Mkutano wa Urusi na Afrika: Putin anataka kuongeza ushawishi

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,329
33,138

Mkutano wa Urusi na Afrika: Putin anataka kuongeza ushawishi​

Putin

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
28 Julai 2023
Wakati Rais Vladimir Putin akifungua mkutano wa kilele wa Urusi na Afrika mjini St Petersburg leo Alhamisi, orodha ya waliohudhuria inatazamwa kwa karibu - huko Paris, Washington, London, na katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa huko New York.
Lakini Waafrika wataliona tukio hilo kwa njia tofauti kabisa.

Kwa wizara za mambo ya nje za Magharibi zinazohangaishwa na azma ya Kremlin iliyotangaza kupanua wigo wake wa kisiasa, kijeshi na kiuchumi kusini mwa jangwa la Sahara, mkutano huo ni kiashirio cha jinsi ushawishi wa Urusi sasa unaweza kuenea na wapi utakutana na ukaribisho wa kirafiki.
Tofauti na mkutano wa awali wa Urusi na Afrika mwaka 2019, uliohudhuriwa na viongozi 43 wa Afrika, wakati huu ni viongozi 17 pekee wanaohudhuria huko St Petersburg.

Lakini ni yupi kati yao atachukua majukumu maarufu ya kuzungumza katika mkutano huo? Je, ni mikataba gani itaingiwa na Bw Putin?

Watunga sera wa Ulaya na Marekani hadi hivi majuzi waliona China kama mshindani wao mkuu barani Afrika - lakini sasa wanajikuta wakitazama kwa masikitiko makubwa kurudi kwa uthubutu wa Urusi, ikidhihirishwa na uwepo wa mamluki wa Wagner nchini Mali, Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR), Libya na, kwa ufupi, kaskazini mwa Msumbiji.

Na bila shaka, uvamizi wa Ukraine umeongeza kwa kiasi kikubwa kutoaminiana kwa nchi za Magharibi juu ya matarajio ya Urusi kote ulimwenguni.

Bado kuna maoni machache kwamba viongozi wa Kiafrika wawe sehemu ya i mtazamo huu. Nchi nyingi za bara hili, hata zile ambazo zimepiga kura mara kwa mara katika Umoja wa Mataifa kulaani shambulio la Ukraine na athari zake, hazitaki kuingizwa katika kuunga mkono "Vita Baridi" mpya au kuwa vibaraka katika mzozo wa ushawishi wa kimataifa.

Vyovyote vile, Urusi ni mmoja tu wa wahusika wakuu kadhaa ambao sasa wanaongeza juhudi za kuwasilisha ushawishi wa kisiasa na kiuchumi barani Afrika - pamoja na sio China tu, bali pia India, Uturuki, mataifa ya Ghuba, Korea Kusini na, bila shaka, mataifa ya Magharibi na Japani.

Baada ya wakati mwingine kuhangaika katika siku za nyuma kuhamasisha misaada ya kimataifa katika kukabiliana na changamoto zao za maendeleo na usalama, serikali za Kiafrika hazipuuzi hatua hizi.
Na Urusi inajua hii. Katika kuelekea mkutano huo, maafisa wake waliahidi mpango mpya wa msaada kwa bara hilo.

Ajenda ya mkutano huo ni pamoja na "jukwaa la kiuchumi na kibinadamu" na wafanyabiashara wa Kiafrika wamealikwa; Kremlin inaahidi misururu ya makubaliano ya kibiashara, uwekezaji, ushirikiano wa kisayansi na kiufundi.

Katika kutekeleza ajenda hii, Urusi inaweza kuendeleza uhusiano wa kitaaluma na utafiti ulioendelezwa wakati wa enzi ya Vita Baridi, wakati Waafrika wengi walisoma katika vyuo vikuu vya Usovieti.

Lakini hiyo haimaanishi washiriki wengi watahudhuria St Petersburg kwa mawazo ya tahadhari - hata kama uungwana wa kidiplomasia utawazuia kuzungumza kwa uwazi.

Ujumbe wa mwezi uliopita wa amani wa viongozi wa Afrika nchini Urusi na Ukraine haukuwa mgumu kuwaambia Bw Putin na Volodymyr Zelensky kwamba vita vinapaswa kukomeshwa, kwa ajili ya ulimwengu mzima.
Na Moscow itakuwa vigumu sana kuimarisha nia njema kwa uamuzi wake wa kuachana na makubaliano ya usafirishaji salama wa nafaka za Ukraine na Urusi kupitia bandari za Bahari Nyeusi, hata kama Bw Putin ameahidi kufidia upungufu huo.

Hiyo inasababisha kuongeza bei ya vyakula katika nchi nyingi za Afrika, na hivyo kusababisha maandamano katika miji kadhaa na shinikizo la kisiasa kwa viongozi.
Protests

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Mali - mshirika mwaminifu wa hivi karibuni ambaye utawala wake kwa kiasi fulani inawategemea wapiganaji wa kundi la Urusi la Wagner kuzuia vikosi vya jihadi - inadai kupokea shehena maalum ya nafaka ya Urusi.
Lakini ni vigumu kufikiria kwamba Bw Putin anaweza kutoa msaada mkubwa kama huu zaidi kwa kundi la washirika wa karibu.

Watumiaji wengi wa nafaka barani Afrika itabidi waendelee kutegemea soko la wazi la dunia - ambapo usambazaji sasa unapungua na bei inaongezeka.

Bw Putin anafahamu vyema msukosuko huu wa kidiplomasia. Je, anaweza kuwa anasubiri mkutano wa kilele labda atoe malipo yanayodaiwa kuwa makubwa kwa mkataba wa nafaka, kwa masharti yaliyobadilishwa kidogo?

Hilo sio suala pekee nyeti kwenye ajenda za Mkutano. Akiwa amefukuzwa Urusi baada ya uasi wake wa hivi majuzi, bosi wa Wagner Yevgeny Prigozhin hivi karibuni aliwaahidi wapiganaji wake kuzingatia zaidi shughuli za Kiafrika.

Licha ya kutoelewana kwake na Bw Putin, hii bila shaka ingesaidia juhudi za Kremlin kupanua uwezo wake wa kushawishi masuala Afrika, hasa katika eneo dhaifu la Sahel - ambapo Rais wa Niger Mohamed Bazoum amepinduliwa na wanajeshi wake.

Wakati Wagner alipohamia Afrika ya Kati (CAR) baada ya Rais Faustin Archange Touadéra kuomba usaidizi wa Urusi ili kuondokana na vikwazo vya silaha vya Umoja wa Mataifa na kujenga upya jeshi lake mwaka wa 2017-18, hii ilionekana kwanza kama nia ya kuangaliwa, iliyolenga kutuma ujumbe kwamba "Moscow imerejea" baada ya zaidi ya miongo miwili ya kutokuwa na ushawishi baada ya kuanguka kwa Umoja wa Kisovyeti.

Lakini kufikia wakati Wagner aliwasili nchini Mali mwaka 2021, kwa mwaliko wa wanajeshi walionyakua mamlaka mwaka mmoja kabla, jukumu lililotekelezwa na Prigozhin katika ajenda ya usalama ya Urusi, lilitazamwa kwa jicho la kutokuaminiana zaidi.

Serikali nyingine nyingi za Afrika Magharibi ziliiona kama tishio la moja kwa moja kwa usalama wa eneo lao. Uhusiano wao na Mali uliharibika ka kiasi kikubwa.

Na mapinduzi yaliyofuata nchini Guinea na Burkina Faso, huku vijana wanaoiunga mkono Urusi wakishangilia katika mitaa ya mji mkuu wa Ouagadougou, yamezidisha umakini wa serikali zilizochaguliwa za Kiafrika kuhusu mkakati wa Moscow. Lakini hiyo haimaanishi kuwa watapuuza mkutano wa kilele wa wiki hii.

Badala yake, pengine watajaribu kuisogeza Kremlin kuelekea njia ya kawaida zaidi ya ushirikishwaji wa vyama vya ushirika, na mbali na usaidizi wa kuvuruga utulivu wa serikali ya kikatiba na kuelekea ubia wa kijeshi wa kawaida kupitia mafunzo na usambazaji wa vifaa na silaha.

Na Urusi itajaribu kupata nia yao njema kupitia muendelezo wa diplomasia yake ya kiuchumi.
Afrika

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Maelezo ya picha,
Tawala za kijeshi katika Afrika Magharibi zinaimarisha uhusiano na Urusi.

Ingawa inakosa rasilimali za kushindana na Marekani, Ufaransa, Ujerumani na Japan au China kama mfadhili mkubwa wa maendeleo, Moscow inazo kadi za inzoringia.
Mwaka jana pengine Urusi ilikuwa chanzo kikubwa zaidi cha mbolea barani Afrika, ikisambaza tani 500,000. Pia bila shaka ina nguvu kubwa katika mafuta, gesi na madini.

Lakini sekta ya biashara ya dharura hivi sasa inabaki kuwa nafaka.
Na itakuwa vigumu kwa Urusi kwa kiasi kikubwa kuisaidia Afrika kwa vifaa vya ziada vinavyohitajika sana - na hivyo kuonyesha kutegemewa kwake kama mshirika - isipokuwa kama kutakuwa na mpango uliorejeshwa wa Bahari Nyeusi ambao pia unaruhusu usafirishaji wa bidhaa za Ukraine.

Mapema wiki hii, Bw Putin alidai kuwa Urusi ilisafirisha karibu tani milioni 10 za nafaka barani Afrika katika nusu ya kwanza ya mwaka huu na kusisitiza kwamba ilikuwa na uwezo wa kuendelea kusambazia bara hilo kwa misingi ya kibiashara na zingine bure bila malipo.

Kuongezeka kwa msaada wa chakula kunaweza kuashiria mabadiliko makubwa ya msimamo kutoka kwa nchi ambayo imekuwa mfadhili mdogo wa misaada ya kibinadamu hadi sasa.
Hata hivyo, hata kama mipango ya kusafirishwa bidhaa kwa usalama kupitia bandari za Bahari Nyeusi itarejeshwa, haionyeshi kwamba Moscow iko tayari na imejipanga kuwa mfadhili mkuu wa msaada wa chakula kwa kiwango kinachotakiwa ili kulinganisha na mataifa kama ya Umoja wa Ulaya au Marekani.

Muktadha wa kisiasa umebadilika sana tangu viongozi wa Kiafrika waliposafiri kwa ndege hadi Sochi kwa mkutano wa kwanza wa kilele wa Urusi na Afrika mnamo 2019.

Katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, ikionekana kuchochewa na nia ya kutaka kuivuruga Ufaransa na mataifa mengine ya Magharibi, Kremlin imeonekana angalau kuwa na huruma kwa wanajeshi ambao wamechukua mamlaka nchini Mali, Burkina Faso na Guinea na ambao wanatazamwa na viongozi wa mataifa jirani kama tishio kwa utulivu wa kikanda.

Msisitizo wa utawala wa Mali kwamba Umoja wa Mataifa uondoe kikosi chake cha kulinda amani, na hivyo kudhoofisha ulinzi dhidi ya kuenea kwa ghasia za wanajihadi, umezidisha wasiwasi wa viongozi wa kikanda - na matokeo yake kuwa macho dhidi ya sera ya Urusi.

Kwa hivyo, hata kukiwa na ongezeko kubwa la nia njema kwa usafirishaji wa nafaka wa Urusi, Bw Putin anaweza kung'ang'ania kumaliza hali ya kutoaminiana iliyoenea Afrika Magharibi, ingawa wageni wake watakuwa wenye busara sana kueleza hilo.

Chanzo: BBC
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom