Je, maisha yako fair? Balaa na tabu...

Financial Analyst

JF-Expert Member
Nov 27, 2017
517
1,000
Je ni kweli haya maisha hayako fair au mtiririko wa magumu na changamoto tunazopitia ni matokeo ya maamuzi yetu. Haya maisha yana macho? kuangalia nani wamkumtembeza na nani wa kumpelekesha, simaanishi utajiri na umsikini, bali ni mateso na furaha, mahangaiko na amani, mikosi na utulivu, balaa na bahati.

Hivi ni kama kuna force kubwa inayo tupitisha katika kila mapito, ni kama hatuna nguvu dhidi yake bali tunafikiri ufanyaji kazi kwa bidii, elimu na ufadhili ndio vyakutufanya succesful, happy and lucky. Hivi kuna watu ni kama wameandikiwa ukakasi katika maisha, achilia mbali maisha yamekuwa triggered kuwa magumu kwa sababu ya pesa kuwa introduced katika mifumo ya maisha, ila kuna watu ndio wanarepresent tabu za dunia, wakikupa stori ya maisha yao hauwezi kumhukumu tofauti bali utawaza sanana na kujiuliza maswali mengi.

Kuna watu maisha yao ni kama movie, ni balaa baada ya balaa, wakati wewe unapanga ratiba ya kukutana na marafiki pic nic baada ya kutatua changamoto ndogo ya mirathi ya familia, yeye anapanga shedule ya kutatua mabalaa yanayo mkumba na kuwa tayari kwa yanayo kuja, kwa maana ameshaona maisha yake ni mfumo wa tabu na mahangaiko. it's no joke.

Ushawahi wahi kushuhudia mtu, familia au jamii fulani ikiwa na mlomlongo wa kupitia magumu mara kwa mara bila huruma, na muda mwingine ni yale yale ya kujirudia. Ushawahi jiuliza kuna changamoto zinatokea maishani mwako lakini sio katika mfumo wa kawaida ila ni kama kuna forces zilizo against you na sio za kawaida, sawa naelewa ile kauli ya matatizo yapo ili yawapate watu ila ndio yampate mama yako maisha yake yote hadi anaenda kaburini. Unaweza kuwa katika tabu zilizoharibu mfumo wa furaha maisha yako then ukaona watu wanatabsamu haukajiuliza hivi watu wanapata ujasiri gani wa kutabasamu coz you have lost all joy in life.

Ushawahi kudhani ni kama una bahati mbaya na kila fursa (sio tu za kiuchumi) zinazokuja..yani unakosa kupata kitu cha muhimu sio kwa sababu umeshindwa bali vinatokea viji-obstacles vya kutoeleweka hadi unapoteza. Ushawahi ona mtu ana-hustle kwa akili na nguvu zote, kiuhalali na bila kukata tamaa ila akasongwa na vielelezo vingi (katika hiyo shughuli au nje ya shughuli) visivyo eleweka vitakavyo mpelekea kumuangushsa au kukosa.

What really determines our path through life, je ni karma (ila kumbuka kuna watu hawa kufanya ubaya ila wanapitia ubaya), je maisha yetu yametayarishwa kuwa tutaishi vipi kabla hatujazaliwa, je tunaishi kutokana na matokeo ya malipo ya ubaya au uzuri wa maisha ya waliotutangulia (family ancestors), Je watu wanaharibiwa maisha kupitia uchawi, laana na kunenewa, Je ni kuwa hatujaamua kumfuata Mungu kikamilifu ndio maana tunapitia tabu, Je tunaishi kutokana na viwango vya bahati zetu., je.?...?...?

Utani-judge kwa sababu upo labda katika nafasi ya amani, utulivu wa moyo na haujakumbwa na misusuko, Labda utaweza kuniambia unalalamika nini kuhusu maisha badala upige kazi, lakin kumbuka ndugu kuna watu tabu zao zimeota mizizi hadi katika nyuso zao, zimewaathiri akili zao na sasa hata zinawafata vizazi vyao. Sio kwamba ni kurithi umasikini, sio kwamba walifanya maamuzi mabaya maishani, sio kwamba ni matajiri, sio kwamba wana ufahamu mbovu, bali ndio hivyo yanawatokea.

20200823_161702.jpg
 

Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
58,190
2,000
Mambo mengine ni bahati tu.

Wewe unafikiri Bill Gates angezaliwa Mmakonde Tanganyika angekuwa bilionea wa dunia alivyokuja kutokea?

Kwa hivyo ile sehemu unayozaliwa tu, wazazi wako ni nani, historia zao, nchi yako ni nchi gani etc mambo ambayo hujaweza kuya control, yana mchango mkubwa sana katika maisha yako.

Of course kuna mengi sana zaidi ya hayo.

Lakini, hii habari nzima ya fairness haipo.

Kwanza ukisema life iwe fair maana yake nini?

Life si kitu chenye consciousness useme kitakuangalia na kukuonea huruma.

Mtu anaweza kuwa fair. Taasisi zilizoanzishwa na zinazoendeshwa na watu zinaweza kuwa fair.

Life yenyewe si mtu wala si taasisi iliyoanzishwa na mtu. Sasa unaposema iwe fair itakuwaje fair?
 

Chiwaso

JF-Expert Member
Oct 21, 2009
5,573
2,000
changamoto tunazopitia ni matokeo ya maamuzi yetu C & P kutoka kwa mleta mada
 

Financial Analyst

JF-Expert Member
Nov 27, 2017
517
1,000
Mambo mengine ni bahati tu.

Wewe unafikiri Bill Gates angezaliwa Mmakonde Tanganyika angekuwa bilionea wa dunia alivyokuja kutokea?

Kwa hivyo ile sehemu unayozaliwa tu, wazazi wako ni nani, historia zao, nchi yako ni nchi gani etc mambo ambayo hujaweza kuya control, yana mchango mkubwa sana katika maisha yako.

Of course kuna mengi sana zaidi ya hayo.

Lakini, hii habari nzima ya fairness haipo.

Kwanza ukisema life iwe fair maana yake nini?

Life si kitu chenye consciousness useme kitakuangalia na kukuonea huruma.

Mtu anaweza kuwa fair. Taasisi zilizoanzishwa na zinazoendeshwa na watu zinaweza kuwa fair.

Life yenyewe si mtu wala si taasisi iliyoanzishwa na mtu. Sasa unaposema iwe fair itakuwaje fair?
sio kwamba nakuceticize, ila how do u prove life is not a conciousness..
 

GLOBAL CITIZEN

JF-Expert Member
Jun 5, 2014
774
1,000
Unauliza maisha yako Fair ukilinganisha na ya nani?

Kwasababu kila mmoja wetu ana share yake ya kutaabika.

Kama hayupo basi na aseme hapa.

Unajua suffering inakuja kwanamna nyingi na tofauti.

Iwe kukosa pesa, ugonjwa, kukataliwa au namna nyingine yoyote ile.

Kwa maana hiyo maisha maana yake ni MASUMBUKO NA TABU NYINGI.

Binafsi mimi najiona kama mtalii tu katika hii dunia.

Shida ikija sawa, isipokuja sawa vilevile.

Siwezi kufanya chochote kuzuia hilo.

Ninachojaribu ni kupunguza tu ukali wa mataabiko ninayokutana nayo kwaku focus zaidi kwenye mambo mazuri yanayonipatia furaha.

Sasa hivi ninavyoandika hili comment sina masumbuko yoyote.

Nipo kwangu natazama documentary huku napata wine

Lakini nafahamu suffering inaweza kuja muda wowote.

Je, nitafanya nini kuhusu hilo?

Jibu ni HAKUNA.
 

Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
58,190
2,000
sio kwamba nakuceticize, ila how do u prove life is not a conciousness..
Swali zuri sana.

Na ili kulijibu vizuri, kwanza tuanze kwa definitions.

Ili tujue wote tupo pamoja.

Naomba unipe definitions mbili.

1. What is life?
2. What is consciousness?
3. What is your epistemology?

Perhaps I should expand on my meaning when I wrote "consciousness". I meant a moral and conscientious concsiousness that distinguish wrong from right.

One can argue that life has consciousness in the context of plants detecting light for photosynthesys, and even bending towards light.

But do the processes of life have a conscientious conscience to protect the weak from the catastrophes of life? Far and above the statistical trends exhibited by natural patterns? Not in particular.

I just watched a documentary on nature. It shiws how global warming us affecting temperatures in the colder parts if the world, and how that temperature droo is causing ice to melt, and how seals are dying by tumbling on cliffs because they are firced to go where they did not have to go before.

The seals do not know how to adapt to climate change.

Do the processes of existence we call "life" care about seals because seals do not know how to adapt?

No. The processes of existence, what we call "life", such as gravity, temperature, time etc, do not care about seals dying.

These processes are just agnostic processes.

Is time going to slow down to let a slow turtle cross the road before a car runs iver the turtle?

No.

Time is not going to slow down for the turtle.

The passage if time is not conscious. Therefore, it neither knows nor care that a turtle exists.

Does the spliting of cells that cause cancer care that you are a poor person without Health Insurance, and therefore it should spare you from the devastation of cancer?

No. Cancer does nit care whether you are poor or rich. It is a process if life that dies not kniw that you are rich or poor.

This is what I mean by saying that life is not conscious.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom