Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Hizo sheria za secular nani kakwambia ni zetu?, wacha ziwekwe sheria zihukumu waislamu wapendavyo wao kuhukumiwa nyinyi ambao si waislamu inauma nini?
Nakubaliana na watu kuwa hiyo ni danganya toto'
 
Hivi kwa nini CCM hushindwa kutekeleza ilani zake baada ya uchaguzi? Hili suala la kadhi lilipewa kipaumbele ili Waislamu waunganike waipe kura CCM. Wameshapata kura, sasa wanasema tutaingiza sheria za Kiislamu kwenye sheria za nchi. Wapi maisha bora yaliyoahidiwa na CCM kwa kila Mtanzania? Kila kukicha ni vilio tu kuanzia Nyamongo hadi Bulankulu. Ni lini Watanzania watagundua uhuni wa CCM ?
 
Acha vioja wewe maisha bora huyaoni huduma zinaboreshwa huoni vyuo vinajengwa mabarabara yanajengwa mashule we uko wapi iyo huduma bora unayoitaka ni ipi unataka uletewe kiroba cha mapesa nyumbani kwako
 
Mkuu Mzee Mwanakijiji,
nadhani utakumbuka kwamba hata mimi nilipendekeza sana sheria hizi za kiislaam kuingizwa ktk sheria zetu badala ya mahakama ya kadhi na na sababu nilizitoa kwa pande zote mbili..
Ajabu umekuja na maswali ambayo nashindwa kuelewa unachojaribu kujenga hapa..
Kwanza kabisa tulisha sema kwamba Mahakama ya kadhi ni sawa na Civil Court inayo deal na kesi (maswala) za MADAI na siii Criminal cases kama mnavyotaka kuzipamba hoja zenu..
Hivyo maswali yako yote hayana nguvu kama utazingatia ni kitu gani kinachuhusiana zaidi na mahakama ya Kadhi..
Kwa mfano ukiwa una wake zaidi ya mmoja nini haki ya mke wa pili na wa Tatu..Sidhani kama wewe unaweza kunijibu.. na huwezi kumjibu hata Musuguli ambaye kaoa wake zaidi ya mmoja kwa kufuata mila na desturi za kabila lake..
Hapa kama wewe Mkristu swafi, nasema tena SAFI, sheria hii haiwezi kukufiokia kwa sababu utakuwa na mke mmoja tu. Ila hata wale wasiokuwa waislaam maadam wameamua kuona mke wa pili au tatu basi hawa wote waktakuwa na haki zao kwa mume aliyewaoa..Hii ni pamoja na watoto wote waliozaliwa ktk ndoa hizo. Kukataa kuwepo kwa sheria kwa sababu tu mnaona jina Kiislaam ni kutofikiri nje ya box la Udini..Kumbuka hata wale unaowaona sii wakristu wanataka sheria pamoja na kwamba dini au mila zao zinawaruhusu..

Kwa hiyo hofu yako ya hukumu na kufikiria sijui waktakatwa mikono au kupigwa mawe haihusiani pamoja na kwamba hata wakristu wakati wa Yesu walitumia adhabu hizo hizo za waislaam mnazozikataa leo. Kifupi hakuna aya wala sura inayokataza hukumu za kiislaam ambazo zimetumika toka enzi ya Ibrahim, hivyo madai yan kwamba hizi ni hukumu za mahakama za Kiislaam ni uzushi ambao mnashindwa kukubali Ukristu wenu wenyewe..

Kifupi mimi naunga mkono sana fikra hizi na labda shida kubwa itakuja pale ambapo kuna watoto nje ya ndoa.. Hapa ningeishauri serikali kutunga sheria ambayo itawabana wazzazi hasa wa kiume kuchukuwa responsibility ya mzazi pindi mtoto atakapojukana mzazi wake ni nani bila kujali swala la ndoa au laa..

Halafu kulingana na taarifa ya taasisi ya DNA imegundulika kwamba kati ya watoto 10 wanaozaliwa, sita huwa sii wa baba aliyejulishwa.. Hii ikiwa na maana ni asilimia 60 ya watoto hufungiwa baba mzazi (biological father)..Inabidi kila penye mashaka DNA ifanyike mapema kuweza kuepuka mgogoro baadaye..
Nje ya hapo mkuu ningependa sana uelewe kwanza nini mahakama ya kadhi kisha jenga hoja zako zinazohoji kesi au swala linalokutatiza toka mahakama hiyo na sii kuhoji tu mahakama kwa sababu ina jina la Uislaam.
 
Tuvunje mahakama ya nchi. Sasa kuna haja gani ya kuwa na mahakama ya kiislamu na kusiwe na mahakama za madhehebu mengine katika nchi moja?
Mkuu mahakama ya madhehebu mengine tunayo.. Kila sheria ktk mahakama zetu ndogo zinafuata misingi ya Kikristu..Sema tu haikusemwa hivyo.
 
Tuvunje mahakama ya nchi. Sasa kuna haja gani ya kuwa na mahakama ya kiislamu na kusiwe na mahakama za madhehebu mengine katika nchi moja?

Ndiyo maana hata mimi napinga huko kuwepo na mahakama ya dhehebu au dini yoyote mkuu. Maana mahakama ina linda sheria za nchi. Kwa maana hiyo ikisha vunjwa mahakama ina maana haina maana tena ya kuwa na Bunge ambalo kazi yake kubwa ni kutunga hizo sheria. Na Bunge lisipo kuwepo basi pia ina maana hamna haja ya kuwa na serikali. Unaona implications za wazo lako?
 
Mwnafalsafa1,
Kwanza nakuuliza unazijua sheria za dini ya Kikristu?..Nipe mojawapo kisha tutaendelea maanake nisije kuwa naandika vitu kuanzisha zogo tu.
 
Mwnafalsafa1,
Kwanza nakuuliza unazijua sheria za dini ya Kikristu?..Nipe mojawapo kisha tutaendelea maanake nisije kuwa naandika vitu kuanzisha zogo tu.

Mkuu sheria za kikristu ni nyingi sasa unataka nitaje moja baada ya nyingine kivipi mkuu? Mimi ni Mkristo kwa hiyo wewe ndiyo useme sheria hii ya mahakama ni ya kikristo. So naomba unielimishe zaidi mkuu. Sheria zipi za mahakama ni za Kikristo? Nauliza tu ili kujua mkuu wangu.
 
Huu ndiyo wakati wa kuiondoa CCM madarakani. Wapinzani waungane, ili waweze kuiondoa CCM madarakani. Hizi ndizo sera ambazo wapinzani walitakiwa wazitumie ili washinde. Chadema, CUF, TLP angalieni kampeni USA; jambo dogo wanalifanya liwe kubwa. Wapinzani wapeni ahadi Waislamu na Wakristo ili MSHINDE. Acheni kulala.
 
Mkuu mahakama ya madhehebu mengine tunayo.. Kila sheria ktk mahakama zetu ndogo zinafuata misingi ya Kikristu..Sema tu haikusemwa hivyo.

Mkuu, ni sheria gani hizo za kikristu zinazofuatwa na mahakama zetu?. Sheria zinatungwa na bunge ambalo ni mchanganyiko wa watu wa madhehebu yote, sasa itakuwaje watunge sheria zinazoegemea upande mmoja?. Na kama mahakama zetu zinafuata sheria za kikristu ni kwanini misahafu na bibilia zinatumika pale mahakamani katika kula kiapo?
 
Kidatu,
Mkuu labda nikuanzie na jambo dogo sana ktk sheria zenu..
KIAPO - Katika sheria zetu tunalazimika kushika Biblia au Msahafu hii sii sheria ya kiislaam au dini nyinginezo..Ni ya Kikristu na waislaam wanashika Msahafu tu kwa kuiga lakini hawatakiwi kisheria..
Na hata maelezo ya kiapo yametokana na ukristu.... Hilo moja.. Pamoja na yote haya ungetakiwa kwanza uzijue sheria za Kikristu kisha utazame sheria zetu kwani sheria hutungwa na watu ambao wameelimika toka shule za kidini na kadhalika hivyo sii hata fikra na upeo wetu unaweza kuishia pale mafundisho yale yalipopendekeza..
 
Ndiyo maana hata mimi napinga huko kuwepo na mahakama ya dhehebu au dini yoyote mkuu. Maana mahakama ina linda sheria za nchi. Kwa maana hiyo ikisha vunjwa mahakama ina maana haina maana tena ya kuwa na Bunge ambalo kazi yake kubwa ni kutunga hizo sheria. Na Bunge lisipo kuwepo basi pia ina maana hamna haja ya kuwa na serikali. Unaona implications za wazo lako?

Hizo ni implications za kukubali mahakama ya kadhi ndani ya nchi ambayo si ya kidini. Kwa kukubali kuanzishwa mahakama hiyo kutazua mtafaruku katika nchi, kwani kila dhehebu litataka kuanzisha mahakama yake. Kama itabidi tuvunje bunge, mahakama ya nchi mpaka serikali yote poa tu ili mradi kila dhehebu kivyake.
 
Kidatu,
Mkuu labda nikuanzie na jambo dogo sana ktk sheria zenu..
KIAPO - Katika sheria zetu tunalazimika kushika Biblia au Msahafu hii sii sheria ya kiislaam au dini nyinginezo..Ni ya Kikristu na waislaam wanashika Msahafu tu kwa kuiga lakini hawatakiwi kisheria..
Na hata maelezo ya kiapo yametokana na ukristu.... Hilo moja.. Pamoja na yote haya ungetakiwa kwanza uzijue sheria za Kikristu kisha utazame sheria zetu kwani sheria hutungwa na watu ambao wameelimika toka shule za kidini na kadhalika hivyo sii hata fikra na upeo wetu unaweza kuishia pale mafundisho yale yalipopendekeza..

Mkuu kiapo si sheria ya Kikristo. In fact amri ya saba ya Mungu kwenye Biblia ni "You shall not make wrongful use of the name of the Lord your God, for the Lord will not acquit anyone who misuses his name." Na kuna sehemu kwenye Biblia Mungu ana kataza watu kuapa. Anasema kusema ndiyo inatosha lakini usiape.
 
Hizo ni implications za kukubali mahakama ya kadhi ndani ya nchi ambayo si ya kidini. Kwa kukubali kuanzishwa mahakama hiyo kutazua mtafaruku katika nchi, kwani kila dhehebu litataka kuanzisha mahakama yake. Kama itabidi tuvunje bunge, mahakama ya nchi mpaka serikali yote poa tu ili mradi kila dhehebu kivyake.

Ndiyo maana nikasema mkuu na narudia tena, mimi sikubaliana na dini au dhehebu lolote lile kuwa na mahakama yake.
 
Mwnafalsafa1,
Mkuu ni lazima unielewe kwanza kabla hujarukia Biblia..
Biblia inakataza kula nguruwe na manyama wasiokuwa na kwato..Wakristu wanafanya nini?..
Nitarudia kusema kwanza elewa sheria za kikristu kisha tutaweza kuendelea na mjadala kwani kiapo cha kushika Biblia kakianzisha nani? - Muislaam!
 
Kidatu,
Mkuu labda nikuanzie na jambo dogo sana ktk sheria zenu..
KIAPO - Katika sheria zetu tunalazimika kushika Biblia au Msahafu hii sii sheria ya kiislaam au dini nyinginezo..Ni ya Kikristu na waislaam wanashika Msahafu tu kwa kuiga lakini hawatakiwi kisheria..
Na hata maelezo ya kiapo yametokana na ukristu.... Hilo moja.. Pamoja na yote haya ungetakiwa kwanza uzijue sheria za Kikristu kisha utazame sheria zetu kwani sheria hutungwa na watu ambao wameelimika toka shule za kidini na kadhalika hivyo sii hata fikra na upeo wetu unaweza kuishia pale mafundisho yale yalipopendekeza..

Mkuu, unajua hata kushika bibilia si sheria ya kikristo?. Hakuna kiapo bali kuna ukweli. Ukisema ndiyo ni ndiyo na hapana ni hapana kwani usilitaje bure jina la bwana mungu wako.
Sheria zinatungwa na bunge la nchi lenye mchanganyiko wa watu wa madhehebu yote, hazitungwi na kanisa wala maaskofu.
 
Back
Top Bottom