Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Nyangumi,Bokassa,Bubu,Koba,Kadogoo,
mmoja kati ya wanaounga mkono tamko la kuvunja uhusiano wetu na Vatican ni Alhaj Ambassador Abbas Sykes. Huyu alipata kuwa balozi wetu Italy na Vatican!!

pamoja na mambo mengine tamko hilo linapinga ziara ya Pope Benedict kwasababu alipata "kuwakejeli" Waislamu.

Mimi napinga ziara ya Papa Tanzania, lakini nafanya hivyo kwasababu naamini gharama zake kifedha ni kubwa mno.

Kuna madai mengi yamewasilishwa Maelezo. Ninasubiri kwa hamu majibu ya RAISI. Suala hili inabidi RAISI a-deal nalo mwenyewe.

NB:
Mimi nafikiri Balozi Sykes na wenzake wange-deal na Mtikila peke yake. Sioni busara ya kuwachanganya Wakatoliki kwa mambo aliyoyafanya Mtikila.
 
kwani hadi sasa hivi kuna tatizo gani. Kwa sababu ninavyofahamu jambo jipya linaanzishwa kukabiliana na tatizo jipya. Kwa sasa mambo yanaendelea vizuri na hakuna sababu ya kuanzisha hii mahakama kwani hapo ndio matatizo yatakapoanza. Wataibuka kina mtikila 100! leo kwenye magazeti waislamu wanataka tuvunje ubalozi na vatican kwa sababu una elements za kidini at the same time wanataka mahakama ya kadhi ianzishwe. Contradiction!
 
hizi nchi maskini tuna shida, badala ya kufikiria maendeleo tunafikiria tu utamaduni wa watu wengine! du toba!

serikali yenyewe imeshindwa kuwalipa vizuri, kuongeza mahakimu na watendaji kazi wake, ......sasa hivi inafikiria kuunda kitu kingine tofauti.

serikali hiyo hiyo imeshindwa kujenga mahakama za kutosha karibu na watu eti sababu haina pesa leo inasema eti inaongeza miundo mingine ya mahakama.

kama mahakama ya kadhi ni sehemu ya ibada, mbona sehemu zilizopo hazitumiki vizuri kama watangulizi walivyosema?

NINAUNGANA NA WENZANGU KUSEMA NO, WITH A CAPITAL LETTER STARTING FROM THE GROUND TO THE ATMOSPHERE UNTIL GETTING A SATISFIED ELLABORATIONS
 
yeah tuvunje mahusiano na nchi zote ambazo katika uongozi wake kuna suala la dini. Tunaweza kuanza na Saudia, UAE, Jordan, Palestine n.k halafu tuendelee na Uingereza na VAtican. Ili Waislamu waonekane kweli wanatetea Katiba wajumuishe katika madai yao nchi hizo zote na mimi niko tayari kuwaunga mkono!!!
 
yeah tuvunje mahusiano na nchi zote ambazo katika uongozi wake kuna suala la dini. Tunaweza kuanza na Saudia, UAE, Jordan, Palestine n.k halafu tuendelee na Uingereza na VAtican. Ili Waislamu waonekane kweli wanatetea Katiba wajumuishe katika madai yao nchi hizo zote na mimi niko tayari kuwaunga mkono!!!

Kwa hapa mie bado naona kihindi hindi, hivi kweli wanatetea katiba kuto ingiza mambo ya dini? Kwani mahakama ya Kadhi wanayo pigania iingie kwenye katiba siyo dini?

Ama swala la Kadhi nalo wameona kwamba si sawa ni la kidini, wame achana nalo, hivyo ili haki iwe sawa wanaona na hayo mengine yashughulikiwe?? Niasaidieni hapa sipati picha!
 
Kwa kweli mimi sikuwa najua kama Serikali yetu inauhusiano rasmi wa kibalozi na Vatikano! kwani tangu enzi za Mwalimu nchi yetu ilikuwa haina dini na katiba yetu iko wazi kabisa kuwa Serikali haina dini!

sasa haya yamekujaje tena kwani leo nimesoma gazeti moja linaripoti kauli za viongozi wa Kiislamu kuitaka Sirikali kusitisha uhusiano huo mara moja soma hapa ..http://www.freemedia.co.tz/daima/2007/11/7/habari3.php na mimi nawaunga miguu na mikono viongozi hao kwa uwamuzi wao na kuwashauri waishitaki Serikali Mahakamani kwa kuvunja katiba ya nchi!

Pumba pumba pumbaaaaaa to the maximum....i think mwasahau kuwa vatican ni state na sio kanisa...kama ni hivyo na mahusiano na other arabic states nazo zifutwee...jamani udini utatufikisha pabaya.....
 
Waislam hususani wa hapa Tanzania na baadhi ya nchi za Africa wasipokaa chini na kujiuliza kwa makini wanaweza kuendelea kuwa walalamishi kuwa wanaonewa na kujenga hoja dhaifu kila mara.

Tukubali tusikubali, matatizo ya Waislam yanasababishwa na dini yao kuwa na "Poor Institutional Capacity". Tukianzia katika utaratibu wao wa kupata viongozi, hawa watu hawana mfumo na miundombinu bora ya kujenga na kupata viongozi walio bora. Kwa mfano, tofauti na Wakristo, hakuna chuo chenye hadhi kinachotumika kumuandaa, kumjenga na kumuimarisha mtu ili aje kutumikia Msikiti kama Sheikh. Utakuta mtu anasoma madrasa kidogo na akishakariri Quran, tayari anakuwa Sheikh. Unakuta mtu elimu yake ni ya chini, hana elimu ya kupambanua mambo na IQ yake ni ndogo anakuwa Sheikh. Wakati mwingine mtu akiwa na pesa yake anajenga msikiti kisha yeye ndio anakuwa Sheikh. Tofauti na madhehebu mengi ya Kikristo, mtu anaandaliwa na anapikwa kielimu na kimaadili kwa muda mrefu hadi anaiva kuwa kiongozi.Hicho ndicho kinachowaangusha hawa wenzetu. Matokeo yake ndio hao tunaowashuhudia wakiropoka hovyo na kutoa hoja dhaifu.

haika mbe...yaani boa uwape ile kitu roho yao inataka....maaana kwa ulalamishi mwee hawa majamaaa hatuwawezi sijui wana p.gani...anyways..sitaki kuamini mtu aliye bring this topic is.......
 
Vatican ni nchi kama nchi nyingine kama saudi arabia inayotumia kurani kama katiba. Tatizo ni nini? Ukivunja uhusiano na vatican unapata faida ipi? Mijitu mingine? Ah
 
go east or west...juu au chini...if ilikwepo zamani ikatolewa..it means waliotoa hawakuwa wajinga...ilionekana ina matatizo isababishayo in jamii na hivyoo no matter wat izuiwe kusiwe na any reason ya kuileta back...
 
Bongo,Siku zote CCM imekuwa ikitawala kiujanja-ujanja kwa kutumia shida na ujinga wertu Watanzania ili wapate ridhaa ya kutawala na hii ni hatari kubwa. Ishara ya hatari hii ni hii Waislamu kudai mahakama ya Kadhi (pamoja na hoja nzuri za Mwkjj kuhusu hoja hii). Ukiangalia kwa undani CCM wametumia shauku (shida) ya kundi mojawapo lenye ushawishi kwenye jamii ili kupata kura za kuendelea kutawala.

Nathubutu kusema iwapo Mahakama hii itakuwepo tutashuhidia kuparanganyika kwa Taifa letu kutakosababishwa na ujanja-ujanja huu wa CCM maana Mahakama ikianzishwa tu lazima makundi mengine yenye ushawishi mkubwa katika nchi hii (Wakristo) nao watadaisheria za Kanisa zitambuliwe Kikatiba na kutumika na kwa hila hizo hizo za CCM kutaka kuendelea kutawala basi watakubali (hawatakuwa na sababu ya kukataa wakati wamekubali kutambua Mahakama na mamlaka ya Kadhi)na hivyo tutashuhudia Taifa letu likiongozwa na sheria tatu tofauti zinazopingana. Mfano, Kanisa haliruhusu talaka wakati Sheria za Kiislamu zinatambua na Serikali hutambua; je, itakuwaje pale ambapo mtu na mke wake au mumewe kila mmoja anataka ifuatwe sheria tofauti kuhusu talaka katika shauri lake? Sijui Makarasinga na Wahindu nao wakitaka sheria za dini zao zitumike itakuwaje.

Hili litapelekea mwishowe kila dini iwe na eneo lake la kujitawala ambapo sheria zake ndiyo zinatambuliwa na kutumika kama vile Islamic territory, Christian territory na Government/Secular territory.

Nathubutu kusema kuwa kama Serikali ya CCM iko makini na haitaki kuliingiza taifa kwenye madhara Mahakama ya kadhi haitakuwapo na ikiwepo basi Sheria za kanisa nazo itapaswa zitumike, what a contardiction! Sulal la Mtikila (ingawa watu wanamwona kuwa ni kama Chizi katika suala la Mahakama ya Kadhi) ni ishara tu ya mambo yatakavyokuwa pindi Mahakama ya kadhi itaanzishwa.

Serikali ya CCM itabidi ituambie kwa nini iwakubalie Waislamu kutumia sheria za kidini katika masuala yao na kutukatalia sisi Wakristo kutumia sheria zetu!

MANENO HAYA ULIYOYASEMA NI KWELI TUPU NA YANAONYESHA BUSARA NA KUTOFUNGAMANA NA UPANDE WOWOTE!WAARABU NA WAZUNGU WALILETA DINI ZAO AFRIKA ZIKATUTENGANISHA,NDUGU KATI YA NDUGU,KIJIJI KATI YA KIJIJI AND SO ON..MWANAKIJI ANADAI KUWA MAHAKAMA YA KADHI ILIKUWEPO WAKATI WA UKOLONI KWA HIYO TUIKUBALI!?NANI KASEMA MFUMO WA UKOLONI ULIKUWA NI WA MANUFAA YA WATAWALIWA?NANI ASIYEJUA KUWA KWA UMBUMBUMBU WETU WATANZANIA CCM NA SERIKALI AKE BADO WANATUMIA KATIBA ILE ILE YA KIKOLONI YENYE KUWANYIMA HAKI WATAWALIWA?NI HIVI KARIBUNI TU WAISLAM WAMEUNDA KAMATI YA KUPINGA UBALOZI WA VATICAN NCHINI KWA MADAI KWAMBA NI YA KIKRISTO NA SERIKALI HAITAKIWI KUWA NA UHUSIANA NA SERIKALI YENYE MWELEKEO WA KIDINI,JE WAKRISTO NAO WAKIZIPINGA BALOZI ZA IRAN NA SAUDI WATAKUWA WAMEKOSEA?JE HIZI ISSUE ZINATUGAWA AMA KUTULETA PAMOJA?NA NI KWELI KUWA AHADI WALIZOTOA CCM ZINAWEZA KUWATOKEA PUANI KWASABABU WALITOA AHADI HIZO ILI WAENDELLE KUKAA MADARAKANI,SASA THIS TIME MAMBO ITAKUWA MSHIKE MSHIKE,NA UPINZANI NAO LAZIMA WATAKOMAA NAO!HIVI KWELI TUNAKOELEKEA KUNA USALAMA?
 
Kwa kweli mimi sikuwa najua kama Serikali yetu inauhusiano rasmi wa kibalozi na Vatikano! kwani tangu enzi za Mwalimu nchi yetu ilikuwa haina dini na katiba yetu iko wazi kabisa kuwa Serikali haina dini!

sasa haya yamekujaje tena kwani leo nimesoma gazeti moja linaripoti kauli za viongozi wa Kiislamu kuitaka Sirikali kusitisha uhusiano huo mara moja soma hapa ..http://www.freemedia.co.tz/daima/2007/11/7/habari3.php na mimi nawaunga miguu na mikono viongozi hao kwa uwamuzi wao na kuwashauri waishitaki Serikali Mahakamani kwa kuvunja katiba ya nchi!

HI WE KADOGOO NGOJA NIKUULIZE SWALI MOJA,NA UKIWEZA KULIJIBU THEN UTAKUWA UMEELEWA NINA MAANA GANI"JE SERIKALI ZA SAUDI ARABIA NA IRANI SI ZA KIDINI?"WAKRISTO NAO WAISHTAKI SREIKALI?MHH HAYA WE TUNAKOELEKEA!
 
yeah tuvunje mahusiano na nchi zote ambazo katika uongozi wake kuna suala la dini. Tunaweza kuanza na Saudia, UAE, Jordan, Palestine n.k halafu tuendelee na Uingereza na VAtican. Ili Waislamu waonekane kweli wanatetea Katiba wajumuishe katika madai yao nchi hizo zote na mimi niko tayari kuwaunga mkono!!!

HAPO SASA TUNAKUBALIANA!
 
Kama utakavyoona katika sehemu ya pili ya makala yangu naamini ipo njia ya kuweza kuwa na mahakama ya kadhi pasipo kuogopa jambo lolote au kuhofia lolote hasa kama itaundwa kwa kufuata kanuni zinazoeleweka.

Sha-shaa mzee, imalizie hiyo makala!! Tuanze mjadala, kwani pamoja na kuona umuhimu wa kujibu hoja za wanaotaka mahakama hiyo, badi sijaona uwezekano wa kufanikiwa wa mahakama hizo!!!!
 
Kadogoo fikiria kwa makini ujumbe wako, ni kama hauelewi uhusiano na vatcan, by the way, mbona haujasema chochote kuhusu mahakama ya kadhi?

hakuna ukweli wowote kwenye ulichokisema na waislam wakishikia bango swala hilo basi wanazua mijadala ambayo mingine wakristo wameinyamazia tu,
 
JMUSHI1, MC na wengine:

Kwanza wanabodi nawasalimia nyote munaonifahamu na musionifahamu kwani ni muda mrefu sana sikuwa nikiandika bali niliamuwa kuwa mtazamaji tu baada ya kuona ushabiki umezidi nani atachaguliwa na nani...

Sasa nikirudi ktk ujumbe wangu wa kuunga mkono tamko la viongozi wa Kiislamu dhidi ya Serikali nadhani baadhi yenu munaufahamu mdogo sana juu ya uhusiano baina ya Serikali na Vatikano kwa upande mmoja na mahusiano na Serikali zenye kuongozwa Kiislamu! kwa kweli kama mutakuwa munajibu hoja kiushabiki shabiki bila ya uchunguzi basi hii inathibitisha mapungufu fulani!

Waislamu wanazungumzia kusitishwa uhusiano ulio rasmi na Vatikano yaani Serikali kuwa na uhusiano wa kiBalozi! sasa munaposema Kama Serikali itasitisha uhusiano na Kanisa Katoliki basi haina budi kusitisha uhusiano na Serikali za Saudia, Iran au Sudan!!!! POINTLESS!!!!!

Kama munakumbuka Miaka 7 iliyopita Maaskofu wa Baraza la Kanisa la Pentekoste la Tanzania(PCT), walitoa kitabu kinachoitaka serikali iitishe kura ya maoni kwanza, kabla ya kuamua kujiunga na Jumuiya ya Mkutano wa Kiislamu, (OIC), ili kupata ridhaa za Watanzania.

Kitabu hicho, kilichopewa jina la "Amani katika Tanzania italindwa kwa:kutenganisha Dini na Mamlaka ya nchi", kinaeleza kuwa kitendo cha serikali ya Tanzania kutaka kujiunga na OIC si jambo dogo. Nijambo linalowahusu Watanzania wote, Waislamu na wasiokuwa Waislam, na hata wale wasiokuwa na dini yo yote.

Kwa mujibu wa kitabu hicho inaelezwa jambo hilo, halifai kujadiliwa kijuujuu tu, kwa kupitia katika vyombo vya habari, na wala haifai kuachiliwa Bunge peke yake kuamua juu ya jambo zito kama hilo.

Halmashauri Kuu ya Maaskofu wa Kanisa la Pentekoste, kwa kupitia katika kitabu hicho, imesisitiza serikali iitishe kura ya maoni ili ipate kuelewa msimamo wa Watanzania wote, wa dini mbalimbali, juu ya jambo hilo.

Katika kutaka kufafanua zaidi juu ya jambo hilo, Halmashauri hiyo imesema, "Lakini si kazi ya Bunge kutunga sheria za kidini, kwa kuwa OIC ni taasisi ya kidini, ni muhimu taasisi nyingine za kidini zilizopo hapa nchini nazo zishirikishwe kikamilifu katika uamuzi mzito kama huu."

Kwa ufupi, Maaskofu wa Kanisa la Pentekoste, katika kitabu hicho, wametilia mashaka uhusiano huo kama utaanzishwa. Wamedai kuwa lengo la misaada inayotolewa na taasisi hiyo ni kwa ajili ya kutaka kueneza imani ya dini hiyo katika nchi wanachama. Maaskofu hao wamesema kuwa kama Tanzaniai tajiunga na taasisi hiyo basi itakuwa ni sawa na kuwasilimisha Watanzania bila ya nidhaa yao!

Inaonekana kuwa kitabu hicho kimetolewa na Kanisa la Pentekoste, kama ni onyo kwa serikali isijiunge na OIC, baada ya kumsikia mgombea wa kiti cha urais wa Zanzibar mwaka 2000, kwa tiketi ya CCM, Rais Amani Karume katika madahalo ulioandaliwa na shirika la utangazaji la BBC, akisema kuwa serikali imekwishafanya utafiti na imeona kuwa Tanzania ijiunge na taasisi hiyo, kwa kupitia serikali ya Muungano, na siyo kupitia serikali ya Zanzibar.

Kwa vyovyote vile, mtazamo huo wa Maaskofu, umekosa uadilifu kama ulivyo msimamo wenu hapa wanabodi. Ni mtazamo ulioelekezwa katika kuuangalia upande mmoja tu wa shilingi na kuupuuzia upande wa pili. Ni mtazamo chongo! Ni sawa na mtu mwenye macho mawili lakini akaamua, kwa makusudi, kufumba jicho moja na kuangalia kwa jicho moja.

Kama serikali ya Tanzania haifai kujiunga na OIC, bila ya kuitisha kura ya maoni, eti kwa sababu OIC ni taasisi ya kidini; basi lazima tukubali kuwa kwa hoja hiyohiyo, serikali hiyo ya Tanzania itakuwa imefanya kosa kuanzisha uhusiano, tena wa kibalozi, na Vatikano, ambayo ni taasisi ya kidini, na siyo nchi yenye raia! kama vile Saudia na Iran!!

Uhusiano huo wa serikali ya Tanzania na Vatikano, ingawa ni uhusiano baina ya nchi hii na Kanisa Katoliki duniani, lakini jambo la kustaajabisha hakuna yeyote anayehoji juu ya uhusiano huo, si serikali wala makanisa ya Kikristo! tena na nyinyi wana Forum munaendeleza wimbo uleule wa kudai Vatikano ni nchi Kamili! tangu lini Taasisi ya kidini ikawa nchi ndani ya nchi!

Mwaka 1992 Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar ilitaka kuwa mwanachama wa O.I.C.ili ijikwamue kiuchumi kutokana na misaada na mikopo isiyo na riba inayotolewa na jumuiya hiyo ya Waislamu.

Hatua hiyo ya Serikali ya Mapinduzi ilizua mtafaruku ndani ya Bunge, CCM, Serikali na katika vyombo vya habari, kwamba ililenga kuiingiza Zanzibar katika Sharia za Kiislamu na hatimaye kuisilimisha Jamhuri ya Muungano.Lakini Bunge, Serikali na hasa Mwalimu Nyerere, waliipinga kweli kweli, Mwalimu Nyerere kwa mikutano ya hadhara na ya waandishi wa habari alipinga hatua ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Muungano kujiunga na Shirika la O.I.C.",

Mtu yoyote mwenye akili timamu anatambua O.I.C. haina malengo ya kusilimisha bali kusaidia nchi wanachama wake kuboresha hali za kijamii kama Msumbiji ni nchi yenye Wakiristo wengi lakini ni mwanachama wa OIC wala hakuna anaesilimishwa huko!

Mlokole Bush alipotaka kuitawala Iraq alidai Sadam anasilaha za maangamizi kama anavyodai Mlokole Mtikila kuwa mahakama za Kadhi ni ugaidi na zikianzishwa basi Wakiristo watakatwa vichwa!! upuuzi ule ule kama madai ya BUSH!!

Wakiristo wa TZ inawahusu nini kuanzishwa mahakama za Kadhi? pilipili ziko shamba zawawasha nini? kama Biblia haina sheria za kuhukumia waumini wake kwanini Waislamu wasiruhusiwe kutumia baadhi ya sheria za Kurani kama vile mirathi na ndoa?

Mbona Zanzibar na Kenya mahakama za kadhi zinafanya kazi kwa ufanisi mzuri sana wala hatujasikia watu kukatwa vichwa!!

Tuache udini na tujibu hoja!
 
Waislamu wanazungumzia kusitishwa uhusiano ulio rasmi na Vatikano yaani Serikali kuwa na uhusiano wa kiBalozi! sasa munaposema Kama Serikali itasitisha uhusiano na Kanisa Katoliki basi haina budi kusitisha uhusiano na Serikali za Saudia, Iran au Sudan!!!! POINTLESS!!!!!

I have seen spin in my life, sir this one is up there!!

Kama serikali ya Tanzania haifai kujiunga na OIC, bila ya kuitisha kura ya maoni, eti kwa sababu OIC ni taasisi ya kidini; basi lazima tukubali kuwa kwa hoja hiyohiyo, serikali hiyo ya Tanzania itakuwa imefanya kosa kuanzisha uhusiano, tena wa kibalozi, na Vatikano, ambayo ni taasisi ya kidini, na siyo nchi yenye raia! kama vile Saudia na Iran!!
Ukichunguza utaona kuwa VAtican ni nchi kamili ambayo ilipata uhuru wake kamili 1929 kwa mkataba wa Laterani kati ya Papa na Mfalme wa Italia. Ni nchi kamili inayochagua kiongozi wake, yenye serikali yake kamili, nembo yake, bendera yake, sarafu yake, posta yake na hata jeshi lake! Siyo TAASISI ya kidini. Kanisa Katoliki ni taasisi, lakini Vatikani ni nchi.

Uhusiano huo wa serikali ya Tanzania na Vatikano, ingawa ni uhusiano baina ya nchi hii na Kanisa Katoliki duniani, lakini jambo la kustaajabisha hakuna yeyote anayehoji juu ya uhusiano huo, si serikali wala makanisa ya Kikristo! tena na nyinyi wana Forum munaendeleza wimbo uleule wa kudai Vatikano ni nchi Kamili! tangu lini Taasisi ya kidini ikawa nchi ndani ya nchi!
unaendelea kujizungusha wewe mwenyewe. Saudi Arabi ni nchi na ndani yake kuna miji mitakatifu ya Maka na Medina. Sisi tuna uhusiano wa Kibalozi na Saudi Arabia, je Serikali yetu ina uhusiano na dini ya Kiislamu? Vatikani ni nchi kamili na haiko ndani ya nchi nyingine!!!! ina mipaka yake inayotambulika kimataifa. Na ndiyo nchi ndogo zaidi duniani.

Wakiristo wa TZ inawahusu nini kuanzishwa mahakama za Kadhi? pilipili ziko shamba zawawasha nini? kama Biblia haina sheria za kuhukumia waumini wake kwanini Waislamu wasiruhusiwe kutumia baadhi ya sheria za Kurani kama vile mirathi na ndoa?
Sasa kama haiwahusu kwanini wanaitaka CCM itimize Ilani wakati ndani ya CCM kuna Wakristu au utakuwa ni mjadala wa Wana CCM waislamu peke yao? Na kule Bungeni ambako wanataka sheria ipitishwe watakuwa na kikao cha Bunge la Waislamu watupu na Wakristu hawatatakiwa kuchangia? Kama kuna ndoa yenye kuhusisha wakristu au wakristu hawana haki zozote kwenye hiyo Mahakama ya Kadhi na kama hawana kwanini wakubali wake zao wafuate maamuzi ya mahakama hiyo? Kama hawataki wakristu watolee maoni wajianzishie na waendeshe wenyewe nadhani hakuna mtu atakayelalamika.
 
Hovyoooooooooo na tena bure kabisa........hao waislam na wakristo wanaopiga makelele yasiyo na msingi wote ni "extremists" hawana tofauti na bin Laden, Pat Robertson au Marhum Jerry Falwell. Ndugu zangu WaTz mnatakiwa kuya-reject mawazo kama hayo huko juu kwa hii thread kwani ni pungumfu mno na primitive kushinda hata amoeba, watu wanatakiwa ku-concentrate kwenye vitu vya maana, issues za maendeleo kwa taifa zima regardless na imani zao za kidini!!!!. Uislam na Ukristo kwanza zote ni dini za KIFISADI, kikoloni na kufikirika..............tupeni kwenye trash udini!!!! Atheist wa Kibongo, yes sir, I said so. Nasubiri kuvurumishiwa kashfa na kubezwa, msipoteza muda kwani yatakuwa makelele ya chura.

kwa mtu ambaye ni atheist kuingia kwenye thread ya mambo ya dini nadhani ndiyo kelele za chura. Ila kuwa atheist nayo ni imani na una haki nayo, sawa sawa kabisa na mtu ambaye anaamini kuwa mwezi umeundwa kwa jibini!
 
Eeeh hii kali. Inabidi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa ki mataifa aanzishe darasa.
 
JMUSHI1, MC na wengine:


Wakiristo wa TZ inawahusu nini kuanzishwa mahakama za Kadhi? pilipili ziko shamba zawawasha nini? kama Biblia haina sheria za kuhukumia waumini wake kwanini Waislamu wasiruhusiwe kutumia baadhi ya sheria za Kurani kama vile mirathi na ndoa?

Tuache udini na tujibu hoja!


Inatuhusu kwa sababu mnataka kutumia pesa zetu za kodi kuendeshea mambo yenu ya kidini na vilevile tunaiheshimu katiba yetu ambayo hairuhusu ubaguzi wa kidini, rangi wala kabila.

Jambo linalotia shaka, kwa nini mnadai Mahakama ya Kadhi itashughulika n a baadhi ya sheria za Quran kama ndoa na Mirathi; Kwa nini isiwe zote? Kutakuwa na manufaa na tofauti gani kutekeleza baadhi ya sheria zenu kwenye mahakama ya Kadhi na zingine kuziacha kwenye mfumo wa Mahakama zingine za Serikali? Kwa nini mnataka hivyo? Mimi sipati picha.
 
Back
Top Bottom