Je, umeshawahi pitia maisha magumu?

Je, umeshawahi pitia maisha magumu?

Nimepitia Challenge nyingi sana kubwa na ndogo, nilichojifunza ni kuwa mitihani ipo kila siku haiishi kamwe kila hatua unayopiga ina aina nyingine za matatizo kwa hiyo ni kukabiliana nayo tu.

"Kila masika na Mmbu wake"

Muhimu ni kuhakikisha unakuwa Problem Solver siyo likija tatizo au ukigonga mwamba unachanganyikiwaaaa Noo! Unatulia kisha unapangua moja baada ya jingine.
 
pia mimi niliwahi kuacha kabisa kwenda kanisani na niliwachukia sn wachungaji,kuna kpnd mambo yng yalienda mlama kazin nkafukuzwa kwa bahati mbaya mambo mengi nlikuwa namshirikisha mchungaji mpaka migogoro yng na mke wng pia nlikuwa kiongoz kanisani,baada kuona mchungaji anapeleka mambo ndivyo sivyo nliandka barua ya kujiudhuru uongozi,aisee mchungaji alinikashfu mbele ya kanisa akdai mi sina hela,nalishwa na mke wng,watu wasje kwangu wala wasinisalimie wala kunisaidia kwa lolote,akaanza kampen ya kuniachanisha na mke wng akawa anamshawishi,ikafkia hatua akampgia simu ma mkwe wng lengo likiwa ni kuhakikisha naachana na mke wng..aah nyie acheni.
 
Watoto wa Bakhresa, Mengi au Mo dewje ktk maisha yao yote kuanzia wakiwa tumboni mwa mama yao hawatokaa wajue maisha magumu ni kitu gani au waje wapitie maisha magumu! Na sis tutafute hela kwa bidii watoto wetu wasije kupitia njia tulizo pitia tujitume tuachane na siasa
Kakuambia nani? Matatizo yapo katika kila hatua " Kila masika na Mmbu wake"

Unamuona Mzee Mengi hana matatizo hee? Unaweza kukuta una amani na furaha kuliko yeye
 
jamani jamani jamani,, hapo mabibo to UD ni mbali kweli kiasi unasema ulipitia wakati mgumu??

anyway inategemea ulikulia malezi gani, inawezekana ulianzia familia ya mboga saba
Kwa wanaoijua Morogoro nilikuwa nachapa miguu Nunge hadi Chamwino kila siku kwa muda wa miaka miwili

Nilipokuja Dar nilikuwa nachapa miguu kutoka Tabata Bima hadi Kigamboni kwa muda wa week mbili mfukoni ni mia mbili tu ya pantoni kwenda na kurudi hahahaha hayo yote nimeyakumbuka leo nilipomuona huyo ndugu yangu Wa UD hadi Mabibo.

Simbezi hata kidogo kila mtu na changamoto zake kwa namna azionavyo.
 
Maisha bana yakikugeuka unaweza kuokota makopo.me toka january mwaka huu niliachishwa kazi dahhh we acha tu nilikuwa kibonge cha mtu sshv nimebaki skeleton
Pole sana Muombe Mungu sana lakini katika maombi hayo usisahau kumuomba Maarifa yaongozane na Ubunifu, Afya na Busara.
 
Hongerah sana mimi mmojawapo ntahitaji hicho kitabu. Kitu nilichojifunza watoto hawa wa mitaani wengi wao ni intelligent! Kwani najaribu kuwaza utaondokaje nyumbani na kwenda kuishi mitaani ukiwa mtoto mdogo bila akili ya ziada ya kuweza kuishi? Basi niishie hapo kwani mengine nitayapata kwenye kitabu! Historia kama hizi zitapunguza hata unyanyapaa kwa watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu. Ni jukumu la serkali na jamii kusaidia ili kusiwe na vulnerable kids, elimu bure ni njia mojawapo.
Ushauri kwa mara nyingine kwa Mheshimiwa Rais vunja wizara ya Afya na hii ya ustawi wa jamii ( hii ishughulikie masuaaya jinsia, wanawake na vijana ( kuwaanzishia ujasiriamali), wazee na walemavu iwe na wizara yake inayojitegemea as Wizara ya Afya kwa changamoto zake pia ibaki ikijitegemea. Ukitaka watendaji wa hii wizara inayohusu Ustawi wa jamii wakereketwa tupo.
Niliondoka nyumbani nikiwa na Miaka 14. Basi tu ID hizi zinatuficha nilipofikisha 16 nilitingisha sana nchi hii kwa vitu vyangu.
 
mi wakati nimemaliza chuo,ilikuwa ni balaa,nilikuwa na mpenz wng wakati mi niko home ye alikuwa bado yuko chuo,sina hata mia sku moja akaja geto jioni mda wa kulala nikashangaa analia tu wakati wa tendo tena anatoa ushirikiano balaa bt coz mi namjua ikabidi nistishe kwanza nikamuulza vp kwani,c akafunguka kwamba kafulia na jana yake kuna mtu alikuwa anapenda kumsalimia sn pale chuon sasa alimwalika menu nje ya chuo nyt coz alikuwa hana ktu ikabd aende jamaa likamnunulia menu,likampa na elf 10,ksha likampeleka lodge klchoendelea,...daah kweli mi nlimuonea tu huruma na nlmsamehe bt alilia usku kucha mi nkawa mmbembelezaji tena,after wote kumalza chuo naye akaja geto she was like me very much lyf lilikuwa tyt balaa ikfka mda wa kulala mnalala mmemalza kila ktu mpaka maji ya kunywa na hamjui tmr itakuaje bt ashukuriwe MUNGU hatukuwahi kulala na njaa,leo ndo mke wangu na tuna watoto 2.
Uuuh I'm touched, Mungu aendelee kuwatunza. Hapo kwenye kusamehe, hongera sana maana wanaume wengi na kusamehe kuchepuka mmh
 
Hayo yote uliyoyaandika , ndio nayapitia sasa. Tena yamekuwa kwa muda mrefu sana.

Ilifika mahala nikaenda SCOAN Nigeria kwa PTB Joshua kwa njia ya bara bara ( nilitumia siku 76 kufika)

Nimekuwa kiroho sana. But matatizo yapo pale pale. Na yanazidi kuongezeka mpaka kukimbiwa na watu wa karibu kabisa, uliowasomesha na kuwainua juu.

Wakwe kukuona kama mwehu, mke kukuona hufai , na kuudharau Wokovu wako.

Mara waseme sitaki Kazi, na kwamba nachagua Kazi. Wakwe wanamsisitiza mke wangu aachane na Mimi kuwa nampotezea muda, sina Kazi.

Nakuwa karibu sana na Mungu kila mara. Na ninafunga na kuomba kila mara.

Hii ni sehemu ambayo naitumia kusali mchana na Usiku..., asubuhi mchana jioni.

Usiku kabla ya saa 6 , Then saa 7-8 , na saa 9-10.

Nimetandaza vyeti vyangu vyote kuanzia chini hadi Postgraduate, na mahitaji ya watu wengine.

Natumia muda kuwaombea maadui

f077592e4c5aa05c1d2e35ac99a56ca1.jpg
Duh.. Pole sana Mkuu ila kwanini huo mda uliotumia kwenda huko Nigeria na gharama zake usingeanzisha kitu na kumuomba Mungu akusimamie katika hilo...

Kwani Mungu wa miujiza yupo Nigeria kwa TB Joshua tu??!! sasa hivi unafanya maombi na kufunga ukiwa katika nchi gani??

Sema usikate tamaa Mkuu.. Ila tusikubali matatizo yetu yakawa ndo chanzo cha umaskini wetu.. Komaa ipo siku utafanikiwa katika kile unachokiamini
 
Mshukuruni mungu kwa kila jambo kwani kila linalotokea kuna makusudi iwe adhabu au njia ya kuvuka ulipo! Tujitambue Na tuwe Na subira kupisha magumu yapite.
 
Hmmm, bado napitia kipindi kigumu sana..... Ninalipa deni la millions of money ambalo sikufaidika nalo, kwa lugha nyingine nimetapeliwa. Nimekuwa na sleepless nights. Ninafanya kazi 24hrs lakini ni kama namfanyia mtu......... Hmmm, Mungu yupo, najua yana mwisho. Ingawa mpaka sasa uzito wangu umepungua, hata concentration yangu kazini imepungua, kama ningekuwa nafanya kazi kwa MTU binafsi nafikiri ningekuwa nilisha timuliwa, lakini Mungu yupo, yataisha.
Hakuna jaribu lisilo na mlango wa kutokea.... Litapita na hili mpendwa
 
Hakuna jaribu lisilo na mlango wa kutokea.... Litapita na hili mpendwa
God is on the throne........ Kama aliruhusu mabaya yanipate, basis anauwezo wa kuruhusu na mema yanipate pia. Asante Dada.
 
Nimekumbuka mbali aseee! Kama kuna mtu alishawahi kupita road ya TABORA TO MPANDA pale kwenye pori la INYONGA lenye 92km tulikwama tulikuwa tunahama kutoka MAGU kwenda MPANDA Gari letu tairi zilibust mpaka speatairi tulilala siku3 hatujala chochote kile zaidi ya maji ya pale kwenye vijito, mbung'o ndo usiseme ni balaa anakuuma mpaka anaacha damu duh! Namshukuru MUNGU sana tena sana maana maeneo yale simba walikuwa si wakuuliza. Very sad sitaki kukumbuka kabisa.
 
kila mtu kwa asilimia kubwa kabisa...misoto hiyo tumepitia... kwa namna tofauti!! Angalawo tumepata hadhiti za kuathimulia watoto wetu!!!!
 
Mshukuruni mungu kwa kila jambo kwani kila linalotokea kuna makusudi iwe adhabu au njia ya kuvuka ulipo! Tujitambue Na tuwe Na subira kupisha magumu yapite.


Yani humu duniani ukifurahi siku mbili siku tano ni huzuni.
Unapopitia magumu kuna watu watakudharau, watakusema vibaya, watakushusha thamani lakini kubwa ni SUBIRA na kumkabidhi Mungu yote, maana bila mapito tupitiayo hatuwezi tambua ukuu wa Mungu.
 
Kuna muda kila kitu hakiendi sawa...
Unaona hakuna haja ya kuexist duniani...
Unajiuliza umefanya dhambi gani kubwa mpaka Mungu akaamua kukuacha uumie kiasi hicho...
Unakaa unatafakari na kuyasikiliza mapigo ya moyo wako,ndipo unapogundua yupo Mungu muweza wa yote asiyeshindwa na kitu chochote
Amani inarejea moyoni
 
Dah kuna wakat unamuona Mungu amekuacha kabisa.

Baba alifarik nikiwa darasa la pili. Nikalelewa na mama. Nikiwa sekondari ghafla mama akapoteza kazi, kila kitu kikavurugika. Hata mafuta ya kujipaka hamna, mimi na wadogo zangu tukawa tunajipakaa mwilin mafuta ya kupikia. Nyumban hamna chakula. Tunaenda shule asubuhi hatujanywa hata chai, tukirud jioni tunakuta mama yetu kapka uji wa mahindi tena hauna chumvi wala mafuta kanywa huo mchana na ucku tunalalia huo uji wa mchana. Ndugu wakatutenga, majiran wakatucheka.

Niachie tu hapa nkikumbuka zaidi machozi hayaishi kwenye macho yangu..

Acheni Mungu aitwe Mungu, yeye ni jana, leo, kesho na hata milele.
 
Back
Top Bottom