Ielewe Siri iliyopo katika Miguu yako katika Ulimwengu wa Roho

Akidu

Member
Sep 19, 2022
47
76
Umewahi kujiuliza kwanini wachawi huwa wanachota mchanga mahali zilipokanyaga nyayo za mtu?

Ndugu mpendwa , miguu yako ina maana kubwa Sana na umuhimu wa kipekee katika ulimwengu wa roho . Na hii ni kwa pande zote mbili , ulimwengu wa Roho wa Nuru na ulimwengu wa roho wa giza.
Kibaya ni kwamba shetani anazitumia Sana Siri nyingi za ulimwengu wa roho ambazo wanadamu wengi wamefichwa na wanaofunuliwa ni wachache Sana. Ndiyo maana Mungu anasema watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa.

Upo muunganiko (connection) mkubwa Sana Kati ya nyayo za miguu yako na nafsi yako ktk ulimwengu wa roho. Nyayo zako zimebeba taarifa zako zote . Mchawi anapopata nyayo zako anaweza kuelewa kila kitu kinachohusiana na maisha yako . Na kama hauna ulinzi wa kiroho , anaweza kufunga kila kitu ktk maisha yako .
Nyayo zako zinapokanyaga juu ya ardhi zinaacha taarifa zako hapo. Na ndiyo maana ardhi ya kwako/ nyumbani kwenu inakutambua na inakusikiliza chochote utakachoiambia. Au hili nalo haulifahamu nije kukufafanulia siku nyingine? Na hapa ndiyo uelewe laana aliyopewa kaini inavyofanya kazi ( kulaaniwa juu ya ardhi).

Yaani ukilaaniwa juu ya ardhi ,nyayo zako zinabeba taarifa . Kwahiyo kila utakapokwenda ukishakanyaga tu mguu wako ktk ardhi nyayo zako zinatoa taarifa ktk ardhi hiyo "huyu mtu ameelaaniwa juu ya ardhi" . Kwahiyo hata ufanye nini uende wapi hutafanikiwa mpk laana ivunjwe..

Kwahiyo nyayo zako zina connection Kati ya ardhi na mbingu .

Labda nikupe changamoto Kidogo ambayo unaweza usiipende wewe mkristo lkn ndiyo maarifa yenyewe nakuongezea Sasa.

Umewahi kujiuliza kwanini wafuasi wa Mwamposa hawayakanyagi mafuta ya upako wakiwa wamevaa viatu??

Ni ukweli kuwa Mungu anapenda usafi , lkn Umewahi kujiuliza kwa kina kwanini manabii wote pamoja na Yesu ,wayahudi walikuwa wanavua viatu walipokuwa wanakaribia mbele za Mungu hata Kama ni porini kwny mifugo? Mungu anamwambia Musa "vua viatu maana mahali hapa ni patakatifu". Ilikuwa ni lazima connection ya nyayo isome kwny ardhi ipeleke taarifa kwenye ulimwengu wa Roho.

Tuliache hilo ni somo la siku nyingine . Turudi kwny mada kuu.

NYAYO ZAKO ZIMEBEBA VITU GANI
?

Shetan anapotaka kuiba muda na wakati wa mwanadamu huwa anapiga na kumfunga MIGUU:

Katika nyayo za miguu kuna vitu 5 wanalenga kukuondolea;

1. Kibali;
- inachafuliwa nyota yako usikubalike na watu bila sbb kila unapoenda. Nyayo zako zimebeba kibali chako.

2. Heshima;
- Unaondolewa heshima uwe mtu wa kudharauliwa ktk jamii na kuonekana hufai . Ndiyo maana hata kimila vijana huinama na kuwashika miguu wazee nao huwashika kichwa.

3. Hatua;
- Unafungwa miguu usipige hatua yyt ya maendeleo au mafanikio. Miguu ndiyo inakufanya utembee huko na huko kutafuta riziki . Ukiishafungwa maana yake hutapiga hatua yyt .

4. Maamuzi;

- wanapokufunga miguu wanakufunga ufahamu wako wa kufikiri usiweze kufanya maamuz ya maana ya kusonga mbele.unapanga mipango mingi mizuri lkn hautekelezi. Hata ukipata wazo zuri kiasi gani utaishia kulisema tu na kuliweka kwny mipango miaka inaenda.

5.Umiliki na utawala;
-Ukifungwa miguu unapoteza umiliki wa mali na ardhi unayoikanyaga. Hutamiliki Mali na Kama ulikuwa nazo utaanza kufilisika.

Haya ni mambo ambayo roho ya umaskini inapomuingia mtu huwa inamuondolea . Na hivi vyote vinaanzia kwenye nyayo zako.

Je ni nini huwa kinafanyika kwny kivuli chako ? Nitakujulisha siku nyingine Mungu akipenda
 
Kwanza kabisa thibitisha uchawi upo, na tueleze unajuaje, unatenganishaje, kwa upande mmoja, huu ni uchawi, na, kwa upande mwingine, hili ni jambo lisilo na uchawi labda sijalielewa tu?

Yani ni hivi, wale mababu zetu walioishi miaka 120 mpaka 200 iliyopita, walikuwa hawajui vyombo vya umeme, hawajui gramafoni, hawajui sayansi ya jiografia ya kutabiri kupatwa kwa jua etc.

Hawa, walivyooneshwa na wazungu hayo yote ambayo hawakuyajua, waliona ni uchawi, waliwaona wazungu kama miungu.

Ndiyo maana waliwaita "mzungu", neno "mzungu" ukiondoa hiyo z unapata "mungu".

Waliamini kuwa hawa watu wana supernatural powers za kiungu.

Lakini, haya mambo yalikuwa natural science tu, leo hata sisi tunaweza kutabiri kupatwa kwa jua, tunaweza kupiga muziki kwenye redio, tunaweza kuwasiliana kutoka mabara tofauti kwa videocalls, bila kuhitaji uchawi.

Sasa, wewe, unapoona kitu cha ajabu ambacho hukielewi, unajuaje huu ni uchawi na si kitu kingine chochote ambacho si uchawi, ila hujakielewa tu?

cc: LIKUD
 
Usipotoa suluhisho nini kifanyike unakuwa bado hujasaodiq jamii ya JF
 
Hivi ma dude kama haya hata wazungu, wachina, wa Hindi, yanawapata pia? Au, ni upuuzi, wa MTU mweusi!

Ukipigwa sana na ufukara na umaskini, lazima utaanza kuwaza vitu vya ajabu!

Ni sawa sawa, upo ghetto unazima taa, vivuli vya vitu vilivyopo chumbani, u bongo unakuambia, ni taswira ya MTU!

Kumbe brain inakuchezea trick.

Kama hii ni kweli, twende tukachukue nyayo za wazungu beach, ili wakifanya mihamara, dollar zao zinaingia kwenye vibubu vyetu
 
Hadithi za kusadikika hizi.

Kwenye kiswahili tuna ziita Tarihi/Visakale

Fiction stories, Fairytales.

Imagination just an illusion.
 
Hivi ma dude kama haya hata wazungu, wachina, wa Hindi, yanawapata pia? Au, ni upuuzi, wa MTU mweusi!
Ukipigwa sana na ufukara na umaskini, lazima utaanza kuwaza vitu vya ajabu!
Ni sawa sawa, upo ghetto unazima taa, vivuli vya vitu vilivyopo chumbani, u bongo unakuambia, ni taswira ya MTU!
Kumbe brain inakuchezea trick.
Kama hii ni kweli, twende tukachukue nyayo za wazungu beach, ili wakifanya mihamara, dollar zao zinaingia kwenye vibubu vyetu
Wengi wetu tunaendesha v8 lakini akili zetu ni zilezile
 
Back
Top Bottom