CHADEMA kubalini matokeo na m-survive, or shupazeni shingo. You go to hell 6ft under Hao Makamanda 19 ni mashujaa, kuendelea Ubunge wao

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,427
113,421
Wanabodi,

Kila nipatapo fursa, huja na makala zangu za kwa maslahi ya taifa. Japo mimi ni kada wa chama cha siasa na sio CHADEMA, ukada wangu, haunizuii kutoa ushauri kwa Chama chochote kukisaidia. Upendo wa kweli ni pale unapoona jirani yako ambaye ni kipofu, haoni mbele, anatembea na mkongojo, unamuona kabisa anahatari ya kuangamia, kwa kuelekea kwenye shimo, unajitolea kumnusuru kwanza kwa kumpigia kelele asimame, na kumweleza mbele kuna hatari, kisha una stretch a helping hand kumshika mkono kumsaidia kumrudisha kwenye mstari, kwenye njia sahihi. CHADEMA, kwa sasa, baada ya kipigo kitakatifu kwenye uchaguzi Mkuu uliopita ambao licha ya dosari ndogo ndogo ni ni huru na wa haki, ambapo upinzani umekataliwa na wananchi, Chadema kimepoteza dira, kimepotea njia, na hakina mwelekeo, hivyo kwa sasa kina hitaji kusaidiwa, kushikwa mkono kuonyeshwa the right way to go!, hiki ndicho ninachokifanya hapa.

Hivyo huu ni ushauri wangu kwa Chadema, Its do or die! Chadema is left with only two options, kuchagua kufa, au kuchagua kuendelea kuishi. The choice is theirs.

Ili CHADEMA kiendelee kuishi ni lazima kiukubali ukweli, kikubalini matokeo ya uchaguzi, kiandike barua NEC, kwanza kufanya due diligence ya majina hayo yamefikaje NEC, wakibaini ni kwa njia ya kughushi, then, this is criminal issue, sio tena issue ya Bunge au NEC, hii ni jinai, waanze kwa kuipeleka polisi, ili kuwaadhibu wahusika kwa kuwavua uanachama hao wahusika wakiwemo hao wasaliti 19, kisha kipeleke majina mapya 19, kiendelee kuvuta ruzuku and survives, or kiendelee kushupaza shingo, kuwa hakiyatambui matokeo ya uchaguzi, hakimtambui rais wa Jamhuri ya Muungano wa hakilitambui Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, then CHADEMA will just go straight to hell by being buried 6ft Under!.

Mbele ya macho ya jamii, hao ambao kwao ni wasaliti, kwa wengine hao ni makamanda mashujaa wapambanaji ambao ni wa kiwango cha makomandoo, ambao wameipigania Chadema kwa machozi, jasho na damu, na licha ya kufutwa uanachama wa CHADEMA, wataendelea kuwa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Ubunge wao sasa utakuwa ni ubunge wa Spika, Ubunge wa Taifa.

Angalizo la Uelewa:
Naomba kutoa angalizo dogo kuhusu uwezo wa uelewa wa Watanzania wenzetu wengi kwenye complex issues kama hii, ni uelewa mdogo!, hivyo hili sakata la wabunge 19 wa Viti maalum CHADEMA, ni complex issue, kueleweka, inakubidi uwe na kichwa chenye uwezo wa uelewa wa kiwango hicho, hivyo wale wa uwezo wa uelewa wa wenzangu na mimi, mkiishia tuu kusoma heading na ku comment, nitawalewa sio kosa lenu, poleni. Ushauri wangu, ishieni hapa, huko mbele ndio mtapotea kabisa.

Wale wenzangu na mimi wa kuzama deep, twendeni mdogo mdogo, na ili uweze kuilewa vizuri mada hii iliyopo mezani, anzia hapa
Haki ya Kila Mtanzania Kushiriki Siasa
Uhuru wa kushiriki shughuli za umma
21.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ya 5, ya Katiba hii na ya sheria za nchi kuhusiana na masharti ya kuchagua na kuchaguliwa, au kuteua na kuteuliwa kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, kila raia wa Jamhuri ya Muungano anayo haki ya kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, ama moja kwa moja au kwa kupitia wawakilishi waliochaguliwa na wananchi kwa hiari yao, kwa kuzingatia utaratibu uliowekwa na sheria au kwa mujibu wa sheria.


Lakini kukatokea kikundi fulani cha watu, kwa sababu wanazozijua wao na kwa maslahi yao, na kwa vile serikali ni yao, wakaipindua katiba kwa kuinyofoa haki hiyo ya kila mtu kushiriki siasa, iliyotolewa na katiba, na kupachika shurti la kudhaminiwa na chama, hivyo kujenga ubaguzi katika kushiriki shughuli za uongozi umma kwa watu kulazimishwa kwanza kujiunga na vyama vya siasa, ndipo upate haki ya kugombee nafasi yoyote ya uongozi wa umma, huku sio kuwatendea haki Watanzania wengine wote, wasiotaka kujiunga na vyama vyovyote vya siasa, kutokana na watu wengine, ukiondoa CCM ambacho ndicho pekee ni chama cha siasa cha ukweli Tanzania, watu wanaviona karibu vyama vingine vyote vya siasa ni vyama vya hovyo hovyo, lakini wana uwezo wa uongozi. Hii ni haki muhimu iliyotolewa na katiba, kitendo cha kuingiza shurti la kudhaminiwa na chama cha siasa ni kinyume cha katiba. Hivyo sheria hii ibadilishwe ili kukidhi kile ambacho katiba ilidhamiria ilipoitoa haki hii, hivyo baada ya mabadiliko hayo ya mlango wa nyuma, kipengele hicho sasa kinasomeka hivi

Uhuru wa kushiriki shughuli za umma Sheria ya 1984 Na.15 ib.6 Sheria ya 1994 Na.34 ya ib.4
21.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ya 5, ya 39 na ya 67 ya Katiba hii na ya sheria za nchi kuhusiana na masharti ya kuchagua na kuchaguliwa, au kuteua na kuteuliwa kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, kila raia wa Jamhuri ya Muungano anayo haki ya kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, ama moja kwa moja au kwa kupitia wawakilishi waliochaguliwa na wananchi kwa hiari yao, kwa kuzingatia utaratibu uliowekwa na sheria au kwa mujibu wa sheria.


Ule uhuru uliotolewa na Katiba wa kila mtu kuwa huru kushiriki shughuli za uongozi, kupitia ibara ya 21, umekuja kunyofolewa na ibara ya 39 na 67 (b)(c) kwa kuweka sherti, ili mtu kuweza kugombea nafasi yoyote ya uongozi wa umma, ni lazima awe ni mwanachama, na mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa hivyo lazima adhaminiwe na chama cha siasa!, Haki zinatolewa na ibara moja ya katiba hiyo hiyo, halafu zinaporwa na ibara nyingine ya katiba hiyo hiyo!. Yaani mtu anatoa zawadi kwa mkono mmoja, halafu huyo uliyempa hiyo zawadi, unatoa mkona mwingine na kumpora!.

Mchungaji Mtikila (Mungu amuweke mahala pema peponi), mwaka 1993, alifungua kesi No. 5 ya 1993, alifanya kuhudi kubwa kukipinga kifungu hiki na Mahakama Kuu kupitia kwa Jaji Lugakingira, (Mungu amuweke mahala pema peponi), ikatamka wazi na bayana kipengele hicho ni batili na kinakiuka katiba ya JMT ya mwaka 1977, hivyo kifutwe, na kutoa haki kwa kila Mtanzania ana haki ya kushiriki kugombea Uongozi wa umma.

Baada tuu ya Mtikila kushinda kesi serikali ikafanya mambo mawili makubwa ya ajabu!, kwanza ilikata rufaa!. Hivi kwa uamuzi kama huu, wa kuwapa haki Watanzania, serikali ilikata kweli kukata rufaa kwa maslahi ya nani?. Pili serikali ilipeleka bungeni kwa hati ya dharura, sheria No. 34 ya mwaka 1994, kufanya marekebisho ya 8 ya Katiba ya JMT na kukichomeka kipengele hicho ndani ya katiba!, hivyo kuibatilisha ile hukumu ya Jaji Lugakingira!. Hapa ndipo ujinga unapoanzia katika siasa zetu kwa Bunge la predominant chama kimoja, kufanya kazi kwa maslahi ya kisiasa ya chama kimoja, hivyo kupoteza haki ya wengi kwa ajili ya kuwanufaisha wachache!.

Hiki kilichofanyika, mimi nakiita ni kitendo cha kihuni!, Watanzania tulifanyiwa uhuni na serikali yetu, kwa kuinajisi katiba yetu!, kitu kimeelezwa ni kinyume cha katiba, kinatoa haki zilizotolewa na katiba, halafu serikali hiyo inakuja kuihalalisha haramu hiyo kwa kuiingiza rasmi kwenye katiba!, huku ni kuinajisi katiba yetu!.

Mchungaji Mtikila, licha ya kuwa ni mwanasiasa, Mwenyekiti wa chama cha siasa cha DP, (Democratic Party), lakini alikuwa ni mtu wa Mungu kiukweli kabisa, kwa sababu hakukubali kabisa katiba yetu inajisiwe!, hivyo akafungua kesi nyingine No.10 ya mwaka 2009 kupinga marekebisho hayo ya 8 ya katiba ya JMT na kuyaita ni ubatili!.

Katika kesi hiyo, Mchungaji Mtikila aliomba mambo makuu mawili makuu

(a) Mahakama itamke ibara 39 na 67 za katiba zilizorekebishwa na marekebisho ya 8 kwa sheria No. 34 ya mwaka 1994, ni batili na kinyume cha katiba.

(b) Kutamka wazi kuwa Kila Mtanzania ana haki ya kugombea kwa mujibu wa ibara ya 21 ya Katiba, bila kulazimishwa kudhaminiwa na chama cha siasa, hivyo mtu anaweza kugombea kama mgombea binafsi.

Mahakama Kuu chini ya majaji watatu, (majaji watatu kisheria inaitwa Half Bench), Manento, Masati na Mihayo, wakayakubali mambo yote ya Mchungaji Mtikila na kumpa ushindi tena kwa kutamka marekebisho hayo ya katiba ni batili!. Lakini serikali yetu ilivyo ya ajabu, ikakata tena rufaa, na safari hii Mahakama Kuu ikakaa Full Bench ya majaji 7, chini ya Jaji Mkuu Mwenyewe, Agustino Ramadhani, akisaidiwa na Jaji Munuo, Jaji Msoffe, Jaji Kimaro, Jaji Mbarouk, Jaji Luanda, na Jaji Mjasir, ambapo tarehe 17 mwezi June, mwaka 2010 ikatoa hukumu ya ajabu kabisa kuwahi kutokea Tanzania!. Tena Mahakama haikuwa peke yake, bali iliwaita mabinga wabobezi wa sheria na katiba kuisaidia, hawa wanaitwa marafiki wa mahakama, kwa kiingereza ni friends of the Court, kisheria wanaitwa Amicus Curiae, hivyo ma Amicus Curiae hawa, Mr. Othman Masoud, Prof. Palamagamba Kabudi, na Prof.Jwan Mwaikusa(Mungu Aiweke Roho yake Mahala Pema Peponi) waliisaidia mahakama kuu ya rufani kufikia uamuzi huu wa ajabu kabisa!.

Uamuzi wa Mahakama Kuu ya Rufaa uliamua kitu cha ajabu sana na hapa naomba ninanukuu
“So as to let the will of the people prevail as to whether or not such [independent] candidates are suitable. We are definite that the Courts are not the custodian of the will of the people. That is the property of elected Members of Parliament”.

Hii kiukweli ni kauli ya ajabu sana kutolewa na mahakama yetu kwenye jambo zito na muhimu kama hili!. Kitendo cha Mahakama kujivua jukumu la kuwa the custodian of the will of the people!, ni kitendo cha ajabu sana na kushangaza sana!. Hakuna will of the people kubwa kuliko katiba!, kama katiba imetoa haki fulani, serikali ikatoa amri kuifuta haki hiyo, au Bunge likatunga sheria ya ajabu kabisa kuifuta haki hiyo, halafu mahakama ikatamka haiwezi kuliingilia Bunge!, huu ni uthibitisho wa Mhimili wa Mahakama kuji submit kwa mhimili wa serikali!, where is the doctrine of separation of powers, checks and balance?!.

Mahakama Kuu ya Rufaa ikaamua kuwa Mahakama haina mamlaka ya kuliingilia Bunge, katika vipengele vya katiba, kumaanisha kwa vile marekebisho hayo ya 8 yamefanywa na Bunge, hivyo ni Bunge ndio lirekebishe kipengele hicho!, kiukweli kabisa, kwa maoni yangu, uamuzi huu sio utii wa mhimili wa Mahakama kwa mhimili Bunge, bali huu ni ukondoo wa hali ya juu kwa Mhimili wa Mahakama kwa serikali na kwa Bunge kwa manufaa ya watu wachache!.

Japo Lengo la Kudhaminiwa ni Lengo Zuri ili Kupata Viongozi Bora, Jee Bado Linahitajika?
Katiba ilisema kila Mtanzania ana haki ya kushiriki uongozi, hili sherti la kudhaminiwa na chama lilitoka wapi, na kwa kwa nini watu walazimishwe kuwa wanachama wa vyama ili wadhaminiwe, ndipo waweze kugombea?.

Watanzania tusikubali mfumo huu uendelee hadi 2025!, tupiganie milango ya wagombea binafsi ifunguliwe, 2025, watu wenye nia ya kugombea, kuwaletea wananchi maendeleo, bila kupitia vyama waingie, washindane kwa hoja na sio kushindana kuhonga, kama hali inavyoendelea sasa!. Hili shurti la vyama likiondolewa, mnaweza kushangaa watu wazalendo wa kweli wa nchi hii, wenye uchungu wa dhati na umasikini wa taifa hili, wakajitokeza kuwatumikia wananchi!.

Auamuzi wa mwisho, ukaamuliwa, Katiba ndio mamla kuu ya juu iko juu ya mamlaka nyingine zote. Kwa vile Bunge ni mhimili, na mahakama ni Mhimili, na mihimili yaote iko chini ya katiba, mhimili mmoja hauna mamlaka ya kuingilia uamuzi wa Mhimili mwingine, hata kama uamuzi huo unaonekana una makosa.

Ikaamuliwa kwa vile sasa kipengele hicho, cha shurti la kudhaminiwa na chama cha siasa, limeingizwa kwenye katiba, mahakama haina uwezo wa kuamuru kipengele cha katiba kufutwe, wenye uwezo wa kukifuta kipengele hicho, ni Bunge ndilo lililo kiingiza kwenye katiba, na uamuzi huo ni wa mwisho, final and conclusive, na unaendelea na sasa ndio umetufikisha hapa kwenye hawa wabunge wanawake 19 makamanda wa Chadema, ni makomandoo na mashujaa wa haki za wanawake.

Baada ya 19 hao kuapishwa, kumewasha moto wa kisiasa kila kona ya nchi, kwa nchi nzima kwa wiki nzima, trends zote za mijadala ya kisiasa ni kuhusu hili la wabunge 19 wa viti maalum wa Chadema.

Baada ya kula kiapo, kwanza KM wa Chadema, JJ.Mnyika aka wa disown, kwa kusema hakupeleka majina yao NEC. NEC wakajibu mapigo majina yaliletwa na KM wa Chadema!. Chadema ikawaita kwenye kikao cha CC ili wajieleze, 19 hao wakagomea kikao. Kikao kikakaa kama a kangaroo court yao kama kawaida yao, bila kuwasikiliza na kuamua kuwavua uanachama, hivyo automatically kupoteza ubunge wao kufuatia udhamini wa chama kuondolewa.

Spika nae kwa kutumia mamlaka yake ya kimhimili, ameahidi kuwalinda. Hii iliishawahi kutokea huko nyuma kwa vyama kuwafuta uanachama wabunge wake na Spika akawalinda, kwa vile Spika ni mhimili, akiisha amua ameamua, hata uende mahakama gani, hautasikilizwa!.
A Way Forward Kwa Chadema
Kama ni kweli Chadema haiyatambui matokeo ya uchaguzi, maana yake, ni sio tuu, hailitambui Bunge, bali pia, hawamtambui Rais wa JMT. Hivyo hawana haja ya kuandika barua popote, na maadam, hawalitambui Bunge, basi iachane na hao wabunge wa Spika. Lakini kwa mfumo wetu, rais wa JMT ni executive president, ni rais mtendaji, kila kinachofanywa mamlaka zote za umma, kinafanywa kwa niaba ya rais wa JMT, ukiisha kuwa humtambui rais, hiyo maana yake pia hulitambui Bunge, kwasababu limetokana na uchaguzi batili, hivyo sasa hao wabunge makamanda 19 wa Chadema ambao kwa Chadema ni wasaliti, lakini kwa wengine ni mashujaa wa haki za wanawake, baada ya kufutwa uanachama wa Chadema, wanapaswa kupoteza ubunge wao, ili wafutwe ubunge huo, ni lazima Chadema, kwanza kikubali matokeo!, kiyatambue!, kiiandikie Tume ya Uchaguzi NEC, kuwa kimekubali matokeo na kimekubali kupokea nafasi zake 19 za viti maalum. Barua hiyo ionyeshe kuwa Chadema wamefanya due diligence na kubaini majina hayo yamefojiwa, hivyo iwakane, hao wabunge 19 waliojipeleka. NEC kwanza itajiridhisha kwamba ni kweli kulifanyika forgery ya hayo majina 19 wa mwanzo, kisha ni NEC ndio itamundikia Spika wa Bunge barua kutangaza nafasi hizo 19 za viti maalum Chadema ziko wazi, na kumpatia majina 19 mapya na halali ya viti maalum wa Chadema, hivyo Chadema wakiandika tuu barua, itakuwa ni wameutambua uchaguzi na wamekubali matokeo, Chadema will survive.

Kwa vile wabunge hao wameisha apishwa ni wabunge halali wa Bunge la JMT, hata kama Chadema imewafuta uanachama, ni mambo ya ndani ya chama, kama ni kweli Chadema haiyatambui matokeo ya uchaguzi, then hao wabunge 19 wa Chadema, hawahitaji kukata rufaa popote, wala kwenda mahakamani kupinga chochote, kwasababu Chadema haiwezi kufanya chochote. Sasa wataendelea na ubunge wao kama wabunge wa Taifa wa Chadema.

Wanachopaswa kufanya ni kutafuta eneo la ofisi hapo Dodoma, wafungue bank account, ruzuku yote ya Chadema, watakabidhiwa wao, na kulisongesha hadi 2025!. Uamuzi huu wa kulisongesha una changamoto moja, baadhi ya hao 19, ni wake wa ndoa wa wana CC wa Chadema, baadhi ni wenzi wanaoishi nao kinyumba kama mke na mume,na baadhi ni 'vidumu' vya viongozi wa Chadema, kuishi nyumba moja, kulala chumba kimoja, kitanda kimoja kati ya kiongozi halali wa Chadema na muasi, ni changamoto!, tena kuna wengine wameisha anza kujenga familia, familia zisiparanganyiwishwe na siasa za kujinga jinga kama hizi!.

Chadema wakiamua kuacha ujinga wa kujifanya hawayatambui matokeo, wakiyatambua, wataandika barua kwa NEC, copy kwa Spika kuwa, wabunge hao sio wanachama wao, wamewavua uanachama hao wasaliti 19, na badala yake, KM atangaze list ya wabunge wanawake wengine 19 wapya, ipeleke NEC, NEC wampe Spika, Spika awatangaze kuwatengua ubunge hao wabunge 19 wasaliti wafutwe ubunge na wabunge wapya wa Chadema waapishwe.
Zeozi hili lina changamoto 2 tuu, Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai, 2- Wameisha kopeshwa mkopo wa magari unaolipwa ndani ya miaka 5!.

Nini Kifanyike, A Way Forward Kitaifa
Kama nilivyowahi kushauri humu, ukosoaji wenye kujenga, huandamana na ushauri wa nini kifanyike kurekebisha kasoro hizi ili kuundoa ujinga huu unaoendelea nchini kwenye siasa zetu, haiwezekani kiongozi achaguliwe na umma wa Watanzania, halafu chama chake kwa sababu za kijinga jinga tuu, kimvue uanachama, ili Tanzania tupate maendeleo ya kweli ya kisiasa, ni lazima tubadilike, sheria za kijinga jinga zenye masharti ya kijinga jinga lazima tuzibadilishe.

  1. Tubadili sheria yetu ya uchaguzi, kile kipengele cha kudhaminiwa na chama kiishie kwenye uteuzi tuu, kiongozi akiishachaguliwa, anakuwa kiongozi wa watu, anaweza kuhama chama bila kupoteza uongozi wake kama ilivyo nchini Kenya na nchi nyingine zenye kuheshimu demokrasia ya kweli na sio hii demokrasia fake ya vyama!.
  2. Tubadili Katiba yetu na sheria yetu ya uchaguzi, kwa kuondoa kipengele cha kudhaminiwa na vyama ili kila Mtanzania mwenye sifa za kugombea uongozi wa nafasi yoyote, aruhusiwe, ila kwenye urais, tuweke vigezo vya ziada, ili asijetokea tajiri mmoja mwenye ukwasi wa kuwanunua watanzania wote, tukajikuta tuna rais wa kununuliwa. Ila kwenye ubunge, udiwani na serikali za mtaa, kila mtu awe free kugombea, hivyo tuwe na wagombea huru, na wagombea binafsi.
  3. Tuibadili Tume yetu ya Uchaguzi iwe Tume huru zaidi na shirikishi, tujenge uwanja sawa wa ushindani wa haki kwa vyama vyote, uchaguzi uendeshwe kwa transparency ya hali ya juu kwa kuruhusu mawakala hadi kwenye tallying, na vyama au taasisi zozote ziwe free kuwa na tallying centers zake, kitu ambacho hakitaruhusiwa na talling centers hizo ni kutangaza matokeo, kama matokeo yote ya uchaguzi hadi wa rais yanahesabiwa kituoni na kubandikwa ukutani, kama hakuna jambo lolote la kificho, yaani nothing to hide, kwanini uzuie independent tallying?!. Uchaguzi wa 2025, kila mwenye uwezo wa kufanya tallying aruhusiwe afanye ila zisitangaze matokeo, hii itazuia bao la mkono!
Hitimisho
Ili Taifa letu lipate maendeleo ya kweli, ni lazima sisi Watanzania tukubali kuwa wakweli toka ndani ya nafsi zetu, kwa kutanguliza mbele maslahi ya taifa na kufanya siasa za ukweli, naamini kabisa rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli, anaweza kuleta maendeleo ya kweli ya taifa letu la Tanzania kwa kuleta maendeleo ya kiuchumi na wakati huo huo akiiacha demokrasia ikishamiri.

Nawatakia Jumanne Njema.

Paskali
Update ya Mchango Very Objective
Swali moja rahisi sana kwako Paskali. CHADEMA ikifa, Watanzania na taifa kwa ujumla tutapata hasara gani? Unaamini NI LAZIMA CHADEMA iendelee kuwepo (exist)?

Maelezo yote hayo marefu sana uliyotoa na ambayo umekuwa ukiyatoa zaidi ya mwaka kuhusu CHADEMA, yanadhihirisha kuwa kwa mazingira ya kisiasa tuliyo nayo Tanzania, HAIWEZEKANI tuwe na mfumo wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa nchini ambao ni BONA FIDE GENUINE.

Halafu, VERY CURIOUSLY, siioni juhudi yako ya dhati kuwaasa wenye dhamana ya kutengeneza mazingira sahihi ya demokrasia ya vyama vingi Tanzania ili kuwezesha vyama kama CHADEMA kuwepo na kufanya shughuli zake kwa ufanisi. Hapo ungeeleweka badala ya kupania kwa makala kadhaa zilizojaa jazba nyingi kutaka CHADEMA IWEPO na ikubaliane na dola tu hata katika mazingira hatarishi kiasi gani!

WHAT’S YOUR REAL MOTIVE?
Mkuu Drifter, kwanza asante kwa mchango wako, very objective, kiukweli tangu nimepandisha uzi huu, wewe ndio mtu wa kwanza kunielewa, kwasababu, kiukweli kabisa, hii jf ya sasa, tuna watu wachache sana, wenye kuweza kusoma bandiko na kisha kujiuliza what is the motive behind.

Chama cha Mapinduzi ni chama cha ukweli na haki, kiliasisiwa na Mwalimu Nyerere, mpenda haki na mtenda haki. Baada ya Mwalimu, CCM ilipitia mageuzi na kuishiwa kuhodhiwa na wenye fedha, hivyo kuzalisha kada kubwa ya makada wa CCM ambao ni makada maslahi, na kwenye uchaguzi, wanakuwa wako tayari kutumia mbinu zozote kushinda uchaguzi. JPM alipoingia, amekuja kuibadili CCM kuirudisha ile CCM ya Nyerere. Sasa ndani ya makada wa CCM, kuna makada wa aina mbili, kuna "CCM Die Hard", hawa ndio wanaotaka kuhakikisha CCM inaupondaponda upinzani na kushinda kwa asilimia 99.9% kwa kutumia mbinu zozote.

Tupo sisi makada "Modern CCM" ambao kutokana na good track ya kazi nzuri ya JPM, CCM innashinda kwa mshindi mzuri safi na clear victory, kushinda kwa haki bila kufanya figisu figisu zozote.

Kwa vile Bunge letu ni Bunge la vyama vingi, mimi naamini kuna baadhi ya wana CCM very genuine, hakupenda kuona baadhi ya wapinzani wakishindwa akiwemo mtu kama Zitto!. Lakini kutokana na wapinzani kukataliwa na wananchi, ili Bunge lichangamke, zile kamati 2 za oversight committee, PAC na LAAC, lazima ziongozwe na wabunge wa upinzania ambao ni vichwa vya ukweli, kwenye hao wabunge wote sijaona watu wa kalibre hiyo ndio maana kila siku, tunamuomba Mwenyekiti wetu, JPM, katika zile nafasi zake 10, awateua wapinzani 4, Zitto, JJ Mnyika, Mbatia na kale kabinti Queen Sendiga.

Ili CCM itawale vizuri inahitaji Upinzani makini, ndio maana kila uchao, naibalasa Chadema humu na ACT Zanzibar, waache ujinga wa kususa. Ili kusasa kwa akili ni kususa kama kwa kususa huko utaachieve something, lakini kususa tuu for the sake of kususa, huku you won't achieve anything huu ni ujinga!.

Karibu tena.
P
 
Tupo tayari chama kife lakini hatutakubali kutumika kama muhuri wa kuhalalisha mateso kwa Watanzania. DEMOKRASIA NI MUHIMU KULIKO UHAI WA CHADEMA, TANZANIA NA WATANZANIA NI MUHIMU KULIKO UHAI WA CHADEMA. Kikubwa zaidi hatusikilizi ushauri wa WANAFKI.
 
Tupo tayari chama kife LAKINI hatutakubali kutumika kama muhuri wa kuhalalisha mateso kwa watanzania, DEMOKRASIA NI MUHIMU KULIKO UHAI WA CHADEMA , TANZANIA NA WATANZANIA NI MUHIMU KULIKO UHAI WA CHADEMA. Kikubwa zaidi hatusikilizi ushauri wa WANAFKI
Kama mnavyoomba misaada isije kwa waathirika wala misaada ya kibinaadam isifike ili watanzania wote wafe halafu wewe na kichaa mwenzako Lissu mpate demokrasia
 
Kwahiyo ni vigumu kundi 19 kuondoka Chadema wataomba msamaha kwakuwa wengi wao wana mahusiano ya mke na mume, wana watoto, wengine ni wedding in waiting n.k
Damu nzito kuliko maji, kwa hilo Chadema wameipiku CCM. Du siasa mchezo mchafu.
 
Maneno mengi sana Pasco. Swali ni moja kwanini CCM na serikali yake wanaingilia uendeshaji wa vyama vingine?! Je, ni kwa sababu Ndugai na bosi wake wamejitungia sheria ya kutokushtakiwa?! Au ni mission ya CCM kuvicontrol vyama pinzani!
 
Maneno mengi sana Pasco. Swali ni moja kwanini Ccm na serikali yake wanaingilia uendeshaji wa vyama vingine ?! Je ni kwa sababu Ndugai na bosi wake wamejitungia sheria ya kutokushtakiwa ?!. Au ni mission ya Ccm kuvicontrol vyama pinzani ?!
Jaduong hiyo sheria ya kutoshitakiwa viongozi wa Ccm nani aliitunga?
 
Tupo tayari chama kife LAKINI hatutakubali kutumika kama muhuri wa kuhalalisha mateso kwa watanzania,DEMOKRASIA NI MUHIMU KULIKO UHAI WA CHADEMA ,TANZANIA NA WATANZANIA NI MUHIMU KULIKO UHAI WA CHADEMA,kikubwa zaidi hatusikilizi ushauri wa WANAFKI
Ameeeeeeeen.
Ikibidi tutaendelea kupigania uhuru wetu na haki kutoka kwa wakoloni weusi, kivingine.
 
Hivi swali lako la usiginaji katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unaofanywa na awamu ya Tano lilikufa "natural death" tangu tulipoambiwa maana ya jina lako kuwa ni "njaa"? Kazi ya Chadema ilikuwa ni moja tu katika context ya "ubunge wa viti maalum wa akina Halima", kuwafutia uanachama kulingana na makosa waliyoyafanya dhidi ya chama, basi! Unataka waandike barua ya nini tena kwa spika Mr. "njaa"? Acha propaganda za chekechea mzee!
 
Wanachopaswa kufanya ni kutafuta eneo la ofisi hapo Dodoma, wafungue bank account, ruzuku yote ya Chadema, watakabidhiwa wao, na kulisongesha hadi 2025!. Uamuzi huu wa kulisongesha una changamoto moja, baadhi ya hao 19, ni wake wa ndoa wa wana CC wa Chadema, baadhi ni wenzi wanaoishi nao kinyumba na baadhi ni 'vidumu' vya viongozi wa Chadema, kushi nyumba moja, kulala chumba kimoja, kitanda kimoja kati ya kiongozi halali na muasi, ni changamoto!, tena kuna wengine wameisha anza kujenga familia, familia zisiparanganyiwishwe na siasa za kujinga jinga kama hizi!. By Pascal Mayalla wa JF
 
Back
Top Bottom