Je, kuna watu wanaoweza kusoma mawazo ya wengine? 🧠

Je, kuna watu wanaoweza kusoma mawazo ya wengine? 🧠

KARIBU KWENYE MADA WANA GREAT THINKERS 🧠 ☕️

Unaweza vipi kusoma mawazo ya mtu mwingine au kujua kinachoendelea kwenye akili yake?

Unaamini kama kuna watu wanaoweza kusoma akili au mawazo ya watu wengine?

Unadhani ni nini huwa kinatokea pale mtu anapoona maandishi ya mtu au akiwa kwenye mazungumzo na mtu mwingine, halafu akagundua kwamba huyu mtu anawaza kitu fulani?

Na ajabu, unakuta baadae yule mtu anafanya kitendo au vitendo vinavyothibitisha kwamba yale aliyogundua mwanzo yalikuwa sahihi

Kisayansi hali hii inaelewekaje?

Hawa watu tunaweza kuwaita watambuzi.watu wenye intuition kubwa wenye uwezo mkubwa wa kuchanganua watu, au ni geniuses?

Na wewe binafsi unaamini unaweza kusoma akili ya mtu?

Kama ndiyo unafanya hivyo kwa namna gani?

Maoni yangu 👇

Kikawaida kabisa, naamini kuna watu wenye uwezo mkubwa sana wa kutambua mambo hata bila mtu kuyaeleza moja kwa moja

Sio kwamba wanatumia akili ya ajabu au wanaingia kwenye akili ya mtu mwingine bali kuna wakati mtu akiwa makini sana anaweza kuona signals ndogo ndogo ambazo watu wengine hawazioni

Hata kama mtu anajaribu kufake au kuficha mawazo yake kwa kuongea au kuandika kitu tofauti na anachohisi, ukiwa makini sana unaweza kugundua kuna kitu hakipo sawa

Ni sawa na mtu ambaye anaweza kukuonyesha kwamba amefurahi sana kwa sababu umepata kazi

Anaweza kucheka kukusifia na kukuambia:

Hongera sana ShesRise_1 nimefurahi kwa ajili yako umepata kazi

Lakini wakati huo huo kuna signals nyingine unaweza kuziona

Labda kwenye facial expression yake namna anavyocheka tone la sauti macho, movements za mikono, posture yake au hata namna anavyoendelea na mazungumzo
Unaona kabisa yeye wa ndani
Na yeye wa njee ni kama mifumo haisomani

Na kama wewe ni mtu ambaye una observation nzuri na ubongo wako unafanya kazi shap utagundua haraka sana

Huyu mtu kwa ndani hafurahii kama anavyosema

So patterns ukiziona unagundua huyu anawaza kwa namna nyingine kabisa tofauti na anachokionesha

Na kinachofanya jambo hili liwe interesting zaidi ni pale unapokuja kugundua kwamba baadae yule mtu anafanya kitu kinachothibitisha kile ulichohisi mwanzo

Swali la mjadala?👇

Hua najiuliza nimeisoma akili yake, au nilikuwa nimeisoma signals zake vizuri na kwa haraka?

Na kama kweli kuna watu wenye uwezo huu mkubwa wa kutambua kile ambacho wengine wanajaribu kuficha...

Uwezo huu unatokana na nini?

Ni intuition?
Ni experience?

Ndio Kuna watu wanauwezo wa kusoma MAWAZO ya mtu na pia Kuna watu wanauwezo wa kusoma AKILI ya mtu.

Intuition na experience ndio vinamsaidia mtu kuweza kujua mtu mwingine anawaza Nini au anafikilia Nini. Ili twende sawa hapa ni lazima uelewe kwamba Kuna kusoma MAWAZO alafu kuna kusoma AKILI ya mtu.

1. UNAWEZAJE KUSOMA MAWAZO YA MTU?

Mara nyingi mtu anapowaza hutoa energy sasa hiyo energy hutoka kama WAVELENGTH ambazo hizo wavelength hupimwa kwa FREQUENCY ( QUANTUM PHYSICS).
Sasa kwa mtu anaetaka kusoma mawazo ya mtu mwingine ni lazima aiset akili yake katika FREQUENCY sawa na zile anazotoa mtu anaewaza. Kupitia hapo utaweza kujua mawazo ya mtu mwingine. Kwa lugha nyingine ndio wanaita TELEPATHY.

Binafsi zamani hizo nilikua naweza kutwist frequency zangu nikaingilia frequency za mtu mwingine. Nilikua natumia njia ya kawaida tuu kwamba mtu amekaa ametulia mimi naweza kukaa sehemu ambapo hanioni ila Mimi namuona alafu namuangalia usoni ndani ya muda wa dakika bhasi naweza kuwa nimeshaingilia FREQUENCY zake na kusoma mawazo yake.
Baada ya hapo mimi naweza kumwambia mawazo aliyonayo pia naweza nikampa hata majibu yake pasipo yeye kuniambia alichokuwa anakiwaza.

NB: Hii tabia niliacha baada ya kuona watu wengi wanawaza mawazo mabaya. Ilikua inanidrain sana energy kukuta mtu anawaza mawazo mabaya.

Njia hii mara nyingi inakuwa ni INTUITION maana unakua hujui usahihi wa jambo lenyewe lakini unaamini ndicho anachowaza na ukija kumuuliza unakuta ni sahihi.

Njia hii huwa haiwi kwa mawazo pekee bali pia inaweza kuwa ni body language au pia inaweza kuwa ni nguvu( energy ).

2.UNAWEZAJE KUSOMA AKILI YA MTU?

Unaweza kuisoma akili ya mtu kutokana na mazingira na pia mazoea(EXPERIENCE).

Mara nyingi akili ya binadamu au kiumbe chochote hufanya mambo yake kwa mazoea. Hivyo ukifuatilia sana mienenondo ya mtu bhasi ni rahisi sana kuisoma akili yake.

Mfano askari upelelezi hufundishwa tabia zote za wezi hivyo kwake yeye ni rahisi sana kuisoma akili ya mwizi endapo atapewa kazi ya kumtafuta. Maana atatumia tuu ile EXPERIENCE aliyonayo kuhusu wezi.

HITIMISHO

Ndio watu wanaweza kusoma AKILI na MAWAZO ya watu wengine. Na njia wanazotumia ni

MAWAZO --> INTUITION

AKILI --> EXPERIENCE
 
Ndio Kuna watu wanauwezo wa kusoma MAWAZO ya mtu na pia Kuna watu wanauwezo wa kusoma AKILI ya mtu.

Intuition na experience ndio vinamsaidia mtu kuweza kujua mtu mwingine anawaza Nini au anafikilia Nini. Ili twende sawa hapa ni lazima uelewe kwamba Kuna kusoma MAWAZO alafu kuna kusoma AKILI ya mtu.

1. UNAWEZAJE KUSOMA MAWAZO YA MTU?

Mara nyingi mtu anapowaza hutoa energy sasa hiyo energy hutoka kama WAVELENGTH ambazo hizo wavelength hupimwa kwa FREQUENCY ( QUANTUM PHYSICS).
Sasa kwa mtu anaetaka kusoma mawazo ya mtu mwingine ni lazima aiset akili yake katika FREQUENCY sawa na zile anazotoa mtu anaewaza. Kupitia hapo utaweza kujua mawazo ya mtu mwingine. Kwa lugha nyingine ndio wanaita TELEPATHY.

Binafsi zamani hizo nilikua naweza kutwist frequency zangu nikaingilia frequency za mtu mwingine. Nilikua natumia njia ya kawaida tuu kwamba mtu amekaa ametulia mimi naweza kukaa sehemu ambapo hanioni ila Mimi namuona alafu namuangalia usoni ndani ya muda wa dakika bhasi naweza kuwa nimeshaingilia FREQUENCY zake na kusoma mawazo yake.
Baada ya hapo mimi naweza kumwambia mawazo aliyonayo pia naweza nikampa hata majibu yake pasipo yeye kuniambia alichokuwa anakiwaza.

NB: Hii tabia niliacha baada ya kuona watu wengi wanawaza mawazo mabaya. Ilikua inanidrain sana energy kukuta mtu anawaza mawazo mabaya.

Njia hii mara nyingi inakuwa ni INTUITION maana unakua hujui usahihi wa jambo lenyewe lakini unaamini ndicho anachowaza na ukija kumuuliza unakuta ni sahihi.

Njia hii huwa haiwi kwa mawazo pekee bali pia inaweza kuwa ni body language au pia inaweza kuwa ni nguvu( energy
Nimesoma hapa mpaka nahisi kicwa kinauma aisee
 
FB_IMG_1789903077473.jpg
 
Aisee! Pole mkuu nimekurudisha shuleni na utu uzima huu😂.
Anyway bahati mbaya nilidhani itakuwa rahisi kuelewana.

Nataka unifundishe namna ya kutumia hizo frequency na kuziunganisha na frequency ya mtu mwingine ili kutambua mawazo yake

Na pia uniambie unaposoma mawazo yake unasoma mawazo yake moja kwa moja au unategemea ishara fulani?
 
Nataka unifundishe namna ya kutumia hizo frequency na kuziunganisha na frequency ya mtu mwingine ili kutambua mawazo yake

Sawa mkuu, kuanzia October naweza kuwa free sana.

Na pia uniambie unaposoma mawazo yake unasoma mawazo yake moja kwa moja bila kutumia moja kwa moja au unategemea ishara fulani?

Yes! Unasoma mawazo yake directly pasipo kufuatia ishara yoyote. Kwasababu mara nyingi mtu anapowaza huwa anatulia hivyo utasoma mawazo yake kupitia ufahamu wake.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom