Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Kidfatu,
Nia na madhumuni ya kushika Biblia ni Kusema UKWELI..hizi habari za kulitamka jina la Mungu na kadhalika hazina mpango..
Ndio au hapana inaweza kusemwa hata na Kafir asiyeabudu Mungu na ikiwa ukweli au sii ukweli.. Dhumuni la kushika Biblia ndilo linatazamwa hapa na limeanzishwa na nani? tena hata ukienda mahotelini na Magereza ni sheria kuweka hizo Biblia hiyo sheria aliiweka nani?..
 
Kidatu,
Mkuu labda nikuanzie na jambo dogo sana ktk sheria zenu..
KIAPO - Katika sheria zetu tunalazimika kushika Biblia au Msahafu hii sii sheria ya kiislaam au dini nyinginezo..Ni ya Kikristu na waislaam wanashika Msahafu tu kwa kuiga lakini hawatakiwi kisheria..
Na hata maelezo ya kiapo yametokana na ukristu.... Hilo moja.. Pamoja na yote haya ungetakiwa kwanza uzijue sheria za Kikristu kisha utazame sheria zetu kwani sheria hutungwa na watu ambao wameelimika toka shule za kidini na kadhalika hivyo sii hata fikra na upeo wetu unaweza kuishia pale mafundisho yale yalipopendekeza..

Acha kuongopa. Kwanza: Kikatiba si sheria kuapa na Msahafu au Qur-an. Unaweza ukaapa bila ya kutumia kitabu chochote cha dini. Pili: Waislamu hawajaiga kuapa kama ulivyoandika. Kuna sura nyingi tu katika Qur-an ambazo Mwenyezi Mungu alikuwa anaapa kwa wakati. Tatu: Hakuna sheria za Kikristo ambazo aziwahusu Waislamu. Sheria nyingi za Conservative Christian hazipo tofauti sana na za Wailsamu.
 
Mwnafalsafa1,
Mkuu ni lazima unielewe kwanza kabla hujarukia Biblia..
Biblia inakataza kula nguruwe na manyama wasiokuwa na kwato..Wakristu wanafanya nini?..
Nitarudia kusema kwanza elewa sheria za kikristu kisha tutaweza kuendelea na mjadala kwani kiapo cha kushika Biblia kakianzisha nani? - Muislaam!

Mkuu kwani hakuna Muislamu asiye kula nguruwe wakati Kurani ina kataza? Mkuu hiyo sheria sijui kaanzisha nani ya kushika Biblia lakini ndiyo nakuambia hiyo siyo sheria ya Kikristo. Swali ninalo kuuliza ni sheria zipi za mahakama ni za kikristo? Kama nimesha kuambia na kukuonyesha kuwa sheria hiyo si ya Kikristo kuna maana gani kuniuliza nani kaianzisha? Mkuu nishasema najua sheria za Kikristo kwa sababu mimi mwenyewe ni Mkristo. Sema mkuu sheria zipi za mahakama ni za Kikristo?
 
Acha kuongopa. Kwanza: Kikatiba si sheria kuapa na Msahafu au Qur-an. Unaweza ukaapa bila ya kutumia kitabu chochote cha dini. Pili: Waislamu hawajaiga kuapa kama ulivyoandika. Kuna sura nyingi tu katika Qur-an ambazo Mwenyezi Mungu alikuwa anaapa kwa wakati. Tatu: Hakuna sheria za Kikristo ambazo aziwahusu Waislamu. Sheria nyingi za Conservative Christian hazipo tofauti sana na za Wailsamu.
Umeandika nini namimi nimesema nini?.

Sikusema waislaam hawatakiwi Kuapa! laa hasha, tunaapa.. sasa wewe unaposema Mungu aliapa alikuwa ameshika Msahafu?..Ndio maana nilitaka kwanza mjue sheria za dini kabla hatujalumbana maanake tunakwenda hata kusikohusika.
 
Kidfatu,
Nia na madhumuni ya kushika Biblia ni Kusema UKWELI..Ndio au hapana inaweza kusemwa hata na Kafir asiyeabudu Mungu na ikiwa ukweli au sii ukweli.. Dhumuni la kushika Biblia ndilo linatazamwa hapa na limeanzishwa na nani?

Mkandara,

Ni wapi panapoonesha kwamba kushika bibilia ama msahafu kumeanzishwa na wakristo?. Unachotakiwa ni kusema ukweli, na kama ukisema uwongo basi utakutana na hukumu ya muumba wako siku ya kiama.
Hata katika kushika misahaafu na bibilia kwani kafir hawezi kushika hivyo vitabu vitakatifu?.

Ninakukumbusha kwamba mahakama za nchi hazifuati sheria za dini yoyote, bali ni sheria zinazotungwa na chombo cha nchi cha kutunga sheria.

Sasa utakaposema sheria za kislamu ziingizwe katika sheria za nchi una maana kwamba hata ambao si waislamu kama mimi tutahukumiwa na sheria hizo?. Ndipo hapo ninaposema ni bora kila dhehebu liwe na mahakama yake kumaliza tatizo hili.
 
Umeandika nini namimi nimesema nini?.

Sikusema waislaam hawatakiwi Kuapa! laa hasha, tunaapa.. sasa wewe unaposema Mungu aliapa alikuwa ameshika Msahafu?..

Mwenyezi Mungu aliapa kwa kutumia WAKATI. Maneno aliyokuwa anayatamka ni Mshahafu (Qur-an).
 
Ndiyo maana nikasema mkuu na narudia tena, mimi sikubaliana na dini au dhehebu lolote lile kuwa na mahakama yake.

Sasa tufanyeje sisi tusiokuwa waislamu kama hawa wenzetu wanataka kuanzisha mahakama yao ndani ya nchi ama kuingiza sheria zao katika sheria za nchi?
 
Sasa tufanyeje sisi tusiokuwa waislamu kama hawa wenzetu wanataka kuanzisha mahakama yao ndani ya nchi ama kuingiza sheria zao katika sheria za nchi?

Mkuu mimi naona the best solution ni kama ambacho nimesha sema na ni kwamba tusiingize sheria za dini yoyote. Kutaka kitu siyo kukipata mkuu. Wewe unaongelea on the assumption ya kama wakianzisha mahakama yao ya Kiislamu mimi naongea the now ambayo ni kuavoid swala hilo lisije leta matatzo baadae.
 
Sasa tufanyeje sisi tusiokuwa waislamu kama hawa wenzetu wanataka kuanzisha mahakama yao ndani ya nchi ama kuingiza sheria zao katika sheria za nchi?

Sasa wewe unataka kufanya nini? KAA ANGALIA TU! Hakuna tatizo lolote kwa Waislamu kuwa na Mahakama yao. Kuna vitu ambavyo Waislamu wanataka vishughulikiwe na Mahakama ya Kadhi kama Mirathi, ndoa nk. Sheria kama hizi haviwezi kuwasumbua waumini wa dini zengine. Nchi nyingi tu zilizoendelea zimeanza na sheria za kidini.
 
Mkuu hizo nchi wewe unazosema zilianza na sheria za kidini ni kwa sababu wananchi wake walikuwa overwhelmingly wa dini fulani. Ndiyo maana unakuta nchi kama Saudi Araba inaongozwa kwa sharia kwa sababu karibia wananchi wote ni Waislamu na nchi si secular bali inadini. Tanzania Waislamu 35% na Wakristo 30% kwa maana hiyo hakuna dini ambayo ina an overwhelmingly the majority. Kabla ya kulinganisha Tanzania na nchi zingine tabua kwanza hali za nchi hizo zilivyo tofauti na kwetu. Tusipende kufanya kila kitu simply because nchi fulani nao walifanya.
 
Mwnafalsafa1,
Mkuu mahakama ya Kadhi hai deal na matatizo unayozungumzia wala hizi sheria sii sawa na zile za Saudi Arabia isipokuwa kwa kesi za madai tu..Mahakama ya kadhi haiendi nje ya majukumu hayo..Nchi haitaongozwa kwa Sheria hivi ni vitu viwili tofauti kabisa wala havifanani.

Nitarudia kusema serikali haikupitisha mahakama ya kadhi isipokuwa baadhi ya sheria za kiislaam kuwa implemanted..Ebu nikuulize wewe tena kama nilivyokmuuliza Mwanakijiji..
Tanzania kuna wanaume wengi tu wameoa wake zaidi ya mmoja.. Nini sheria unayofikiria wewe inafaa kutumika kuwapa haki wanawake wale waliolewa na mume mmoja!

Nipe mawazo yako na pengine jaribu kuhakikisha hayafanani ya Kiislaam, tuone kama utaweza kuleta haki..Nitafurahi sana kama utaweza kunipa tiba ya mgogoro mkubwa unawapata jamaa zetu, na pengine nitafanya subira yawezekana mchango wako unaweza kuonyesha hakuna haja ya kuvuta sheria hizo za Kiislaam.
 
Mkuu tatizo ni kwamba ni vigumu kuwa na sheria za dini moja halafu zisi ingiliane na sheria za nchi. Kwa sababu sheria za katiba zinaweza kucontradict za dini na vise versa. Sheria ikisha ingizwa kwenye katiba ina maana imekua ya nchi. Hauwezi kuingiza sheria kwenye katiba halafu useme hii itakuwa ya watu fulani to kwa maana hiyo katiba itakua imesha wabagua baadhi ya watu. Mimi pingamizi langu ni hilo la kuingiza hizo sheria au baadhi ya sheria kwenye katiba ambayo ni ya wananchi wote. Sasa mkuu does it make sense kusema hizo sheria zitaingizwa kwenye katiba lakini hazita wahusu watu wa dini nyingine?
 
Mwnafalsafa1,
mbona unzunguka hovyo!.. mimi nimekuuliza swali dogo sana, achana na dini nipe hiyo katiba unataka/unapendekeza isomeke vipi kuhusiana na swali nililouliza..mawazo yako yanaweza kujenga kulko hizo sheria za kiislaam..
Nipe dawa, wanawake wanafukuzwa majumbani wakishaachwa na waume zao wengine hufukuzwa mume akisha kufa. They need sheria ya kuwalinda..They need Ur help. Nipe hiyo sheria.. Au fikra zako haziwezi kuondokana na neno Polygamy! huwezi kufikiria nje ya kabati hilo!.. jaribu nasubiri mawazo yako.
 
Mwnafalsafa1,
mbona unzunguka hovyo!.. mimi nimekuuliza swali dogo sana, achana na dini nipe hiyo katiba unataka/unapendekeza isomeke vipi kuhusiana na swali nililouliza..mawazo yako yanaweza kujenga kulkiko hizo sheria za kiislaam.. nipe dawa wanawake wanafukuzwa majumbani wakishaachwa na waume zao wengine hufukuzwa mume akisha kufa They need sheria ya kuwalinda.. Nipe hiyo sheria au fikra zako haziwezi kuondokana na neno Polygamy! huwezi kufikiria nje ya kabati hilo!.. jaribu nasubiri mawazo yako.

Mkuu katiba ina sheria za mirathi. Siyo wanawake wa kiislamu tu wanaoweza kukumbana na matatizo hayo. Wanawake wote ambao wapo kwenye ndoa wanalindwa na sheria za nchi. Kila dini ina tafsiri yake ya ndoa lakini kote huko kukitokea tatizo wanaenda mahakamani. Ndiyo maana ndoa inafungwa kanisani msikitini lakini inavunjwa wapi? Mahakamani. Kwa hiyo kujibu swali lako. Kila mwananchi analindwa na katiba pamoja na hao wanawale wa Kiislamu.
 
Tanzania kikatiba walikubali kuwa secular state kwa maana sheria za nchi hazitakuwa na dini yoyote. Hiyo ni kwa mujibu wa katiba. Mengine mengi tutabishana sana ila mpaka hapo Tanzania itakapo acha kuwa a secular state sheria za nchi haziwezi kuwa na influence ya dini yoyote iwe ya Kiislamu au Kikristo.
 
Mwnafalsafa1,
Mkuu vipi tena.. Hivi ukiulizwa swali dogo mbona unazungukaaaa wakati ni rahisi kusema sijui au mkuu swala hilo zito kwangu badala ya kujaribu kukunja chuma..Mimi nataka wewe unipe jibu maanake siku zote unapokataa kitu uwem na njia bora zaidi.. Hivyo nambie tuijadili. Hiyo katiba hutungwa na nataka wewe uwe mtunzi (mchango wako) au nisomee sheria hiyo unayoijua wewe.
 
Mkuu mbona wewe umekwepa swali la sheria zipi za mahakama ni za Kikristo? Haha. Ukakaa kimya na kujipanga kuja kivingine. Mpaka sasa swali langu hauja jibu una ng'an'gania mimi nikujibu la kwako. Au utasema na mimi nakuonea? Kama hautaki swala dogo liwe tatizo jibu swali langu nililo kuuliza kwanza na mimi nitajibu lako. Hiyo si ndiyo haki mkuu? Haya tuanza. Swali langu lilikuwa sheria zipi ulizo sema wewe ni za Kikristo na zipo kwenye katiba. Ukatoa sheria moja hiyo nimesha kudisprove, Sasa sema sheria nyingine.
 
Natumai utajibu swali langu hapo juu. Na kuhusu swali lako wewe nishakuambia kuwa sheria zinazo linda wanawake katika ndoa zipo. Unless useme sheria hii ambayo inapaswa kumlinda mwanamke inamuonea mwanamke kwa sababu hii la sivyo bado naendelea kukuambia kuwa hizo sheria za kumlinda mwanamke zipo. Sizijui zote. Wewe ambayo unaona haitamfaa mwanamke wa kiislamu ndiyo uje hapa useme haitamfaa mwanamke wa kiislamu kwa sababu hii. Ukifanya hivyo utaanza kunishawishi nikubaliane na hoja yako. Sasa na mimi naomba ujibu swali langu.
 
Back
Top Bottom