Je, umeshawahi pitia maisha magumu?

Je, umeshawahi pitia maisha magumu?

Nimesoma huu uzi wote bila kujali ni usiku wa manane. Kwenye kila hali iwe Furaha au huzuni yupo Mungu anayetuona na anayetujibu. Hata usiku uwe mzito kiasi gani kumbuka lazima kutapambazuka tu. Imarisha imani kwa Mungu wa Ibrahim uone atakavyokughasi kwa mibaraka tele hadi wanaokuzunguka wabaki na kigugumizi.
Hakuna situation isiyo na mwisho yote tuyapitiayo ni ya muda.
Kila mtu kwa wakati wake bila kujali ametokea familia gani lazima atakuwa amepitia magumu kwa namna moja au nyingine. Wengine hadi sasa wanapitia magumu. Suluhu ya kudumu ya matatizo haya sio mganga bali kumlilia Mungu maana ana suluhu za kudumu za matatizo yetu. Onjeni muone ya kuwa Bwana yu mwema. Ukimuonja hutatetereka kamwe na hakutakuwa na jaribu litakalokukatisha tamaa kwa maana mtetezi (Mungu) wako yuko hai na muda sio mrefu atasimama kufanya intervention.
 
c66408da119a29202f3cf52460118c56.jpg
[/QUOTE]
Duuh sina hata cha kuandika sema leo huu wimbo umenikaa sana moyoni. My poor cousin sister has given birth to triplets, unfortunately she lost all her babies. It shall be well with her soul.....by Angel Bernard

1.Nionapo amani kama shwari
Ama nionapo shidaaa
Kwa mambo yote umenijulisha
Ni salama rohoni mwanguuu

CHORUS
Salamaa, rohoniiiii
Ni salama, rohoni mwanguuuu

2. Ingawa shetani alinitesa
Nalijipa moyo kwanii
Kristo Uliuona unyonge wangu
Ulikufa kwa roho yangu
Na dhambi zangu zote, wala si nusu
Ziliwekwa msalabani
Wala sichukui laana yake
Ni salama rohoni mwangu

××××CHORUS

Eeh Bwana himiza
Siku ya kuja
Panda itakapolia
Wala sitoogopa
Ni salama rohoni mwangu
huu wimbo umekuwa pona yangu baada ya kupitia kipindi kigumu,, pamoja na nyimbo za matumaini za Tumaini Choir Arusha.. Kuna nguvu katika sala,, hakika Bwana Yesu huinua
Duuh sina hata cha kuandika sema leo huu wimbo umenikaa sana moyoni. My poor cousin sister has given birth to triplets, unfortunately she lost all her babies. It shall be well with her soul.....by Angel Bernard

1.Nionapo amani kama shwari
Ama nionapo shidaaa
Kwa mambo yote umenijulisha
Ni salama rohoni mwanguuu

CHORUS
Salamaa, rohoniiiii
Ni salama, rohoni mwanguuuu

2. Ingawa shetani alinitesa
Nalijipa moyo kwanii
Kristo Uliuona unyonge wangu
Ulikufa kwa roho yangu
Na dhambi zangu zote, wala si nusu
Ziliwekwa msalabani
Wala sichukui laana yake
Ni salama rohoni mwangu

××××CHORUS

Eeh Bwana himiza
Siku ya kuja
Panda itakapolia
Wala sitoogopa
Ni salama rohoni mwangu
 
Nimesoma huu uzi wote bila kujali ni usiku wa manane. Kwenye kila hali iwe Furaha au huzuni yupo Mungu anayetuona na anayetujibu. Hata usiku uwe mzito kiasi gani kumbuka lazima kutapambazuka tu. Imarisha imani kwa Mungu wa Ibrahim uone atakavyokughasi kwa mibaraka tele hadi wanaokuzunguka wabaki na kigugumizi.
Hakuna situation isiyo na mwisho yote tuyapitiayo ni ya muda.
Kila mtu kwa wakati wake bila kujali ametokea familia gani lazima atakuwa amepitia magumu kwa namna moja au nyingine. Wengine hadi sasa wanapitia magumu. Suluhu ya kudumu ya matatizo haya sio mganga bali kumlilia Mungu maana ana suluhu za kudumu za matatizo yetu. Onjeni muone ya kuwa Bwana yu mwema. Ukimuonja hutatetereka kamwe na hakutakuwa na jaribu litakalokukatisha tamaa kwa maana mtetezi (Mungu) wako yuko hai na muda sio mrefu atasimama kufanya intervention.
Kwenye tamaa za mwili unamtaja mungu,!!! Ujui wengi waliofanikiwa wamejificha tu kwenye bibilia. Lakini wana mambo ya ajabu kweli.
 
Aisee sikia kwa mtu tu yasikupate wewe!

Nakumbuka mwaka 2013 ulikuwa kama mwaka wa mikosi kwangu,mwaka huo nilikuwa nauguza baba yangu miezi miwili hospitali kwa tatizo la kansa.Mwezi wa sita akafariki,sijapoa na machungu ya msiba mwezi wa nane nikaachishwa kazi.Baada ya kuachishwa kazi,niliandamwa na matatizo lukuki ambayo nikianza kusimulia hapa naweza nikaishia kulia tu.

Kwa ufupi amani kwenye ndoa yangu ikaisha kabisa,nikagombana na mke wangu(nahisi kwa kuwa maisha aliyozoea akawa hayapati tena),akaamua kuondoka nyumbani kwenda kwao,kuna nyumba niliyokuwa najenga,akabeba hati zote za manunuzi ya kile kiwanja akaondoka nayo.Nimekaa miaka miwili bila kazi mpaka mwaka huu ndo nimeamua kujiajiri mwenyewe.Daah,ngoja niishie hapa wakuu!Inaumiza sana.
pole sana mpendwa.. ukifanikiwa huyo mkeo akuonee ng'ambo...Mkono wa MUNGU Uwe juu yako, akuondolee maumivu yako na upate hitaji lako
 
Naam... Paulo anasema na Wafilipi.

"Si kwamba nasema haya kwa kuwa nina mahitaji; maana nimejifunza kuwa radhi na hali yo yote niliyo nayo.
12 Najua kudhiliwa, tena najua kufanikiwa; katika hali yo yote, na katika mambo yo yote, nimefundishwa kushiba na kuona njaa, kuwa na vingi na kupungukiwa.
13 Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.
Hili neno huwa linanipa nguvu sana.
 
UMENIKUMBUSHA MBALI SANA.
Nimezaliwa katika kijiji kimoja kinaitwa Kayombo, huko Bukene, Nzega, Tabora. Nilipitia maisha magumu kwa kweli, lakini tu niseme kwamba, yawezekana mimi sikupita maisha magumu, bali wapo wengi ambao pengine walipitia magumu zaidi yangu.

Nilikuwa napenda kusoma toka nikiwa shule ya msingi, na aidha kwa mipango ya Mungu, ama kutamani niwe kama wengine, nilikuwa na ndoto kubwa sana siku moja niwe mmoja kati ya wasomi nchini, japo sikujua msomi katika kitivo gani, ila tu nilichokuwa nakijua ilikuwa tu siku moja nami niitwe msomi. Nakumbuka mwalimu wangu nikiwa darasa la tano, aliniuliza swali, ningependa kuwa nani maishani. Nilichomjibu ni kwamba, 'nataka kuwa waziri' wala uwaziri wenyewe sikujua maana yake.

Nilikuwa nikiishi na mama yangu kipenzi, na nikiwa kama mtoto wa kiume pekee na wa mwisho kati ya watoto wengine saba, nyumbani mimi ndiye nilikuwa faraja ya mama, kazi zote za kiume mimi ndo nilikuwa wa kuzifanya kutokana na ukweli kwamba, baba alifariki dunia nikiwa na umri wa miaka mitatu, kwa mujibu wa maelezo ya mama yangu.

Kutokana na familia yangu kutokuwa na uwezo wa kutosha, niliingizwa katika shirika moja la WORLDVISION INTERNATIONAL, shirika ambalo silipendi kama nisivyompenda shetani katika maisha yangu, kama mtoto mfadhiliwa aishie katika mazingira magumu, na nilikuwa mmoja kati ya watoto wanne tarafa ya Bukene tuliochaguliwa kuliwakilisha shirika hilo kwenye maombolezo ya MTOTO WA AFRIKA mkoani Shinyanga mwaka 2005, sherehe ambayo hufanyika kila siku ya Tarehe 16 June, safari ambayo huwa naisemea kama safari iliyofungua ukurasa mpya katika maisha yangu.

Nilifanikiwa kumaliza elimu ya msingi na kufaulu kwa ufaulu mkubwa tu (alama 213/250), nikapangiwa kuendelea na masomo ya sekondari katika shule moja ya kata, karibu kabisa na nyumbani. Maisha nyumbani kiukweli yalikuwa magumu, maana nililazimika kujishugulisha na kazi anuai ambazo kwa namna moja, ama nyingine zilitakiwa zinipatie kipato ambacho angalau ningeweza kununua mahitaji nyumbani na kununua nguo zangu pamoja na ada, na moja kati ya kazi nilizozipa kipaumbele ilikuwa ni kukata na kuchoma mkaa.

Kama nilivyosema hapo juu kwamba, kati ya mashirika ambayo sipendi hata kuyasikia ni WORLDVISION INTERNATIONAL, na hapa sintozungumza ni kwa sababu gani, nitatoa mawasiliano ili nipate kukupatia kitabu changu kinachokwenda kwa jina la A SPITTING COBRA, nilichokiandika si punde, kwa muktadha wa riwaya ya wasifu (AUTOBIGRAPHICAL NOVEL).

MAISHA MAGUMU AMBAYO SINTOYASAHAU.


Kama mada tajwa juu, maisha magumu niliyopitia ambao unaweza kuyasoma pia katika kitabu changu, ni pale nilipokuwa kidato cha kwanza, nilikutana na kesi nikiwa na rafiki yangu, kuwa tumefanya mapenzi mchana kweupe, na kupewa suspension ya wiki mbili na kuripoti na wazazi. Niliamua kuondoka nyumbani nikiwa nimekata tamaa kabisa ya kusoma tena. Najua wengi watajiuliza, 'suspension ya wiki moja tu ndiyo ilinifanya niondoke nyumbani na kukata tamaa kiasi hicho!'. Mengi utayasoma kwenye kitabu hicho ikiwa ni pamoja na swali hili, lakini tu kwa ufupi ni kwamba, nilamua kutoroka nyumbani na kukimbilia mkoa jirani wa Shinyanga, ambapo wala sikujua naenda kufikia wapi, ila tu nachoweza kusema ni kwamba, ilinibidi nilipofika Shinyanga kulala nje na nililala kama siku tatu, nikiwa na machokoraa wengine.

Ndipo nilipopata msamalia na kuhifadhi kwake na kunifanya kama sehemu ya familia yake. Mengi nimeyapitia ambayo ningependa ku-share jamvini ili tujifunze kitu, lakini niseme, fuatilia kitabu changu cha A SPITTING COBRA, na kupata copy yake, niandikie pepe anwani hujumasr@gmail.com au kwa simu nambari +255 785 777 710, nitakupatia copy hiyo.

Kwa sasa nipo chuo kikuu cha Dodoma, nasoma shahada ya Elimu katika sanaa ( Bachelor of Education in Arts (Linguistics).

Nikisema maisha magumu, simaanishi kwamba nimeyasoma kwenye kitabu, bali nimeyaishi.


World Vision ilikufanya nini rafiki?wewe ndo yule katibu kata siku hzi pale Ishinabulandi nini?au we ni wa zamani sikuku kuta BUKENE ADP at that time?
 
acha kabisa!!!Haya maisha mpk unamuuliza Mungu uliniumba ili niteseke au?!
unakaaa usiku mpk kunakucha usingizi hauji na unatamani kusikuche!
Ndugu wanakudharau mpk watoto wadogo mnoo!!
yaani jamani nyie!

Kumbuka unapoenda kulala waza mema ambayo Mungu amekutendea. Ukiwaza mabaya tu ndio maana unakosa usingizi, Pia Kama Mtu unasoma bible au quruhan na kuelewa hayo mambo ya shida yameeelezwa vizuri na jinsi ya kuwa na Amani ya moyo japo unapitia shida. Mwenyezi Mungu anajua shida unayopitia (kumbukumbu 3:25,26
 
Kuna hili unakuta ndugu wanaomba msaada/hela yaani ikifika mwisho wa mwezi kila mtu anataka fedha(wengine wana nguvu zao kabisa).Kimbembe usiwape oo mara anajidai,mke wake kampa kabali na maneno chungu nzima.Ki ukweli ndugu ndiyo huwa wanarudisha nyuma maendeleo ya mtu ni bonge la tatizo
 
Hmmm, bado napitia kipindi kigumu sana..... Ninalipa deni la millions of money ambalo sikufaidika nalo, kwa lugha nyingine nimetapeliwa. Nimekuwa na sleepless nights. Ninafanya kazi 24hrs lakini ni kama namfanyia mtu......... Hmmm, Mungu yupo, najua yana mwisho. Ingawa mpaka sasa uzito wangu umepungua, hata concentration yangu kazini imepungua, kama ningekuwa nafanya kazi kwa MTU binafsi nafikiri ningekuwa nilisha timuliwa, lakini Mungu yupo, yataisha.
 
mimi bado napitia sijaweza kuchomoka kwenye tatizo la ajira
Usichague sana ajira kama unachambua mawe kwenye mchele, mwanzo wa ajira ndogo ndio njia ya ajira kubwa, kumbuka umuri hauna subira.
 
Kuna mahali inafika unaona kama dunia haitaki ushirikiano nawe,unaona wote ni kama wamekutenga hakuna anaejali matatizo yako hata wale wa karibu yako hawakuoni.

Unabaki wewe na Mungu wako tu,ni kipindi kigumu kwakila mtu. Tumepita na tunaendelea kupita kwenye changamoto mbalimbali....

Muhimu ni kua karibu na Mungu zaidi na atakuvusha salama.
Pamoja kuwa karibu na Muumba pia ukumbuke uliootoka, ulipo na uendako, heshimiana na watu kwakuwa huijui kesho yako itapitia mikono gani kukufikia, iheshimu kila senti tano uliyonayo, toa msaada umpendezae Mungu nafsi yako na umsaidiaye maana hujui kesho utasaidiwa na nani.
 
Pamoja kuwa karibu na Muumba pia ukumbuke uliootoka, ulipo na uendako, heshimiana na watu kwakuwa huijui kesho yako itapitia mikono gani kukufikia, iheshimu kila senti tano uliyonayo, toa msaada umpendezae Mungu nafsi yako na umsaidiaye maana hujui kesho utasaidiwa na nani.
Hapo kwenye kuheshimu kila mtu umesema kweli... Ni vema kuheshimiana bila kujali umri,kipato au status aliyonayo mtu.

Na kumuheshimu mtu huko sio lazima uwe unamfahamu kwakumuona... Binafsi humu Jf kuna watu wamefanyika msaada mkubwa sana kwangu wengine hata sijawaona.

Hua nabaki kumshukuru Mungu kwajili yao,inatia moyo sana pale mtu anapositisha shuhuli zake kwajili ya kukusaidia wewe uvuke mahali fulani.

Hakika njia za Mungu hazichunguziki,katika mazingira yoyote amini Mungu yuko nawe. Usikate tamaa wala usimdharau mtu. Usitumie ulichonacho vibaya wala nafasi uliyonayo usimnyanyase mwingine bali ufanyike baraka kwa wengine.
 
Daaah I remember those days nikiwa na miaka 9 wazazi wote walifariki Bahati walikuwa hawana hata kiwanja pamoja na kwamba walikuwa watumishi siwazi walaumu sana bse tulizaliwa sita inawezekana ni katika pilikapilika za kutulea, Nakumbuka cku tunarudishwa nyumbani kwa Babu na Gari la Serikali msoto ukaanzia hapo Ashukuriwe Baba mdogo aliyesomeshwa na Baba kutukumbuka kutupeleka shule wote sita hakika hatukumuangusha tumetusua life ile kwa kweli imenifanya kuwa nasomesha ndugu zangu wenye mwerekeo.wanaohang kijiini
 
Shida hazina mwenyewe ila kama matatizo hayo ikiwa Mungu mwenyewe ndo anakupitisha kwenye hizo shida hauwezi chomoka mpaka urekebishe mambo...fulani...
 
Haya matatizo niliyopitia na ninayoendelea kuyapitia katika hii miezi ya karibuni, nimegundua kwamba, kufikwa na matatizo ni tatizo ila kukosa mtu wa kushare nae hayo matatizo (hata wa kumhadithia tu) ni tatizo zaidi!
Mbaya zaidi pale unapowaamini wawili watatu na kuwaambia lakini wanakua 'judgemental',..prayer remains the only confidant

Ila Mungu ndo kila kitu, i ll never lose hope!
 
mi wakati nimemaliza chuo,ilikuwa ni balaa,nilikuwa na mpenz wng wakati mi niko home ye alikuwa bado yuko chuo,sina hata mia sku moja akaja geto jioni mda wa kulala nikashangaa analia tu wakati wa tendo tena anatoa ushirikiano balaa bt coz mi namjua ikabidi nistishe kwanza nikamuulza vp kwani,c akafunguka kwamba kafulia na jana yake kuna mtu alikuwa anapenda kumsalimia sn pale chuon sasa alimwalika menu nje ya chuo nyt coz alikuwa hana ktu ikabd aende jamaa likamnunulia menu,likampa na elf 10,ksha likampeleka lodge klchoendelea,...daah kweli mi nlimuonea tu huruma na nlmsamehe bt alilia usku kucha mi nkawa mmbembelezaji tena,after wote kumalza chuo naye akaja geto she was like me very much lyf lilikuwa tyt balaa ikfka mda wa kulala mnalala mmemalza kila ktu mpaka maji ya kunywa na hamjui tmr itakuaje bt ashukuriwe MUNGU hatukuwahi kulala na njaa,leo ndo mke wangu na tuna watoto 2.
 
Back
Top Bottom