Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Acheni ubinafsi huo jamani, serikari inawajibu wa kuhudumia makundi mbalimbali ya kijamii ya kitanzania. Halafu mbona waislamu kwa miaka yote hapa nchini wanafanya kazi Ijumaa wakati ni siku yao ya kuabudu? Msiogope kukatwa mikono na kupigwa mawe mahakama ya kadhi ni maalumu kwa waislamu tuu. Mbona kenya ipo na hatujasikia malalamiko kama mtoayo nyie? Zaidi ya hoapo ilikuwepo tangu enzi za mkoloni wa kiingereza ila ilitilewa kiujanja baada ya uhuru mwaka 1963.

Wakristu wanapumzika jumapili si kwa vile ni siku yao ya kuabudu bali imani yao inasema kuwa wafanye kazi siku sita na ya saba waitenge kwa KUPUMZIKA na kumuabudu mungu. Kama vile ilivyo Sabbath kwa wayahudi ambapo hata kupika siku hiyo hakuruhusiwi. Sidhani kama waislamu wanakatazwa kufanya kazi siku ambayo wanaabudu! Vile vile sidhani kuwa kuna sheria inayomkataza mtu kufanya kazi jumapili na kupumzika ijumaa. Ni utaratibu tu ambao shirika au mtu aliyejiajiri anaweza kuufuata.

Kabla ya kutumia suala la Kenya kama mfano, ni lazima tuangalie mazingira yaliyopelekea mahakama hizo kuanzishwa na kama hayo mazingira na sababu yapo kwetu hivi sasa.
 
Kaka unajua zaidi ya hili. Hizi ni balozi za mataifa (sovereign states) na sio balozi za asasi za kiimani kama ilivyo VATICAN. Ndio maana hata katika UN Vatican ina status tofauti na Tanzania ama IRAN......

Sina tatizo na kuwa na ubalozi wa VATICAN popote pale lakini si busara kwa mtu kama wewe kuingia kwenye hii tone ya ushindani iliyojaa ubabaishaji badala ya kuendelea kuwa objective kama ulivyoanza hapo mwanzoni....hizi arguments za kiushindani/kipinzani zina wenyewe....na wewe si mmojawapo....waachie kina mtikila, mrema na bassalehh na wa aina yao humu barazani...

Tanzanianjema

Vatican City [ˈvætɪkən ˈsɪti] (help·info), officially State of the Vatican City (Italian: Stato della Città del Vaticano), is a landlocked sovereign city-state whose territory consists of a walled enclave within the city of Rome. At approximately 44 hectares (110 acres), and with a population of around 800, it is the smallest independent state in the world by both population and area.[2][3][4]
http://en.wikipedia.org/wiki/Vatican_City

Vatican ni nchi kama walivyoeleza hapo juu pamoja na kuwa makazi ya kiongozi wa asasi ya kidini. Kwa hali hiyo ni theocracy kama ilivyo Iran.
 
Wa-Katholic wote makao makuu ya uumini wao upo Vatican, ambako kuna mahakama inayoweza kutoa hukumu kwa a Katholic kiongozi na ile hukumu ikatambuliwa na serikali yetu.

Bado unachanganya entity ya Vatican (kwa ukamilifu City of Vatican) na Holy See. Nchi ya Vatican ina judicial system yake kama nchi nyingine yeyote. Ni kama vile mcheza mpira anavyomtambua kiongozi wa Fifa kama kiongozi wake katika masuala ya mpira. Uamuzi wa Fifa kuhusu kiongozi wa TFF utatambuliwa na serikali lakini hii haina maana kuwa miongozi yake ni sheria nchini kwetu!

Kwa maelezo zaidi, soma hapa:http://en.wikipedia.org/wiki/Vatican_City
 
Samahani mwenzio siamini katika WIKIPEDIA ambayo kila mtu hata Mswahili wa Pwani anaweza kuweka yake......

tanzaninajema

Touche! haya hii ni kutoka kwenye website ya Vatican City yenyewe:

Vatican City is the smallest independent state in the world in terms of inhabitants and size. It occupies an area of 44 hectares. The borders are represented by its walls and the travertine pavement curve that joins the two wings of the colonnades in St Peter’s Square. Beyond the territory of the State, Vatican jurisdiction also covers some extraterritorial areas within and outside Rome.

http://www.vaticanstate.va/EN/homepage.htm
 
Mchundo

kuna vitu viwili hapa mnaongelea kitu kile kile lakini kwa mtazamo tofauti:

mfano: IMF sio USWIS ila IMF makao makuu yake yapo USWIS na IMF ikitoa order kuhusu maswala yoyote ya kipesa ktk nchi yoyote duniani Si kwamba USWIS ndio imetoa order hiyo.

Kanisa katoliki makao makuu yake yapo ktk nchi ya VATICAN na masuala mengi ya kikatoliki kote duniani yanatolewa na makao makuu ya kanisa hilo ambayo yapo VATICAN ,ieleweke hapa sio NCHI ya VATICAN inayoamua mambo ya Katoliki.

Na kinachochanganya wengi hapa ni kua RAIS wa VATICAN pia ni POPE.Na ifahamike kua POPE anapotembelea nchi hua wakati mwingine anaenda kama RAIS WA VATICAN na mialiko mingine anaenda kama Kiongozi wa kanisa.

Sema ni vigumu tu kumuita PAPA RAIS WA VATICAN kama ilivyokua vigumu kusema MWALIMU RAIS NYERERE na watu mara nyingi kama sio mara zote ukitanguliza neno MWALIMU basi RAIS linapotea lenyewe outomatically.
 
Hapo nipo SIDE B na mimi.
Point hii siielewi kabisa
4. Inafaa tuvumiliane. Waislam wamevumilia wakristo (eg. kuwa na Ubalozi wa Vatican na ubalozi wa Italy), kwa hiyo Wakristo nao wawe wavumilivu uwepo wa Mahakama ya Kadhi.

QUOTE]
Kuwa na ubalozi ni sawa na kuwa na mahakama?

Uvumilivu utaendelea kuwepo..ila hapa hakuna uhusiano..
Balozi za nchi mbalimbali si sehemu ya serikali yetu..hawahitaji pesa ya walipa kodi wetu kujiendesha..isitoshe hizo ni nchi.Mahakama ya kadhi sio ubalozi au uwakilishi wa aina ya ubalozi.
Ukitaka kulinganisha uvumilivu huu ni hivi:#
Waislamu wamevumilia kuwepo ubalozi wa Vatican na Italy na nchi nyingine
Wakristo wamevumilia ubalozi wa Iran, Pakistan, na nchi nyingine
Tuweke hoja zenye kujenga na si kushabikia dini!
 
Hapo nipo SIDE B na mimi.
Point hii siielewi kabisa
4. Inafaa tuvumiliane. Waislam wamevumilia wakristo (eg. kuwa na Ubalozi wa Vatican na ubalozi wa Italy), kwa hiyo Wakristo nao wawe wavumilivu uwepo wa Mahakama ya Kadhi.

QUOTE]
Kuwa na ubalozi ni sawa na kuwa na mahakama?

Uvumilivu utaendelea kuwepo..ila hapa hakuna uhusiano..
Balozi za nchi mbalimbali si sehemu ya serikali yetu..hawahitaji pesa ya walipa kodi wetu kujiendesha..isitoshe hizo ni nchi.Mahakama ya kadhi sio ubalozi au uwakilishi wa aina ya ubalozi.
Ukitaka kulinganisha uvumilivu huu ni hivi:#
Waislamu wamevumilia kuwepo ubalozi wa Vatican na Italy na nchi nyingine
Wakristo wamevumilia ubalozi wa Iran, Pakistan, na nchi nyingine
Tuweke hoja zenye kujenga na si kushabikia dini!


you nailed it sista!..
 
mfano: IMF sio USWIS ila IMF makao makuu yake yapo USWIS na IMF ikitoa order kuhusu maswala yoyote ya kipesa ktk nchi yoyote duniani Si kwamba USWIS ndio imetoa order hiyo.

Makao makuu ya IMF yako Washington DC na sio Uswis!
 
Hapo nipo SIDE B na mimi.
Point hii siielewi kabisa
4. Inafaa tuvumiliane. Waislam wamevumilia wakristo (eg. kuwa na Ubalozi wa Vatican na ubalozi wa Italy), kwa hiyo Wakristo nao wawe wavumilivu uwepo wa Mahakama ya Kadhi.

