nimejifunza kitu ilaa mimi pia nilikuwa na mpango wakuangiza mashine za kuoshea magar so ni website gan ina bidhaa nzur kama izoo na zenye quality
 
Mwenye uzoefu na gari za mazda demio anipatie. Nataka kujua spare zake zinapatikana hapa Tanzania kwa urahisi au gharama ni kubwa sana?

Umepotea njia cheki hapahapa jukwaani kuna uzi unaoelezea mambo ya ununuzi wa magari. Karibu kila kitu kimediskasiwa huko
 
Imekuwa ni shida sana kwa watanzania wengi kununua bidhaaa katika masoko haya ya mtandaoni kwani mengi huwa hayakupi fursa ya kutumiwa mzigo wako moja kwa moja Tanzania. baadhi ya thread zilianzishwa na zimeelezea mengi sana kuhusiana na manunuzi haya ya mtandaoni, ila tulipata ufumbuzi mdogo. Nimejaribu kupitia pitia forums nyingi nichanganue namna mbadala ya kupata mizigo bila ya kutumia gharama nyingi. hii ni kwa kutumia FOWARDING COMPANIES ambazo kazi yake ni 1: Kukupatia anuani ya Marekani (au popote iliopo ila nashauri marekani au uingereza UK) au US Shipping Address 2:Kupokea mzigo kwenye soko ulilotumia (eidha amazon,ebay au lolote lile lisilo ship Tanzania) 3:Kukutumia mzigo wewe hapo ulipo kwa wakala kama DHL,FEDEX,UPS,USPS NK baada ya kujua kazi ya fowarding company unahitaji kuwa na vigezo vifuatavyo (kwa wageni wasiofahamu/hawajapitia previous threads:

1:CREDIT CARD (KADI YA BENKI) INAYOFANYA ONLINE PURCHASES;
Hii inapatikana almost bank zote hapa Tanzania (kasoro NMB sina uhakika), ni kadi yeyote ya visa au mastercard unachotakiwa ni kwenda kwenye tawi la benki yako na kuomba fomu ya kuruhusu kadi yako ifanye malipo ya mtandaoni(online purchases) na mara nyingi huchukua maximum 24hours kuactivate.

2:KUJIUNGA NA PAYPAL
Hiii ni kampuni inayolinda malipo yako kwa kutomuonesha muuzaji details (nyaraka) za kadi yako kama number na css ambayo vitampa muuzaji access ya kuchukua pesa zako. Ila kwa paypal utalindwa na kurudishiwa pesa pale panapotokea shida au huduma mbaya.

3:KUJIUNGA NA FOWARDING COMPANY

Hii hatua ni ya wewe kwenda kwenye website (tovuti) za hizi fowarding company na kujiunga (sighnup) nazo/nayo ili zianze kukupatia huduma... nitaelezea chini zaidi kuhusu ipi ni ipi na huduma zao zikoje na faida na hasara za kila moja ili ujichagulie wewe mwenyewe binafsi

4:KUTAMBUA SOKO BORA LENYE HUDUMA NZURI(ONLINE MARKET)
Hapa tunazungumzia website za masoko kama ebay,amazon, bestbuy, apple.com, dell.com, toshiba.com nk.. masoko haya ndipo utakapo nunua bidhaa yako.

PROCESS NZIMA KUANZIA UNANUNUA MPAKA MZIGO UNAKUFIKIA IKOJE?
hii iko hivi.... 1:Ingia katika soko lako ulilolichagua au unalopendelea, hapa nasuggest kutumia sana amazon(ndilo ninaloliamini) amazon ukiingia utakuta bidhaa nyingi ila kuwa makini kuchukua zile bidhaa zilizo na alama ya prime chini...alama hiyo inamaanisha kuwa huo mzigo unauzwa, utapakiwa, na kutumwa na amazon wenyewe, so no utapeli hapo, yani u get what u wanted. 2:Nunua na kuagiza kitu kwenda kwenye address ya fowarding company ulioichagua, hivyo mzigo ulioununua utaenda moja kwa moja kwenye company yako, wao wakishaupata watakutumia e-mail uthibitishe au uchague courier wa kukutumia mzigo wako, hapo ndio utachagua either dhl,ups,fedex nk.wao watakutumia na kuchukua kiasi chao cha pesa ya huduma na kukutumia mzigo pamoja na kukupatia tracking number ya kujua mzigo wako ulipo na utaupokea vyema.

FOWARDING COMPANIES ZENYEWE:

1: MYUS.COM link- MyUS.com - #1 International Shipping, Mail and Package Forwarding Service - MyUS.comhii ni company niliyoitumia na nina expirience nayo ya mizigo miwili, hawa ni waaminifu wana charge pesa kidogo na huwa hawachukui muda kukutumia mzigo wako. yaani unafika leo hata ukitaka utumwe leo unatumwa, na utafika upesi sana bila ya zengwe lolote.
Ubaya wao: wanatumia sana DHL ambayo kwa mizigo mikubwa ni gharama sana kwa mtanzania wa kawaida, kiasi cha dola kumi kujiunga na huduma zao
Uzuri wao: watakutumia mzigo hata kama utakuwa hauna pesa kwenye account yako, watakujulisha ni duka lipi lina discount ya kutumia huduma zao, watakukumbusha kulipa deni lao, utapewa muda wa miezi miwili kulipa pesa yao,

2:COMGATEWAY
link-http://comgateway.com/ hawa pia ni fowarding company nzuri sana (thanks tu Mwl.RCT), nimepitia site yao na uona wana policy nzuri sana,cha kwanza ni sales tax-free U.S. online shopping yaani punguzo la kodi ya kufanya manunuzi marekani,hii inapelekea huduma zao kuwa nafuu zaidi,pia wana ushirika na shipping courie DHL na FEDEX hivyo kufanya huduma zao kuwa rahisi zaidi.pia wanakupa habari kuhusu discount za masoko mbalimbali kama myus..

3:BORDERLINX
link- Buy in the USA, ship to Belgium with Borderlinx hawa pia ni wazuri sana na hawana tofauti sana na stackry ... wanawiana ingawa ni competitors wakubwa hivyo inakupa urahisi wa kuwatumia..hawa pia hawana registration fee na wanakupa option tofauti tofauti za kutumiwa mzigo wako.

4:SHIPITO
link-USA Address & Mail Forwarding – Shipito.com | English hii pia ni kampuni kongwe ya fowarding na wao gharama zao ni nafuu sana ingawa wanapokea malalamiko mengi sana kutoka kwa wateja wao ukiangalia kwenye forums nyingi.ila kiujumla ni wazuri kwasababu malalamiko ni madogo kulinganisha na ufanisi na pia wanajua na ni wazoefu sana na kazi yao

5:STACKRY
link- Stackry - US shopping, global shipping hii nayo haina tofauti na myus isipokuwa hawa wao hawana kiasi cha kulipia kujiunga nao na wao pia wanakupa option nyingi za kutumia mizigo yako na mabo yao pia ni mazuri kulinganisha na comment wanazopokea kutoka kwa wateja wao. waungwana ni hayo tu niliyo nayo, kazi kwenu ni kufanya utafiti na pia kuangalia na kuchunguza mabo kabla ya kuchukua uamuzi. STACKRY na BORDERLINX walikuwa recommended sana na wanasifiwa mno angalia hii link -http://tech-vise.com/10-parcel-forwarding-services-for-international-shoppers/ pitia hizo websites na ujionee mwenyewe chagua moja na utazame kama wanakufaa.

HUU NI MTAZAMO WANGU BINAFSI WAKUU please evaluate kindly.

nilikuwa nataka kuonyesha steps ila naona thread haitoshi . maana nimeagiza mzigo na nimechukua hatua zote ili mpate kuona ila ithink there r limits.. help Mwl.RCT

VP sis tunaoagiza mizgo China njia gani rahisi kwetu kampuni gani inafaa
 
Kuhusu manunuzi huko china, Nilijaribu kununua kitu ali express kwa kutumia alipay, ile kujaribu kuunganisha kadi yangu ya visa kwenye ali pay nikakuta Tanzania haimo katika orodha ya inchi zinazoweza kutumia ali pay.

Nlijaribu kuwasiliana na jamaa wa ali pay wakaniambia bado wako kwenye mazungumzo ya kutuwezesha kutumia hiyo njia ya malipo salama ambayo ki ukweli ina watumiaji wengi kuliko paypal na inakubalika sana china.
Nilichogundua ni kuwa Tanzania bado iko nyuma sana kwenye mambo ya biashara ya mtandaoni duniani na serikali haifanyi juhudi ya kutosha kuruhusu watanzania na sisi kushiriki kwenye biashara hiyo ambayo inakua kila siku.

Labda kuingia Kwa JPM hapa kazi tu inaweza kuharakisha mambo
 
Jamani nawashukuru sana kwa uzi wenu. Lakini mimi nina tatizo moja tu.

Most of hizo forwarding companies mlizozielezea ni za US na zinaship mizigo from US to other countries.

Shida yangu kubwa ilikuwa ni kupata forwarding company ambayo ni ya UK au ina warehouse UK na wanaship mizigo kuja bongo.
Asanteni
 
  • Thanks
Reactions: P.J
Tukupatua tovuti..na blog . domain name hosting kwa bei nsuri sana karibuni.. whatsapp 0769338868
 
habari zenu wanajukwaa,naomba kujuzwa iwapo kuna kampuni au mtu binafsi anayetoa huduma ya manunuzi nje ya nchi.namaanisha kufanya process zote toka manunuzi hadi mteja kupokea mzigo wake ofisini kwao.natanguliza shukrani.
 
Jamani nawashukuru sana kwa uzi wenu....... Lakini mimi nina tatizo moja tu..... Most of hizo forwarding companies mlizozielezea ni za US na zinaship mizigo from US to other countries..... Shida yangu kubwa ilikuwa ni kupata forwarding company ambayo ni ya UK au ina warehouse UK na wanaship mizigo kuja bongo...
Asanteni
Mzigo wa aina gani? Company zipo nyingi tu, na watu kila siku wanasafirisha mizigo
 
habari zenu wanajukwaa,naomba kujuzwa iwapo kuna kampuni au mtu binafsi anayetoa huduma ya manunuzi nje ya nchi.namaanisha kufanya process zote toka manunuzi hadi mteja kupokea mzigo wake ofisini kwao.natanguliza shukrani.
Fafanua kidogo.
Unahitaji mtu au company ikununulie mzigo kutoka nje na kukuletea tz? Which country huo Mzigo unahitaji?
 
Mwenye uzoefu na gari za mazda demio anipatie. Intems of spare je kwa nchini zinapatikana? Je zipo kama IST au swift kwa ukubwa.
Usije kununuwa mazda ni bomb kabisa, zina engine ya ford, ford ni gari mbovu kabisa.
 
Kuhusu manunuzi huko china, Nilijaribu kununua kitu ali express kwa kutumia alipay, ile kujaribu kuunganisha kadi yangu ya visa kwenye ali pay nikakuta Tanzania haimo katika orodha ya inchi zinazoweza kutumia ali pay.

Nlijaribu kuwasiliana na jamaa wa ali pay wakaniambia bado wako kwenye mazungumzo ya kutuwezesha kutumia hiyo njia ya malipo salama ambayo ki ukweli ina watumiaji wengi kuliko paypal na inakubalika sana china.
Nilichogundua ni kuwa Tanzania bado iko nyuma sana kwenye mambo ya biashara ya mtandaoni duniani na serikali haifanyi juhudi ya kutosha kuruhusu watanzania na sisi kushiriki kwenye biashara hiyo ambayo inakua kila siku.

Labda kuingia Kwa JPM hapa kazi tu inaweza kuharakisha mambo
Mkuu nini faida ya kununua mtandaoni?? Ilihali hapa tanzamia unalipia bei kubwa sana ktk kodi mara 3 zaid ya thaman ya bidhaa??
 
Jamani nawashukuru sana kwa uzi wenu....... Lakini mimi nina tatizo moja tu..... Most of hizo forwarding companies mlizozielezea ni za US na zinaship mizigo from US to other countries..... Shida yangu kubwa ilikuwa ni kupata forwarding company ambayo ni ya UK au ina warehouse UK na wanaship mizigo kuja bongo...
Asanteni
WAtumie hawa
Code:
 https://www.forward2me.com/
How It Works

Step 1 - You sign up to get a forward2me UK address

Follow the simple steps to sign up with forward2me and receive your personal UK forwarding address. After you create your account (currently free until end of March 2016), you will receive your new address.

Step 2 - You order your goods

Go to your favourite UK or EU shops such as Amazon UK and order your goods using your forward2me address as the delivery address.

Step 3 - We receive your parcel

Upon receiving your parcel we may elect to check its contents to ensure it can be safely and legally shipped to your forwarding address. Please note that it is your responsibility to ensure you only send items that may be legally and safely imported to your country of residence. We will then send you an e-mail informing you of its arrival.

Step 4 - We ship your parcel

You can login to your account and select your preferred courier and pay for the shipping. You can pay with a credit card, PayPal or bank transfer account. If you make payment before 11:00am UK time on a work day then we will typically ship the same day.

Step 5 - Your parcel arrives at your doorstep

Depending on the courier you select you can expect to receive delivery of your parcel within 1 to 4 working days of the date of dispatch from our depot. This can vary depending on local customs processes which are outside our control. Customs duties may be payable depending upon the destination country and are your responsibility. You will need to sign for your goods when they arrive.
 
Mkuu nini faida ya kununua mtandaoni?? Ilihali hapa tanzamia unalipia bei kubwa sana ktk kodi mara 3 zaid ya thaman ya bidhaa??
Inategemea ni bidhaa gani unahitaji, Sio kila bidhaa ni ya kuagiza nje ya nchi. Tunaagiza nje ya nchi bidhaa ambazo
  • Hazipatikana kiurahisi /huwezi pata kabisa hapa Tanzania mfano: "Kindle paperwhite"
  • Kwa soko la ndani baadhi ya bidhaa bei yake ya kununua ni x2 au x3 ya ghalam za kununulia nje ya nchi + shipping + kodi , Sababu yule anayeuza naye anahitaji faida
  • Tunaagiza nje ya nchi ili kubapata bidhaa madhubuti, bila kujali ghalama utakayotumia kufikisha mzigo hapa Tanzania.
  • Kuna bidhaa hazitozwi kodi, Hivyo ukinunua na ukapata Free shipping utajikuta umeokoa nusu ye fedha ambayo ingepotea iwapo ungenunua hapa nchini.
 
habari zenu wanajukwaa,naomba kujuzwa iwapo kuna kampuni au mtu binafsi anayetoa huduma ya manunuzi nje ya nchi.namaanisha kufanya process zote toka manunuzi hadi mteja kupokea mzigo wake ofisini kwao.natanguliza shukrani.
Natoa hiyo huduma. Na mzigo wako utaupata popote ulipo. Hivi karibuni nitaweka Thread maalumu kwa kazi hii. Nitumie PM au email mw1rct(at)gmail.com
 
Inategemea ni bidhaa gani unahitaji, Sio kila bidhaa ni ya kuagiza nje ya nchi. Tunaagiza nje ya nchi bidhaa ambazo
  • Hazipatikana kiurahisi /huwezi pata kabisa hapa Tanzania mfano: "Kindle paperwhite"
  • Kwa soko la ndani baadhi ya bidhaa bei yake ya kununua ni x2 au x3 ya ghalam za kununulia nje ya nchi + shipping + kodi , Sababu yule anayeuza naye anahitaji faida
  • Tunaagiza nje ya nchi ili kubapata bidhaa madhubuti, bila kujali ghalama utakayotumia kufikisha mzigo hapa Tanzania.
  • Kuna bidhaa hazitozwi kodi, Hivyo ukinunua na ukapata Free shipping utajikuta umeokoa nusu ye fedha ambayo ingepotea iwapo ungenunua hapa nchini.
Mkuu unaweza kutusaidia labda kwa uzoefu wako ni bidhaa zipi ambazo unapata free shipping na zipi hupati

Maana wengine mfano mimi sijawahi kuagiza ila nimejikuta navutika niagize maelezo yako nimeyaelewa sana.
Ahsante
 
Free shipping hutegemea mambo mengi kama.
  1. Je huo mzigo unataka usafirishwe kwa njia ipi (a) Taratibu ambapo huchukua siku 15 hadi 60 ndipo mzigo ukufikie (b) Njia ya haraka - Hapa lazima ulipie shipping cost - ambapo kamuni kama DHL, ARAMEX, TNT n.k wanahusika
  2. Ukubwa / Uzito wa mzigo husika - Kadri mzigo unavyokuwa mkubwa ndio jinsi ghalama ya kusafirisha huongezeka.
  3. Seller husika wa hiyo bidhaa
Ni vigumu kusema kuwa bidhaa A, B na C hizi lazima upate free shipping. Hapana haiwezekani

Ila kuna baadhi ya site hutoa free shipping (huchukua muda wa siku 14 - 21) kwa bidhaa zao zote. Bila kujali mzigo mkubwa kiasi gani. Ila ukihitaji kwa haraka ndipo utalipia Mfano hii site:
Code:
 http://www.gearbest.com

Pia kwa soko kam ebay unapotafuta bidhaa yeyote weka tiki mahala walipo andika "free internetional shipping"
free.png

Sijui kama nitakuwa nimejibu swali lako vyema.

Karibu
 
Nimekuelewa mkuu kupita maelezo
 
Back
Top Bottom