Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Mkandara,

Kikwete did not run on introducing sharia law into Tanzania. Alificha sana msimamo wake.

Can a wrong become a right "because Kikwete espoused it while he was running"? Kwani ni lazima Wislamu wasimike mahakama yao serikalini? Kwanini wasianzishe tu bila kuifanya sehemu ya serikali?

Waislamu wanataka mahakama ya kadhi iwafunge wakosaji Keko? Wanataka mahakama hiyo itumie polisi wa serikali? Wanataka mahakimu wake walipwe na seriakali? Kwa nini wanataka kulazimisha asasi ya kidini iwe sehemu ya serikali?

Wanadini wapeleke mashitaka ya kidini kwenye mahakama za kidini bila kutumia serikali au kupitia serikalini.

Serikali ya Tanzania si ya dini na haina dini. Litakuwa kosa baya kama serikali italazimishwa, na Rais wake pamoja na mabwana ndio wachache, kuikubali mahakama ya kidini iwe mahakama ya kiserikali
 
This issue, in my opinion is being used by the CCM government as a "red herring" so as to divert the attention of Tanzanians from EPA, Richmond, Kagoda, Kiwira scandals that otherwise would weaken the CCM government.
If the govt is so keen to solve people's problems and keros why do they keep quiet in so many issues that wananchi feel, and need solutions? How many times have opposition MPs, and in some cases even some CCM MPs have requested issues of great importance to this nation's debate be discussed and the Govt has dodged?
Tanzanians, don't be duped into discussions that will eventually divide Tanzanians (religious, tribal) and benefit nobody than those who want to divert national attention into scapegoat debates!! (sponsored by ineffective leaders)
 
Augustine Moshi inaelekea ni mjinga wa maana ya mahakama ya kadhi kwahiyo unahitaji kuelezwa kwa kina kwani unaonekana you are ill informed about it ndo maana unatoa maoni yasiyo na mashiko na hilo limekuwa tatizo lenu!walioiweka kwenye Ilani sio wehu!
 
Mzee mwana kijiji unaongea pumba kuhusu mahakama ya kadhi nyamaza!

Wewe point zako ziko wapi? ama umesahau this is JF tunapo thubutu kuongea kwa uhuru na uwazi?, Kama yeye kaleta pumba, wewe mwaga mchele, lakini we si kiranja humu ndani wa kuchagua nani kaleta jema na nani kaleta baya.. kama waona pumba ruka hoja zake hulazimishwi kuzisoma.

By the way, Mahakama ya kadhi ianze tu hata leo hii, lakini kivyao vyao.. si kwa mgongo wa serikali hapo hamna gogoro.
 
Augustine Moshi inaelekea ni mjinga wa maana ya mahakama ya kadhi kwahiyo unahitaji kuelezwa kwa kina kwani unaonekana you are ill informed about it ndo maana unatoa maoni yasiyo na mashiko na hilo limekuwa tatizo lenu!walioiweka kwenye Ilani sio wehu!

Hizi lugha ndo zinatufanya tunaiogopa mahakama ya kadhi kama ukoma. Watu wenyewe hamuaminiki mihasira nje nje na hamchelewi kujilipua kwa mabomu. Tunawahurumia akina mama maana ndo watakuwa wahanga wakubwa wa hii mahakama huku midume ikichekelea tu. Mahamakama ya kadhi Tanzania "a big NO". Kisingizio eti walioiweka si wehu, kwani waliwauliza watanzania wakawakubalia? Si ilikuwa janja yao ya kutafuta kura tu. After all wapiga kura wengi wako vijijini na ukienda kuwauliza kwamba, jamani mnafahamu kuwa CCM waliahidi mahakama ya kadhi wakichaguliwa, watakwambia hicho kitu hawakijui wala hawajawahi kusikia. Na kusema kweli hili suala halikuwa wazi kwani hata mimi niliipigia kura CCM na kitu kama hicho sikuwahi kukisikia vinginevyo nisingewapa kura yangu.

Kinachonishangaza zaidi ni kwamba; kwani mmeshindwa kuwafundisha watu wenu maadili mema waishi kwa hayo na kama hawataki kwanini mnataka kuchukua nafasi ya MUNGU kutoa hukumu? Maana hili ni suala la dini. Nje ya dini tuache mahakama za kawaida zifanye kazi zake.
 
Niliona link ya ripoti ya Bunge kuhusu mfumo wa Mahakama ya Kadhi kwenye website ya Bunge la Tanzania ila haifunguki. Kuna mtu anaweza kutupa ripoti hiyo ili tuijadili? Maana hatujui Bunge limesemaje juu ya jinamizi hili la Mahakama ya Kadhi linalotaka kuharibu amani ya nchi yetu!
 
Augustine Moshi,
Mkuu una hakika au unazungumza tu ili mradi..
Kati ya ahadi za Kikwete ambazo ni controversial na hazikubaliki ni pamoja na OIC, mahakama ya kadhi na Muafaka wa Zanzibar...sema hakuzifanyia kampeni kwa sababu maalum..Watu wengi walifahamu hilo na nadhani hapa JF (Jamboforums) kabla ya uchaguzi tulizungumzia sana.. hii thread ni ya pili labda tu hukumbuki..usione kurasa nyingi ukafikiria ndio kwanza tunalizungumzia.

Kitu kimoja tu ambacho nitaendelea kusema ni kwamba sisi Wadanganyika ni wapumbavu wa kutupwa tena sii kidogo hata elimu zetu bado ni za kikabila, kidini na kadhalika.. Ebu mkuu wangu soma huko nyuma watu wanavyotukana Uislaam! inahusu nini kuyasema haya yote wakati mimi nina sababu nyingi na za msingi kwa nini sijawa Mkristu..
Ni imani yangu mimi na haihusiani kabisa na kutoa maneno machafu kisha ati tunajiita sisi wote ni Watanzania..Kwa misingi gani?..
Binafsi napinga mahakama ya kadhi kama Muislaam kwa sababu ya malengo yake kutimiza wajibu wa dini ktk mazingira yasiyokubalika..Wengi wetu ni waislaam na wakristu kwa majina na sii ibada..
Kwa mfano sidhani kama kanisa litakuwa linawatendea haki Wakristu ikiwa wataanzisha mahakama inayohusiana na Poligamy.. wazee wetu wengi wakristu wana wake zaidi ya mmoja hivyo sheria hii itaweza vipi kufanya kazi ktk jamiii ambayo haifuati dini kama msingi wa maisha yao..Hivyo Mapadre wanaweza kabisa kuona kila sababu ya kusimamisha sheria hiyo lakini sidhani kama wananchi wapo tayari..Sasa maadam sikubaliani na wazo hilo nianze kumtukana Yesu, kwa matusi mazito yasiyobebeka, kweli hii ni akili jamani..
Je inatokana na kuwakomoa au kuleta suluhu...

Mambo mengi yanayohusiana na mahakama ya kadhi yataleta ugonvi mkubwa sana katika familia nyingi za Kiislaam. Kuna watu wamezaa nje ya ndoa, kuna wale waliooa wake/waume sii waislaam. Na kikubwa zaidi mambo yote haya yana watoto ambao ndio hasa wanatakiwa kutazamwa iwe mirathi au lolote lile.. Kikubwa zaidi dini iendelee kufundisha waumini wake, wajihadhari na kufuru au matendo yasiyokubalika ktk dini lakini huwezi kusimamisha sheria kwa watu wasiofanya ibada..
 
Augustine Moshi,
Mkuu una hakika au unazungumza tu ili mradi..
Kati ya ahadi za Kikwete ambazo ni controversial na hazikubaliki ni pamoja na OIC, mahakama ya kadhi na Muafaka wa Zanzibar...sema hakuzifanyia kampeni kwa sababu maalum..Watu wengi walifahamu hilo na nadhani hapa JF (Jamboforums) kabla ya uchaguzi tulizungumzia sana.. hii thread ni ya pili labda tu hukumbuki..usione kurasa nyingi ukafikiria ndio kwanza tunalizungumzia.

Mkuu Mkandara Kikwete angepiga kampeni kwa ahadi ya OIC na mahakama ya Kadhi, hangeiona hiyo milango ya Ikulu.

Sasa maadam sikubaliani na wazo hilo nianze kumtukana Yesu, kwa matusi mazito yasiyobebeka, kweli hii ni akili jamani..

Lakini Mkuu, mbona hayo unayoita matusi yameporomoshwa kutoka pande zote ? Hebu shuhudia hii ya leo
Augustine Moshi inaelekea ni mjinga wa maana ya mahakama ya kadhi kwahiyo unahitaji kuelezwa kwa kina kwani unaonekana you are ill informed about it ndo maana unatoa maoni yasiyo na mashiko na hilo limekuwa tatizo lenu!walioiweka kwenye Ilani sio wehu!
 
- Hivi sisi wananchi wenye elimu na tumeona mengi sana kwenye dunia, na tuko hapa kuwapa usahuri kila siku kuanzia viongozi wetu mpaka wananchi, ni lina tutaweza ku-overcome udini? Ukabila na undugunization?

- Ni lini tutaweza kujadili dini katika siasa za taifa letu, bila kukwaruzana?

Respect.

FMEs!
 
Mag3,
Mkuu unajua kumtukana mtu ambaye ni mwanabofdi hii ni vitu vilwili tofauti na kumtukana mtume au dini usiyoabudu..Uzito ni tofauti kabisa pamoja na kwamba sikubaliani na mawazo ya mwandishi..Pamoja na yote haya Mjinga au Ill imformed sii matusi, tatizo ni lugha yetu na kutokubali kuitwa mjinga kwani fikra zetu sisi tuna elimu ya kila kitu..Kiswahili chetu kimetafsirika vibaya,i Mjinga ni mtu ambaye hana elimu inayohusika, hivyo katika maswala ya dini kweli hata mimi mjinga.... mjinga kweli kwa mambo mengi sana..siwezi bishana na Daktari kuhusiana na ponya ya magonjwa..Hata hizi siasa za Bongo mimi bado mjinga tena sana ndio maana kila siku utanikuta hapa JF kupata darasa..
Mwisho mkuu ni kweli Kikwete asingeweza kutumia ahadi zile ktk kampeni yake na wala hakuwa na haja kwani sisi hatukuwa na maswali zaidi ya kutazama sura yake.. Kama vile unavyompenda demu, maswali mengine huja baada ya kumweka sawa...
 
Mimi namshukuru Mkandara. Anataoa hoja zake kistaarabu. Ni kawaida yake.

Kwa kweli kwenye Uislamu mimi ni mjinga. Naomba kueleweshwa yafuatayo;

1. Mwislamu akivunja amri ya dini yake anaweza kukamatwa na kufikishwa Mahakama ya Kadhi? Kama sio lazima akamatwe kwanza basi yanini kutaka iwe na nguvu za kiserikali?

2. Adhabu zinazoweza kutolewa na Mahakama ya Kadhi ni zipi? Zinapingana na sheria za nchi? Inaweza kumfunga mtu? Inaweza kuamuru mtu apigwe mawe au akatwe mkono?

Naona Mkandara umeashiria kwamba Mahakama ya Kadhi itaweza kutumika dhidi ya wazinzi. Kama hivyo ni kweli basi Wabunge wetu walio Waislamu, na hata JK mwenyewe, hawataiogopa?

Mkandara naomba unijibu swali la msingi (nakuuliza wewe kwani unajibu kistaarabu, bila matusi): Ni kwanini Mahakama ya Kadhi lazima iwe sehemu ya serikali? Hukumu zake zinaweza kuwa incompatible with the law of the land?
 
Augustine Moshi,
Shukran sana na heshima iwe juu yako mkuu..
Mahakama ya kadhi mkuu ni sawa na civil court haina maswala ya jinai ama kutoa hukumu inayohusiana ufunjaji wa sheria za dini isipokuwa ni kutoa suluhu pale wafuasi wawili wa dini wanapotaka sheria itumike ktk kutoa suluhu fulani..

Na nijuavyo mimi hizi korti zimekuwepo hata kabla ya Uislaam nikiwa na maana ni korti za jadi za Kiarabu ambazo zilikuja chukua baadhi ya maagizo ya dini na kuyaweza kuwa mila na tamaduni za waislaam wote. Kama vile Ukristu na sheria tunazotumia ktk Civil korti hukumu nyingi zinafuata maisha na mafundisho ya dini yakichukua baadhi ya tamaduni na mila za wazungu ktk mazingira yao..

Moja ya sababu kubwa ni kwamba kuna mambo mengine ambayo sheria iloandikwa hayawezi ku solve hatya kama utafikiria vipi isipokuwa hekima na busara ndizo hutumika zaidi na zimeweza kuchangia sana ktk muundo wa mahakama kama hizi..
Nitakupa mfano mmoja toka ktk hadith (non fiction events) za Kiislaam..Lakini unajua nini?.. nitawauliza nyie msokuwa waislaam mjaribu kujibu kutroa suluhu ya swla kama hili kiasi kwamba pande mbili zisizokubaliana sifikie suluhu..Nitaibadilisha kidogo tu yaani iweze ku fit na mazingira yetu..

Chukulia wewe ni mzee wa kijiji huko Usukumani.. Ni mfuga mifugo una ng'ombe wako kibao na unaaminiwa sana kwa hekima na busara hapo kijijini...
Imetokea kwamba kuna mzee anakaribia kufa na kabla hajafa alikuita na kuacha Usia kwamba Akifa mali zake - ng'ombe 17 wagawanywe kama ifuatavyo kwa watoto wake watatu..
1. Mtoto mkubwa atachukua 1/2, anayefuata apewe 1/3rd na mdogo kabisa atapewa 1/9th ya hesabu ya hao ng'ombe..

Sasa wewe kama msomi, mwenye hekima na Busara huyo mzee kafa, watoto wake wamekufuata ufanye suluhu ya swala hili.. Utawagawa vipi hawa ng'ombe 17 kwa watoto watatu kama alivyoagiza marehemu!..Huu ni mfano tu ktk kukupa hekima ya dini...
 
Noamba unieleweshe ni kwanini Waislamu wanataka kuihusisha serikali katika kuanzisha Mahakama ya Kadhi.

Wazee wengi vijijini sehemu nitokayo wakiwa na matatizo ya ndoa wanakwenda kwa kiongozi wa dini (Padri). Shughuli za suluhu za kidini hazihitaji ziwe za kiserikali.
 
Augustine Moshi,
Sii swala la sababu gani ila ni kufahamu kwamba hukumu inayotolewa hapa inakubalika kitaifa na sii mtu huyo aende tena mahakama za serikali na kutafuta maamuzi yanayoppingana na sheria ya dini.
kama nilivyosema civil court zimefuata sheria nyingi za dini ya Kikristu.. hilo kubali kwanza mkuu..Hivyo sii rahisi watu kwenda kwa Padre kwa maswala kama haya ila huenda kupata Ushauri na mtu anaweza kufuata au asifuate..Mara nyingii sana watu huenda kwa Padre kwa maswala ya Unyumba, matatizo ya mtoto asiyesikia au vitu ambavyo vinahitaji rehma za kiongozi huyo..Lakini huwezi kukuta watu wanagombania mirathi ya ng'ombe wakamfuata Padre ambaye hana ufunuo ama maagizo yanayompa nguvu kisheria kuwagawa hao ng'ombe..Lakini basi ikiwa kasoma hadithi kama hii ityamwezesha Ku solve hilo tatizo kwani sii lazima awe Muislaam/Mkristu kupatanisha watu..
Kifupi ni kwamba Uislaam ni kwetu sote tunaoamini haki na usawa, haijalishi hioli jina la mahakama ya kadhi kuwa tatizo kwa wasioamini Uislaam.. na ukitazama vitu vingi wanavyosimamia mahakama ya kadhi ni vitu vinavyotusumbua sana, sisi wote Waislaam kwa wakristu isipokuwa kila mmoja wetu huchukua approach tofauti kutokana na kutokuwepo mwongozo.
Sasa kama hao ng'ombe hawakugawanywa inavyostahili, hawa ndugu watapoteza udugu wao na pengine kuuana kitendo ambacho kimeshindikana kupatiwa suluhu kisheria..

Hivyo basi nitakupa jinsi Imam Ali Ibn Taalib alivyofanya.....
Mkuu wangu alimchukua ng'ombe wake mmoja akawapa watoto hao wakapata ng'ombe 18 kisha akawagawa kama will ya baba yao ilivyosema.. Yaani sasa wana ng'ombe 18 (17+1)..
- Mkubwa akachukua wake 9 = 1/2 ya 18
- Anayefuata akachukua wake 6 = 1/3 ya 18
- Na mdogo akapata 2 = 1/9 ya 18

Jumla yake ni ng'ombe 17 = (9+6+2)

Mzee akachukua ng'ombe wake alobakia kamaliza Ubishi..
Laa sivyo hawa watu wangechinjana kwa mali ya Urithi......sii swala ya imani ya dini zao tena..
 
Hivyo basi nitakupa jinsi Imam Ali Ibn Taalib alivyofanya.....
Mkuu wangu alimchukua ng'ombe wake mmoja akawapa watoto hao wakapata ng'ombe 18 kisha akawagawa kama will ya baba yao ilivyosema.. Yaani sasa wana ng'ombe 18 (17+1)..
- Mkubwa akachukua wake 9 = 1/2 ya 18
- Anayefuata akachukua wake 6 = 1/3 ya 18
- Na mdogo akapata 2 = 1/9 ya 18

Na kama hauna ng'ombe?

Amandla.............
 
Fundi Mchundo,
Na kama hauna ng'ombe?

Mkuu hekima iliyopo katika mfano huu ndiyo inayo apply kwa mahakama ya kadhi..Ukiwa huna Ng'ombe ina maana wewe siii mfugaji huwezi kuamua mambo ya wafugaji.. Ndilo swala la Waislaam kudai mwamuzi awe mwenye ng'ombe pia..
Katika mtazamo wangu nasema sii lazima swala la Maamuzi mengi ya nchi yetu yatokane na dini bali hali halisi ya wananchi na sii dini (ufugaji) kwani waislaam wengi leo hii sii wafugaji tena..

Wakati huo huo swala la mgao kama huu hauhitaji uwe na ng/ombe maadam wapo wafugaji jirani unaweza kwenda azima mmoja..Korti zetu (civil court) zinaweza kabisa ku apply baadhi ya sheria toka dini ya Kiislaam ikiwa tu zina fit na society nzima hasa ktk maswala ya urithi na ndoa zaidi ya mke mmoja..Wapo wakristu na pagani walio na mke zaidi ya mmoja, watoto waliozaliwa nje ya ndoa na kadhalika...

Wakuu nitarudia tena kusema tusiwe tunapinga vitu tu kwa sababu waoadai ni Waislaam wakati tupo tayari kusikiliza na kupitisha ndoa za Kishoga ktk sheria zetu...Ama tumeweka sheria ndani ya katiba yetu kupinga ndoa za Kishoga wakati nchi nzima sii ya mashoga..
Hivyo swali kama la Mh. Moshi, kwa nini waislaam wanataka kuihusisha serikali ktk mambo yao naweza kuuliza pia kwa nini serikali inajihusisha na mambo ya mashoga! sisi wote sii washoga!..
 
Back
Top Bottom