Je, umeshawahi pitia maisha magumu?

Je, umeshawahi pitia maisha magumu?

Dah kuna wakat unamuona Mungu amekuacha kabisa.

Baba alifarik nikiwa darasa la pili. Nikalelewa na mama. Nikiwa sekondari ghafla mama akapoteza kazi, kila kitu kikavurugika. Hata mafuta ya kujipaka hamna, mimi na wadogo zangu tukawa tunajipakaa mwilin mafuta ya kupikia. Nyumban hamna chakula. Tunaenda shule asubuhi hatujanywa hata chai, tukirud jioni tunakuta mama yetu kapka uji wa mahindi tena hauna chumvi wala mafuta kanywa huo mchana na ucku tunalalia huo uji wa mchana. Ndugu wakatutenga, majiran wakatucheka.

Niachie tu hapa nkikumbuka zaidi machozi hayaishi kwenye macho yangu..

Acheni Mungu aitwe Mungu, yeye ni jana, leo, kesho na hata milele.
 
We acha tu...............kila kukicha aheri ya jana ndo maisha yangu
 
Duh! Noma sana, kumbe wenye shida ni wengi. Ofcoz mi nipo ktk wakat mgumu sikuwahi kufikiria yaan ndoto zangu zote zimezimwa na ugonjwa flan wa ajabu ajabu tu. I don't know how my tomorrow would be...
 
Dah kuna wakat unamuona Mungu amekuacha kabisa.

Baba alifarik nikiwa darasa la pili. Nikalelewa na mama. Nikiwa sekondari ghafla mama akapoteza kazi, kila kitu kikavurugika. Hata mafuta ya kujipaka hamna, mimi na wadogo zangu tukawa tunajipakaa mwilin mafuta ya kupikia. Nyumban hamna chakula. Tunaenda shule asubuhi hatujanywa hata chai, tukirud jioni tunakuta mama yetu kapka uji wa mahindi tena hauna chumvi wala mafuta kanywa huo mchana na ucku tunalalia huo uji wa mchana. Ndugu wakatutenga, majiran wakatucheka.

Niachie tu hapa nkikumbuka zaidi machozi hayaishi kwenye macho yangu..

Acheni Mungu aitwe Mungu, yeye ni jana, leo, kesho na hata milele.
Umeiva Ki Maisha..yaani umekomaa/umepevua ki ufahamu.
 
pia mimi niliwahi kuacha kabisa kwenda kanisani na niliwachukia sn wachungaji,kuna kpnd mambo yng yalienda mlama kazin nkafukuzwa kwa bahati mbaya mambo mengi nlikuwa namshirikisha mchungaji mpaka migogoro yng na mke wng pia nlikuwa kiongoz kanisani,baada kuona mchungaji anapeleka mambo ndivyo sivyo nliandka barua ya kujiudhuru uongozi,aisee mchungaji alinikashfu mbele ya kanisa akdai mi sina hela,nalishwa na mke wng,watu wasje kwangu wala wasinisalimie wala kunisaidia kwa lolote,akaanza kampen ya kuniachanisha na mke wng akawa anamshawishi,ikafkia hatua akampgia simu ma mkwe wng lengo likiwa ni kuhakikisha naachana na mke wng..aah nyie acheni.
NI balaa kubwa,,,
Kipindi upo katika hali ngumu,utashangaa wale wanaomkufuru Mungu ndio mambo yao yako vyema!!
Very SAD.
 
kuna wakati pesa ipo, kula ni uhakika, kuvaa sio tatizo but mtu unakosa amani ya moyo "PEACE OF MIND" hii kitu imenitesa sana japo mengine mengi nimepitia. kullalia maboksi nje, kuumwa mpaka unaomba mungu ufe lakini mpaka leo bado niko hai.
Ilifikia hatua nikadikira hadi kujinyonga na kusema atamuomba tena Mungu kwa lolote maana hanisaidii, lakini upendo wake ni wa ajabu nia yangu ikabadilika.
Sina marafiki mtaani maana niliishaona ni mzigo tu, wamebaki wa mitandaoni kama hivi jf nikiingia nitahuzunikia humu, nitacheka humu, nitaelimika humu, nitaelimisha humu.... mbali na mitandao ni kazi, kumwomba Mungu na kulala.
 
mi wakati nimemaliza chuo,ilikuwa ni balaa,nilikuwa na mpenz wng wakati mi niko home ye alikuwa bado yuko chuo,sina hata mia sku moja akaja geto jioni mda wa kulala nikashangaa analia tu wakati wa tendo tena anatoa ushirikiano balaa bt coz mi namjua ikabidi nistishe kwanza nikamuulza vp kwani,c akafunguka kwamba kafulia na jana yake kuna mtu alikuwa anapenda kumsalimia sn pale chuon sasa alimwalika menu nje ya chuo nyt coz alikuwa hana ktu ikabd aende jamaa likamnunulia menu,likampa na elf 10,ksha likampeleka lodge klchoendelea,...daah kweli mi nlimuonea tu huruma na nlmsamehe bt alilia usku kucha mi nkawa mmbembelezaji tena,after wote kumalza chuo naye akaja geto she was like me very much lyf lilikuwa tyt balaa ikfka mda wa kulala mnalala mmemalza kila ktu mpaka maji ya kunywa na hamjui tmr itakuaje bt ashukuriwe MUNGU hatukuwahi kulala na njaa,leo ndo mke wangu na tuna watoto 2.
Mkuu story yako inahuzunisha ila pia ilitawaliwa na penzi la kweli.
Mmetoka mbali na Mungu awajaalie muwe pamoja mpaka mwisho.Ni wanawake wachache sana wanaweza ivumilia hiyo hali.
 
Daaah I remember those days nikiwa na miaka 9 wazazi wote walifariki Bahati walikuwa hawana hata kiwanja pamoja na kwamba walikuwa watumishi siwazi walaumu sana bse tulizaliwa sita inawezekana ni katika pilikapilika za kutulea, Nakumbuka cku tunarudishwa nyumbani kwa Babu na Gari la Serikali msoto ukaanzia hapo Ashukuriwe Baba mdogo aliyesomeshwa na Baba kutukumbuka kutupeleka shule wote sita hakika hatukumuangusha tumetusua life ile kwa kweli imenifanya kuwa nasomesha ndugu zangu wenye mwerekeo.wanaohang kijiini
Mwenyezi Mungu azidi kukubariki kwa hilo.Wachache hukumbuka fadhila ila wengi husahau
 
kuna wakati pesa ipo, kula ni uhakika, kuvaa sio tatizo but mtu unakosa amani ya moyo "PEACE OF MIND" hii kitu imenitesa sana japo mengine mengi nimepitia. kullalia maboksi nje, kuumwa mpaka unaomba mungu ufe lakini mpaka leo bado niko hai.
Ilifikia hatua nikadikira hadi kujinyonga na kusema atamuomba tena Mungu kwa lolote maana hanisaidii, lakini upendo wake ni wa ajabu nia yangu ikabadilika.
Sina marafiki mtaani maana niliishaona ni mzigo tu, wamebaki wa mitandaoni kama hivi jf nikiingia nitahuzunikia humu, nitacheka humu, nitaelimika humu, nitaelimisha humu.... mbali na mitandao ni kazi, kumwomba Mungu na kulala.
Ni kujipa moyo na kushukuru kwakila jambo
 
Yako ni cha mtoto Watu tulikimbiwa na wazazi wrote,Ila Leo ni Msomi Na Pesa ,,Wote 5 Children wana Degree Nilichowambia Madogo Tuwapende sana Wazazi wetu,,Leo Nawapenda sana Wazazi wangu kuliko wote
 
Nina Vita kubwa sana katika Ulimwengu wa Roho, kwasababu shetani na majeshi yake yote wananifahamu vizuri sana , that I am a noble person ( A righteous branch and the repairer of the broken walls) ; Naelewa kuwa wanaumiza vichwa sana jinsi ya kunimaliza kwa muda mrefu wameshindwa.

Wakati nazaliwa, nilizaliwa nikatoka na chupa ya uzazi kama mnyama; na hata baada ya kuipasua chupa wakanikuta kondo la uzazi limeniviringa mara tatu shingoni.

Nikiwa na 3 years, niligundulika kuwa ni bubu, nikakatwa karimi.

Baadae nikapata mke mwenye HIV+ na nimeishi nae kwa zaidi ya 8 years bila kupata maambukizi wala watoto wangu kupata maambukizi. What a mighty God.

So nina elewa kuwa Mwili wangu sio wa kawaida, kwasababu ya kuepuka vifo vingi sana. Niliwahi kutekwa na Magaidi zaidi ya mara 2 na hawakuweza kunifanya kitu.

I know the truth, wa haya yote. Sio kwa nguvu zangu.

Kaka usimwache Mungu.
 
Kipindi hiki tunapitia wakati mgumu sana kwa maana ya mazoea au style ya maisha ime-change!! Utulivu unatakiwa .
 
Unakutana na mtu mnayefahamiana halafu anakukwepa hataki hata salamu.!
Sababu anaona hata mavazi yako yamechoka/pauka/chakaa🙁
 
Back
Top Bottom