Je, ni uchawi au saikolojia?

Je, ni uchawi au saikolojia?

Kwanza hiyo mistari ya bibilia sijaiweka kwa sababu nina iamini sana hapana

Nimeweka kama sehemu tu ya kuonesha dhana ya uchawi ni ya kale sana

Sawa, kama umeweka hiyo mistari ya Biblia kuonyesha tu kwamba dhana ya uchawi ni ya kale, basi hilo halijibu swali la msingi: uchawi ulianza wapi, nani aliufundisha, na kwa kusudi gani?

Qur’an haisemi kwamba uchawi ulianzishwa na Mungu. Badala yake, Qur’an 2:102 inataja kwamba watu walijifunza uchawi na inaonya juu ya madhara yake.

Na Biblia yenyewe inautaja uchawi kama jambo lililokuwepo na kulikataza (Kutoka 22:18; Kumbukumbu 18:10–12).

Kwa hiyo kusema “dhana ya uchawi ni ya kale” hakuthibitishi kwamba uchawi haupo. Uzee wa dhana si ushahidi wa uongo wake. Kama unadai kwamba ni hadithi iliyobuniwa na wanadamu, basi lete ushahidi wa hilo.

Na kuhusu “nani alianzisha uchawi?” — swali hilo haliwezi kujibiwa kwa kudhani kwamba kwa kuwa Mungu ameumba viumbe wenye uwezo fulani, basi Mungu ndiye aliyewafundisha uchawi. Qur’an inatofautisha wazi kati ya uumbaji wa Mungu na matendo ya viumbe wenye hiari.

Kwa hiyo tusichanganye mambo mawili: Mungu kuumba viumbe si sawa na Mungu kuanzisha au kuamuru uchawi.
 
Sawa, kama umeweka hiyo mistari ya Biblia kuonyesha tu kwamba dhana ya uchawi ni ya kale, basi hilo halijibu swali la msingi: uchawi ulianza wapi, nani aliufundisha, na kwa kusudi gani?
Hilo swali la msingi ameuliza nani?

Kwa sababu mimi kwenye bandiko langu kutumia mistari ya Biblia na Qur’an sio kwamba et nakubaliana na uchawi na bla bla zake hapana

Nilitumia hiyo mistari kama sehemu tu ya kuonesha hiyo dhana ya uchawi ambayo ki msingi haina faida yoyote ilianza zamani sana

Sasa wewe mkuu mpaka sasa nikipitia reply zako nashindwa kuelewa unaongelea kitu gani

Mimi binafsi sikubaliani na habari za uchawi naamini baadhi ya mambo watu wanayodai ni uchawi sometimes ni issue ya saikolojia
 
Nimekuelewa mkuu. Sikusema kwamba wewe unaamini uchawi wala kwamba mistari uliyoweka ina maana unakubaliana nao. Hoja yangu ilikuwa kwenye swali la chanzo na uhalisia wa uchawi, kwa sababu ulisema dhana hiyo ilianza zamani sana na kwamba baadhi ya mambo yanayoitwa uchawi yanaweza kuwa ya kisaikolojia.

Kwa hiyo nilikuwa natenganisha mambo mawili: mjadala wa kihistoria kuhusu dhana ya uchawi, na imani kwamba uchawi wenyewe upo. Kama wewe unaona kwamba uchawi hauna msingi na baadhi ya matukio yanaelezeka kisaikolojia, hilo ni jambo linaloweza kujadiliwa kwa ushahidi.

Lakini kusema tu kwamba “dhana ya uchawi ni ya kale” hakutoshi kuthibitisha kwamba uchawi haupo. Vivyo hivyo, mimi sikudai kwamba kila jambo linaloitwa uchawi lazima liwe uchawi.

Tukubaliane kwanza kwenye swali tunalolijadili, ndipo tutazame ushahidi bila kuchanganya hoja.
 
Kama ni hivyo mbona ni rahisi sana KUTHIBITISHA mkuu………. Kwasababu hiyo ni pure science

Changamoto ni kwamba kila mtu anaye AMINI uchawi anakuja na NADHARIA yake

Mfano, ni kweli wachawi wanaruka na ungo, wanageuza watu fisi, wanahamisha hela au mazao shambani kwenda kwao nk nk kwa kuchanganya vitu kadhaa?
Sasa wewe kwa akili zako timamu unaona kuna ugumu gani wa kuthibitisha hapo?

Kwanza umejujaje? Wewe ni mchawi au mchawi alikupa hizo taarifa? Au unasikia tu kwa watu?
Nachokiona ktk majibu yako ni gape LA maarifa
 
Nimekuelewa mkuu. Sikusema kwamba wewe unaamini uchawi wala kwamba mistari uliyoweka ina maana unakubaliana nao. Hoja yangu ilikuwa kwenye swali la chanzo na uhalisia wa uchawi, kwa sababu ulisema dhana hiyo ilianza zamani sana na kwamba baadhi ya mambo yanayoitwa uchawi yanaweza kuwa ya kisaikolojia.

Kwa hiyo nilikuwa natenganisha mambo mawili: mjadala wa kihistoria kuhusu dhana ya uchawi, na imani kwamba uchawi wenyewe upo. Kama wewe unaona kwamba uchawi hauna msingi na baadhi ya matukio yanaelezeka kisaikolojia, hilo ni jambo linaloweza kujadiliwa kwa ushahidi.

Lakini kusema tu kwamba “dhana ya uchawi ni ya kale” hakutoshi kuthibitisha kwamba uchawi haupo. Vivyo hivyo, mimi sikudai kwamba kila jambo linaloitwa uchawi lazima liwe uchawi.

Tukubaliane kwanza kwenye swali tunalolijadili, ndipo tutazame ushahidi bila kuchanganya hoja.
Mkuu hebu nyooka nikuelewe
Unaamini uchawi upo au haupo
Halafu tuendelee
 
Kwahiyo tunakubaliana HAKUNA UTHIBITISHO kwamba uchawi upo?
Ndio hadi sasa hakuna uthibitisho wa kisayansi wa uchawi, na ndio sababu kuu ya kuonekana hakuna uchawi.
 
Hilo swali la msingi ameuliza nani?

Kwa sababu mimi kwenye bandiko langu kutumia mistari ya Biblia na Qur’an sio kwamba et nakubaliana na uchawi na bla bla zake hapana

Nilitumia hiyo mistari kama sehemu tu ya kuonesha hiyo dhana ya uchawi ambayo ki msingi haina faida yoyote ilianza zamani sana

Sasa wewe mkuu mpaka sasa nikipitia reply zako nashindwa kuelewa unaongelea kitu gani

Mimi binafsi sikubaliani na habari za uchawi naamini baadhi ya mambo watu wanayodai ni uchawi sometimes ni issue ya saikolojia
Kumbe unazungumzia baadhi ya mambo tu?
 
Ndiyo baadhi ya mambo
mengine ni theory kabisa hata hayapo
Leo mchana nilikuwa nasikiliza kipindi cha njia panda ambacho huwa kinarushwa kila jumapili katika radio ya clouds fm, huwa wanaalika wageni pale ambao wanaeleza changamoto zao hasa zinakuwa za kiafya ili wapate kuchangiwa wakapate matibabu.

Sasa kuna mdada katika kuelezea changamoto za mtoto wake mwenye kuhitaji msaada akaeleza tukio moja kwamba mwanae alikuwa anachelewa sana kutembea, imani ikaja kuwa karogwa hivyo huyo mtoto akapelekwa kwa mganga akachanjwa dawa na kweli akaanza kutembea.

Sasa nikajiuliza hapo saikolojia imefanyaje kazi kwa huyo mtoto ambaye hata hakuwa akielewa kinachoendelea hadi akaweza kutembea baada ya kutumia dawa ya mganga ambayo mama yake ndiye aliamini mwanae karogwa?
 
Ina maana huyo mtoto alitembea papo hapo mara baada ya kuchanjwa?

Usikute muda wa kutembea mtoto ulikua ni huo

Hii baado haiwezi kua sababu tuseme uchawi upo

Hapo tukimuuliza aligunduaje huo ulikua uchawi hawezi kutoa majibu
 
Leo mchana nilikuwa nasikiliza kipindi cha njia panda ambacho huwa kinarushwa kila jumapili katika radio ya clouds fm, huwa wanaalika wageni pale ambao wanaeleza changamoto zao hasa zinakuwa za kiafya ili wapate kuchangiwa wakapate matibabu.

Sasa kuna mdada katika kuelezea changamoto za mtoto wake mwenye kuhitaji msaada akaeleza tukio moja kwamba mwanae alikuwa anachelewa sana kutembea, imani ikaja kuwa karogwa hivyo huyo mtoto akapelekwa kwa mganga akachanjwa dawa na kweli akaanza kutembea.

Sasa nikajiuliza hapo saikolojia imefanyaje kazi kwa huyo mtoto ambaye hata hakuwa akielewa kinachoendelea hadi akaweza kutembea baada ya kutumia dawa ya mganga ambayo mama yake ndiye aliamini mwanae karogwa?
Hili ndio TATIZO KUBWA SANA la watu wa IMANI………….. kazi yenu ni KUSIKIA kisa cha kichawi na kisha KUAMINI 100%

Ndio maana tunasema IMANI huwa haitaki matumizi sahihi ya AKILI………….. Nyie ndio mkiambiwa na wachungaji wenu chochote MNAKUBALI tu
 
Uchawi upo, majini yapo na kila ulichoambiwa kipo wala sio saikolojia kama unavyoamini

Kwanini technolojia ya kupaa isihalalishwe ili kupunguza foleni hilo jambo haliwezekani kwa sababu lipo kiimani, litawezekana tu kama wote mnaimani ya uchawi maana litakuwa jambo la kawaida, ila as long as ipo nguvu kinzani na mambo ya giza hilo jambo halitakaa liwezekane
 
Back
Top Bottom