Je, umeshawahi pitia maisha magumu?

nzalendo

JF-Expert Member
May 26, 2009
11,726
12,006
Hapa ninamaanisha kufilisika/kufulia, kukosa uhakika wa kupata angalau chai kwa siku, kutengwa na ndugu.

Kukosa kazi muda mrefu, kuugua na watu kukutenga, kukosa kodi ya nyumba/mahali pa kulala, kusingiziwa kwamba hutafuti kazi au kusemwa umelogwa ndugu kusema una laana.

Kukatishwa tamaa kwamba Mungu kakuacha, kwamba unasali uongo, kudharauliwa na mambo kama hayo.

Je, uliweza vipi kuchomoka katika hali hiyo?
 
Kuna mahali inafika unaona kama dunia haitaki ushirikiano nawe,unaona wote ni kama wamekutenga hakuna anaejali matatizo yako hata wale wa karibu yako hawakuoni.

Unabaki wewe na Mungu wako tu,ni kipindi kigumu kwakila mtu. Tumepita na tunaendelea kupita kwenye changamoto mbalimbali....

Muhimu ni kua karibu na Mungu zaidi na atakuvusha salama.
 
Yan hizo zote nimeshazipitia siwez kuja kusahau kwenye maisha yangu kabisa nilala chin kwa kulalia nguo zangu na kula mkate kama chakula kwa muda wa wiki nzima. Kuna wakati nilitaman kujiua niliumwa vibaya sana halafu hakuna mtu sio rafik wala ndugu anayekupa ushirikiano wa dhati. Oh MGD sitak kukumbuka kabisa.
 
Nilichojifunza hizo nyakati huwa haziishi, na hakuna maisha ambayo yatakua hayana changamoto sema zitatofautiana tu.
Hali kama hizo zimeniimarisha sana, hata nikipata tatizo kubwa, si panic, najipa moyo tu, kama niliweza kumudu matatizo makubwa na Mungu akanivusha, hata hili lililopo mbele yangu litapita.

Hauna kazi, unadaiwa kodi, mbaya zaidi mwenye nyumba mnaishi nae nyumba moja na una afamilia. Hiyo hali unaweza kutamani uyeyuke. Hapo haujaambiwa wife kajifungua katikati ya hiyo hali! Lakini mara zote, Mungu ni mwema sana.
 
Hapa nina maanisha kufilisika/kufulia kukosa uhakika wakupata angalau chai kwa siku. kutengwa na ndugu. kukosa kazi muda mrefu, Kuugua na watu kukutenga, kukosa kodi ya nyumba./mahali pa kulala, kusingiziwa kwamba hutafuti kazi au kusemwa umelogwa ndugu kusema una laana.

Kukatishwa tamaa kwamba Mungu kakuacha,kwamba unasali uwongo
Kudharauliwa na mambo kama hayo na je?

Uliweza vipi kuchomoka katika hali hiyo?

Usiombe Yakufike ndugu nimekutana na Mengi yakatishayo tamaa ila nimesimama kiume mpaka kinaeleweka usife Moyo aupo pekee yako
 
Matatizo huwa yanayokea hapa duniani na kwa wanadamu tuu,, na tukianza kusimuliana unaweza usiamn KBS,, umefukuzwa chuo kwa kusingizwa unafika hm ndugu zako na wazaz wako hawkuhitaj nyumban,, mchumba wako uliyemtambulisha kwenu anakuambia ukifukuzwa hunioi,, unajaribu biashara hata watej wote hapo mtaan hamna anayekuja kwako kuanzia asbh ad jion,, utatamn ucngefika KBS dunian
 
nakumbuka tulivotimuliwa UD halafu kitaa kitambo kinoma, one day sina hata nauli ya kuelekea geto(mbezi ya kimara) najiandaa kutembea na mguu nkakutana na mshkaji akanipa 500, bila kuomba wala nn yaani hapo ndipo unapoamini mungu yupo

au una nauli ya kwenda mjini na kurudi halafu konda anasahau kukudai nauli
 
1465826824129.jpg
 
Unakua huna hela kiasi kwamba hata ukikwea daladala na kumuona konda ana mihela ile unatamani kumnyang'anya.

Enzi za chuo hii ilintokea sana maana safari ya kutoka Udsm hadi Mabibo kwa miguu si ya kitoto, halaf ukifika hostel wachanganya Maji na sukari unakandamiza kitu cha mkate. Umasikin ni kitu cha kulaani sana jaman
 
Haya matatizo niliyopitia na ninayoendelea kuyapitia katika hii miezi ya karibuni, nimegundua kwamba, kufikwa na matatizo ni tatizo ila kukosa mtu wa kushare nae hayo matatizo (hata wa kumhadithia tu) ni tatizo zaidi!

Ila Mungu ndo kila kitu, i ll never lose hope!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom