Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Wewe sasa mchokozi!
Hizi mahakama zinatambuliwa na sheria za nchini mwetu? Ziko katika katiba ya nchi? Au ni kwa ajili ya wakatoliki na asiyetaka kuzitumia (hata kama ni mkatoliki) halazimishwi?

Mimi kitu kikuu ambacho sikielewi na ningomba kuelimishwa.
tuseme mahakama ya kadhi ipo na ikahukumu mtu na mtu akaikataa hukumu je kadhi itafanya nini?

ama inamhukumu mtu yeye anageuka anasema mimi sio muislamu itafanya nini zaidi.?
 
Mzee Mwanakijiji Tanzania kuna Mashekhe wa aina mbali mbali na wengi wao wamesoma tu Qur’an lakini kwa bahati mbaya hawakusoma Biblia au Turat(Torah).
1.Ndoa kwa mfano imelezwa vizuri ni nani mtu aoe na ni wake wangapi. Vile vile talaka pia zimelezwa katika Qur’an na jinsi zinzvyotolewa.
2. Sasa Muislamu akioa mke wake wa Kikristo/Kiyahud katika ofisi ya Kiserikali inayohusika na ndoa hiyo Mahakama ya kadhi haitaitambua ndoa hiyo?
3. Kama Muslamu ana Life Insuarance yake na akafariki hiyo Mahakama ya kadhi itawarithisha vipi mke na wanawe?
4.Sheria za Life Insuarance zinataka mke apewe urithi na watoto. Lakini pengine aliyefariki ameandika statement maalum kuhusu urithi wake basi hiyo statement itafuatwa na Kampuni ya Life Insuarance kwa vile huo ndio WASIA WA MWENYEWE.
5. Katika Qur’an amendikwa kwamba mtu ukiona kwamba pengine siku zako za kufa haziko mbali umuachie mkeo posho la mwaka mmoja. Wangapi wanafanya hivi?

6.Watanzania wangapi ambao wanaifuata Qur’an kama inavyotakiwa?
7. Kuna vitu vingi ambavyo Mwenyenzi Mungu amevirahisha kwa waja wake. Kwa mfano mtu mwezi wa Rammadhani akiwa safarini anarusiwa kula na akirudi kwakwe azilipe zile siku ambazo hakufunga. Pia swala ya aduhuri na alaasiri anaweza kuzijumlisha akiwa safarini , Ishaa na Maghribi pia.
8.Kama mwenyewe Mnyenzi Mungu amarahisisha vitu kwa waja wake kwa nini sisi Watanzania tunataka kuvifanya vigumu?
9.Watanzania wangapi wanafuata Sunna za Mtume?,Waulize hao Mashekhe wa Tanzania Mtume Muhammad (S.A.W) alikuwa akiamka usiku na kuswali rakaa 11 za Swalat TAHJUUD na kumalizia na swala ya WITRI kabla ya swala ya Alfajiri(Asubuhi), ni wangapi kati ya hao Mashekhe wanaofanya hivyo?

TUSIVURUGE NJI KWA SABABU YA KUUNDA MAHAKA YA KWANZA!

“OBEY THE PROPPHET (Muhammad (S.A.W)) AND OBEY THOSE IN POWER”.hii ni aya mojawapo katika Qur’an. “Those in Power” hapa ni serkali na mahakama yake.

Huyu mwoga.

Ungejaribu hata kunyamaza kusoma michanga ya wengine,Hoja zako hazina base yoyote.
 
siyo uchokozi nina maana mbili:

a. Kwanza mahakama za kidini zinawezekana tanzania kwani tayari zipo (kwa wakatoliki na hata waanglikana wanazo)

b. Pili hazihitaji baraka ya serikali kwani haziko katika mfumo wa utoaji haki wa serikali. NI sehemu ya dini.

sasa hapa uchokozi ni upi?

Uchokozi ni kuwa unatupeleka kwenye suala la ubalozi. Wengine watasoma tu kuwa mahakama zipo na kuunganisha masuala ya Vatican na kupandisha munkhari!

Wenzetu wanachotaka ni utambuzi wa kisheria ili wapate mgao! Na bado hatujakubaliana kuwa hao waislamu tunaowazungumzia ni wepi maana hata waismailia wanajiita waislamu!
 
Zitto leo bwana alikuwa anatafuta umaarufu tu wa kwamba na yeye alichangia. Point yake pekee ilikuwa ni kidokezo cha utafiti wa REDET kuwa katika kila watanzania 10 ni wawili tu wanaoaminiana. Basi. After that akaanza kutoa hotuba badala ya hoja kama vile kuhimiza umoja, kwamba watu waache kugwanyika kwa misingi ya dini, etc) ili kujaza time slot.

Yule naye muoga mwingine.
Simamia kwenye ukweli hata kama utawaumiza baadhi ya marafiki zako.Watu kama yy wako wengingi,kwa maneno mengine ufunguzi wa HUTUBA yake umesema kila kitu HATUAAMINIANI kuvumuliana kumepungua.
 
Uchokozi ni kuwa unatupeleka kwenye suala la ubalozi. Wengine watasoma tu kuwa mahakama zipo na kuunganisha masuala ya Vatican na kupandisha munkhari!

sasa wakileta hoja ya Ubalozi mbona tunazo balozi za jamhuri za Kiislamu kama Morocco, Libya na Iran? Na kwa upande wa Iran kiongozi wake ni Ayatollah?
 
Mkuu! Mkosoea basi kwa hoja na kutueleza maimuna wengine kwa nini hoja zake ni baseless!

Lazima niwe mkweli hapa Fundi,
Mimi ni Muisilamu na huyu bwana anajina lenye kufanana na imani yangu,baada ya kutetea maslai ya imani yetu yy ana onyesha degree ya uwoga,kwa kunukuu aya bila ya maelezo ya kina na sababu za kushushwa kwa hizo aya.Anaweza akawa miongoni ya wale waisilamu wasio taka mahakama hii that is...fine,lkn angeweza tu kunyamaza na kusoma tu (mimi mfano nimekua hapa toka hii thread ilipo kuwa posted na sija changia kitu kwani sina elimu ya dini na si juu how does that KADHI COURT works,ila kwasababu tu inaweza kuwanufahisha watu wa imani yangu (kwa jinsi nilivyo oana wabunge wakitetea na michango ya wana Jf) then niko nao).

Nadhani utakua umenielewa,alitakiwa mtu amwambia aache
 
Hii idea simply ni unfeasable!! Sasa mahakama ya kadhi ikitoa hukumu na mtu akaikataa itakuaje? kwa hiyo waweke na polisi wao?
Au sheria ya dini ikiwa inapingana na sheria ya nchi itakuaje?
Mnakumbuku ilitokea Nigeria mwanamke alihukumiwa kupigwa mawe na mahakama ya kadhi serikali ikabidi iingilie kati.

Pia sheria ya kidini inatambuliwa na mahakama zetu kwenye mambo kadhaa yakiwemo ya urithi i.e Muislamu akifariki wanatumia sheria ya kiislamu kugawa urithi kama hakuacha Last Will and Testament. Sasa kwanini hiyo haitoshi?

Pia kama itaruhusiwa mahakama ya kiislamu kutakuwa na slippery slope! Kwanini kusiwe na mahakama za kila aina ya makundi? Wakristo, wapagani, hindus na hata makundi yasiyo ya kidini.

Vilevile kusema kuna mahakama za Kikristo ni kupotosha watu, kuwa na systems za kuresolve disputes baina na watu sio sawa na kuwa na mahakama.
 
Huyu mwoga.

Ungejaribu hata kunyamaza kusoma michanga ya wengine,Hoja zako hazina base yoyote.

Ana point ya maana, ukweli ni kwamba intrepretation ya sheria za kiislamu una utata sehemu nyingi.
Kuna watu wanaamini kabisa kua kujilipua ndio njia ya kufika mbinguni! Na kwa sababu ya nature ya religion hauwezi ukawaeleza wakuelewe "faith" haifuati reason wala logic, wanaamini kwa sababu wanaamini. Sasa hili litakua handled vipi?
 
Mahakama zote uzushi mtupu, achilia mbali ya kadhi.

Sasa kwenye mizani bora kidogo hizi za kiserikali zina rationale ya kwamba ni bora half baked justice kuliko a wild wild west anarchy.

Kukubali hiyo ya Kadhi ni kurudi nyuma kwenye mambo ya medieval courts.
 
Originally Posted by Mzee Mwanakijiji
mbona Kanisa Katoliki lina Mahakama zake na hakuna anayegomba tena wao hadi kukata rufaa ni Vatikani kwenyewe?

Wewe sasa mchokozi!
Hizi mahakama zinatambuliwa na sheria za nchini mwetu? Ziko katika katiba ya nchi? Au ni kwa ajili ya wakatoliki na asiyetaka kuzitumia (hata kama ni mkatoliki) halazimishwi?

Mkuu jaribu kuelewa hoja kabla ya kukurupuka, alichosema mkuu pale juu ni kwamba Katoliki lina mahakama zake, sio za dunia au za bongo,

Mahakama za Vatican, kuwa functiionable sio lazima zitambuliwe na sisi Tanzania, na hata hizo za Tanzani zikikubaliwa sio lazima zitambuliwe na Vatican, lakini haina maana kuwa hazitatambuliwa kama mahakama popote zilipo, kulingana na sheria za lile taifa!

Ahsante Mkuu!
 
Hivi hao watu kweli wasingeweza kuanzisha mahakama yao huko Bakwata, na baadaye kuifahamisha serikali kuwa wameanzisha, kani ilikuwa ni lazima hili suala liende bungeni?

Mimi ninaamini hili halikupaswa kuepelekwa bungeni, ilikuwa ni hawa watu kuamua wenyewe huko kwenye dini yao, kwani wangekuwa wanavunja sheria ya Jamhuri? Kuipeleka hii ishu bungeni yalikuwa ni makosa makubwa politically,

Wabunge walipaswa kuikata kabisa hii hoja, na kuwaomba hao ndugu wakaamue wenyewe mambo yao ya ndani ya dini huko kwao, kwani Jamatini huwa hakuna mahakama? Lini umewasikia Wadosi wakipelekana Mahakama ya Kisutu? Kwani wao hawana matatizo huko kwenye society yao?

I mean mijadala mingine ni kushusha hadhi ya taifa!
 
Mkuu jaribu kuelewa hoja kabla ya kukurupuka, alichosema mkuu pale juu ni kwamba Katoliki lina mahakama zake, sio za dunia au za bongo,

Mahakama za Vatican, kuwa functiionable sio lazima zitambuliwe na sisi Tanzania, na hata hizo za Tanzani zikikubaliwa sio lazima zitambuliwe na Vatican, lakini haina maana kuwa hazitatambuliwa kama mahakama popote zilipo, kulingana na sheria za lile taifa!

Ahsante Mkuu!

Mwanakijiji amemisslead kama ndio alichokua anamaanisha, kasema Kanisa Katoliki lina mahakama zake, unachosema wewe ni Vatican ina mahakama zake, Vatican ni nchi kama Tanzania, sasa kivipi nchi isiwe na mahakama?
 
Hapana wewe hapa ndio unataka kutu-misslead, katika uliwengu wa siasa inafahamika kuwa Vatican ni makao makuu ya kanisa la Katolic, na unaweza ukatumia any of the two names kuwakilisha hoja na ikaeleweka kwa wenye elimu, labda tu kwa wasio na elimu ambao sidhani kuwa wapo hapa JF!

Mkuu jaribu kutafuta hoja inayoweza kulisaidia taifa letu badala ya hizi nyepesi nyepesi ambazo hazina elimu yoyote kwa wananchi na taifa kwa ujumla. Nilifkiiri umeacha ssa kumbe bado tu? Karibu tena mkuu!
 
Kanisa katoliki lina Mahakama hiyo ni kweli.

Mfano padre akiamua kuoa Hukumu yake inatoka Vatican atengwe na kanisa,ama aitwe vatican akapigwe sara ama atubu.

Kuna askofu mmoja zambia aliamua kuoa.Vatican ilimuita akakaa vatican na akatubu lakini baadae alitimukia Marekani tena akaenda kuungana na mke wake ndipo vatican ilipotoa hukumu ya kutengwa na kanisa.

Kuanzia Askofu wote duniani wanateuliwa wote kutoka vatican.
hivyo kanisa katoliki lina mahakama wana ndoa wakikosana hua wanakimbilia kwa father ama wazee wakanisa wanawahukumu kwa sheria za mahakama hiyo mfano wa hukumu KANISA halitambui talaka ya aina yoyote ile isipokua kifo.
 
Originally Posted by Dr.Khamis
Mzee Mwanakijiji Tanzania kuna Mashekhe wa aina mbali mbali na wengi wao wamesoma tu Qur’an lakini kwa bahati mbaya hawakusoma Biblia au Turat(Torah).
1.Ndoa kwa mfano imelezwa vizuri ni nani mtu aoe na ni wake wangapi. Vile vile talaka pia zimelezwa katika Qur’an na jinsi zinzvyotolewa.
Kuelezwa vizuri katika Quran si hoja kuwa kusikuwepo mahakama ya kadhi,ikumbukwe hii field pana kama zilivyo zingine katika Quran na hadith,kuna ambao wana PhD katika hiyo field.Kadhi ni mtu mwenye hiyo taaluma na anahukumu kwa mujibu wa mafundisho na mazingira ya tukio husika.

2. Sasa Muislamu akioa mke wake wa Kikristo/Kiyahud katika ofisi ya Kiserikali inayohusika na ndoa hiyo Mahakama ya kadhi haitaitambua ndoa hiyo
?

Bro ...hapo naomba ufikirie vema uone pumba ipo wapi.

3. Kama Muslamu ana Life Insuarance yake na akafariki hiyo Mahakama ya kadhi itawarithisha vipi mke na wanawe?
4.Sheria za Life Insuarance zinataka mke apewe urithi na watoto. Lakini pengine aliyefariki ameandika statement maalum kuhusu urithi wake basi hiyo statement itafuatwa na Kampuni ya Life Insuarance kwa vile huo ndio WASIA WA MWENYEWE.
Insurance kama ni sehemu halali ya marehemu itagaiwa kama mali zingine kwa mujibu wa sheria husika.........Bro,katika vitu vya mwanzo vinavyozingatiwa katika mirathi kwa mujibu wa uislam ni WASIA WA MAREHEMU......hapa unahitaji kwenda shule juu ya hilo.

5. Katika Qur’an amendikwa kwamba mtu ukiona kwamba pengine siku zako za kufa haziko mbali umuachie mkeo posho la mwaka mmoja. Wangapi wanafanya hivi?

Bro,hapo naomba ushahidi wa hiyo aya katika Quran...pia kama kuna maelezo yoyote ikiwa huyo marehemu hakuwa na hilo posho mwaka inakuwaje?

6.Watanzania wangapi ambao wanaifuata Qur’an kama inavyotakiwa?

Dah...,Bro,hii ni challenge kwangu...nashukuru sana kunikumbusha,ALLAH atujalie kuifanyia kazi.

7. Kuna vitu vingi ambavyo Mwenyenzi Mungu amevirahisha kwa waja wake. Kwa mfano mtu mwezi wa Rammadhani akiwa safarini anarusiwa kula na akirudi kwakwe azilipe zile siku ambazo hakufunga. Pia swala ya aduhuri na alaasiri anaweza kuzijumlisha akiwa safarini , Ishaa na Maghribi pia
.
Hapo umepatia....hizo aya zapatikana katika Suratul Baqara,ingawa kwa mwenye kutaka kutekeleza hiyo rukhsa akiwa safarini(akiwa mgonjwa kwa case ya kufunga Ramadhani) anahitaji maelezo ya namna ya kufanya....yaani ajue anajumlishaje hizo alasiri na adhuhur(kwa mfano)

8.Kama mwenyewe Mnyenzi Mungu amarahisisha vitu kwa waja wake kwa nini sisi Watanzania tunataka kuvifanya vigumu?
Hapa ndugu taratibu kidogo.....kuna speficity katika utekelezaji wa ibada,sio mtindo wa logic....,mwanamke akiwa katika hedhi ni rukhsa kutoswali na hatakiwi kulipia ile swala ilyompita,lakini hata mtu uwe mgonjwa vipi maadam unafahamu(uko conscious) watakiwa uswali...sasa ukianza kuleta logic...utauliza swali..kwa nini mwenye hedhi ambaye ni mzima kiafya asiswali na huyu mgonjwa alazimike kuswali....,kurahisishiwa katika moja haina maana ni the same katika lingine.

9.Watanzania wangapi wanafuata Sunna za Mtume?,Waulize hao Mashekhe wa Tanzania Mtume Muhammad (S.A.W) alikuwa akiamka usiku na kuswali rakaa 11 za Swalat TAHJUUD na kumalizia na swala ya WITRI kabla ya swala ya Alfajiri(Asubuhi), ni wangapi kati ya hao Mashekhe wanaofanya hivyo?
Hii ni challenge nyingine......nimeipokea,shukran tena.......ALLAH atuongoze katika hili

TUSIVURUGE NJI KWA SABABU YA KUUNDA MAHAKA YA KWANZA!
Sifikirii kwamba litachukua sura hii......

“OBEY THE PROPPHET (Muhammad (S.A.W)) AND OBEY THOSE IN POWER”.hii ni aya mojawapo katika Qur’an. “Those in Power” hapa ni serkali na mahakama yake.
Yap...hii ni quotation sahihi,kuwa na hiyo mahakama hakuendi kinyume na hii quotation kabisa...hii inatufundisha kuwa tunapokuwa katika chini ya mamlaka fulani..hata kama si ya kiislam tunatakiwa tutii viongozi wa pale so long kuwa hawatutoi katika uislaam ama kutuzuia na ibada....na ndio maana hata hizi habari za maandamano and the like kama kuchochea vurugu n.k ni vitu ambavyo kwa uelewa wangu wa uislam ni vya kupingwa...napongeza hatua zinazochukuliwa katika kuendea hili suala la kadhi kuwa si kwa kutumia fujo(kwa mujibu wa thread hii...maana siko Tz sijui inakuaje)
 
Dr Khamis
Ni kweli MUNGU amerahisisha mambo ila binadamu tunajaribu kuyafanya magumu,

Haya ni maoni yangu si kila jambo liliondikwa ktk vitabu vitakatifu lazima litekelezeke lilivyo ,linategemeana kwanza na mazingira na wakati.

Naomba msamaha kwayeyote nitayemuudhi kwa mfano huu na swali hili.

Je Waislamu UGAIBUNI ina maana hawali nyama ya aina yoyote ?? maana kama ni kuku ,ng'ombe zinachinjwa kwa machine ,tena mashine hiyohiyo inamkatakata nguruwe pia.Hakuna cha uelekeo wala nini kuku anatupwa mashine inafanya kazi.Mmeshasikia wanagoma kula nyama??

Vitu vyote vinategemea mazingira na wakati na kwa mazingira yetu TZ hiyo kadhi inatakiwa iwe taasisi ndani ya BAKWATA.
 
Hapana wewe hapa ndio unataka kutu-misslead, katika uliwengu wa siasa inafahamika kuwa Vatican ni makao makuu ya kanisa la Katolic, na unaweza ukatumia any of the two names kuwakilisha hoja na ikaeleweka kwa wenye elimu, labda tu kwa wasio na elimu ambao sidhani kuwa wapo hapa JF!

Mkuu jaribu kutafuta hoja inayoweza kulisaidia taifa letu badala ya hizi nyepesi nyepesi ambazo hazina elimu yoyote kwa wananchi na taifa kwa ujumla. Nilifkiiri umeacha ssa kumbe bado tu? Karibu tena mkuu!

Wewe naona umeshindwa kujitetea! Sasa unarukia hoja za watu tu. Zijibu basi hoja zangu kama kweli ni "nyepesi, nyepesi".

Ndio Vatican na Catholic Church viko joined at the hip, lakini kusema vatican ina mahakama ni tofauti na kusema Kanisa lina mahakama. Marekani ina mahakama, je sheria za mahakama hiyo zinaweza kukugusa mtanzania ambaye upo nchini mwako? Na zaidi ya hilo tunatoa kodi yetu kuendesha hiyo mahakama? Hapana.

Basicly hiyo point ya vatican kuwa na mahakama ni irrelevant kwenye sababu za kuanzisha mahakama ya kadhi.
 
Kanisa katoliki lina Mahakama hiyo ni kweli.

Mfano padre akiamua kuoa Hukumu yake inatoka Vatican atengwe na kanisa,ama aitwe vatican akapigwe sara ama atubu.

Kuna askofu mmoja zambia aliamua kuoa.Vatican ilimuita akakaa vatican na akatubu lakini baadae alitimukia Marekani tena akaenda kuungana na mke wake ndipo vatican ilipotoa hukumu ya kutengwa na kanisa.

Kuanzia Askofu wote duniani wanateuliwa wote kutoka vatican.
hivyo kanisa katoliki lina mahakama wana ndoa wakikosana hua wanakimbilia kwa father ama wazee wakanisa wanawahukumu kwa sheria za mahakama hiyo mfano wa hukumu KANISA halitambui talaka ya aina yoyote ile isipokua kifo.

Organization yoyote inakua na rules and regulations na sometimes kuna structure za kutatua matatizo yanayotokea.
Lakini kuziita hizi ni mahakama tunakua "tunamisslead" kwa sababu hazina nguvu nje ya organization hiyo.
Kama huo mfano wa wanandoa, ni kwa vile tu imani yao inawatuma ndo wanaenda huko, wakiamua wanaweza kuifuta ndoa yao kisheria na hakuna kitu kanisa linaweza kufanya zaidi ya kutoitambua talaka.
 
Mkuu jaribu kuelewa hoja kabla ya kukurupuka, alichosema mkuu pale juu ni kwamba Katoliki lina mahakama zake, sio za dunia au za bongo,

Mahakama za Vatican, kuwa functiionable sio lazima zitambuliwe na sisi Tanzania, na hata hizo za Tanzani zikikubaliwa sio lazima zitambuliwe na Vatican, lakini haina maana kuwa hazitatambuliwa kama mahakama popote zilipo, kulingana na sheria za lile taifa!

Ahsante Mkuu!

Tatizo ni uelewa. Aliyeleta hoja tumemalizana sasa na wewe unataka kuingilia! Ulichokizungumza na alichozungumza huyo unayetaka kumfafanulia ni vitu viwili tofauti. Ufafanuzi wako unapwaya! Nani aliyesema ni lazima Mahakama za Tanzania zitambuliwe na Vatican ili ziwe functional ( sio functionable!). Halafu unatoka kwenye specifics (Tanzania na Vatican) kwenda kwenye general (popote zilipo .......sheria za lile taifa!) bila kuunganisha unachotaka kusema. Mimi sijakuelewa. Nilidhani mahakama ili iwe functional ni lazima itambulike na sheria za nchi ilipo. Ama sivyo ni makubaliano tu ya jamii yasio na uzito wowote kisheria!
 
Back
Top Bottom