John Haramba
JF-Expert Member
- Feb 4, 2022
- 365
- 1,373
Ubalozi wa Tanzania uliopo Urusi umetoa taarifa juu ya njia ambazo wanafunzi Watanzania walipo katika Chuo cha Taifa cha Sumy Nchini Ukraine wanazotakiwa kutumia pamoja na namba za simu kwa ajili ya mawasiliano wakati watakapokuwa wanaelekea sehemu salama kupokelewa.
Wanafunzi wanatakiwa kuelekea eneo la Sudja, watapokelewa na Jeshi la Urusi kisha kusafirishwa hadi Belgorod, hapo watakabidhiwa kwa maofisa wa Ubalozi wa Tanzania Nchini Urusi kwa taratibu za kurejeshwa Tanzania.
Wanafunzi wameshauriwa kutoka kwa makundi wakiwa na bendera ya Tanzania ili kuwatambulisha kwenye safe corridor, pia wanaweza kuwasiliana na timu ya mapokezi kwa namba za simu walizowapatia.