Hayo yote uliyoyaandika , ndio nayapitia sasa. Tena yamekuwa kwa muda mrefu sana.
Ilifika mahala nikaenda SCOAN Nigeria kwa PTB Joshua kwa njia ya bara bara ( nilitumia siku 76 kufika)
Nimekuwa kiroho sana. But matatizo yapo pale pale. Na yanazidi kuongezeka mpaka kukimbiwa na watu wa karibu kabisa, uliowasomesha na kuwainua juu.
Wakwe kukuona kama mwehu, mke kukuona hufai , na kuudharau Wokovu wako.
Mara waseme sitaki Kazi, na kwamba nachagua Kazi. Wakwe wanamsisitiza mke wangu aachane na Mimi kuwa nampotezea muda, sina Kazi.
Nakuwa karibu sana na Mungu kila mara. Na ninafunga na kuomba kila mara.
Hii ni sehemu ambayo naitumia kusali mchana na Usiku..., asubuhi mchana jioni.
Usiku kabla ya saa 6 , Then saa 7-8 , na saa 9-10.
Nimetandaza vyeti vyangu vyote kuanzia chini hadi Postgraduate, na mahitaji ya watu wengine.
Natumia muda kuwaombea maadui