Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Ikiwa Wamaasai wameweza kuwa na mfumo na utaratibu wao wa mila na uongozi sioni kwanini Waislamu washindwe kuwa kitu kimoja na kumchagua Kadhi Mkuu. Wamaasai wana utaratibu wa kuchagua Laigwanan ktk jumuiya ndogo ndogo, halafu kutokana na hao huchaguliwa kiongozi wa Laigwanan wote.


Naaam, naungana nawe 100%
 
Fundi Mchundo,


Mkuu hekima iliyopo katika mfano huu ndiyo inayo apply kwa mahakama ya kadhi..Ukiwa huna Ng'ombe ina maana wewe siii mfugaji huwezi kuamua mambo ya wafugaji.. Ndilo swala la Waislaam kudai mwamuzi awe mwenye ng'ombe pia..
Katika mtazamo wangu nasema sii lazima swala la Maamuzi mengi ya nchi yetu yatokane na dini bali hali halisi ya wananchi na sii dini (ufugaji) kwani waislaam wengi leo hii sii wafugaji tena..

Wakati huo huo swala la mgao kama huu hauhitaji uwe na ng/ombe maadam wapo wafugaji jirani unaweza kwenda azima mmoja..Korti zetu (civil court) zinaweza kabisa ku apply baadhi ya sheria toka dini ya Kiislaam ikiwa tu zina fit na society nzima hasa ktk maswala ya urithi na ndoa zaidi ya mke mmoja..Wapo wakristu na pagani walio na mke zaidi ya mmoja, watoto waliozaliwa nje ya ndoa na kadhalika...

Wakuu nitarudia tena kusema tusiwe tunapinga vitu tu kwa sababu waoadai ni Waislaam wakati tupo tayari kusikiliza na kupitisha ndoa za Kishoga ktk sheria zetu...Ama tumeweka sheria ndani ya katiba yetu kupinga ndoa za Kishoga wakati nchi nzima sii ya mashoga..
Hivyo swali kama la Mh. Moshi, kwa nini waislaam wanataka kuihusisha serikali ktk mambo yao naweza kuuliza pia kwa nini serikali inajihusisha na mambo ya mashoga! sisi wote sii washoga!..

Mimi sijakuelewa, Mkuu. Kwa hekima iliyomo katika mfano wako maana yake ni kuwa kila kikundi ni lazima kiwe na mahakama yake. Kama ni hivyo, basi kwa nini tuishie kwenye dini tu? Kwa nini tusiwe na mahakama ya wakina mama tu? Na baada ya hapo, ya wakina waislamu nao watahitaji mahakama yao tofauti? Na baada ya hapo, wakina mama waislamu vikongwe nao watadai mahakama yao tofauti. Na baada ya hapo wakina mama waislamu vikongwe wazaramo nao watadai mahakama yao tofauti. Mwisho wake utakuwa nini?

Kama tumekubaliana kuwa sisi ni nchi moja basi ni lazima kama raia wa nchi hiyo tukubaliane kuwa na chombo kimoja cha sheria kitakacho tuhukumu sote bila kujali tofauti zetu. Tunapoanza kudai vyombo tofauti ndiyo mwanzo wa nyufa katika utaifa wetu. Hekima zilizomo katika utofauti wetu ndizo zichukuliwe na kutajirisha sheria zinazotuongoza sote na si vinginevyo.

Ndicho hiki kinachotuponza katika Muungano wetu. Kama tungekubaliana toka awali kuwa muungano huu utakuwa na chombo ambamo walioungana wote wataonekana sawa mbele yake, tusingefika hapa. Labda tusingekuwa na muungano lakini tusingekuwa na haya matatizo yanayoendelea kila siku ya kila upande kutomwamini mwengine.

Mfano wako kuhusu mashoga hauhusiani na alichokiuliza Augustine. Mashoga wa Tanzania ( ambao hakuna mtu anaweza kudai kuwa hawako) hawajawahi kusimama na kudai upendeleo wowote wa kikatiba. Ni sisi tulio wengi ndio kwa nguvu za wingi wetu tunawawekea sheria za kuongoza matendo yao. Mfano wako utakuwa na mantik kama unadai kuwa katiba ilitungwa na wakristu bila kuwahusisha waislamu. Kwa maneno mengine, una-question legitimacy ya katiba iliyopo. Na kwa sababu hiyo, kwamba hiyo katiba ni ya kikandamizi basi waislamu inabidi wapewe upendeleo wa pekee kufidia dhulma iliyofanywa dhidi yao! Kama huu ndio msimamo wako, basi bora uwe wazi. Hauwezi kutaka kubaki na keki yako na uile wakati huo huo!

Amandla.....
 
Fundi Mchundo,
Hujanielewa kwa sababu hujaweka attention ktk hoja zangu..
Mimi pia sikubaliani na mahakama za kadhi hilo kwanza lakini tunapishana sababu. Nyie wengi wenu mnafikiria ndani ya box, ndani ya kabati la U mimi na wao kwa sababu huwezi kusema hili ni Taifa moja lakini wakati huo huo unataka makubaliano yatoke hoja za upande mmoja tu..

Swala la mahakama ya kadhi linatokana na utata wa mambo yanayohusiana na sheria zilizopo. Sii Wakristu wote wanakubali maswala ya waislaam yainginizwe ktk sheria zetu lakini mambo mengi ya Wakristu yamo ktk sheria zetu..Kwa hiyo makubaliano haya unayoyasema ni ya Upande mmoja tu na waislaam ni wafuasi wa kufuata kilichomo ktk sheria.. Ni sawa na CCM walivyotuletea Ujamaa, sisi wote tulifuata tu hata kama hukubaliani..Siasa za Kibepari zilikuwa marufuku na kama wanabisha watafute nchi wakaishi.. Huu ndio mtazamo wa wengi hapa JF.

Culture yao Waislaam haikubaliki, wala haikuunganisha na culture za makabila, dini na jinsia nyinginezo ktk katiba ya nchi yetu..ndio maana wanataka chombo chao wao wenyewe kama vile mashoga haihusiani na kukuhukumu wewe, bado hamtaki.. mngekubali kuweka sheria zao ktk mahakama ya madai usingesikia habari hizi za mahakama ya kadhi..

Huo mfano hapo juu hautazami makundi yaliyopo baina yetu hata kidogo isipokuwa yanatazama maamuzi ya maswala yanayohusiana na makundi yetu.. Ikiwa kuna tatizo la Unyumba mahakama zetu zina sheria inayohusiana na mwanamke, mtoto na mume... lakini at the same time sidhani kama kuna sheria zinazohusisha mke wa pili, wa tatu na wa nne..Mipango ya Mirathi na kadhalika jambo ambalo Wakristu hawawezi kulikubali kutokana na imani ya dini yao...Hata ktk sheria kuu, leo hii tuna Madangulo, Casino na kadhalika yote haya yanakubalika kisheira na kwenu lakini Muislaam hakuulizwa kama iruhusiwe!..hofu ya dini ya Muislaam is not an issue..

Kama unavyomwona Mh. Mengi anakataa kuwa na mke wa pili kwa hofu ya kupotosha dini yake wakati ana kimada wakati hajamtalakia mke wa kwanza..... Sielewi kama inakubalika kidini hasa ktk dhehebu la katoliki.. At the sametime huyu kimada wa Mengi hana sheria, akizaa na Mengi mtoto wake ni Haramu, hivyo kinachomweka pale ni kuchuma na future isiyofahamika.. Je, kuna haja ya kuweka sheria kuwalinda hawa wanawake..Ni sheria ipi - Kuwazuia wanaume wasiwe na mke zaidi ya mmoja? au kuwapa mirathi halali wake na watoto wanaokuwa ktk relation kama hizi..na vipi Waislaam wata fit vipi ktk sheria hizi. huu ndio mtazamo kwa wote na sii kundi moja tu.
Sasa makahama ya kadhi inapendekezwa kwa sababu kesi kama hizi ni nyingi sana.. na maamuzi mengi yanayoweza kufikiwa kidini hayakubaliki na mhusika mathlan wanawake wengi wengi waliozaa nje ya ndoa au kuwekwa unyumba kupoteza kabisa urithi pindi mzee anapokufa.. Hufukuzwa ndani ya nyumba na adha hizi huwapotezea maisha watoto...
Mimi sii Mtaalam lakini nakwamia hivi kati ya watoto 5 masklini wa Kitanzania, watatu wamezaliwa nje ya ndoa au baba kuwakataa baada ya kuingiza jiko jipya..Wapo vijana wengi sana tumeishi nao tena watoto wa viongozi wakubwa serikalini leo hii wananyanyaswa kwa sababu mzee kaingiza jiko jipya.. Mtazame Steve utafikiria sii mtoto wa Mkapa.. (samahani Steve) lakini ndio ukweli pamoja na kwamba unauma..
Sheria zetu haziwalindi watoto, hivyo waiuslaam na mahakama ya kadhi wanaona kama nyie hamtaki kuwalinda watoto wenu sisi tunataka kuwalinda.. Kama hamtaki kuingiza sheria zetu ktk katiba then let us do our own thing kwa faida ya kizazi chetu..
 
Swala la mahakama ya kadhi linatokana na utata wa mambo yanayohusiana na sheria zilizopo. Sii Wakristu wote wanakubali maswala ya waislaam yainginizwe ktk sheria zetu lakini mambo mengi ya Wakristu yamo ktk sheria zetu..Kwa hiyo makubaliano haya unayoyasema ni ya Upande mmoja tu na waislaam ni wafuasi wa kufuata kilichomo ktk sheria.. Ni sawa na CCM walivyotuletea Ujamaa, sisi wote tulifuata tu hata kama hukubaliani..Siasa za Kibepari zilikuwa marufuku na kama wanabisha watafute nchi wakaishi.. Huu ndio mtazamo wa wengi hapa JF.

Culture yao Waislaam haikubaliki, wala haikuunganisha na culture za makabila, dini na jinsia nyinginezo ktk katiba ya nchi yetu..ndio maana wanataka chombo chao wao wenyewe kama vile mashoga haihusiani na kukuhukumu wewe, bado hamtaki.. mngekubali kuweka sheria zao ktk mahakama ya madai usingesikia habari hizi za mahakama ya kadhi..

Huo mfano hapo juu hautazami makundi yaliyopo baina yetu hata kidogo isipokuwa yanatazama maamuzi ya maswala yanayohusiana na makundi yetu.. Ikiwa kuna tatizo la Unyumba mahakama zetu zina sheria inayohusiana na mwanamke, mtoto na mume... lakini at the same time sidhani kama kuna sheria zinazohusisha mke wa pili, wa tatu na wa nne..Mipango ya Mirathi na kadhalika jambo ambalo Wakristu hawawezi kulikubali kutokana na imani ya dini yao...Hata ktk sheria kuu, leo hii tuna Madangulo, Casino na kadhalika yote haya yanakubalika kisheira na kwenu lakini Muislaam hakuulizwa kama iruhusiwe!..hofu ya dini ya Muislaam is not an issue..

Kwa hiyo pamoja na kupinga kuweko na Mahakama ya Kadhi, msimamo wako ni kuwa hii katiba yetu ni ya kigandamizi kwa waislamu kwa sababu haitambui sheria za kiislamu? Ninavyojua mimi ni kuwa sheria yetu inaruhusu polygamy kitu ambacho hakiruhusiwi katika umisheni lakini ni ruksa kwa waislamu na wanaofuta imani za asili! Sasa kama hao wa-misheni ndio waliojitungia hiyo katiba kwa nini basi wasifanye polygamy kuwa kosa la jinai?

Nani aliyekwambia kuwa dini ya kikristu inaruhusu madangulo na casino? Kama madangulo yangekuwa yanakubalika kisheria kwa nini hatuoni matangazo yao kwenye luninga kuvutia wateja? Kuweko kwa madangulo katika nchi zenye wakristu wengi hakumaanishi kuwa dini hizo zinatambua madangulo. Mbona naambiwa hata iran yapo! Mbona hata Pemba au Unguja ambako wako waislamu wengi bado kuna wanawake na wanaume wanaojiuza?

Unadai kuwa dini yako inawapa haki watoto ambao katika sheria zetu hatuwapi. Dini ambayo haitambui watoto waliozaliwa nje ya ndoa au watoto waliokuwa adopted. Hao nani atawapa haki kwa kosa ambalo si la kwao maana hawakuomba kuzaliwa nje ya ndoa au kuwa adopted! Ni wapi atakambilia mjane ambae hakujaliwa kuzaa na mumewe atakapoambiwa kuwa kutokana na imani yake basi urithi wake ni robo tu ya mali aliyochuma na mume wake ( Quran 4:12)? Atakimbilia wapi mjane aliyeolewa na mmisheni atakapoambiwa za mume wake kuwa katika dini yake muislamu hawezi kurithi kwa asiye muislamu ( kama alivyoshauri Sahih al-Bukhari)? Au mtoto wa kike aliyemuuguza mzazi wake hadi mauti yanapomkuta ( wakati kaka yake akipiga maisha ) atakapoambiwa kuwa kaka yake atarithi mara mbili zaidi yake kwa sababu tu ni mwanaume ( Quran 4:11)? Na usikute sehemu kubwa ya hiyo mali ni yeye aliyempa mzazi wake!

Ninavyoona mimi hii mahakama ni namna nyingine tu ambayo sehemu ya jamii inayopendelewa ( wanaume katika uislamu) wanataka kuendeleza dhulma yao dhidi ya wengine.

Amandla.......
 
Kuna mambo yanafichwa. Nani atagharammia mishahara ya mahakimu na wafanyakzai wa mahakama hiyo?

Kama hakimu wa mahakama iliyoanzishwa na serikali akitoa Court Order kwamba "kwa vile Dar kuna Waislamu wengi, basi nyama ya nguruwe ni marufuku" si itabidi Polisi wasimamie utekelezaji wake?

Mirathi anayozungumzia Mkandara inashughulikiwa kwenye mahakama za kawaida. Kama kuna Waislamu wanaotaka ishughulikiwe kidini, si wako radhi kufanya hivyo? Kama wanataka kuwe na kulazimisha waende mahaka zilizopo.

Nadhani hii mahakama ni hatua ya kwanza, ya ujanja ujanja, katika kutaka Tanzania itumie SHARIA LAW. Kama JK akitulazimishia hii mahakama, basi atakuwa anatutakia ugomvi wa kidini kama ilivyo huko Nigeria.
 
Kuna mambo yanafichwa. Nani atagharammia mishahara ya mahakimu na wafanyakzai wa mahakama hiyo?
Mahakama hii ikitambulika kikatiba na kuwemo katika mfumo wa serikali basi bajeti yake ni lazima ibebwe na serikali. Si mishahara tu bali hata sehemu itakapoendeshea shughuli zake itabidi serikali iiwezeshe! Na sitashangaa hao wanaodai mahakama hii watakapodai kuwa Kadhi Mkuu atambulike sawa na jaji kiongozi pamoja na stahili zake zote. Na je wakiunganishwa katika mfumo wa mahakama Kadhi Mkuu atawajibika kwa Jaji Mkuu? Au muislamu asiyeridhika na mahamuzi ya mahakama hiyo ataweza ku-appeal kwa Mahakama Kuu? Na mahakama hiyo itahusika vipi katika matatizo ya ndoa mseto?

Hakuna mtu anaepinga kuwepo kwa mtindo wa kuamua matatizo yao kidini nje ya mfumo wa serikali. Mbona wamisheni na wanaofuata imani za kiasili wanao? Wakatoliki wakipata matatizo kimbilio la kwanza ni kwa paroko. Masuala ya mirathi yalikuwa yakishughulikiwa kijamii mpaka tulipotambua kuwa mila na desturi zetu zilikuwa zikitoa upendeleo kwa upande mmoja. Lakini hata hivyo bado sehemu kubwa inashughulikiwa kijamii.

Wanachodai wenzetu ni kubadilisha mfumo huu na kuiingiza katika mfumo wa utendaji wa kiserikali ambao kwa wao wanaona ni wa kikristu. Mimi hili si kubaliani nao. Ingawa kweli mfumo wa sheria tulionao umejengwa kwenye msingi wa judaeo-christian tradition, hauna maana kuwa ni wa kikristu. Mbona astronomy na sehemu kubwa ya hisabati imejengwa kutokana na michango ya waislamu ( Thabit ibn Qurra n.k.)? Sasa wamisheni nao akatae kutumia fractions kwa sababu aliyezigundua alikuwa ni muislamu? Katika dunia ya sasa hatuwezi kudai purity. Ni lazima tutambue kuwa tumechanganyikana kwa kiasi kikubwa kwa hiyo ni wajibu wetu kuunda vyombo ambavyo havitatoa upendeleo kwa upande mmoja dhidi ya mwengine. Mpaka sasa sijasikia vipi mfumo wa mahakama tulio nao unavyomnyima haki yake muislamu. Mfumo ambamo watekelezaji wake wengi ni waislamu!

Amandla.......
 
Mkuu FM, umetoa darasa haswaa, maelezo yako yanasomeka na kueleweka vema kwa lugha rahisi na ufafanuzi fasaha. Asante sana Mkuu, Ubarikiwe.
 
Fundi Mchundo,
Mkuu unapoweka hizi Quotes zako ni muhimu unieleze vizuri una maana gani na nini solution au hoja yako inayopingana.. Wewe unatafuta mahala usipokubaliana na Quran ambayo ndio sababu zimekufanya wewe usiwe Muislaam na kuziweka hapa..Kutokuwa kwako Muislaam inatosha kukufanya wewe usiweze kuelewa Uislaam na hukubaliani na Quran laa sivyo ungekuwa Muislaam..Kama vile mimi nisivyoelewa Ukristu na yanayotokana nayo..
Kisha basi unanielezea habari za mke au mjane aliyezaa nje uka iquestion Quran wakati huna jibu kutoka Biblia wala sheria zetu..mahakama ya kadhi ni kwa waislaam wanaoamini na kufuata
mafundisho yake...
Sasa wewe nambie sheria au Biblia inasema nini kuhusisna na kesi hizo hizo ulizozisema tungalie kama ni solution kwa vizazxi vyote vya Kitanzana..Sidhani kaa unalo jibu sidhani ila unaona raha sana ku quote Quran wakati huna jibu toka Biblia wala sheria za nchi yetu..
katiba siku zote ipo ku solve matatizo ya wananchi wake iwe Waislaam wakristu au vyovyote vile na wewe au mimi hatuna haki ya kupinga kitu maadam kinatoka upande wa pili.. unless wewe una definition tofauti.. Ndio maana Mashoga wanaomba sheria yao..Wanawake wanomba sheria zao hii yote inatokana na mapungufu ndani ya katiba aidha kwa kutazama fungu moja la jamii.. sasa unataka kunambia huko San Fransisco wanakoruhusu mashoga kufunga ndoa na kubatuana (Kikatiba) wanalazimisha pia wasiokuwa mashoga wakafunge nao ndoa..au mtu mzima Ubatuliwe!... tena basi hata Mapadre/ Masheikh ni wanachama wa Jumuiya hizi lakini sijasikia mtu akiacha dini kwa sababu ya watu hawa..

Kitu msichotaka kusikia nyie ndugu zangu ni pale tunaposema katiba yetu au sheria zetu zimetokana na Ukristu..which is true, lakini ina sound vibaya kwenu. Sheria za nchi zote za Ulaya zimetokana na dini hii hivyo unapoiga sheria za Muingereza ina maana unachukua mila na desturi za Kikristu..Leo hii Somalia na nchi zinajiita za kiislaam zinaiga au zimechukua mila na desturi za Kiarabu na kuzifanya sheria.. Hilo wazi kabisa na waislaam huitwa kila majina kwa sababu tu wanakubali wanachokifanya ila Wakristu wanaojificha nyuma ya Utaifa wakitumia mila za Kizungu (kikristu) hawataki kukubali ukweli..
Ukweli utabakia kwamba nchi zote za Ulaya na mashariki ya kati walipata Uhuru wao kwa kutumia dini na ndio maana dini inahusishwa sana ktk katiba za nchi hizo tofauti na sisi.. nambie sababu iliyotufanya sisi kutumia sheria za mkoloni ambaye hatuna mila wa desturi zinazofanana..WHY...kama sii Ukristu!

Mimi nimesema sikubaliani na mahakama ya kadhi kwa sababu, mazingira yetu bado yanafuata zaidi mila na desturi zetu za kiasili ktk maswala mengi yanayohusiana na mahakama ya kadhi..Hivyo ni vizuri kuyaongeza ktk sheria zetu yale tu yanayoweza ku fit in.. na mazingira yetu. Kama wewe unapinga mke kuchukua robo ya mali nambie nini solution yake..na sio mke kufukuzwa kabisa asipewe kitu kwa sababu hajaolewa (kulingana na biblia).. ndivyo Ukristu unavyosema kama hujaolewa U have no right kabisaaa! hata kama umezaa na mume Je huu ni kweli au Uongo!.. sasa unapo question mwanamke anayeondoka na robo ukasema atakwenda wapi mbona huyo asiyeondoka na kitu humpi haki ktk hoja zako?..
 
Mkandara. Walaumu waliotafsiri Quran na kutuwekea mtandaoni. Mbona wewe unashutumu ukristu na mengi maovu (kama vile kuunga mkono madangulo, casino na kusema mke asipewe chochote anapotalakiwa) bila kuweka uthibitisho!Nilikuuliza, mbona ukristu unapinga ndoa ya mke zaidi ya mmoja lakini hizo sheria zetu zinaruhusu?

Amandla....
 
Fundi Mchundo,
Mkuu unapoweka hizi Quotes zako ni muhimu unieleze vizuri una maana gani na nini solution au hoja yako inayopingana.. Wewe unatafuta mahala usipokubaliana na Quran ambayo ndio sababu zimekufanya wewe usiwe Muislaam na kuziweka hapa..Kutokuwa kwako Muislaam inatosha kukufanya wewe usiweze kuelewa Uislaam na hukubaliani na Quran laa sivyo ungekuwa Muislaam..Kama vile mimi nisivyoelewa Ukristu na yanayotokana nayo..
Kisha basi unanielezea habari za mke au mjane aliyezaa nje uka iquestion Quran wakati huna jibu kutoka Biblia wala sheria zetu..mahakama ya kadhi ni kwa waislaam wanaoamini na kufuata
mafundisho yake...
Sasa wewe nambie sheria au Biblia inasema nini kuhusisna na kesi hizo hizo ulizozisema tungalie kama ni solution kwa vizazxi vyote vya Kitanzana..Sidhani kaa unalo jibu sidhani ila unaona raha sana ku quote Quran wakati huna jibu toka Biblia wala sheria za nchi yetu..
katiba siku zote ipo ku solve matatizo ya wananchi wake iwe Waislaam wakristu au vyovyote vile na wewe au mimi hatuna haki ya kupinga kitu maadam kinatoka upande wa pili.. unless wewe una definition tofauti.. Ndio maana Mashoga wanaomba sheria yao..Wanawake wanomba sheria zao hii yote inatokana na mapungufu ndani ya katiba aidha kwa kutazama fungu moja la jamii.. sasa unataka kunambia huko San Fransisco wanakoruhusu mashoga kufunga ndoa na kubatuana (Kikatiba) wanalazimisha pia wasiokuwa mashoga wakafunge nao ndoa..au mtu mzima Ubatuliwe!... tena basi hata Mapadre/ Masheikh ni wanachama wa Jumuiya hizi lakini sijasikia mtu akiacha dini kwa sababu ya watu hawa..

Mkandara. Mara nyingi unachanganya mambo. Utaniziuaje kuzungumzia mifano kutoka katika Quran wakati katika mahakama hayo ya kadhi, Quran ndiyo itakayotumika kufikia maamuzi? Nimekuambia kuwa dini yako ya kiislamu haimtambui mtoto aliyezaliwa nje ya ndoa na mtoto wa kufikia. Ninavyoelewa, hawa katika katiba yetu wana haki sawa na wengine ili mradi huyo mwenye hao watoto awatambue kisheria. Ukitaka nitoe mifano katika biblia kujenga hoja unakosea maana sijawahi kusema na sikubaliani kuwa katiba yetu ni ya kikristu. Kwa msingi huo biblia haina nafasi katika sheria zetu kama ilivyo Quran. Hauwezi kutumia vitabu hivyo katika mahakama zetu kama utetezi. Ndivyo inavyopaswa iwe.

Kudai kuwa mahakama ya kadhi ( unayotuambia kuwa unaipinga) ni kwa ajili ya waislamu wanaoamini na kufuata sheria zake si kweli. Ni mara ngapi waislamu wamegombea kumzika mtu wanaodai ni muislamu mwenzao wakati huyo mfu alikuwa akiishi kama mkristu? Nani atakaeamua kuwa huyu ni muislamu safi kwa hiyo anastahili shauri lake linastahili kusikizwa katika mahakama ya kadhi? Uamuzi huo utakuwaje kwenye ndoa baina ya watu kutoka dini tofauti? Haya yote mnayakwepa katika kujaribu kutudanganya kwamba kuna kitu waislamu pyua ambao ndio watahusika!

Mashoga katika nchi za magharibi ( ambazo hazijitambui kisheria kama nchi za kikristu kama unavyotaka kutudanganya) wanadai haki zao ndani ya katiba za nchi zao. Kama walivyofanya watu weusi na wanawake kabla yao. Hawadai waundiwe vyombo vyao au sheria zao peke yao bali wapewe haki sawa kama wengine. Kama sheria inaruhusu watu kuoana basi nao waruhusiwe kuoana mbele ya sheria hiyo hiyo. Ndio maana wanafungisha ndoa serikalini na si kwenye vyombo vyao wenyewe. Kama waislamu wanaona kuna haki wananyimwa ndani ya katiba basi wajenge hoja hizo sheria zibadilishwe ili kuhakikisha wanapata haki yao. Si kudai chombo mbadala. Kwa mfano ( ambao unataka kuupotosha) sheria zetu zinatambua mtu aliye muislamu au mwenye imani za kiasili kuoa zaidi ya mke mmoja. Watoto wanaotokana na ndoa hizo wana haki sawa kama vile walivyo watoto wanaotokana na ndoa ya mke mmoja. Panapotokea matatizo katika ndoa hizo, ushauri unafuatwa kutokana na maelekezo ya dini hizo. Au Mkuu unataka kutuambia kuwa ndoa au talaka iliyotambuliwa na mamlaka za kiislamu haitambuliwi katika sheria? Unadai sheria hizo ni za kikristu. Mbona dini za kikristu hazitambui talaka lakini talaka inatumbuliwe na sheria zetu? Wakatoliki wanaweza kutalakiana kisheria lakini kanisa likakataa kutambua talaka hiyo. Kwa hali hiyo hao walio talakiana hawawezi kufunga ndoa kanisani lakini wanaweza kufanya hiyo serikalini! Bado unadai kuwa hizi sheria ni za kikristu?

Mimi sijawahi kupinga kuwa sheria zetu zinatokana na judaeo-christian traditions. Huo ulikuwa ni msingi lakini wakati wa enlightenment wenzetu walipinga kanisa kuwa na sehemu katika utawala na kutenganisha sheria hizo na ukristu. Wakina Galileo walisakamwa sana kwa kudai kuwa dunia ni mviringo na inazunguka jua, kitu kilichoonekana kupinga maandiko yaliyomo katika biblia. Ndiyo maana nchi nyingi za magharibi zinaruhusu utoaji wa mimba na haki sawa kwa mashoga n.k. vitu ambavyo wakristu safi wanapinga sana. Au unadhani aliyempiga risasi yule daktari mtoaji mimba alikuwa muislamu?

na sio mke kufukuzwa kabisa asipewe kitu kwa sababu hajaolewa (kulingana na biblia).. ndivyo Ukristu unavyosema kama hujaolewa U have no right kabisaaa! hata kama umezaa na mume Je huu ni kweli au Uongo!.. sasa unapo question mwanamke anayeondoka na robo ukasema atakwenda wapi mbona huyo asiyeondoka na kitu humpi haki ktk hoja zako?..

Wapi panaposema hivi katika biblia? Biblia inakataza watu kujamiana nje ya ndoa. Lakini haizungumzii namna haki ya walio katika ndoa ( au nje ya ndoa) katika mirathi. Biblia si Quran. Biblia inasema siku moja upumzike na kumuabudu Mungu wako bila kukupangia muda au mara ngapi ufanye hivyo. Quran inakupangia muda, mara ngapi na uelekee wapi wakati unamuabudu muumba wako. Sheria zetu haziruhusu mtu kumfukuza mwenzie bila kumpa sehemu ya walichochuma pamoja. Jaribu kufanya hivyo katika nchi za magharibi uone yatakayokupata. Kukwepa hilo, ndiyo maana wenzetu wana pre-nuptial agreements. Hata hivyo kama upande mmoja utaonekana kudhulumika, mahakama itaweza kuweka pembeni hayo makubaliano ili haki ifanyike. Watafanya hivyo bila kujali dini ya mhusika. Kwetu wengi wanaowadhulumu wakina mama wanafanya hivyo kwa misingi ya mila na utamaduni na wala si ukristu.

Waislamu hamuwezi kudai kuwa wakristu wasichangie katika mjadala huu maana hatma ya nchi yetu inatuhusu wote. Na gharama za hiyo mahakama tutazibeba sote, wakristu na waislamu. Kwa hali hiyo ni haki yetu kupinga kwa sauti kubwa kama ilivyo haki yenu kutetea kwa kadri ya uwezo wenu. Hoja zote zikiwekwa wazi, ndipo uamuzi ufanyike. Kutaka kutulazimisha ati kwa vile si dini yetu hatutakubali. Kamwe.

Amandla......
 
Last edited:
A section of Christians have opposed the anchoring of Kadhi courts in the new constitution.

The Evangelical Alliance of Kenya (EAK) said Islam was like any other religion in the state and having Kadhi courts entrenched in the constitution would be seen as special treatment.

“Kadhi courts should never be entrenched or enhanced in the constitution. They should be governed by Act of Parliament just like other churches are,” said EAK General-Secretary Wellington Mutiso at a press conference in Nairobi.

EAK threatened to mobilise its Pentecostal churches and development agencies members into voting against the draft constitution once it gets to the referendum stage.

The Alliance is the umbrella body for many Pentecostals, charismatic and evangelical development agencies in the country.


The church leaders were reacting to Monday's meeting between Justice and Constitution Affairs Minister Mutula Kilonzo and Supreme Council of Kenya Muslim (SUPKEM).

At the meeting the minister had assured SUPKEM that Kadhi Courts will be entrenched in the constitution.

This would mean that the Kadhi Courts would be separated from the mainstream Judicial system.

The Pentecostal leaders argued this would create a parallel Judicial system and would imply that the state was enhancing religious practices and spending tax payers money to finance the Chief Kadhi.

This would work against national unity and cohesion as the other would feel discriminated against, they added.

“The courts we have are able to settle disputes between people of all religions, customs and traditions,” the secretary-general read in a statement by EAK Bishops Bonifes Adoyo and Stephen Kabachia.

Quoting the Bomas draft Art 10, they said the statement by the minister was contradictory to the provision which bars any preferential treatment of any religion.
 
Last edited by a moderator:
This would mean that the Kadhi Courts would be separated from the mainstream Judicial system.


The Pentecostal leaders argued this would create a parallel Judicial system and would imply that the state was enhancing religious practices and spending tax payers money to finance the Chief Kadhi.

Parallel Judicial system? What will be next?
 
Haya sasa, kumekucha nako huko Kenya. Hope wamesikia jirani zao TZ tunavyoipinga hii mahakama ya kazi. Wapinge kwa kweli haifai maana inakula pesa za walipa kodi wa dini zote kitu ambacho ni sawa na unyonyaji wa aina yake. Na mahakama yenyewe ni ya kunufaisha wanaume tu pale kunapotea tatizo linalowahusisha mwanaume na mwanamke
 
inabidi waafrika tuache upumbavu wa kugeza mambo ya kiarabu na kuangalia mambo ya maendeleo..kadhi ndo upuuzi gani..si mkaish uarabuni mnaotaka..msitake kuleta utamaduni wa waarabu kwetu..mahakama zilizopo zinatosha..
 
Kadhi courts should never be entrenched or enhanced in constitution of any country which is not Islamic.
 
Hawa jamaa ni wajanja sana. Muda si mrefu utasikia kuwa Kenya ni nchi ya Kiislamu. Afadhali baadhi yao wameshtukia mkakati huo!
 
Na Leon Bahati, Dodoma (Mwananchi)

SERIKALI imetoa msimamo wake kwamba, Tanzania haitaunda Mahakama ya Kadhi na badala yake itatafsiri sheria za Kiislamu na kuzijumuisha kwenye sheria za nchi, ili zitumike kwenye mahakama za kawaida hapa nchini.

Uamuzi huo wa serikali unatokana na mapendekezo yaliyowasilishwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Tume ya wataalamu waliochambua mapendekezo ya utafiti uliofanywa na Kamati ya Kurekebisha Sheria.

Hata hivyo, uamuzi huo wa serikali ulipingwa vikali na Mbunge wa Kigoma Kusini, Manju Msambya (CCM), ambaye alisisitiza kuwa haoni kosa kwa Waislamu kuundiwa mahakama hiyo.

Msimamo wa serikali ulitolewa bungeni jana na Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe wakati akiwasilisha makadirio na matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2009/10.

Hata hivyo, Chikawe alisema mchakato wa kufikia hatua ya kuzijumuisha sheria hizo za Kiislamu kwenye sheria za nchi lazima upate maoni kutoka kwa madhehebu yote ya Kiislamu nchini.

''Hivi sasa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imeanzisha mchakato wa kukusanya mawazo na maoni kutoka kwa viongozi wa madhehebu yote ya dini ya Kiislamu kwa nia ya kuorodhesha misingi ya dini ya Kiislamu, hususan ile inayohusu sheria binafsi kwa madhumuni ya kuihuisha misingi hiyo katika sheria za nchi, kwa kuzingatia sheria ya The Islamic Law Act, sura ya 375 ya mwaka 1964,'' alifafanua Chikawe na kuongeza:

''Kimsingi baada ya viongozi hawa wa dini kukubaliana kuhusu misingi hii, basi Waziri wa Sheria atatoa tamko kuhusu misingi hiyo na baada ya hapo kwa mujibu wa Ibara ya tatu ya sheria hii, matamko haya yatakuwa ni sheria zitakzotambuliwa na mahakama zetu zote hapa nchini.''

Alisema lengo la serikali la kutumia mfumo huo ni kuweka utaratibu utakaolinda haki za waumini wa Kiislamu bila kuathiri misingi ya Katiba ya nchi.

Chikawe alisema utaratibu kama huo umekuwa ukitumika nchini Afrika Kusini ambako kuna waumini wengi wa Kiislamu na imeonyesha mafanikio.

Akichangia hotuba hiyo, Msambya alipinga utaratibu huo wa serikali na kutaka serikali iunde moja kwa moja mahakama za kadhi ili kutatua matatizo yahusuyo waumini wa Kiislamu.

Vilevile, Msambya alitaka Tanzania ijiunge na Jumuiya ya Uislamu Duniani (OIC), kwa kile alichoeleza, nchi itafaidika kwa mambo mengi kama ilivyo Uganda na Msumbiji.

Katika hatua nyingine, Msambya alilishutumu Kanisa Katoliki nchini kwa kutoa waraka ambao unawafundisha waumini wake kuhusu namna ya kuchagua viongozi bora.

Waraka huo wa Kanisa Katoliki ulikuwa unawaasa waumini wake wasiwachague viongozi ambao wana tabia ya kubadilika badilika kama kinyonga.

Msambya ambaye hakutaja moja kwa moja dhehebu la dini lililotoa waraka, alisema unapingana na kanuni kwamba watu wasichanganye dini na siasa.

Akizungumza kwa jazba, Msambya alisema alichukizwa na kitendo cha waziri ambaye hakumtaja, kwamba alipoulizwa na waandishi wa habari kuhusiana na waraka huo, aliusifu akisema ni mzuri kwa sababu ni moja ya elimu ya kupiga kura.

Hoja ya kuwepo kwa Mahakama ya Kadhi ilianzishwa wakati wa serikali ya awamu ya tatu lakini ilizimwa, kisha ikafufuliwa tena miaka mitatu iliyopita na kuwagawa wanasiasa na wananchi katika makundi mawili. Wako waliounga mkono na wengine waliipinga kwa maelezo kwamba itasababisha vurugu na mgawanyiko katika jamii.


Maswali:
- Kwa kuingiza baadhi ya sheria za dini ya Kiislamu katika sheria za nchi kunaondoa haja ya kuwepo mahakama ya kadhi? Yaani, mahakama za kawaida zitumikee kufanya kazi ya mahakama za Kadhi?

- Je, mahakama za kawaida za nchi zinapotoa hukumu kwa mujibu wa kufuata sheria za Kiislamu je Muislamu analazimika kutii hukumu hizo kana kwamba ni za mahakama ya kidini?

- Je adhabu zitakazotolewa kwa mtu anayevunja sheria hizo mpya zitaendana na adhabu zinazotolewa kama ingekuwa ni mahakama ya Kiislamu?

- Kwa vile sheria hizo zitaingizwa kwenye sheria za kawaida za nchi, je zitawahusu vipi wananchi wengine? Kama zitawekwa kwa ajili ya waislamu tu je hicho si kinyume na Katiba ambapo mamlaka ya nchi inapitisha sheria za kibaguzi (moja za wananchi wote na nyingine za waislamu tu)?

- Kwanini serikali isiamue kuweka mazingira ambapo Mahakama ya Kadhi inaundwa na Waislamu wenyewe kwa misingi ambayo wao wanaikubali na pale ambapo kunahitajika msaada wa serikali basi ijulikane ni kwa vipi na kwa namna gani?
 
Duh...naona bado mambo hapa mabichi kabisa, tunaendelea kuahirisha tatizo...

Kwa vile sheria hizo zitaingizwa kwenye sheria za kawaida za nchi, je zitawahusu vipi wananchi wengine? Kama zitawekwa kwa ajili ya waislamu tu je hicho si kinyume na Katiba ambapo mamlaka ya nchi inapitisha sheria za kibaguzi (moja za wananchi wote na nyingine za waislamu tu)?

apo ndo mtego ulipo!
 
Kwa kifupi hii ni janja ya CCM hawana mpango wa kuleta sheria za aina hiyo maana kesi ya katiba kuvunjwa na ubaguzi zitafunguliwa .Walijua kwamba Mrema alitaka kuwaingiza kwenye mtego wa kuigawa Nchi na wamesha amka sasa na wameamua mapema ili wahukumie kwenye uchaguzi ujao .Hakutakuwa na jambo kama hilo hata baada ya maoni ya waislam .
 
Sasa sheria za waislamu ziingizwe kwenye katiba ya nchi ina maana hata wasio waislamu wata hukumiwa na sheria hizo hizo? Na Tanzania si tunadai ni secular state sasa sheria za dini zitageuzwaje kuwa sheria za nchi? Na je wakianzisha mahakama ya kiislamu hiyo haitaonekana na upendeleo iwapo itagundulika adhabu za moja wapo ya mahakama(aidha ya nchi au ya kiislamu) ni nzito au nyepesi kuliko ya mahakama nyingine? Kuna ulazima wa waislamu kuwa na mahakama yao wenyewe na wata hakikisha vipi sheria zao hazitaingiliana na sheria za nchi? Tatizo watanzania tuna kimbilia kujiingiza kwenye mambo. Hapa kuna baadhi ya watu watakuja na kusema oh mbona nchi fulani wana mahakama ya serikali na ya kiislamu?! Tusi kimbilie kuingiza vitu ambavyo haviendani na hali yetu kwa ajili ya kuridhisha tu baadhi ya makundi ambao wao kila siku wanaona tu kuwa wanaonewa au wenzao wana pendelewa.
 
Back
Top Bottom