QUOTE]
Kuwa na ubalozi ni sawa na kuwa na mahakama?

Uvumilivu utaendelea kuwepo..ila hapa hakuna uhusiano..
Balozi za nchi mbalimbali si sehemu ya serikali yetu..hawahitaji pesa ya walipa kodi wetu kujiendesha..isitoshe hizo ni nchi.Mahakama ya kadhi sio ubalozi au uwakilishi wa aina ya ubalozi.
Ukitaka kulinganisha uvumilivu huu ni hivi:#
Waislamu wamevumilia kuwepo ubalozi wa Vatican na Italy na nchi nyingine
Wakristo wamevumilia ubalozi wa Iran, Pakistan, na nchi nyingine
Tuweke hoja zenye kujenga na si kushabikia dini!

Tanzania ikitokota..........Tatizo hoja zote zinabase kwenye ushabiki wa kidini kwani ndivyo watanzania tulivyolelewa. Wengi wetu tunachukulia dini zetu kama UTAMBULISHO unaotutofautisha na "WENGINE" ama "WAO" kwa mabaya na mazuri. Hatuchukulii dini hizi kama imani za kutuongoza jinsi ya kuishi vizuri na hao tuwaonao wengine ama "WAO". Watanzania tumejazwa prejudices kuhusiana na u-mimi, u-sisi na u-wao.

Hivi kodi yangu ikitumika kumwezesha muumini wa dini nyingine ni dhambi ama ni kosa? Naamini uzalendo ni kusaidiana, utaifa ni kusaidian na hata ukristo ama uislamu ni kusaidiana.....ama naishi dunia nyingine?

Well, tukimaliza hili turudi kwenye UCHAGA, UHINDI, Unyanda za juu, u-maisha bora, uswahili.....

Masikini tanzania yetu......twaibomoa kiulaini kama vile haikujengwa na misingi imara....

Tanzanianjema
 
Tanzania ikitokota..........Tatizo hoja zote zinabase kwenye ushabiki wa kidini kwani ndivyo watanzania tulivyolelewa. Wengi wetu tunachukulia dini zetu kama UTAMBULISHO unaotutofautisha na "WENGINE" ama "WAO" kwa mabaya na mazuri. Hatuchukulii dini hizi kama imani za jinsi ya kusihi na hao wengine. Watanzania tumejazwa prejudices kuhusiana na sisi na wao.

Hivi kodi yangu ikitumika kumwezesha muumini wa dini nyingine ni dhambi ama ni kosa? Naamini uzalendo ni kusaidiana, utaifa ni kusaidian na hata ukristo ama uislamu ni kusaidiana.....ama naishi dunia nyingine?

Well, tukimaliza hili turudi kwenye UCHAGA, UHINDI, Unyanda za juu, u-maisha bora, uswahili.....

Masikini tanzania yetu......twaibomoa kiulaini kama vile haikujengwa na misingi imara....

Tanzanianjema

Nakubaliana na wewe kuwa inabidi tuvumiliane. Lakini je kila dini ikiomba iwe na mahakama yake, hili litawezekana? Nadhani kwanza tungeelezwa ni vipi mfumo wa sasa unaonekana kutowatendea haki waislamu. Na pakiwa na hizo system mbili, ipi ndiyo itakayokuwa ya mwisho? yaani je mtu akiona hajatendewa haki upande mmoja ataweza kukimbilia kwingine?
 
Mahakama ya kadhi will never re-exist under the current consititution and current multiethnic tz mainland!

Hebu fikiria, wakristo tz wana imani mbalimbali na wana madhehebu mengi zaidi ya 'miamoja' ambayo ukiyachunguza vizuri utayakuta yamejikita zaidi katika misingi ya hisia za kikabila. Na ni wazi kwamba madhehebu haya yamegeuka kuwa vyama au taasisi za ama kikabila, kimikoa au kimajimbo. Kwa mfano: Wapare na Wajita wana chama chao ambacho ni SDA(Sabato), Wachaga na Wahaya chama chao ni KKKT, wasukuma nao wana chama chao cha AICT(African Inland Charch of Tanzania),...etc...etc. Labda dhehebu pekee lisilo na misingi au itikadi za kikabila ni roman catholic ambalo liko kila mkoa wa tz mainland. Which means, kama serikali itaruhusu kuanzishwa kwa mahakama ya kadhi inayotambuliwa na katiba ya nchi na inayosimamiwa na sheria itakayotungwa na bunge la tz, basi ijiandae pia kuanzisha utitiri wa mahakama zingine za aina na itikadi hiyo hiyo ambazo zitakidhi misingi au mahitaji ya kila kabila au kila dhehebu na imani yake.

Binafisi naishauri serikali iachane na mjadala wa mahakama ya kadhi. Pia nawashauri waislamu waijadili hii hoja ya kadhi katika vikao ndani ya madhehebu yao na wala wasiishirikishe serikali au bunge letu tukufu.

Mambo ya imani waachiwe wanaimani wenyewe kwani katiba ya tz imetoa mwongozo ulio wazi katika uanzishwaji na usimamizi wa taasisi zozote za kidini. Katiba vilevile inatoa uhuru kwa kila dini au dhehebu kuendesha mambo yake bila kusimamiwa na serikali ali mradi wasivunje sheria za nchi.

Watanzania na serikali yao wako huru kujiamulia mambo yao wenyewe na kamwe hawawezi kulazimishwa kuiga kila kitu kinachofanywa na nchi jirani au nchi yoyote duniani, hasa pale inapodhihirika waziwazi kuwa hakuna sababu ya msingi au ulazima wowote wa kufanya hivo!
 
MANENO HAYA ULIYOYASEMA NI KWELI TUPU NA YANAONYESHA BUSARA NA KUTOFUNGAMANA NA UPANDE WOWOTE!WAARABU NA WAZUNGU WALILETA DINI ZAO AFRIKA ZIKATUTENGANISHA,NDUGU KATI YA NDUGU,KIJIJI KATI YA KIJIJI AND SO ON..MWANAKIJI ANADAI KUWA MAHAKAMA YA KADHI ILIKUWEPO WAKATI WA UKOLONI KWA HIYO TUIKUBALI!?NANI KASEMA MFUMO WA UKOLONI ULIKUWA NI WA MANUFAA YA WATAWALIWA?NANI ASIYEJUA KUWA KWA UMBUMBUMBU WETU WATANZANIA CCM NA SERIKALI AKE BADO WANATUMIA KATIBA ILE ILE YA KIKOLONI YENYE KUWANYIMA HAKI WATAWALIWA?NI HIVI KARIBUNI TU WAISLAM WAMEUNDA KAMATI YA KUPINGA UBALOZI WA VATICAN NCHINI KWA MADAI KWAMBA NI YA KIKRISTO NA SERIKALI HAITAKIWI KUWA NA UHUSIANA NA SERIKALI YENYE MWELEKEO WA KIDINI,JE WAKRISTO NAO WAKIZIPINGA BALOZI ZA IRAN NA SAUDI WATAKUWA WAMEKOSEA?JE HIZI ISSUE ZINATUGAWA AMA KUTULETA PAMOJA?NA NI KWELI KUWA AHADI WALIZOTOA CCM ZINAWEZA KUWATOKEA PUANI KWASABABU WALITOA AHADI HIZO ILI WAENDELLE KUKAA MADARAKANI,SASA THIS TIME MAMBO ITAKUWA MSHIKE MSHIKE,NA UPINZANI NAO LAZIMA WATAKOMAA NAO!HIVI KWELI TUNAKOELEKEA KUNA USALAMA?

Mkuu heshima mbele!!
Hapo umenena kwa mwenye ufahamu ameelewa!
 
Mahakamama ya kadhi katika mataifa mengine imetumika kama stepping stone kuelekea katika mataifa ya kiislamu. Mfano rahisi ni vita inayoendelea Somalia. Wana mgambo wa mahakama ya kadhi hatimaye wakishinda vita wanataka kuweka serkali ya ki islamu. Kwa nini kwa mfano Egypt inapambana kabisa na vikundi vinavyopendelea serkali iwe radically islamic? Kwa vyovyote hata nao wanayo mashaka yao.

Back to tz mbona katika sheria yetu kuna tayari allowance ya mambo yanayoamuriwa kwa sheria za kiislamu (customarily) kutambuliwa provided hayapingani na sheria mama? Sasa kinachotafutwa ni nini?

Suppose mwislamu ambaye amtenda kosa alikuwa ameanza ku backslide wenyewe wanaita ku retard je haki zake kama raia zitaheshimiwa hata kama ndani ya uislamu ameanza kuonekana si mwaminifu? Je sheria hii ikipita mwislamu atakayeamua to cross boarders toka uislamu kwenda imani nyingine haki yake ya kuamua kuabudu anachotaka itaheshimiwa? Kuna maswali ya muhimu sana ya kujibiwa hapa. Ikiwa hata mwislamu mzuri akagundua udhaifu fulani katika sheria ya kiislamu akataka jambo lake lishughulikiwe na mahakama ya kawaida itawezekana? Je ili jambo lifike katika mahakama hii itakuwepo fursa ya mhusika au wahusika kuridhia? Nisaidieni. Hasa MMWKJJ naona unajitahidi kuwa independent thinker!
 
Mahakama zote uzushi mtupu, achilia mbali ya kadhi.

Sasa kwenye mizani bora kidogo hizi za kiserikali zina rationale ya kwamba ni bora half baked justice kuliko a wild wild west anarchy.

Kukubali hiyo ya Kadhi ni kurudi nyuma kwenye mambo ya medieval courts.

UMENENA!!

NARUDIA TENA NA TENA, WAUMINI WA DINI HIZI TANZANIA WAKO PARTIAL SANA!. WENGI DINI NI FASHENI KUNA WAISLAMU KIBAO NA WAKRISTO KIBAO AMBAO HAWAISHI KAMA DINI ZAO ZINAVYOTAKA.

KWA MANENO MENGINE MAHAKAMA YA KADHI ITAFANYA WAISLAMU WAJUE KUWA WAKO WACHACHE MNO NCHI HII, KUHAMA DINI MOJA KWENDA NYINGINE AU KUTOKUWA NA DINI NI RAHISI,

WAISLAMU FIKIRIENI MARA MBILI MTAUUA UISLAMU HAPA NCHINI BILA WENYEWE KUJUA!!!!!!!!!!!!(hii na kwa aliyeona mbali sana na anayejua how these courts operate na pia anyejua hali ya commitment ya waislamu kwenye dini yao) kama wasemavyo wengine dini hizi tumeletewa na tunazitolea mimacho ona sasa, badala ya kwaza na kujadili elimu, maji, afya, viboreshwe watu wanawaza mahakama ya kadhi. na ashakum si matusi wanaowaza hayo hali zao za elimu ni duni.marekani wangewaza hivyo at least wameendelea tuko kwenye nchi zinazoongoza kwa umaskini duniani watu wwanawaza mahakama ya kadhi.nonsense!!!!!!!!!

Waberoya
 
Hii hoja haina msingi, Mrema siyo mtawala, na hana Ilani ya uchaguzi ya kufanya jambo hilo. Ni aibu kwa Rais kudai lawama zimuendee Mrema wakati chama chake ndio kilichoidaka hoja hiyo tangu wakati wa Mkapa na ni wao walioiweka kwenye Ilani yao siyo Mrema aliyewawekea. Hoja ya Mahakama ya Kadhi imekuwepo kwa muda mrefu, Mrema ni kiongozi wa kwanza aliyeiweka hadharani (badala ya watu kunung'unika chini kwa chini).
Kama CCM wanaona hoja hii ni ya "mrema" basi waiondoe kwenye Ilani yao na kuwaomba radhi watanzania kuwa waliingiza hoja ya Mpinzani kwenye Ilani yao na ya kwamba hoja hiyo haitekelezeki, na hiyo angalau itakuwa ni ahadi ya kwanza ya CCM ambayo hawataweza kuitekeleza rasmi. Na kutoka hapo basi tutasonga mbele. Serikali yetu haina tabia ya kukubali makosa hata kama yanawakodolea usoni!

Tukisema kuwa kila manung'uniko ya watu yajengewe hoja basi Tanzania hapatatosha.
Mimi nimekutana na manung'uniko ya wazee fulani maeneo ya Tegeta wakiwa wametoka kwenye swala ya jioni. Walichokuwa wanadai ni juu ya Tanzania kuwa nchi ya Kiislamu. Wanadai kwamba nchi hii ni ya waislamu isipokuwa Nyerere aliwanyang'anya. Na haikuishia hapo, nilienda Kilosa, Moro na kukuta habari hiyo kwa vijana wa kiislamu. Nadhani kuna matatizo mengi yanayoambatana na masuala ya watu kushindwa ama kujijenga wao wenyewe ama kuijenga nchi.
Hatuwezi kujenga nchi kwa kutumia minong'ono. Jana nilichangia mada hii alini nimeshangazwa kwmba siioni article yangu. Kuna machache nilijaribu kuyagusia ambayo yametuweka pabaya sana. kimsingi ni kwamba hakuna mkristo anayepinga suala la kadhi kama litajadiliwa katika misikiti na kuanzishwa katika misikiti. Huko ndiko iliko ibada yenyewe. Inapokuja kuwa kwenye katiba ni sawa na kutuambia kuwa wote tunatakiwa tuwe waislamu.
Kuna vikao mbalimbali vya nchi waislamu, na moja ya ajenda ya waarabu ni kuiteka Afrika na kuifanya himaya yao na hasa baada ya kugundua kuwa panaweza kuwa na rasilimali ya mafuta. Kuna matatizo mengi tunayoletewa na waarabu bila wenyewe kuyaona, ila kimsingi yanatuumiza watanzania. Leo hii tunataka kumsahau Chenge, na kuanza kushughulikiana wenyewe kwa wenyewe.
Hii ni ajabu, na kama hatutaamka basi tutatawaliwa na wale waliotufanya wajinga mpaka pale ambapo tutakufa woote na kubaki koo na familia zao tu!!
 
Ngoja nitoke nje ya maada kidogo,
hivi kilitokea nini mpaka tukaacha dini zetu? ukianza kuhoji kwa mawazo huru nasio ya kitheolojia za dini fulani nadhani tunaweza ambulia kitu fulani mfano-

1.Ilikua je hawa wazungu walio ua babu zetu kama akina mkwawa,kubeba maeneo yao ya rutuba,kuchukua malighafi zetu kwa mabavu,kuwatia mijiledi babu zetu ,kuwalaghai babu zetu,kuwafanyisha kazi ngumu LAKINI DINI zao tukaziona sahihii maana walituhubiria wao wasichotenda na ni kinyume kabisa.

2.Hawa waarabu nao waliua babu zetu kinyama,wkawauza babu zetu kama nguruwe na nguchiro wakawatia chapa kwa kutumia chuma la moto ktk miili yao,wakafanya kila aina ya unyama LAKINI DINI zao tukazikubari na kuzipa kipao mbele

Je hizi DINI zinatufaa sie waafrika Je ni SABABU ya sisi waafrika kua nyuma BAADA ya sisi kukataa DINI zetu.Je kukataa dini zetu yawezwa fananishwa na MWANA amkatae BABA yake ama MAMA yake na kupata laana ya asili.
Je kukataa kwa dini zetu kuna kalaana kaasili kalitupata na kusababisha kua waafrika NDIVYO TULIVYO?
Je HII hali tuliyonayo wafrika ni ADHABU endelevu amabayo miungu wetu wanatu adhibu kwa kakataa dini yetu?
Je nini matatizo yetu?
Je kinachogomba AFRIKA na kusababisha haya ni mapambano yanayotokea ya mafahali wawili yani miungu wa wazungu na miungu wa waarabu na nyasi kuumia yani sisi waafrika wakati huo miungu wa aafrika akikaa kando bila msaada kwetu na akitucheka maana tulimkana.

Mimi ninavyoona MUNGU wa BIBLIA na MUNGU wa QURAN si mmoja hawa ni wawili tofauti kabisa na ukisoma utagundua sio mmoja .Mfano ukiangalia maelezo wa MUNGU wa BIBLE anaonekana kua ni YESU na akasisitiza mimi yani yeye ni alpha na omega na akasema yoyote atakaye kuja baada ya mimi ni MWONGO. lakini baada ya miaka 500 akaja mtume MSW kitu ambacho kinaonyesha hatoki kwa YESU aliko.

Kumbe yawezekana kukawa na mungu mwingine wetu waafrika tuliyemkana.Na tukirudia labda mambo yatatulia maana atakua wetu wote waafrika hatutarumbana tena kuhusu kadhi,hatutawekeana tena masharti ya kuona,.Ama ninyi mnaonaje??
 
Back
Top Bottom