Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Wengi wametoa hoja, matusi, kejeli etc. Mahakama ya kadhi hatohukumiwa mlevi, mwizi, mzinzi, au yeyote asiyekuwa muisilamu. Mahakama hii ni kwa ajili ya maswala yanayomuhusu muisilamu na imani yake maelekezo ya dini yake na itikadi zake katika ndoa, talaka, mirathi na wasia.

Ama maswala ya jinai yote hata wizi, kubaka, ugaidi, biashara haramu, na matatizo mengineo yote yatatawaliwa na sheria iloyopo ama inayotumika nchini. Mahakama ya kadhi haingilii maswala ya wanaogombana au kudaiana madamu sheria ya nchi ipo.

Sasa mimi nashangaa kuona mtu asiyekuwa muisilamu anatowa hoja juu ya kisichomuhusu. Mahakama ya kadhi haimuhitaji asiyekuwa muisilamu kumfafanuliya ya uisilamu maana hayo hayamuhusu kamwe.

Iwapo wakristo wanazo hukumu zao wenyewe zinazotakiwa na dini yao basi kwanini nao wanyimwe haki yao hiyo ya kuabudu?

Yote yaamuliwe ila hukumu ya muumba isichezewe. Tusijifanye ni watu wazuri wa kuongea sanaaaa wakati utumbo mtupu.

Uhuru wa kuabudu uheshimiwe popote pale.
 
kama umekubaliana na mwkjj basi mimi nitasema hivi.

1. Mahakama ya kadhi itakua ni hiari ama utashi wa mtu kwenda huko na kama ndiyo basi hakuna haja yakuunda kwa sheria na inapaswa kuundwa hivyo hivyo ki utashi huko msikitini. Maana ya kuunda kitu kwa sheria ni ukikivunja lazima sheria ifuatwe na kama ni hiari basi hakuna haja yakupigiana kelele na wabunge kupitisha hiyo sheria.

2. Kama umekubaliana na mwkjj kua Kadhi inafanya kazi tofauti tofauti kulingana na nchi basi KADHI sio SEHEMU YA IBADAA ya WAISLAMU.

Kama unamajibu mengine naomba majibu.

not to disrespect,unajua ungekua Muislam ungenielewa vizuri lkn nitakupa mfano,
Kwa muumini wa roman catholic akiwa haja batizwa na hayuko kwenye jumuiya ya ushirika anaoishi ni vigumu kuoa au kuzikwa na wanaushirika huo au makanisa yote( nimejua hayo kwani mimi nilikua huko).
Sasa uisilamu pia unataratibu zake ikiwa ni;
1.kumjua mungu na mtume wake
2.kuikubari quraan (inajumuisha sheria na taratibu zake ambayo hukumu zimo ndani yake)
Na mambo mengine yanapata matano kwa ujumla wake ndio mtu anakua muislamu kamili,na huwezi kua muislam mapaka huyatimize na kukiuka moja wapo unatia walakini uislam wako.
Sasa ili imani iwe ya kweli lazima ufate yaliyomo ndani ya quraani na waisilamu wote wanajua ukikubari kuwa muisilamu utakubari na sheria zake,sio kitu tena cha kuchagua kufata au kutofata.
 
Naona huo moto wamekosea walikouwasha ilibidi wauwashe kunako husika.
 
Kuna wakati wa kila kitu kwenye maisha kama kwenye siasa pia, mimi binafsi sioni sababu ya kunyimwa kwa kikundi kimoja cha jamii matakwa flani kama haya ya Kadhi, lakini kuwe na understanding kisheria kuwa mahakama hizo hazitakuwa na anything to do na sheria zetu za Jamhuri,

Na kwamba serikali yetu haitatambua anything kutoka kwenye hizo mahakama isipokuwa ndoa tu, katika demokrasia ni vigumu sana kuwanyima wananchi wanachotaka ambcho hakivunji sheria, nisichoelewa hapa ni kimoja ni kwa nini hii hoja ilipelekwa bungeni?

Kwa sababu hawa wananchi wangeweza kuanzisha hiyo Kadhi yao bila ya kutupigia kelele taifa zima, kwa sababu kama ni ruzuku ninaamini kuwa kila kundi kubwa la kidini ni lazima lipewe fungu na serikali, lakini Jamhuri haiwezi kuitegmea mahakama ya Kadhi as an alternative kwa heshima ya the rule of law, halafu wakuu ninaomba tuwe watulivu kidogo na hii debate kwa sababu kuna wananchi wanajaribu kuchota hoja hapa na hasa viongozi wetu wngi wapo hapa kutafuta cha kusema, tuheshimu taifa hapa maana hizi ndio ishu hasa zinagusa taifa moja kwa moja!

Ahsante wakuu!
 
not to disrespect,unajua ungekua Muislam ungenielewa vizuri lkn nitakupa mfano,
Kwa muumini wa roman catholic akiwa haja batizwa na hayuko kwenye jumuiya ya ushirika anaoishi ni vigumu kuoa au kuzikwa na wanaushirika huo au makanisa yote( nimejua hayo kwani mimi nilikua huko).
Sasa uisilamu pia unataratibu zake ikiwa ni;
1.kumjua mungu na mtume wake
2.kuikubari quraan (inajumuisha sheria na taratibu zake ambayo hukumu zimo ndani yake)
Na mambo mengine yanapata matano kwa ujumla wake ndio mtu anakua muislamu kamili,na huwezi kua muislam mapaka huyatimize na kukiuka moja wapo unatia walakini uislam wako.
Sasa ili imani iwe ya kweli lazima ufate yaliyomo ndani ya quraani na waisilamu wote wanajua ukikubari kuwa muisilamu utakubari na sheria zake,sio kitu tena cha kuchagua kufata au kutofata.

Mkuu Wangu Sanda Matuta,

Heshima mbele kaka, naomba kukuuliza what hii hoja yako has to do na Jamhuri, au taifa yaani sisi taifa at large hii hoja yako inatuhusu vipi?
 
Wengi wametoa hoja, matusi, kejeli etc. Mahakama ya kadhi hatohukumiwa

1. mlevi, mwizi, mzinzi, au yeyote asiyekuwa muisilamu.

2. Mahakama hii ni kwa ajili ya maswala yanayomuhusu muisilamu na imani yake maelekezo ya dini yake na itikadi zake katika ndoa,

3. talaka, mirathi na wasia.

Mkuu Heshima mbele,

Mawili ya juu ni sawa kabisa, lakini hili la tatu ni la sheria za Jamhuri period, no way tunaweza kuzipa hizo mahakama wajibu mzito kama huo, kwa sababu kuna wakristo walio oa wa-Islam na vice versa, ni ana madhumuni mojawapo hasa ya kuwa sheria za jamhuri kimsingi ni pamoja na kwenye hili la tatu, hilo hatuwezi kulitoa kwenye sheria za Jamhuri.
 
Wengi wametoa hoja, matusi, kejeli etc. Mahakama ya kadhi hatohukumiwa mlevi, mwizi, mzinzi, au yeyote asiyekuwa muisilamu. Mahakama hii ni kwa ajili ya maswala yanayomuhusu muisilamu na imani yake maelekezo ya dini yake na itikadi zake katika ndoa, talaka, mirathi na wasia.

Ama maswala ya jinai yote hata wizi, kubaka, ugaidi, biashara haramu, na matatizo mengineo yote yatatawaliwa na sheria iloyopo ama inayotumika nchini. Mahakama ya kadhi haingilii maswala ya wanaogombana au kudaiana madamu sheria ya nchi ipo.

timtim, hapa inabidi utuambie unajuaje kuwa haitakuwa hivyo; Mahakama za Kadhi katika nchi nyingine zimetoa hukumu hadi makosa ya jinai (mifano ya Nigeria na Sudan inanijia). Kwanini mahakama za kadhi za Tanzania zitakuwa tofauti kama sheria wanayofuata ni ile ile? Ni kitu gani kitazuia mahakama ya kadhi kutoa hukumu kwenye masuala ya jinai, hasa maeneo ambayo siyo tu ni makosa katika utawala wa kiraia lakini pia ni makosa katika Uislamu?

Kwa mfano, wizi ni kosa na lina adhabu katika civil law na lina adhabu katika Islamic law. Kama mwizi ni Muislamu je ahukumiwe kwa sheria ipi? Je akitaka ahukumiwe kwa sheria ya Kiislamu, serikali inaweza kukataza? Na hapa itabidi mtu aeleze ni kwanini sheria ya mwanadamu (civil law) itiiwe wakati sheria ya Mungu ipo (divine law)? Je muislamu anatakiwa kutii ipi kati ya hizo?

Sasa mimi nashangaa kuona mtu asiyekuwa muisilamu anatowa hoja juu ya kisichomuhusu. Mahakama ya kadhi haimuhitaji asiyekuwa muisilamu kumfafanuliya ya uisilamu maana hayo hayamuhusu kamwe.

Hapa nakubaliana na wewe; binafsi wala tusingelizungumzia suala hiili kama lisingeletwa kwenye Bunge lenye wakristu na waislamu na watu wa dini nyingine (wapo Singasinga na kina Kingunge). Sisi wengine tungepigwa marufuku kabisa kulizungumzia suala hiili kama lingekuwa linazungumziwa na jumuiya za Kiislamu na waislamu wenyewe. Lakini kwa kulileta kwenye Bunge la Muungano ambapo wabunge waliochaguliwa walichaguliwa na watu wa dini na imani mbalimbali kumelifanya jambo hilo kuwa fair game.

Kama hawataki watu wasio Waislamu walitolee hoja, basi waliondoe Bungeni na lifutwe kwenye Ilani ya CCM (Chama chenye Waislamu na Wakristu na watu wenye imani nyingine). Unaonaje?

Vinginevyo, unaweza kupendekeza kuwa Bunge letu likutane kama Bunge Maalumu ambapo ni wabunge waislamu peke yao wajadiliane kuhusu Mahakama ya Kadhi. Na kwa vile Rais ni Muislamu basi itakuwa hata rahisi wao wakajadiliana na Rais Muislamu akatia sahihi.

Iwapo wakristo wanazo hukumu zao wenyewe zinazotakiwa na dini yao basi kwanini nao wanyimwe haki yao hiyo ya kuabudu?

Hawanyimwi, lakini hujasikia Wakatoliki wameenda Bungeni kuomba Bunge litunge sheria ya kutambua mahakama za Kanisa au maamuzi ya mahakama hizo. Wao wanajua hiyo ni sehemu ya dini yao. Kwanini baadhi ya Waislamu hawatambui hilo?

Yote yaamuliwe ila hukumu ya muumba isichezewe. Tusijifanye ni watu wazuri wa kuongea sanaaaa wakati utumbo mtupu.

Uhuru wa kuabudu uheshimiwe popote pale.

Ukweli mtupu, na uhuru huo wa kuabudu uheshimiwa na watu wote ili wengine wasijihisi kuwa wana haki ya kuabudu zaidi kuliko wengine kiasi cha kutaka kuingizwa kwenye Katiba. Tukimkatalia mmoja upendeleo huo, tuwakatalie wote.
 
Asante Field Marshall ES.

Sijuwi iwapo kinachotafutwa ni ruzuku tuu bali mahakama hiyo ikubalike kikatiba.

Ama upande wa ruzuku, nashangaa sana. Maana ukiunda chama cha siasa eti munapewa ruzuku kwa bla bla sembuse swala la kidini ambayo ni ustawi wa jamii wa Taifa letu kulitolea nje.

Nadhani ni roho mbaya za baadhi ya watu na simaanishi wakristo maana wapo wakristo wengi ambao wanaunga mkono mahakama ya kadhi madamu ni itikadi ya hao waisilamu na imani zao.
 
Mkuu Wangu Sanda Matuta,

Heshima mbele kaka, naomba kukuuliza what hii hoja yako has to do na Jamhuri, au taifa yaani sisi taifa at large hii hoja yako inatuhusu vipi?

Sidhani FM,

Nilijaribu kumjibu huyo Bwn hapo juu (soma hizo posts za juu) aliye taka kujua kama nina maelezo ya ziada baada ya post iliyo jibu ya Mkjj.
Nilikuwa nataka kuweka usawa wa hoja zetu kwa kueleweshana misingi ya imani zetu.
Ila Kadhi court inakila kitu na Taifa hili kwani wano dai hiyo mahakama ni watu wa taifa hili na ili utawala wa sheria uheshimiwe basi haki ya kuabudu pia ihishemiwe
 
not to disrespect,unajua ungekua Muislam ungenielewa vizuri lkn nitakupa mfano,
Kwa muumini wa roman catholic akiwa haja batizwa na hayuko kwenye jumuiya ya ushirika anaoishi ni vigumu kuoa au kuzikwa na wanaushirika huo au makanisa yote( nimejua hayo kwani mimi nilikua huko).
Sasa uisilamu pia unataratibu zake ikiwa ni;
1.kumjua mungu na mtume wake
2.kuikubari quraan (inajumuisha sheria na taratibu zake ambayo hukumu zimo ndani yake)
Na mambo mengine yanapata matano kwa ujumla wake ndio mtu anakua muislamu kamili,na huwezi kua muislam mapaka huyatimize na kukiuka moja wapo unatia walakini uislam wako.
Sasa ili imani iwe ya kweli lazima ufate yaliyomo ndani ya quraani na waisilamu wote wanajua ukikubari kuwa muisilamu utakubari na sheria zake,sio kitu tena cha kuchagua kufata au kutofata.

MIMI sikatai kuhusu KADHI ila
Je ktk QURAN kuna sehemu inasema ili hiyo kadhi ikamilike lazima iwepo ktk sheria za nchi?

Ninachoona kutokana na maelezo ya wengi ni kua KADHI itafanya kazi tu kama wahusika watakubaliana kwenda huko na ktk hiyo kinakifanya kua chombo cha kiihari na kukilazimisha kukijenga kwa misingi ya sheria za nchi unaona lkabisa hakuna umuhimu.
Maana kama ni sehemu ya ibada na ni chombo cha utashi kingeanzishwa tu huko misikitini .

Labda ningependa kukuuliza KADHI inatakiwa ianzishwe kimsingi wa sheria za KIFILAUNI ili iwe je?

Hichi chombo kitakachokua kimepitishwa na mafisadi na sheria zake kua pamoja na sheria wanazotumia MAFISADI kitakua vipi SEHEMU ya IBADA?
 
Ila Kadhi court inakila kitu na Taifa hili kwani wano dai hiyo mahakama ni watu wa taifa hili na ili utawala wa sheria uheshimiwe basi haki ya kuabudu pia ihishemiwe

Mkuu Sanda,

Naomba kujua one thing hapa, sheria zetu zinasema nini kuhusu ishu kama hizi za kikundi kimoja katika society kudai kuanzisha mahakama yake? Maana maneno yako ni mazito, lakini tuende chini mpaka kwenye sheria zetu kwanza maana otherwise tutakuwa tunafukuza upepo, au?
 
MIMI sikatai kuhusu KADHI ila
Je ktk QURAN kuna sehemu inasema ili hiyo kadhi ikamilike lazima iwepo ktk sheria za nchi?

Ninachoona kutokana na maelezo ya wengi ni kua KADHI itafanya kazi tu kama wahusika watakubaliana kwenda huko na ktk hiyo kinakifanya kua chombo cha kiihari na kukilazimisha kukijenga kwa misingi ya sheria za nchi unaona lkabisa hakuna umuhimu.
Maana kama ni sehemu ya ibada na ni chombo cha utashi kingeanzishwa tu huko misikitini .

Labda ningependa kukuuliza KADHI inatakiwa ianzishwe kimsingi wa sheria za KIFILAUNI ili iwe je?

Hichi chombo kitakachokua kimepitishwa na mafisadi na sheria zake kua pamoja na sheria wanazotumia MAFISADI kitakua vipi SEHEMU ya IBADA?

Nazani sijaelewa swali/maswali yako Mkamap,
 
Mkuu Sanda,

Naomba kujua one thing hapa, sheria zetu zinasema nini kuhusu ishu kama hizi za kikundi kimoja katika society kudai kuanzisha mahakama yake? Maana maneno yako ni mazito, lakini tuende chini mpaka kwenye sheria zetu kwanza maana otherwise tutakuwa tunafukuza upepo, au?

FM,

Sitaki kuingia sana kwenye sheria (kwani i know not),ila kwa ufasa katiba yetu inatoa haki kwa vikundi vya dini kutekeleza ibada zao ipasavyo (kama ujuavyo hata Roman Catholic wanazo pia mahakama zao ingawa hazitambuliwi kikatiba kwani haziko registared lkn ndivyo ibada zao au imani yao iavyo hitaji,kwani kwenye waumini mambo mengi yanatokea vifo,ndoa,utengano(devorce),maugomvi na mambo mengi kadha wakadha,inafikia mpaka vedict inatoka Vatican.)
Hivyo hivyo kwa Waislam mambo kama hayo yanatokea wanapaswa kuwa na kitu kama hicho,sasa tatizo linakuja hapa;Bakwata kama chombo SUPPOSELY cha waislamu kilichowekwa na SERIKALI kina kitengo kama hicho cha ku-sattle disputies LAKINI waislam walio wengi hawakiaami chombo hichi(BAKWATA) kwanza walio viongozi sio wasomi wazuri wa qurani na sheria zake wengine WAGANGA (kitu kibaya kabisa kwenye Uislam(shiriki),wengine ndio hivyo hivyo tena sio wasomi kiasi cha kuutukanisha uislam kama dini isiyo ya wasomi .
Kupukana na yote haya wame opt kuwa na KADHI atakeye kua na nguvu kuliko MUFTI wa Bakwata,sasa hili ni tatizo kwa serikalli kwani mamraka atakayo kuwa nayo Kadhi yata hatarisha interests za serikali ambayo inaona bora kuwapo kwa BAKWATA na si KADHI.
Na kwakuwa Bakwata inapata hizo ruzuku kotoka huko serikalini then itahusu fungu hilo liende kwa kadhi alfu yeye a alocate kwa Bakwata hilo ni tishio pia kwani wanajua kwamba wapo waislam wachache in favour of Bakwata.
Na ili kutambulika kisheria na kua mamraka huru lazima ipate barraka za serikali na hicho ndio kigugumizi chote kipo hapo
 
OK
ngoja nikuulize swali moja moja

1.Je ktk QURAN imeandikwa ili IBADA ya KADHI ikamilike lazima iwe ndani ya KATIBA YA SERIKALI ya nchi husika??

jibu lipo kwenye post yangu ya mwisho kabla ya hii,read btn lines ingawa sio mjuzi sana wa qurani.
 
Asante Field Marshall ES.

Sijuwi iwapo kinachotafutwa ni ruzuku tuu bali mahakama hiyo ikubalike kikatiba.

Kama ni sehemu ya Ibada na dini tayari inakubalika. Unataka kusema ili Shahda isemwe na Waislamu lazima Katiba itambue uwepo wa hiyo Shahda? Mbona mahakama za Kikatoliki zipo na zinatambulika Kikatiba lakini hazijaingizwa kwenye Katiba, kwanini hii ya Kiislamu lazima iingizwe kwenye Katiba?
 
Heshima kwako mkuu MKJJ,

Ni kweli si lazima kwa serikali kutambua shahada.
Ila nadhani kwenye post yangu hapo juu nimetoa mwanga kidigo,
HILI NI TATIZO DOGO NDANI YA TATIZO KUBWA!
 
jibu lipo kwenye post yangu ya mwisho kabla ya hii,read btn lines ingawa sio mjuzi sana wa qurani.

Unazidi kunitisha zaidi unaposema KADHI kuwepo kutahatarisha Interest za serikali sijui unamaa ipi? Ni je KADHI ita claim yenyewe ndio iendeshe serikali au una maana gani? Hasa unaposema Kahdi yenyewe itajishugurisha na milathi ,ndoa za waislamu tu sasa ningependa unifafanulie zaidi JE interest ya serikali ya TZ ktk Mirathi na ndoa za wananchi wake inafaidika vipi? na nivipi sereikali itahatarishwa interest zake kwa ndoa na mirathi ya waislamu.?

Pili swali hujalijibu sijaona sehemu yoyote ile uliyojibu ya kua.

KADHI ili iwe KADHI ktk QURAN imeandikwa lazima iwe ndani ya KATIBA ya nchi??

Na je inakua je? KADHI kua IBADA kama kila Nchi inaendeshwa kivyake vyake .
Mimi kwa uelewa wangu mdogo IBADA ktk DINI yoyote inaendeshwa sawasawa kote duniani yani matendo ya ibada yanakua na mtiririko uleule.SASA KADHI inakua je ni sehemu ya IBADA kama kila kundi linakua na IBADA yenye kutofautiana MTIRIRIKO? mfano kama kadhi zingine zinahukumu kunyonga,kupigwa mijeledi ,kupondwa mawe WAKATI kadhi zingine zitajishughurisha na milathi na ndoa tu.
 
FM,

Sitaki kuingia sana kwenye sheria (kwani i know not),ila kwa ufasa katiba yetu inatoa haki kwa vikundi vya dini kutekeleza ibada zao ipasavyo (kama ujuavyo hata Roman Catholic wanazo pia mahakama zao ingawa hazitambuliwi kikatiba kwani haziko registared lkn ndivyo ibada zao au imani yao iavyo hitaji,kwani kwenye waumini mambo mengi yanatokea vifo,ndoa,utengano(devorce),maugomvi na mambo mengi kadha wakadha,inafikia mpaka vedict inatoka Vatican.)
Hivyo hivyo kwa Waislam mambo kama hayo yanatokea wanapaswa kuwa na kitu kama hicho,sasa tatizo linakuja hapa;Bakwata kama chombo SUPPOSELY cha waislamu kilichowekwa na SERIKALI kina kitengo kama hicho cha ku-sattle disputies LAKINI waislam walio wengi hawakiaami chombo hichi(BAKWATA) kwanza walio viongozi sio wasomi wazuri wa qurani na sheria zake wengine WAGANGA (kitu kibaya kabisa kwenye Uislam(shiriki),wengine ndio hivyo hivyo tena sio wasomi kiasi cha kuutukanisha uislam kama dini isiyo ya wasomi .
Kupukana na yote haya wame opt kuwa na KADHI atakeye kua na nguvu kuliko MUFTI wa Bakwata,sasa hili ni tatizo kwa serikalli kwani mamraka atakayo kuwa nayo Kadhi yata hatarisha interests za serikali ambayo inaona bora kuwapo kwa BAKWATA na si KADHI.
Na kwakuwa Bakwata inapata hizo ruzuku kotoka huko serikalini then itahusu fungu hilo liende kwa kadhi alfu yeye a alocate kwa Bakwata hilo ni tishio pia kwani wanajua kwamba wapo waislam wachache in favour of Bakwata.
Na ili kutambulika kisheria na kua mamraka huru lazima ipate barraka za serikali na hicho ndio kigugumizi chote kipo hapo

Sanda, kitu ambacho watu wengi hawakijui ni kuwa Kadhi ni Jaji tu na Hakimu si mtawala. Na katika sheria zetu tumedefine Kadhi kuwa ni kiongozi wa dini wa Kiislamu i.e Shehe. Vivyo hivyo sheria hiyo Angalia sheria ya ndoa ya 1971 inamtambua Kadhi kuwa ni :

''kadhi'' means a Muslim priest or preacher or a leader of a Muslim
community who has been licensed under this Act to celeberate
marriages in Islamic form;

Na pia hilo linarudiwa sheria hiyo inapomtafsidi Mtumishi wa Dini kuwa ni:

'minister of religion'' means any minister, priest or other person
who is empowered to celebrate marriages by the laws of any
religion according to the rites of which marriages may be celebrated
under the provisions of this Act, and includes a kadhi;

kwa maana hiyo basi kisheria tayari Makadhi wapo vinginevyo wanaofungisha ndoa za Kiislamu ni kina nani? Kwa hiyo naamini hoja ya mahakama sasa ni kujaribu aidha kuunganisha au kuongeza majukumu ya Kadhi.

Sasa utaona kitu ambacho watu wanataka siyo Kadhi (kwani tayari wapo na wanatambulika kisheria) lakini wanachotaka ni kuwa Kadhi awe Hakimu pia.
 
Unazidi kunitisha zaidi unaposema KADHI kuwepo kutahatarisha Interest za serikali sijui unamaa ipi? Ni je KADHI ita claim yenyewe ndio iendeshe serikali au una maana gani?

Pili swali hujalijibu sijaona sehemu yoyote ile uliyojibu ya kua.

KADHI ili iwe KADHI ktk QURAN imeandikwa lazima iwe ndani ya KATIBA ya nchi??

Na je inakua je? KADHI kua IBADA kama kila Nchi inaendeshwa kivyake vyake .
Mimi kwa uelewa wangu mdogo IBADA ktk DINI yoyote inaendeshwa sawasawa kote duniani yani matendo ya ibada yanakua na mtiririko uleule.SASA KADHI inakua je ni sehemu ya IBADA kama kila kundi linakua na IBADA yenye kutofautiana MTIRIRIKO? mfano kama kadhi zingine zinahukumu kunyonga,kupigwa mijeledi ,kupondwa mawe WAKATI kadhi zingine zitajishughurisha na milathi na ndoa tu.

Mkuu,

Naomba tuelewane,interest za serikali ziko nyingi sio mfano,taking over the rule of law hapana.
Bakwata na serikali wana mahusiano ya karibu sana,mahusiano ambayo yana watia shaka waisilamu walio wengi ikiwemo na mimi,sasa kama kuta kua na siri kati ya Bakwata na Serikali sidhani kama serikali ita kuwa willing kushare hizo siri na chombo ambacho yenyewe haija husika hata kidogo katika kuiunda (yaani kama hiyo bill itapita basi waislamu wataunda chombo chao wao wenyewe na chombo hicho kitakua na mamaraka ya juu zaidi kuliko Bakwata na serikali itabidi itake isitake ishirikiane nacho hicho chombo) nakama hiyo itakuwa basi chombo hicho ndicho kitahusika na walfare ya waisilamu na uisilamu jambo lolote ambalo litaonyesha kuwakandamiza(au interests zao)
waisilamu au uisilamu litapingwa.

Pili Kadhi court haikuandikwa kwenye katiba ,ila serikali kupitia Bunge inatakiwa kuipitisha nakuikubari kama chombo cha Kiisilamu,na hiyo ndiyo nilisema ndio TATIZO kwani baada ya hapo BAKWATA will be out of the picture.
Serikali haitaki kuipoteza bakwata kwa sababu kadha wa kadha ikiwa kubwa ni chombo kilicho undwa na J.K.Nyerere baada ya kuvunja EAMWS kwa sababu zake za KIHISTORIA.

Tatu,ili ibada itimie kwa muisilamu mambo kama ndoa,mirathi,taraka na mfumo mzima wa maisha ya musilamu baada ya swala na dhaka nilazima yafatwe kama ilivyo takiwa ndani ya qurani na wanotaka kufahamu kwani si wote wenye kujua wanenda kwa KADHI ambaye ni msomi wa hari ya juu katika dini kwa maelezo ya ufasaha.

Mwisho,hizo habari za kunyongwa,mijeredi na kupigwa mawe ni Utawara wa SHARIA ambacho ni kitu tofauti na mahakama ya KADHI.
 
Back
Top Bottom