Je, kuna watu wanaoweza kusoma mawazo ya wengine? 🧠

Je, kuna watu wanaoweza kusoma mawazo ya wengine? 🧠

umenielewa kwa asilimia buku 1000%. fanya hilo zoezi kila mara na matokeo utayaona. kumbuka, akili inajifunza kutokana na marudio (repetitions). kitu cha muhimu, tawala akili yako usiruhusu akili yako ikutawale
Mwanafunzi sina kipengele
Karibu tena mkuu
Ahsante kwa ku share 🙏🙏
 
Ningekuwa karibu na wewe ningekuomba zitaje herufi kuanzia A-Z na baada ya kutaja hizo herufi nngekutajia jina lako halisi.

Kwa njia ya maandishi humu ni ngumu kujua jina lako halisi ila naweza kuhisi katika jina lako kuna herufi "S" japokuwa sina uhakika sana, pia yamkini una rangi ya chocolate.... maana njia ya maandishi kumsoma mtu ni ngumu kwangu kuliko nikiwa nae live kutokana na mbinu za kisaikolojia nazotumia.

Nilishafungua simu ya rafiki yangu mara mbili pasipo yeye kunitajia password nilimwambia tu tucheze mchezo wa kuhesabu 1-10 huku nikimuangalia kwa umakini baadhi ya vitu kuanzia tone ya sauti, movement za vidole, body movements, blink nk...

alivyomaliza kuhesabu nikachukua simu yake nikafungua password akabaki anashangaa.
 
Ningekuwa karibu na wewe ningekuomba zitaje herufi kuanzia A-Z na baada ya kutaja hizo herufi nngekutajia jina lako halisi.

Kwa njia ya maandishi humu ni ngumu kujua jina lako halisi ila naweza kuhisi katika jina lako kuna herufi "S" japokuwa sina uhakika sana, pia yamkini una rangi ya chocolate.... maana njia ya maandishi kumsoma mtu ni ngumu kwangu kuliko nikiwa nae live kutokana na mbinu za kisaikolojia nazotumia.

Nilishafungua simu ya rafiki yangu mara mbili pasipo yeye kunitajia password nilimwambia tu tucheze mchezo wa kuhesabu 1-10 huku nikimuangalia kwa umakini baadhi ya vitu kuanzia tone ya sauti, movement za vidole, body movements, blink nk...

alivyomaliza kuhesabu nikachukua simu yake nikafungua password akabaki anashangaa.
Ohoooo sawa mkuu
Hongera kwa ujuzi wa mambo

Ni vile hatuwezi kuonana live ningesadiki maneno yako
 
Nauliza swali njee ya mada kuna baadhi ya watu wanakuwa na pupa am too emotional pindi anakutana na watu haswa wale anaowapenda unakuta utulivu unapunguwa ni mtu anacheka na kutabasamu hili mwalimu namba ufafanuzi
 
KARIBU KWENYE MADA WANA GREAT THINKERS 🧠 ☕️

Unaweza vipi kusoma mawazo ya mtu mwingine au kujua kinachoendelea kwenye akili yake?

Unaamini kama kuna watu wanaoweza kusoma akili au mawazo ya watu wengine?

Unadhani ni nini huwa kinatokea pale mtu anapoona maandishi ya mtu au akiwa kwenye mazungumzo na mtu mwingine, halafu akagundua kwamba huyu mtu anawaza kitu fulani?

Na ajabu, unakuta baadae yule mtu anafanya kitendo au vitendo vinavyothibitisha kwamba yale aliyogundua mwanzo yalikuwa sahihi


Kisayansi hali hii inaelewekaje?

Hawa watu tunaweza kuwaita watambuzi.watu wenye intuition kubwa wenye uwezo mkubwa wa kuchanganua watu, au ni geniuses?

Na wewe binafsi unaamini unaweza kusoma akili ya mtu?

Kama ndiyo unafanya hivyo kwa namna gani?

Maoni yangu 👇

Kikawaida kabisa, naamini kuna watu wenye uwezo mkubwa sana wa kutambua mambo hata bila mtu kuyaeleza moja kwa moja

Sio kwamba wanatumia akili ya ajabu au wanaingia kwenye akili ya mtu mwingine bali kuna wakati mtu akiwa makini sana anaweza kuona signals ndogo ndogo ambazo watu wengine hawazioni

Hata kama mtu anajaribu kufake au kuficha mawazo yake kwa kuongea au kuandika kitu tofauti na anachohisi, ukiwa makini sana unaweza kugundua kuna kitu hakipo sawa

Ni sawa na mtu ambaye anaweza kukuonyesha kwamba amefurahi sana kwa sababu umepata kazi

Anaweza kucheka kukusifia na kukuambia:

Hongera sana ShesRise_1 nimefurahi kwa ajili yako umepata kazi

Lakini wakati huo huo kuna signals nyingine unaweza kuziona

Labda kwenye facial expression yake namna anavyocheka tone la sauti macho, movements za mikono, posture yake au hata namna anavyoendelea na mazungumzo
Unaona kabisa yeye wa ndani
Na yeye wa njee ni kama mifumo haisomani

Na kama wewe ni mtu ambaye una observation nzuri na ubongo wako unafanya kazi shap utagundua haraka sana

Huyu mtu kwa ndani hafurahii kama anavyosema

So patterns ukiziona unagundua huyu anawaza kwa namna nyingine kabisa tofauti na anachokionesha

Na kinachofanya jambo hili liwe interesting zaidi ni pale unapokuja kugundua kwamba baadae yule mtu anafanya kitu kinachothibitisha kile ulichohisi mwanzo

Swali la mjadala?👇

Hua najiuliza nimeisoma akili yake, au nilikuwa nimeisoma signals zake vizuri na kwa haraka?

Na kama kweli kuna watu wenye uwezo huu mkubwa wa kutambua kile ambacho wengine wanajaribu kuficha...

Uwezo huu unatokana na nini?

Ni intuition?
Ni experience?

Au kuna kitu kingine ambacho bado Labda wengi wetu hatujakifahamu kwa undani
Na kama kipo je ni kitu gani?

Nataka kusikia mawazo yenu🧠

Cc: Marcostilone

ShesRise_1 ✋️
nishawai kukutana na mtu anaweza kusoma mawazo ya mtu mwingine hata km unafikiria ndani kwa ndani bila ya kutoa sauti,nnakumbuka ilikuaa posta mpya nilikua nnaenda kukutana na mtu nimkabidhi hela, nilikua nna pesa ndani ya bag nikawa nnatembea kwa wasiwasi wa kuibiwa nikaenda kusimama kwenye kituo cha basi cha mwenge kile kinatizamana na crdb pale posta mpya, pale niliposimama akaja kusimama jamaa wa makamo, kimoyo moyo nikawa nnasema huyu asije akawa mwizi akapora bag langu la hela cha ajabu akaniuliza tu kwanini unaniita mimi mwizi? asee nikabaki nimeduwaa nikaondoka chap nikajua uyu sio binadamu wa kawaida.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom