Wenye nguvu ya giza walivyopendelewa

Extraseen

Senior Member
Feb 18, 2017
140
136
Maumivu yangu katika maandishi

Unaweza zoea "ukiwa" katika maisha yako kiasi kwamba ukiona mtu anacheka unajiuliza hivi huyu yupo dunia ipi?

Guys, kuna maisha na kuna mapito. Kuna laana na kuna kuchukiwa. Siku zote usiombe Mungu akachukia familia yako wala asitie laana kwenye familia yako maana

Kuna kusaga meno na kuna kulia machozi ya damu

Kuna kudharauliwa na kutemwa mate

Kuna kushushwa kabla huja jishusha

Balaa zaidi nikukutana na watumishi fake wanao taka kutumia mateso yako kukutoa hela kwa kivuli cha mungu kawaagiza utoe sadaka flani ili akusamehe. Amini nakuambia usiombe usiombee!

Utashughudia hatua za maendeleo ya wenzako na wewe utakuwa ngazi ya kukanyagiwa wawo wafike juu. Ogopa sana hasira za Mungu. Ogopa sana maana hata usali na kutubu vipi kama asha piga muhuri wa mateso katika uzao wenu utaomba aridhi ipasuke.

Kuna wakati huwa najiuliza mara yangu ya mwisho kuwa na tabasamu la kweli usoni mwangu ni lini, wala sikumbuki nalitafuta sana jibu katika kipindi cha miaka mingi nyuma silioni, kile ninaweza kiona kwangu ni huzuni, ukiwa, maumivu ya moyo, maisha ya siyo na ladha, kutengwa, kufungiwa gereza kuu la ajira, mikono yangu kuwa locked na pingu isifanye biashara.

Mifuko yangu imetobolewa isikae na hela, hisia zangu zime kuwa diluted na chuki usipende wala kupendwa. Macho yangu yamekuzwa nishughudie maendeleo ya wengine na akili yangu imefungwa isifanye chochote katika dunia.

Kila nisalipo naona kabisa sala zangu hazina nguvu wala hazi mfikii muumba. Nikiwaza ukiwa wangu tangu nikiwa na miaka 3 mpaka nafikia utu uzima huu, najiuliza ikiwa tuna ambiwa mungu halali wala hafungi macho ilikuwaje mimi na ndugu zangu tukayapitia yote yale na mpaka sasa nayapitia haya yote?

Huwa najiuliza maswali ya wapi jicho lake lilipo kuwa hata mimi na ndugu zangu tuka yapitia yote haya? Najiuliza ule mpango wa wenye hila kutudhulumu haki yetu ya amani hapa duniani na kumuuwa baba na kaka yangu mkubwa, na bado wameendelea kuangamiza ukoo wa baba yangu, je! Mungu hakuona? Bila shaka aliona je! Ukimnya wake kwa miaka yote hii 30 ni kwamba haoini mateso yetu?

Je, yanayoendelea mpaka sasa hayaja mguswa kutoa adhabu yake kwa wahusika? Je, kama kuna kisasi cha Mungu cha adhabu kwetu, let' say kwamba mababu zetu wali muudhi akaachia laana ikaja kwetu sisi wa kizazi cha 4, je katika kulia kwetu na kuomboleza bado adhabu hizo za mababu hazi sameheki kwetu?

Je, hawa wanao tumia uchawi kutesa familia nzima na bado wana raha katika maisha yao na bila aibu wana jisema wazi wazi kuwa wata mmaliza yeyote atakaye inua mdomo kudai haki au kuulizia kifo cha baba mzazi, je hawa wame mpa nini mungu ata awafanye watabasamu na kuishi katika nyumba yetu?

Je, inatupasa tuishi kwa kulipiziana kisasi kwa kuwa haki kwa mungu haipatikani? Je, na mimi nikibuni mbinu yangu ya kuwaangamiza wale wanao wafanya ndugu zangu kuwa vichaa na kuuwa wengine, mungu ata nilinda kama anavyo walinda wale? Je huu uchawi unao tumika kuuwa wasio na hatia umepewa baraka na maandiko? Kama jibu ni hapana mbona maandiko yana sema usimuache mchawi aishi ila hawa wanaishi na kila mwaka wanauwa na kutesa watu kwa magonjwa, je hayo maandiko hayatendi kazi kwa ulimwengu wa sasa?

Kuna mengi sana nimejiuliza bila kupata majibu sana sana naogopa kuishia kumkufuru mungu wangu, ila naamini sistahili haya nipitiayo sasa, kwa kuwa nimeshughudia baadhi ya watu mbali mbali wakifanya kufuru na ushirikina mkubwa ambao mm sikusubutu hata kuya waza ila wao wana ishi kwa mafanikio na baraka za kila wafanyacho, ila uzao wa mama yangu umekuwa na mateso makali tangu utotoni mwao na bado wanataabika mpaka leo hii, na ukitafuta kikubwa walicho mkosea mungu hukioni.

Namuomba mungu sana kabla ya kufa kwangu angalao anifungulie kosa langu na ndugu zangu ni nini nipate amani maana nimetafuta tangu tukiwa na miaka mi3 ni mateso katika hii dunia, najaribu kuwaza ndugu zangu kwa mri ule walimkosea nini mungu hata aruhusu wawe mateka wa nguvu za giza, mateso yao kwa miaka yao yote mpaka sasa! Sina maana ya kupinga kazi ya mungu ila nautafuta ukweli wa fedhea hizi katika familia mauwaji, dhuluma na kusoma na kukosa kazi, biashara haziendi, kuchukiwa kwetu na kudharaulika.

Natamani siku moja niandike kitabu cha mapito yangu ya adhabu ya laana za mababu zinavyo ni andama mm wa kizazi cha 4.

Watu wajifunze kuwa hata ukiwa mwema kwa Mungu kama kuna muhuri wake ulifanyika juu ya kizazi chenu huta epuka muhuri huo.
 
Uchawi haupo. Achana na imani za kipumbavu.

Ujinga bado ni tatizo kubwa sana Tanzania. Watu bado wanaamini mamboya kipumbavu kama uchawi, ushirikina, ulozi, sijui miujiza na ujinga mwingine.

Hii nchi maendeleo yako mbali sana.
Uchawi haupo kweli au unatudanganya, Mungu nae unaamini yupo?
 
Kwanza kwa imani jiweke karibu sana na Allah, Amini mwenyezi Mungu hakosei na kila linalompata mja Allah alishalikadiria. Itahbitishe imani yako kwa Allah pekee na huenda ktk subra yako na Allah akakujibu kwa ukubwa wake na mambo yote yakabadilika na kuwa mepesi na kusahau yote uliyowahi kupitia.

Fanya toba, kama ni muislam simama usiku swali tahajud kwa hakika Allah yupo karibu sana na anasikia na wala hakawii sema kwa kibinadabu tunaona mateso yamekua ya muda mrefu. Hakika ya toba hufuta madhambi.

Namwomba mwenyezi Mungu kwa ukubwa wake , kwa uwezo wake ashushe rehma zake kwako akafanye yote yaliyo magumu kwako kua mepesi, akulinde na shari zote na akutahibitishe imani yako ktk dini ya mwenyezi Mungu mpk mwisho wako.

Pia usimshirikishe mwenyezi Mungu na kitu chcht amini yeye pekee anatosha, yeye pekee ndio wa kumtaka msaada na kumwabudu na yeye pekee mwombe akuongoze ktk yale aliyoaridhia

Mungu akufanyie wepesi
 
Kwanza kwa imani jiweke karibu sana na Allah, Amini mwenyezi Mungu hakosei na kila linalompata mja Allah alishalikadiria. Itahbitishe imani yako kwa Allah pekee na huenda ktk subra yako na Allah akakujibu kwa ukubwa wake na mambo yote yakabadilika na kuwa mepesi na kusahau yote uliyowahi kupitia..
Baby zu nina shida. Hii Zu ni Zuhra, Zulfa au?
 
images (14).jpeg

Nagawa utajiri
 
Kama Anakuroga,,wewe Uwa Kabisa Hiyo Mburunyenge. Kuna Mmoja Na Mimi Najaribu Kumpa Muda Nione Kama Atabadirika...Nitamfuta Kabisa Hata Kile Anachokitafuta Hata Kipata Kabisaa..
Sina kitu mkononi nimefilisika kabisa, ila naomba kama unaweza niondolea hawa watu wawili wanao itesa familia yangu. Nitakupa Hekari 3.5. zipo Morogoro hichi ndicho nilichofanikiwa kumiliki kwa mkono wangu na jasho langu maishani mwangu.

Nimefilisika hakuna hata senti ya kula, ila Kama una njia ya kuwaondoa hawa watu wawili ili ndungu zangu watoke kwenye mateso wanayofanyiwa basi ntakupa hizi ekari3 na nusu.. zipo Mbele kidogo ya Chalinze eneo linaitwa Bwawani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana mkuu.

Amani ya Mungu idumu kwenu, idumu na kwa wengine pia.
 
Ogopa sana maana hata usali na kutubu vipi kama asha piga muhuri wa mateso katika uzao wenu utaomba aridhi ipasuke.
Isaya 49:15 Je! Mwanamke aweza kumsahau mtoto wake anyonyaye, hata asimhurumie mwana wa tumbo lake? Naam, hawa waweza kusahau, lakini mimi sitakusahau wewe.

Isaya 49:16 Tazama, nimekuchora katika vitanga vya mikono yangu; kuta zako ziko mbele zangu daima.

MUNGU hawezi kukusahau kabisa !!!
 
Isaya 49:15 Je! Mwanamke aweza kumsahau mtoto wake anyonyaye, hata asimhurumie mwana wa tumbo lake? Naam, hawa waweza kusahau, lakini mimi sitakusahau wewe.
Isaya 49:16 Tazama, nimekuchora katika vitanga vya mikono yangu; kuta zako ziko mbele zangu daima.


MUNGU hawezi kukusahau kabisa !!!
Kwa Haya Maumivu ya Moyo na Msongo wa Mawazo.. Na Taarifa za Mateso ya Ndugu zangu yanavyo nitesa akili.. maana Degree niliyosoma haina samani vyeti viko kabatini.. Siiajiriki.. Biashara nilizo fanya zote zimekufa.

Alafu kila siku unauza vitu vya ndani ili upate kula .. Ukijaribu kusema usamehe ili Mungu afanye kazi yake, Ghafla unapokea Simu ya Ndugu flani kawa kichaa mara kesho Mama tatizo hili mara kesho kutwa Unaambiwa Walio wazulumu wanauza nyumba yenu Mara ghafla Ndugu yako mwingine Ameacha kazi anakunywa tu pombe mpaka ana lala mitaroni. Ghafla unaambiwa ndugu mwingine Kachanganyikiwa ameonekana ana ongea mwenyewe njiani.. ukimfuatilia unaambiwa Ana lala kwenye Mito maporini..

AJABU WATOTO WOTE TULIZALIWA KWENYE FAMILIA BORA BABA ALIKUWA BOSS MKUBWA SABA BANK KUKU(BOT) TULIZALIWA WAZIMA WOTE MPAKA WATU WANAFIKIA MIAKA 30 WENGINE 35 GHAFLA WOTE WANACHANGANYIKIWA ALAFU WANO TUFANYIA WANA TAMBA KABISA MITAANI KUWA WATA TUMALIZAA.. Hivi unadhani kama yote haya yanatoke Je Hayo maandiko yako yangekuwa yana wezekana yasinge tekelezeka ?
 
Unataka kujiongezea laana kwa kumwaga damu? Ili waje walupie tena vizazi vyako?

Kwanza unatakiwa umtambue adui yako ndiyo utashinda, naona umemtaja Mungu kama adui then ukawataja hawa watu wawili ba uko tayari kuua

ADUI yako hujamtambua bado yuko anakuangalia anacheeekaaa

Pambana na shetani ndio adui yako hao watu wanatumiwa tu kukufikia sababu ukiwaua hao watainuliwa wengine kukusulubu, utaua wangapi?
Natambua kabisa maadui zangu, Wala Sina niliposema Mungu ni adui.. ila nimehoji iweje yote hayo yatokee mbele ya Uso wa Mungu ? Kama ni Adui na mjua ni Shetani kupitia hawa Watu. Je, ikiwa neneo linasema Usimuache mchawi aishi.. je mbona nimesali miaka karibia 6 kuomba neneo hilo likatimie ili Familia yangu iepuke mateso mbona neneo hilo lisitimie? Ina maana tunatakiws tuteseke na wao wafurahie maisha.. kwa mujibu wa neno lipi? Je kama Wame muuwa Baba, na Kaka, na sasa wa Nyemelea kuutuuwa na Sisi.. Je uwo ulinzi wanaopewa na Mungu na sisi tukifanya kwa nini tusilindwe?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa Haya Maumivu ya Moyo na Msongo wa Mawazo.. Na Taarifa za Mateso ya Ndugu zangu yanavyo nitesa akili.. maana Degree niliyosoma haina samani vyeti viko kabatini.. Siiajiriki.. Biashara nilizo fanya zote zimekufa.. Alafu kila siku unauza vitu vya ndani ili upate kula .. Ukijaribu kusema usamehe ili Mungu afanye kazi yake, Ghafla unapokea Simu ya Ndugu flani kawa kichaa mara kesho Mama tatizo hili mara kesho kutwa Unaambiwa Walio wazulumu wanauza nyumba yenu Mara ghafla Ndugu yako mwingine Ameacha kazi anakunywa tu pombe mpaka ana lala mitaroni.. Ghafla unaambiwa ndugu mwingine Kachanganyikiwa ameonekana ana ongea mwenyewe njiani.. ukimfuatilia unaambiwa Ana lala kwenye Mito maporini.. AJABU WATOTO WOTE TULIZALIWA KWENYE FAMILIA BORA BABA ALIKUWA BOSS MKUBWA SABA BANK KUKU(BOT) TULIZALIWA WAZIMA WOTE MPAKA WATU WANAFIKIA MIAKA 30 WENGINE 35 GHAFLA WOTE WANACHANGANYIKIWA ALAFU WANO TUFANYIA WANA TAMBA KABISA MITAANI KUWA WATA TUMALIZAA.. Hivi unadhani kama yote haya yanatoke Je Hayo maandiko yako yangekuwa yana wezekana yasinge tekelezeka ??

Sent using Jamii Forums mobile app
Pole sana kwa yaliyo na yanayoendelea kukukuta lakini nikwambie mambo haya

1. Kuna jambo lolote ambalo ukilikumbuka unasema hili niliweza kufanikiwa?

Note: Yaani MPANGO mkubwa wa shetani ni kituweka mbali na MUNGU kwa namna Yoyote ile

Hata mimi kipindi cha nyuma niliona kujiua ndio suluhisho lakini ukweli ni MUNGU ndio amekuwa suluhisho
 
Pole sana kwa yaliyo na yanayoendelea kukukuta lakini nikwambie mambo haya

1. Kuna jambo lolote ambalo ukilikumbuka unasema hili niliweza kufanikiwa ??

Note:Yaani MPANGO mkubwa wa shetani ni kituweka mbali na MUNGU kwa namna Yoyote ile ,

Hata mimi kipindi cha nyuma niliona kujiua ndio suluhisho lakini ukweli ni MUNGU ndio amekuwa suluhisho
Ndugu kama Ni kusali na kutubu kwa ajilimya ndugu zangu nimefanya sana nimepiga goti na kufunga sana.. nimefikia hatua ya kusali mara Saba kwa siku.. Lakini Ndio kwanza imefikia mahali Nauza vitu vya ndani ili nile.. Ajira hakuna Biashara hakuna.. Na ndugu ndio kwanza wana taabika.. Je Unadhani Kuna njia nyingine ya Kumtafuta Mungu zaidi ya hizi nilizofanya? Je! Mungu haoni Maangaiko ya viumbe wake??

Naamini Mungu Anataka tuache kuwa wapole.. Kama ni upole wa Familia yangu umekuwa mkubwa kupitiliza.. Nahisi uruma ya mama yangu na ndugu yangu inatuponza na huenda uruma yetu ina mchukiza Mungu.. Hatuna Budi na sisi Kuanza Malipizi kwa Kasi kubwa tena bila huruma.
 
Sina kitu mkononi nimefilisika kabisa.. ila naomba kama unaweza niondolea hawa watu wawili wanao itesa familia yangu.. Nitakupa Hekari 3.5. zipo Morogoro hichi ndicho nilichofanikiwa kumiliki kwa mkono wangu na jasho langu maishani mwangu..

Nimefilisika hakuna hata senti ya kula.. ila Kama una njia ya kuwaondoa hawa watu wawili ili ndungu zangu watoke kwenye mateso wanayofanyiwa basi ntakupa hizi ekari3 na nusu.. zipo Mbele kidogo ya Chalinze eneo linaitwa Bwawani.
Una ekari 3.5 ya ardhi ya kugawa bado unalia!!! We una matatizo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom