu Mahakama ya Kazi ni "Jinsi gani itafanya kazi" katika frame ya mfumo wa sheria tulio nao. Mifano inayotolewa hapo juu kwa kweli inaonesha kuwa watu wengi hawajui hata mahakama ya Kadhi ikoje. Naomba nisema yafuatayo:

1. Mahakama ya Kadhi inaweza kuwepo hata kwenye nchi ambayo ni secular (isiyofuata dini). Nchi ambazo mahakama za kadhi zipo ni pamoja na Israeli (ya wayahudi) na India (ya Wahindi). Nchi kama Afrika ya Kusini nayo inazo na sehemu kadhaa za Pakistani utazikuta. Lakini baadhi ya nchi zenye waislamu wengi kama Uturuki na Indonesia hazina mfumo wa Mahakama ya Kadhi ambao tunaweza kusema siyo wenye msimamo mkali kama wa baadhi ya nchi.

2. Mahakama za Kadhi siyo za aina moja (not homogeneous). Kutegemeana na nchi mahakama za kadhi zinatofautiana sana kuanzia uwezo wake, sheria zake, na msimamo wake kuhusu mambo mbalimbali. Kuanzia kuvunjika kwa Uhalifa wa Umma wa Kiislamu, nchi mbalimbali za Kiislamu au jamii mbalimbali za Waislamu zimetengeneza Mahakama za Kadhi kuendana na mazingira yake na mahali pake.

Hivyo Mahakama ya Kadhi ya Israeli siyo sawa na Mahakama ya Kadhi ya Sudan na kwa hakika siyo sawa na Mahakama ya Kadhi ya India (India hazitambuliki kisheria lakini zipo kwenye maeneo yenyewe Waislamu wengi). Hivyo, tunapozungumzia mahakama ya kadhi tusichukulie mfano wa nchi fulani au nchi nyingine kwani hakuna mfano unaokubalika wa uendeshaji wake ambao waislamu wa Tanzania watalazimika kuufuata.

3. Ukizingatia 2 hapo juu utaona basi mahakama za kadhi zinatofautiana hususana linapokuja suala la makosa ya jinai. Kwenye nchi kama Sudan mahakama zao za kadhi ndizo zinaamua mambo yote hata ya jinai, wakati zile za India na Israeli zimeacha makosa yote ya jinai kwenye mikono Serikali. Miaka ile kule Indonesia (Hata Tanzania kabla ya Uhuru) mahakama za kadhi zilitoa maamuzi siyo kwa waislamu tu bali hata kwa wasio waislamu alimradi wanaamua wenyewe kwenda kuamuliwa na mahakama hizo.

Mfano mzuri wa hilo ni mahakama tunazoziona kwenye TV za kina Jaji Judy. Mtu halazimiki kwenda kwenye mahakama hizo za "TV" lakini akitaka kesi yake ya madai (siyo ya jinai) iamuliwe huko basi anatia sahihi fomu kadhaa na kujiweka chini ya maamuzi ya mahakama hizo. Hivyo, endapo mahakama za kadhi zitarudishwa nchini basi kuna uwezekano wa baadhi ya watu wakijua faida ya hukumu ya mahakama hizo kulinganisha na ile ya mahakama za serikali wakaamua kutatua migogoro ya madai chini ya Kadhi.

4. Jambo kubwa ambalo kwa Tanzania linasumbua sana na hapa nakubaliana na wengi ni ulazima wa mahakama hizo aidha kuingizwa kwenye Katiba au kuendeshwa na serikali. Hoja ya watetezi wa mahakama ya kadhi ni kuwa wanataka iwe hivyo ili hukumu zake zitambulike kisheria. Hoja hii inaweza kuwa na nguvu endapo tu wanachotaka ni kuhusiana na masuala ya jinai.

Lakini kama jumuiya ya Waislamu wanaona kuwa ulazima wa mahakama ya Kadhi ni sehemu ya ibada ya Muislamu au kukamilisha din basi wanajikuta kwenye matatizo makubwa kwa sababu endapo serikali isiyo na dini ikaamua kuingiza ibada ya dini moja kwenye Katiba na kutambua ibada hiyo kwa maneno mengine itakuwa imetangaza de facto kuwa serikali hiyo ni ya dini hiyo moja. Na hapa ndipo watu wengine wanatishwa.

5. Naamini kama Waislamu kweli wanataka kuanzisha mahakama ya Kadhi wanaweza kufanya hivyo wao wenyewe na wakishauriana na serikali kuhusu wigo wa upana wa nguvu za kisheria. Kwa vile tumesema kuwa Mahakama ya Kadhi inaweza kuwa hadi kwenye masuala ya jinai basi ni lazima kuwe na mipaka ya aina fulani.

Hapa ndipo naona haja ya serikali kubadilisha Katiba au Sheria na kuweka kipengele kama hiki:

"Taasisi yoyote ya kidini inaruhusiwa kuanzisha utaratibu wake wa kukata mashauri na kutoa haki kwa kuzingatia kanuni kubwa zifuatazo:
1. Haitatoa hukumu kuhusu makosa ya jinai
2. Haitatiooa hukumu kwenye kesi zinazohusisha muumini wa dini zaidi ya moja
3. Haitatoa hukumu kwa mtu yeyote ambaye hayuko tayari kujiweka chini ya taratibu hizo/mahakam hizo.
4. Mtu yeyote anayeamua kukata shauri au kutafuta hukumu kwenye mahakama ya kidini apewe nafasi na haki ya kutambua kuwa uamuzi huo wa kidini hautakatiwa rufaa kwenye mahakama yoyote ya serikali. Mtanzania akianza jambo lolote kwenye mahakama ya dini basi utaratibu wa rufaa ni huo huo wa kidini.
5. Mahakama za kidini hazitaendeshwa, kufadhiliwa, au kwa namna yoyote ile kupata malipo kutoka serikalini. "
 
Haya ni matusi na maneno yasiyo na maana.
Lakini ukija kwenye UTANZANIA upande mwengine bado unawavulia,hizo choko choko ulizoandika humo huzioni kuna wenzio wengi wameandika maneneo kama hayo still bado wanawavumilia hivi wakijibu si tutafika pabaya?
Achana na fikra potofu,kama kuna jambo la maana mnaweza kusema ni UBORA WAISILAMU WAANZISHE HIYO MAHAKAMA KWA PESA ZAO NA WAENDELEE KUABUDU NA SIO KUWAFANYA WAISILAMU NI WAJINGA NA SI WASOMI KAMA NYINYI.
Lakini on the other hand,inaweza kuwa si makosa yako labda wa yule aliyepotosha HISTORIA ya nchi hii lakini nadhani hujachelewa its just a matter of time kabla ya ukweli ha\uja\wa\ wazi.

...hii garbage yako peleka mwembechai labda watakusikiliza...you're pathetic!
 
umejibu vyema
Sasa inabidi tuangalie mtazamo na maudhuhi.
Je kama mimi na mke wangu wote tupo waisilamu tukakosana mke wangu akanishitaki kwa kadhi na mimi nikakataa ni kasema hii kesi nitaikubali tu kama ikiwa kwenye mahakama za public je kadhi atanifanya nini?

Na je Kadhi ikinihuku nikaikataa hukumu kwa makusudi kadhi itanifanya nini?

Na je kadhi ikinihukumu harafu mimi nikasema sio mwislamu je kadhi itafanya nini?

Naomba majibu ya maswali hayo ili tujadili zaidi.

Je unataka nikujibu zaidi ya hayo maelezo ya MWKJJ!?
 
Je unataka nikujibu zaidi ya hayo maelezo ya MWKJJ!?

kama umekubaliana na mwkjj basi mimi nitasema hivi.

1. Mahakama ya kadhi itakua ni hiari ama utashi wa mtu kwenda huko na kama ndiyo basi hakuna haja yakuunda kwa sheria na inapaswa kuundwa hivyo hivyo ki utashi huko msikitini. Maana ya kuunda kitu kwa sheria ni ukikivunja lazima sheria ifuatwe na kama ni hiari basi hakuna haja yakupigiana kelele na wabunge kupitisha hiyo sheria.

2. Kama umekubaliana na mwkjj kua Kadhi inafanya kazi tofauti tofauti kulingana na nchi basi KADHI sio SEHEMU YA IBADAA ya WAISLAMU.

Kama unamajibu mengine naomba majibu.
 
Back
Top Bottom