Je, kuna watu wanaoweza kusoma mawazo ya wengine? 🧠

Je, kuna watu wanaoweza kusoma mawazo ya wengine? 🧠

Potezea huyo boya kaenda kwenye uzi wa kazi mbalimbali kapigwa KO kaja tena huku. Mpotezee achana naye akili zake hazina akili
Unajua unaongelea nini? 😂 Mbona unakuwa unajistukia kama ngedere mkuu?
 
Shukran mkuu asante kwa maoni mjarabu

Hapo kwa wanyama imekaaje
Maana unaweza ukawa unatembea
Ukakutana labda na paka asikimbie akasimama anakukazia macho hii imewahi kunikuta mara nyingi
Lugha mama ni mitetemo hii hatujifunzi, tunazaliwa nayo ipo kwa viumbe vyote hivyo kwa wanyama hii ndo tunatumia kuwasiliana nao.
Paka kukukazia macho kwa experience yangu ni kitendo cha kuku scan mara nyingi ni kuwa ameona kitu interest kwako, kitendo atachofanya baada ya hapo ndo litakuwa jibu sahihi kwanini alikukazia macho.

Mara nyingine ikikutokea hali kama hiyo jaribu kuonesha nia ya urafiki kwa hisia (usifanye kitendo chochote cha nje ila kuwa tu relaxed). Hapa nashindwa namna nzuri ya kuelezea lakini kwa lugha rahisi ni kuwa uwe mtulivu na makini ukimuangalia bila kuwa na hisia zozote negative kwake, ukiweza ku master hizo hisia subconsciously hakika utaona reaction fulani ya huyo paka kwako kama absolute signal kabisa ya mawasiliano kati yako na yeye. Na kinyume chake ukionesha hisia za uadui hata kabla hujamsogelea yeye tayari atakuwa anawaza kama wewe unavyomuwazia.
 
KARIBU KWENYE MADA WANA GREAT THINKERS 🧠 ☕️

Unaweza vipi kusoma mawazo ya mtu mwingine au kujua kinachoendelea kwenye akili yake?

Unaamini kama kuna watu wanaoweza kusoma akili au mawazo ya watu wengine?

Unadhani ni nini huwa kinatokea pale mtu anapoona maandishi ya mtu au akiwa kwenye mazungumzo na mtu mwingine, halafu akagundua kwamba huyu mtu anawaza kitu fulani?

Na ajabu, unakuta baadae yule mtu anafanya kitendo au vitendo vinavyothibitisha kwamba yale aliyogundua mwanzo yalikuwa sahihi

Kisayansi hali hii inaelewekaje?

Hawa watu tunaweza kuwaita watambuzi.watu wenye intuition kubwa wenye uwezo mkubwa wa kuchanganua watu, au ni geniuses?

Na wewe binafsi unaamini unaweza kusoma akili ya mtu?

Kama ndiyo unafanya hivyo kwa namna gani?

Maoni yangu 👇

Kikawaida kabisa, naamini kuna watu wenye uwezo mkubwa sana wa kutambua mambo hata bila mtu kuyaeleza moja kwa moja

Sio kwamba wanatumia akili ya ajabu au wanaingia kwenye akili ya mtu mwingine bali kuna wakati mtu akiwa makini sana anaweza kuona signals ndogo ndogo ambazo watu wengine hawazioni

Hata kama mtu anajaribu kufake au kuficha mawazo yake kwa kuongea au kuandika kitu tofauti na anachohisi, ukiwa makini sana unaweza kugundua kuna kitu hakipo sawa

Ni sawa na mtu ambaye anaweza kukuonyesha kwamba amefurahi sana kwa sababu umepata kazi

Anaweza kucheka kukusifia na kukuambia:

Hongera sana ShesRise_1 nimefurahi kwa ajili yako umepata kazi

Lakini wakati huo huo kuna signals nyingine unaweza kuziona

Labda kwenye facial expression yake namna anavyocheka tone la sauti macho, movements za mikono, posture yake au hata namna anavyoendelea na mazungumzo
Unaona kabisa yeye wa ndani
Na yeye wa njee ni kama mifumo haisomani

Na kama wewe ni mtu ambaye una observation nzuri na ubongo wako unafanya kazi shap utagundua haraka sana

Huyu mtu kwa ndani hafurahii kama anavyosema

So patterns ukiziona unagundua huyu anawaza kwa namna nyingine kabisa tofauti na anachokionesha

Na kinachofanya jambo hili liwe interesting zaidi ni pale unapokuja kugundua kwamba baadae yule mtu anafanya kitu kinachothibitisha kile ulichohisi mwanzo

Swali la mjadala?👇

Hua najiuliza nimeisoma akili yake, au nilikuwa nimeisoma signals zake vizuri na kwa haraka?

Na kama kweli kuna watu wenye uwezo huu mkubwa wa kutambua kile ambacho wengine wanajaribu kuficha...

Uwezo huu unatokana na nini?

Ni intuition?
Ni experience?

Au kuna kitu kingine ambacho bado Labda wengi wetu hatujakifahamu kwa undani
Na kama kipo je ni kitu gani?

Nataka kusikia mawazo yenu🧠

Cc: Marcostilone

ShesRise_1 ✋️
Mimi nasoma hadi mawazo ya kuku
 
Lugha mama ni mitetemo hii hatujifunzi, tunazaliwa nayo ipo kwa viumbe vyote hivyo kwa wanyama hii ndo tunatumia kuwasiliana nao.
Paka kukukazia macho kwa experience yangu ni kitendo cha kuku scan mara nyingi ni kuwa ameona kitu interest kwako, kitendo atachofanya baada ya hapo ndo litakuwa jibu sahihi kwanini alikukazia macho.

Mara nyingine ikikutokea hali kama hiyo jaribu kuonesha nia ya urafiki kwa hisia (usifanye kitendo chochote cha nje ila kuwa tu relaxed). Hapa nashindwa namna nzuri ya kuelezea lakini kwa lugha rahisi ni kuwa uwe mtulivu na makini ukimuangalia bila kuwa na hisia zozote negative kwake, ukiweza ku master hizo hisia subconsciously hakika utaona reaction fulani ya huyo paka kwako kama absolute signal kabisa ya mawasiliano kati yako na yeye. Na kinyume chake ukionesha hisia za uadui hata kabla hujamsogelea yeye tayari atakuwa anawaza kama wewe unavyomuwazia.
Shukran sana mkuu nimekuelewa sana 🫡
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom