Joseph Kussaga na ufisadi wake katika entertainment Tanzania

Hi hawa jamaa (Kina Kusaga) hawawezi kumgundua Afro kutokana na hizi threads zake kweli?. Ikiwa ni hivyo, wasiwasi wangu ni kwamba watamla nyama akiwa hai!
 
Kwa Afro-Sugu whining duo: If you can't beat 'em, join 'em. Period. That's the hard truth right there!
 
Kwanza karibu kwenye jamvi.

Pili, sidhani kama ni sawia sisi kuanza kukuuliza ufafanuzi wa hizo tuhuma zako.

Unachotakiwa kufanya ni kwamba baada ya kuanisha vipengele vya ufisadi wa bw. Kusaga, unatakiwa sasa upige hatua moja mbele, utoe ufafanuzi wa hizo hoja zako ndipo sasa nasi tupate nafasi ya kuzichambua moja baada ya nyingine, vinginevyo utaonekana wewe ni hater tu ama la unaleta udaku tu hapa.

Mwita nimekupa THANKS....ushauri wako ni wa msingi!Tunasubiri utekelezaji wa mtoa mada!
 
Ikiwa ni post yangu ya kwanza,ningependa kuwajulia hali wana JF na wadau wote wenye nia njema na nchi yetu Tanzania.

Leo nimeamua kuidadicate post yangu ya kwanza kwa wanaentertainment wote wa Tanzania ambao wengi wao ndoto zao zinaishia hewani kutokana na ufisadi unaofanywa na The Don of entertainment Tanzania Mr. Joseph kussaga kama anavyopenda kujiita The Don aka Mullah.

vifuatavyo ni vipengele ambavyo niko tayari kuvielezea kwa atakae taka kujua kiundani jinsi bwana huyu alivyoishikiria nchi kwenye nyanja ya burudani kwa maslahi yake binafsi.

  • Udhamini(sponsorships)
  • Bongo flava
  • Wafanyakazi wake(watangazaji na wengineo)
  • Polisi
  • Tanesco
  • kumbi za starehe
  • Umalaya
  • na chochote kuhusiana na burudani Tanzania.
Mimi ni mmojawapo wa watu wake wa karibu ambao katika wachache waliofanikiwa kujikwamua kutoka kwenye himaya yake na nimeamua kujitoa muhanga na kuweka hadharani chochote wana JF ambacho kinawakwaza kuhusiana na Ufisadi unaoendelea kwenye burudani Tanzania.

Kwakuwa ningependa kufafanua kimpangilio ndiyo maana nimeweka vipengele hivyo hapo juu ili niweze kuvifafanua inapobidi. Kutokana na ufisadi huu kuwa mkubwa na wenye network nyingi ningependa kufafanua kipengele kwa kipengele kama nilivyoviorodhesha hapo juu lakini iwapo ntatakiwa kufanya hivyo.

Nawakaribisha jamvini wana jamii ili tuweze kuutokomeza ufisadi huu kwa maslahi ya taifa.

Ahsanteni na karibuni.

- Udaku, majungu bin fitina wrong number mkuu! Joe ni mfano wa kuigwa kutoka mfanyakazi wa chini sana wa Bima mpaka the Don wa entertainment wa taifa, ana mapungufu kama bin-adam yes amekuibia mahakama zipo, amekupiga mahakama zipo, umalaya ni matatizo ya binafsi, ni kiongozi wa taifa hapana ni self made Billionea,

- Self billionea, matokeo udaku, fitina, chuki, majungu na wivu, wakikushinda jiunge nao!

Respect.

FMEs!
 
Huyu jamaa hatumuwezi maana kaisha mkamata JK , hakuna kufurukuta fungu la uchaguzi lote liko kwake maana radio yak itatumika ku hamasisha vijana kupiga kura,

Lakini lipi halikutarajiwa hapa?

Hii yote ni adhabu ya sisi wananchi kukubaliana na mfumo wa utawala wa kama genge la mafioso. Nadhani unakumbuka ile kauli ya mnene mmoja kuwa 'kaa unataka biashara zako ziende vizuri kuwa mwananchama wa CCM'. Hawa akina Kusaga et al ndio walewale mapusha wa hawa mafioso. Hawa ni kama mumiani, Wanahakikisha wanamkamua mvuja jasho mpaka tone lake la mwisho la damu.

Sidhani.
 
Anachosema hapa Afro siyo kitu kigeni katika masikio ila inapendeza zaidi kama yeye alikuwa huko jikoni. Thread ya Mr.2 na zinduka imeeleza sana issue za hawa jamaa.

mkuu, weka kila kitu wazi kabisa, ukiweza taja na majina ya wahusika, let JF be mahakama ya raia inayotoa adhabu za kisaikolojia!

Sawa kabisa Wabby,

Sielewi watu humu wakoje? Muanzisha thread nadhani anastahili kupongezwa, namchukulia kama whistleblower ambaye anafichua uovu ambao unaitafuna jamii. Sasa kaa tungekuwa na competitive investigative journalism hii ingekua start-up point nzuri sana kwenda kwenye bottom line ya hii ishu ili kujua mbivu na mbichi. Tatizo la waTz wengi, hata humu JF ni watu kutotaka kujiuliza maswali magumu. Hawataki tafakari nzito na ni wepesi wa kusingizia wanaonewa wivu.
 
....
Leo nimeamua kuidadicate post yangu ya kwanza kwa wanaentertainment wote wa Tanzania ambao wengi wao ndoto zao zinaishia hewani kutokana na ufisadi unaofanywa ...

  • Wafanyakazi wake(watangazaji na wengineo)
QUOTE]

Mkuu, nafaham baadhi ya watangazaji hawapigi nyimbo za underground bila mshiko, hili liko wazi na bongo flava community wanalielewa.

Niliwahi sponsor underground na ilikuwa kawaida kuombwa pesa ya kuwapa watangazaji ili nyimbo zipigwe redioni. Kibaya zaidi ili utoke unahitaji nyimbo yako ipigwe pale, wahindi bila kuiskia nyimbo yako imepigwa na wale jamaa huuzi kitu.

Ili kujua kuhakikisha siingizwi mjini na underground kuna siku niliandamana nao wakati wanapeleka mshiko na nilishuhudia watangazaji wawili maarufu wakikamatishwa ule mshiko. Kutoka pale nikatumia connection zangu nikaunganishwa na kigogo mmoja pale redioni ambaye alikiri na kusema yeye binafisi hana la kufanya maana watangazaji wanapower kuzidi yeye kutokana na kuwa karibu na owner. The guy went as far as saying I quote 'angalia magari ya thamani wanayoendesha pesa wanatoa wapi?'

Nilishajitoa kwenye huu udhamini kama miaka mitatu sasa hivyo kama wamebadilika ni hivi karibuni.
 
JF ina mambo mazito..
Mengine majungu,mengine kweli tupu mengine loh
Haya mheshimiwa Afro endelea kutupa Dataz za bwana kusaga
 
Ikiwa ni post yangu ya kwanza,ningependa kuwajulia hali wana JF na wadau wote wenye nia njema na nchi yetu Tanzania.

Leo nimeamua kuidadicate post yangu ya kwanza kwa wanaentertainment wote wa Tanzania ambao wengi wao ndoto zao zinaishia hewani kutokana na ufisadi unaofanywa na The Don of entertainment Tanzania Mr. Joseph kussaga kama anavyopenda kujiita The Don aka Mullah.

vifuatavyo ni vipengele ambavyo niko tayari kuvielezea kwa atakae taka kujua kiundani jinsi bwana huyu alivyoishikiria nchi kwenye nyanja ya burudani kwa maslahi yake binafsi.

  • Udhamini(sponsorships)
  • Bongo flava
  • Wafanyakazi wake(watangazaji na wengineo)
  • Polisi
  • Tanesco
  • kumbi za starehe
  • Umalaya
  • na chochote kuhusiana na burudani Tanzania.
Mimi ni mmojawapo wa watu wake wa karibu ambao katika wachache waliofanikiwa kujikwamua kutoka kwenye himaya yake na nimeamua kujitoa muhanga na kuweka hadharani chochote wana JF ambacho kinawakwaza kuhusiana na Ufisadi unaoendelea kwenye burudani Tanzania.

Kwakuwa ningependa kufafanua kimpangilio ndiyo maana nimeweka vipengele hivyo hapo juu ili niweze kuvifafanua inapobidi. Kutokana na ufisadi huu kuwa mkubwa na wenye network nyingi ningependa kufafanua kipengele kwa kipengele kama nilivyoviorodhesha hapo juu lakini iwapo ntatakiwa kufanya hivyo.

Nawakaribisha jamvini wana jamii ili tuweze kuutokomeza ufisadi huu kwa maslahi ya taifa.

Ahsanteni na karibuni.
Ona sasa umeweka mambo nusu nusu unasababisha jukwaa badala ya wadau kujadili wanaanza kuuliza maswali... alafu mwenyewe hujibu umeingia mitini!

Hapo unatakiwa uweke mambo hadharani straight away vinginevyo uache usirushe kitu hewani hadi utakapokuwa na data za kutosha!

Nafikiri umenipata!

Karibu Jamvini
 
Kwa sababu tunahamu sana kujua karibu mambo yote uliyo list hapo - mkuu afro wewe anza moja baada ya jingine kama ulivyoyapanga - tukimaliza kulijadili then unaingia kwenye jingine - inaonekana kuna mvuto hapa.

tuanze na hili la udhamini (sponsorship) kama ulivyoorodhesha mkuu -- twende kazi..
 
- Udaku, majungu bin fitina wrong number mkuu! Joe ni mfano wa kuigwa kutoka mfanyakazi wa chini sana wa Bima mpaka the Don wa entertainment wa taifa, ana mapungufu kama bin-adam yes amekuibia mahakama zipo, amekupiga mahakama zipo, umalaya ni matatizo ya binafsi, ni kiongozi wa taifa hapana ni self made Billionea,

- Self billionea, matokeo udaku, fitina, chuki, majungu na wivu, wakikushinda jiunge nao!

Respect.

FMEs!

Pamoja na mtazamo/ msimamo wako ambao unaangalia upande mmoja wa shilingi, lakini pia inabidi ujue kwamba Ze Don anaweza kuyafanya haya yote yanayoelezwa au akafanya baadhi kama si yote. Kimsingi hizi tuhuma zipo siku nyingi sana huko mitaani, kwahiyo afro kuzileta hapa jf sio jambo la ajabu wala jambo geni. Labda ambacho watu wengi walikuwa hawajui ni jinsi gani au namna gani huyu ze don anavyotekeleza unyonyaji kwa wasanii.

Ze don anaweza kuwa mfano mzuri wa kuigwa kwa yale mazuri anayofanya na kwa njia halali sio kujifunza kutoka kwake namna ya kuwanyonya watanzania wenzake.
 
Najua mwanzoni itakuwa ngumu kueleweka kwakuwa maswali mengi yatajitokeza kutokana na thread hii,Ila ningependa kufafanua zaidi kwamba mimi sikuwa mshiriki wa Kussaga bali nilikuwa muajiliwa niliye kifungoni kama wasanii wanavyowekwa kifungoni lakini imefikia wakati nimeshindwa...mimi fani yangu kubwa ni mwana burudani,nilijitoa Clouds FM miezi michache iliyopita na kujaribu kuendeleza fani yangu kimwenyewe mwenyewe lakini mambo yanayonikuta ni kwamba nimefungiwa njia zote na huyu jamaa na hakuna njia yoyote ya mimi kujiendesha binafsi kwakuwa nyanja nyingi zinazohusiana na Entertainments zimeshabanwa.Labda nibadilishe fani au nikubali kuendeshwa na huyu jamaa kama anavyotaka yeye.

wengi watafikiri ni udaku au majungu au Chuki lakini si hivyo kabisa.kuna mambo mengi sana ya kifisadi yanaendelea katika fani hii ambayo kwa mimi binafsi ninauhakika tunaweza kuyakemea kwa maslahi ya jamii. mi nafikiri tuwe wavumilivu na tuijadili hoja hii kiupole zaidi.

taratibu tu kamanda tutakupata - we endelea kumwaga data - mi ndiyo ninaipitia thread hii asubuhi hii - duh.
 
Kipanya upoooo.......we pia si ulikuwa CLOUDS, hebu toa ushahidi wako.
 
who the hell is this JOse Kusaga..

mambo ya kina Julius na udaku wao..kama ana tuhuma za kutoa rushwa mpelekeni PCCB coz rais kawapa meno kudeal hadi na watu wa private sector..

tunaongea sana..
 
Hi hawa jamaa (Kina Kusaga) hawawezi kumgundua Afro kutokana na hizi threads zake kweli?. Ikiwa ni hivyo, wasiwasi wangu ni kwamba watamla nyama akiwa hai!

Sasa hivi bongo nayo, Life imedinda na kusababisha baadhi ya watu kuwa MAFIA ili kutembea juu ya mstari.

Afro kama amekaa na hao MAFIA, lazima atakuwa anajua namna ya kucheza nao.

Bongo sasa u-MAFIA umekua sana, vijana wadogo siku hizi wanataka wamzidi RM kifedha, na shortcut yao ni u-MAFIA.

Afro umeleta mjadala mzuri sana hapa, na hii ndiyo dawa ya ma-MAFIA.

Tukijaaliwa nitaandika maana kamili ya MAFIA.

Tukiuacha ushamiri nchini, Future ya Tanzania ni DEAD END!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Ni kweli unapokuwa na jambo ambalo una uhakika nalo bora ueleze kinagaubaga siyo blablaa. hebu fafanua kwanza kuhusu TANESCO, na huo ufisadi ulianza lini na umefikia wapi kwa sasa? ili kama kweli hatua za kisheria zichukuliwe zidi yake.

Isije ikaja dhana ya kuwa wabongo wakishaona mtu anafanikiwa lzm majungu yaanze ili kumchafulia jina lake.

Tueleze hizo tuhuma ili tuelewe je ni fisadi au ni ile dhana ya kuzushiana mambo ili kuchafuliana majina tu.
 
Back
Top Bottom