Uzi wa mawazo ya usiku

Uzi wa mawazo ya usiku

life255

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2026
Posts
587
Reaction score
1,470
USIKU HUU NIMEKAA KIMYA, LAKINI NDANI NINA KELELE NYINGI SANA.

Sina mzuka wa kitu chochote leo. Hata jambo la kawaida kabisa kama kupata chakula cha usiku limekuwa jambo kubwa kwangu. Nimekaa tu nikitazama maisha, nikijiuliza nimefika hapa kwa sababu gani na kesho nitainukaje.

Kuna muda mtu anachoka kuelezea matatizo yake. Unaamua kukaa kimya, lakini mawazo ndiyo yanazidi kupiga kelele. Unawaza familia, maisha, pesa, kesho, makosa uliyowahi kufanya na mambo ambayo ungependa kuyabadilisha lakini huna uwezo nayo kwa sasa.

Watu wakikuona unaweza kuonekana uko sawa, lakini ndani unakuwa unapambana vita ambavyo hakuna anayeviona.

Usiku kama huu ndipo mawazo yanakuwa mengi zaidi. Unajiuliza, “Nitaendelea hivi mpaka lini?” Unataka kubadilika, unataka kusimama, unataka kuwa mtu mwingine kabisa… lakini mazingira yanakukumbusha kila dakika kwamba bado hujafika unapotaka kufika.

Sina ombi kubwa leo. Nimeamua tu kusema ukweli wangu kama ulivyo. Kama unapitia kipindi kama hiki, ujue hauko peke yako.

Mungu atupe nguvu ya kuvuka haya tunayopitia. 🤲🏾

Leo ni usiku mgumu, lakini bado naamini kesho inaweza kuwa tofauti.
 
Mawazo usiku
Screenshot_2026-07-12-13-54-17-31.png
 
TAREHE: 27Septemba 2026

YAHUSU: TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI – PASSENGER SERVICE OFFICER (PSO) - 160

Ofisi ya Rasilimali Watu inapenda kuwatangazia wafanyakazi wote fursa za ajira mpya za Passenger Service Officer - PSO (160).

Mambo Muhimu ya Kuzingatia:

1. Sifa za Elimu:Kuanzia Kidato cha Nne, Kidato cha Sita, Stashahada, Shahada ya Kwanza hadi Shahada ya Uzamili.
2. Jinsi ya Kuomba:Maombi yote yanapaswa kuwasilishwa kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya Careers - Mofat Transport and Logistics.
3. Mwisho wa Maombi (Deadline):Tarehe 05 Oktoba 2026Maombi yatakayochelewa hayatapokelewa.


Ofisi ya Rasilimali Watu
Mofat Company Ltd
 
Kampuni ya usafiri ya Mofat imetangaza nafasi 360 za ajira, zikiwemo nafasi 200 za madereva wa Mabasi Yaendayo Kasi (BRT) na nafasi 160 za Maafisa wa Huduma kwa Abiria.

Kwa nafasi za udereva, waombaji wanatakiwa kuwa na elimu ya msingi, kidato cha nne au kidato cha sita, pamoja na leseni ya udereva Daraja C iliyothibitishwa na Jeshi la Polisi. Aidha, wanapaswa kuwa na cheti cha PSV kutoka VETA au NIT, cheti cha BRT kutoka NIT, na uzoefu wa angalau miaka mitatu katika udereva wa mabasi au magari ya abiria.

Kwa upande wa Maafisa wa Huduma kwa Abiria, waombaji wanatakiwa kuwa na cheti, stashahada au shahada ya kwanza katika fani husika kutoka taasisi inayotambulika. Fani zinazokubalika ni pamoja na huduma kwa wateja, usafirishaji na usimamizi wa ugavi (Transport and Logistics), utawala wa biashara, uhusiano wa umma na fani nyingine zinazohusiana.

Kampuni hiyo imeeleza kuwa tarehe ya mwisho ya kupokea maombi kwa nafasi za udereva ni Oktoba 9, 2026, na kwa maafisa wa huduma kwa abiria ni Oktoba 5, mwaka huu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom