Kwanini polisi nchini Urusi wanaacha kazi na kujikita katika nyanja zingine?

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,331
33,141
Imeandikwa na OLESYA GERASIMENKO / Ikahaririwa na LORNA HANKIN / Ikahakikiwa na BY SAM HORTI
Putin on a poster with a police man

CHANZO CHA PICHA,AFP
Katika nyakati za alfajiri mnamo tarehe 14 Januari mwaka 2020, vilio vilisikika katika jumba la ghorofa katika wilaya ya kusini mwa Urusi Leningradsky.
Akiwa ameshtuka na kuogopa, mkazi mmoja aliipigia polisi simu kuripoti kile kilichosikika kama shambulio dhidi ya mwanamke.
Lakini hakuna aliyekuja.
Mayowe yaliendelea, pamoja na kishindo kikubwa na vilio vya kuomba msaada. Simu sita zaidi zilipigwa kwa huduma za dharura lakini bado hakuna maafisa wa polisi waliowasili kusaidia.
Majirani, sasa wakihofia mabaya zaidi, waliamua kuchukua hatua wenyewe, wakavunja mlango wa jumba hilo na kuingi ndani.
Lakini walikuwa wamechelewa.
Kelele zilikuwa hazisikiki tena. Mwanamke alikuwa ameshafariki dunia.
Polisi hawakuchukua hatua kwa wakati ufaao.
Vera Pekhteleva alikuwa amedungwa kisu mara nyingi, kupigwa na kunyogwa na mpenzi wake wa zamani kwa kutumia chuma, katika shambulio liliodumu kwa saa tatu na nusu.
Vera Pekhteleva

CHANZO CHA PICHA,FAMILY HANDOUT
Maelezo ya picha,
Vera Pekhteleva aliteswa kabla ya kuuawa na mpenzi wake wa zamani - na polisi hawakujitokeza.

Wakati huo, polisi walisema hakukuwa na maafisa au magari ya kushika doria katika eneo hilo kutekeleza kazi yao.
Lakini baadaye, maafisa watano walipatikana na hatia ya kusababisha kifo kwa uzembe na walihukumiwa kifungo cha miezi 18 jela, na kusimamishwa kazi kwa miaka miwili.
Mahakama ilisema hukumu hizo, ambazo zilionekana na wengi kuwa nyepesi, zinafaa kwa sababu uhaba wa maafisa ulikuwa tatizo kwa "kikosi kizima".
Urusi ina mojawapo ya vikosi vikubwa zaidi vya polisi duniani, ikiajiri zaidi ya maafisa 900,000 kuhudumia idadi ya watu milioni 146, kulingana na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Urusi.
Ina takriban maafisa 630 kwa kila watu 100,000 - zaidi ya mara mbili ya Marekani au Uingereza.
Lakini mwezi Agosti, Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani Vladimir Kolokoltsev alisema nchi hiyo ina uhaba "mkubwa" wa maafisa wa polisi, ambao unaweza kuathiri viwango vya uhalifu.
Ukubwa wa eneo la Urusi na ukosefu wa wafanyikazi kunaweza kulaumiwa kwa kiasi fulani.
Lakini matatizo ya hivi majuzi yanatokana na kupungua kwa idadi kubwa ya wafanyakazi - na wengi wa maafisa hao wanaoondoka ni maafisa wazoefu na wenye vipaji.

Mishahara duni, msongo wa mawazo na ufisadi​

Maafisa wengi wa zamani wa polisi ya Urusi wameiambia BBC kwamba wanaacha kazi katika kikosi cha polisi na kuamua kujiunga na kazi mbadala zisizowaletea msongo wa mawazo na zenye malipo mazuri.
“Bado hawajaongeza mshahara kabisa,” afisa wa zamani kutoka Rostov Kusini Magharibi mwa Urusi, amesema.
“Baada ya mfumuko wa bei, mshahara hautoshelezi mahitaji.” Amecha kazi ya polisi na kugeuka kuwa udereva wa teksi.
Rafiki wake, ambaye pia alikuwa afisa wa polisi, sasa anafanya kazi ya kuwapelekea watu bidhaa.
Wawili hao hupokea mshahara maradufu zaidi ya ule waliokuwa wakilipwa wakiwa bado maafisa wa polisi.
“Nilifika cheo cha meja (cheo sawia na sajenti nchini Uingereza). Lakini mtu anayefanya kazi ya kuuza duka analipwa vizuri ikilinganishwa na mimi - kazi ambayo ni hatari sana. Ni mtu mjinga tu ambaye anaweza kujiunga na kikosi cha polisi kwa sasa,” afisa huyo wa zamani kutoka Rostiv alisema.
BBC imegundua kwamba maafisa wa polisi ambao wanafanyishwa kazi kupita kiasi sasa wanakataa kufungua kesi zilizowasilishwa na umma, hata baada ya taarifa kutolewa.
"Kila mtu huwa na siku 10 za kuchunguza taarifa, ama ziwe tano au 50, bila shaka, ubora wa kazi unazorota," anasema afisa mmoja wa upelelezo kutoka eneo Siberia la Urusi.
"Ikiwa kuna msururu wa mambo 10 au zaidi wanapaswa kufanya - kuwaita majirani, kuwahoji mashahidi, kutembelea eneo la uhalifu - watafanya moja au mbili, na kuandika kwamba 'haikuwezekani' kukamilisha mengine."
Kisha wanakataa kufungua mashtaka - kwa hivyo hakutakuwa na uchunguzi," anasema.
Police van and police officer in Russia

CHANZO CHA PICHA,EPA
Maelezo ya picha,
Maafisa wengi wa zamani wa polisi wa Urusi waliiambia BBC kuwa wanaacha kazi ili kujiunga na kazi zingine zisizo na mahitaji mengi na zinalipa vizuri zaidi

Kadiri idadi ya maafisa inavyopungua, shinikizo kwa wale waliosalia huongezeka.
Maafisa wa zamani wameambia BBC kuwa hii inasababisha ufisadi.
"Maafisa wanatupilia mbali ushahidi, wanakamata watu wengi zaidi, tunashuhudia hii kila wakati," anasema mkuu wa polisi kutoka jiji la Urusi la Tomsk.
"Itakuwa mbaya zaidi. Kutakuwa na ushahidi wa uwongo, kulenga kukandamiza watu fulani, hakutakuwa na wakati wa kuchunguza chochote vizuri.
"Una uongozi na unahitaji kuondokana nao?
Ni rahisi zaidi kumburuta mshukiwa wa kwanza hadi kituoni na kumpiga, kwa hivyo lawama anachukua yeye."
Baadhi ya maofisa wanafungiwa kwa matendo yao – hiyo inakuwa ni kupunguza nguvu zaidi.
Hilo lilimtokea Sergei, afisa wa zamani wa polisi wa miaka sita, aliyefungwa jela kwa kumpiga mlanguzi wa dawa za kulevya.
Sergei anasema alihisi shinikizo la kumkamata mfanyabiashara huyo na kumpiga tu alipokuwa karibu kula dawa zake ili kuficha ushahidi.
Pia anaiambia BBC kuwa rasilimali za polisi zilikuwa kidogo sana ikamlazimu kujilipia mahitaji muhimu ya kazi.
"Nilikuwa nikitumia gari langu, nilinunua karatasi yangu, wino, na mashine ya kuchapisha; kompyuta yangu, meza yangu, kiti changu, petroli yangu... Niliweka vigae vyangu vya sakafu [ofisini], nikatengeneza kila kitu."
Afisa wa zamani kutoka Urusi ya kati anasema kuwa nafasi zilizoachwa wazi hazijajazwa kwa muda mrefu.
"Kumekuwa na uhaba kwa miaka mingi. Nilianza kazi mwaka 2015, na watu wawili tu ndio wamejiunga na timu yetu katika miaka minane iliyopita, wakati 15 wameondoka."
Na kwa mujibu wa vyanzo kadhaa vya BBC, ikiwa ni pamoja na sajini wawili na meja mmoja, Wizara ya Mambo ya Ndani ilifanya msako wa maafisa ambao walikuwa na uhusiano na mwanasiasa wa upinzani, Alexei Navalny, ambaye amekuwa akishikiliwa katika gereza la mbali tangu 2021.
Maafisa wa muda mrefu, wenye uzoefu walifukuzwa kazi katika kukabiliana na hili.
Chanzo kimoja kilisema Huduma ya Usalama ya Shirikisho la Moscow ilikusanya orodha ya wafuasi wa Navalny kulingana na hifadhidata iliyodukuliwa ya anwani za barua pepe

Athari ya vita dhidi ya Ukraine​

Idadi ya maafisa wa polisi nchini Urusi ilikuwa ikipungua hata kabla ya kuanza kwa vita nchini Ukraine.
Awali, vita viliwashawishi baadhi ya maafisa kusalia katika kikosi cha polisi.
Maafisa wa polisi wa Urusi wana kinga dhidi ya kuitwa kwenda kushiriki vitani, kwa hivyo baadhi ya maafisa wa polisi walikuwa wakikaribia kustaafu, wakati Urusi ilipoivamia Ukraine wengi waliamua kubaki ili kuepuka kupigana katika vita.
"Aidha ungeamua kusalia, au uliondoka na kuandikishwa jeshini,” anaeleza ofisa mmoja kutoka Moscow. "Najua kulikuwa na wasimamizi ambao waliandika orodha ya kila mtu ambaye alitishia kuacha kazi na kuipitisha moja kwa moja kwa waajiri [wa jeshi]. Kila mtu alikuwa na hofu kubwa."
Lakini huku vita vikiendelea, idadi ya maafisa wa polisi inapungua.
Kikosi hicho hakiwezi kujaza mapengo yaliyopo - mbali na kuajiri wafanyakazi 40,000 wa ziada ambao Wizara ya Mambo ya Ndani inasema wanahitajika huko Donetsk na Luhansk, maeneo ya Ukraine ambayo Urusi inayakalia kwa kiasi fulani.
.

CHANZO CHA PICHA,REUTERS
Maelezo ya picha,
Maafisa wa polisi wa Urusi hawaruhusiwi kutoa maoni yao kuhusu vita

Urusi inatabiri kuwa itahitaji maafisa wengine 42,000 kufikia 2026 ikiwa itachukua maeneo zaidi.
Kwa maafisa wa polisi waliopo kazini, kutoa maoni yao juu ya vita hairuhusiwi.
Hawaruhusiwi hata kuiita vita.
"Maafisa lazima wafunge midomo yao," mpelelezi mmoja anasema.
"Hatuwezi kuwa na maoni ya kibinafsi kuhusu 'operesheni maalum ya kijeshi' - au watatufuta kazi."
BBC pia imeambiwa maafisa wanachoka sana kwa sababu ya kazi za ziada zenye kutokana na vita.
Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Ndani kutoka miji mitatu ya Urusi ya Tomsk, Yekaterinburg na Yaroslavl wanadai kuwa sasa wanatumia muda wao mwingi kuchunguza na kupitia tena "mashtaka yanaendelea kujitokeza kila siku kwa watu wanaolidharau jeshi".
"Watu siku zote wanatafuta kisingizio cha kushutumu mtu," mkuu wa zamani kutoka Tomsk anasema.
"Hakuna mtu karibu... Kila mtu amekwenda kumuangalia bibi fulani ambaye aliona kitu kinachofanan na bendera ya Ukraine.
"Naona tunakoelekea," anasema. "Tayari kuna msisitizo juu ya uhalifu dhidi ya serikali. Kwenda mbele, kesi nyingi zitakuwa katika kitengo hiki," anatabiri.
"Kuhusu matatizo ya kweli yanayoathiri watu wa kawaida? Utekaji nyara, wizi, ubakaji, mauaji ... hakutakuwa na muda wa kufanya uchunguzi." chanzo BBC
 
Warusi waungane kumng'oa Putin na genge lake ili kuiokoa Urusi.
Mimi nilidhani umechukizwa tu na uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine,kumbe una chuki ya kudumu dhidi ya taifa la Urusi wakati huna vinasaba na n hi hiyo.
Matatizo yapo Kila nchi duniani.usa Kuna matatizo kibao,polisi wanua watu weusi kwa makosa mepesi kabisa,hujasema wananchi wawatoe Marais wao,vijana wadogo wa kimarekani wanauana wenyewe kwa wenyewe mashuleni hujasema wamarekani wawatoe Marais wao.
Acha chuki.
 
Lazima mjue kua Putin kaingia cha kike,ainue tu dela lake achuchumae.
Asingevamia ukraine 2022 angebaki na crimea halafu hizi rasilimali anazopoteza vitani angetumia kuimarisha hali ya maisha!
sasahivi uchumi unazorota,jeshi lake linapungua nguvu taratibu,raia wanakufa na ukraine wameshaamua kua wanaitaka mpaka crimea..jamaa kabugi.
 
Vp kule Tanganyika,hali ikoje?
 
Naona tunatofautiana uelewa.
Putin tayari keshaikomboa Dunia.
Mafanikio anayoyapata yaendelea kuishangaza Dunia.
Kaifanya Dunia ijionee yenyewe kua kumbe NATO ni kwa ajili ya vi nchi vidogo TU.
 
Hao polisi wa Russia wanafanya kazi katika mazingira magumu sana na inaonekana hawana tofauti sana na polisi wa hizi "Shithole Countries" ambao ili mpate angalau unafuu kidogo lazima muisaidie chama tawala kupora uchaguzi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom