Je, kuna watu wanaoweza kusoma mawazo ya wengine? 🧠

Je, kuna watu wanaoweza kusoma mawazo ya wengine? 🧠

Hujalazimishwa ukae huko mbona
Rudi mjini acha kulialia
Mkuu huwa unanipa dozi 😂😂😂

Sio kama napenda inanilazimu mkuu, nimefunga mwaka Sasa show zangu ni chaka to chaka, mjini napita kama naaga maiti😡😡.

Anyway I read some of your pattern, You're personality is nice.
 
KARIBU KWENYE MADA WANA GREAT THINKERS 🧠 ☕️

Unaweza vipi kusoma mawazo ya mtu mwingine au kujua kinachoendelea kwenye akili yake?

Unaamini kama kuna watu wanaoweza kusoma akili au mawazo ya watu wengine?

Unadhani ni nini huwa kinatokea pale mtu anapoona maandishi ya mtu au akiwa kwenye mazungumzo na mtu mwingine, halafu akagundua kwamba huyu mtu anawaza kitu fulani?

Na ajabu, unakuta baadae yule mtu anafanya kitendo au vitendo vinavyothibitisha kwamba yale aliyogundua mwanzo yalikuwa sahihi

Kisayansi hali hii inaelewekaje?

Hawa watu tunaweza kuwaita watambuzi.watu wenye intuition kubwa wenye uwezo mkubwa wa kuchanganua watu, au ni geniuses?

Na wewe binafsi unaamini unaweza kusoma akili ya mtu?

Kama ndiyo unafanya hivyo kwa namna gani?

Maoni yangu 👇

Kikawaida kabisa, naamini kuna watu wenye uwezo mkubwa sana wa kutambua mambo hata bila mtu kuyaeleza moja kwa moja

Sio kwamba wanatumia akili ya ajabu au wanaingia kwenye akili ya mtu mwingine bali kuna wakati mtu akiwa makini sana anaweza kuona signals ndogo ndogo ambazo watu wengine hawazioni

Hata kama mtu anajaribu kufake au kuficha mawazo yake kwa kuongea au kuandika kitu tofauti na anachohisi, ukiwa makini sana unaweza kugundua kuna kitu hakipo sawa

Ni sawa na mtu ambaye anaweza kukuonyesha kwamba amefurahi sana kwa sababu umepata kazi

Anaweza kucheka kukusifia na kukuambia:

Hongera sana ShesRise_1 nimefurahi kwa ajili yako umepata kazi

Lakini wakati huo huo kuna signals nyingine unaweza kuziona

Labda kwenye facial expression yake namna anavyocheka tone la sauti macho, movements za mikono, posture yake au hata namna anavyoendelea na mazungumzo
Unaona kabisa yeye wa ndani
Na yeye wa njee ni kama mifumo haisomani

Na kama wewe ni mtu ambaye una observation nzuri na ubongo wako unafanya kazi shap utagundua haraka sana

Huyu mtu kwa ndani hafurahii kama anavyosema

So patterns ukiziona unagundua huyu anawaza kwa namna nyingine kabisa tofauti na anachokionesha

Na kinachofanya jambo hili liwe interesting zaidi ni pale unapokuja kugundua kwamba baadae yule mtu anafanya kitu kinachothibitisha kile ulichohisi mwanzo

Swali la mjadala?👇

Hua najiuliza nimeisoma akili yake, au nilikuwa nimeisoma signals zake vizuri na kwa haraka?

Na kama kweli kuna watu wenye uwezo huu mkubwa wa kutambua kile ambacho wengine wanajaribu kuficha...

Uwezo huu unatokana na nini?

Ni intuition?
Ni experience?

Au kuna kitu kingine ambacho bado Labda wengi wetu hatujakifahamu kwa undani
Na kama kipo je ni kitu gani?

Nataka kusikia mawazo yenu🧠

Cc: Marcostilone

ShesRise_1 ✋️
kwa uelew a wangu nadhani suala la kusoma akili ya mtu (mind reading) linategemea kitu kinachoitwa "mindset". akili ya mtu hufanya kazi kutokana na frequency na frequency hubeba taarifa, sasa hizi taarifa (mawazo) hayazalishwi kwenye akili ila akili inapokea hizo taarifa kutokana na "tuning" ya akili ya mhusika. sasa ukiweza ku "tune" akili yako kwenye frequency sawa na akili ya mwingine, mawazo yake na yako yatakua kitu kimoja ila inahitaji uelewa wa kutosha kutofautisha hizi taarifa(mawazo), kitaalam inaitwa "precognition". hili ni swala tata sana kwenye saikolojia. unaweza kuelewa swala hili kwa kuangalia namna redio zinavyofanya kazi. ukiwasha redio yako bila ku "match" frequency yoyote ina maana hutapokea taarifa yoyote, ila ukiseti redio yako kwenye frequency fulani , bila shaka taarifa zote kwenye hiyo frequency utazipata bila shida.
 
Watu wenye uwezo wa kusoma mawazo ya wengine wapo kila mtu anaweza kusoma mawazo ya mtu kwa kusoma body language ya mtu
body language ni matokea na matokea yanaweza kutafsiriwa kwa namna tofauti tofauti, ndio maana kwenye body language unaweza kusoma akili ya mtu labda kwa asilimia 2 (kwa uwiano), ila ili uwe na uhakika na kile anchowaza mtu ni lazima uende kwenye "root cause" na kuweza kutambua uwanja mzima wa mawazo unaounganisha watu wote (mental field) na hapo ndipo unapoweza kupata taarifa kwa usahihi zaidi
 
kwa uelew a wangu nadhani suala la kusoma akili ya mtu (mind reading) linategemea kitu kinachoitwa "mindset". akili ya mtu hufanya kazi kutokana na frequency na frequency hubeba taarifa, sasa hizi taarifa (mawazo) hayazalishwi kwenye akili ila akili inapokea hizo taarifa kutokana na "tuning" ya akili ya mhusika. sasa ukiweza ku "tune" akili yako kwenye frequency sawa na akili ya mwingine, mawazo yake na yako yatakua kitu kimoja ila inahitaji uelewa wa kutosha kutofautisha hizi taarifa(mawazo), kitaalam inaitwa "precognition". hili ni swala tata sana kwenye saikolojia. unaweza kuelewa swala hili kwa kuangalia namna redio zinavyofanya kazi. ukiwasha redio yako bila ku "match" frequency yoyote ina maana hutapokea taarifa yoyote, ila ukiseti redio yako kwenye frequency fulani , bila shaka taarifa zote kwenye hiyo frequency utazipata bila shida.
Naweza vipi kuunga frequency yangu na ya mtu mwingine
Kwa namna gani?
Inabidi tuwe kwenye hali gani mimi pamoja na huyo mtu ninaetaka kujiunganisha nae?

Naomba ufafanuzi mkuu🙏
 
Naweza vipi kuunga frequency yangu na ya mtu mwingine
Kwa namna gani?
Inabidi tuwe kwenye hali gani mimi pamoja na huyo mtu ninaetaka kujiunganisha nae?

Naomba ufafanuzi mkuu🙏
frequency kwenye saikolojia ni "totallity of the psyche" (ngumu kumeza kidogo, ila usiliteme), mtu akiwa na huzuni kwa mfano, huyu mtu yupo kwenye specific condition, anakuwa kama kituo cha mawasiliano, sasa wewe unatakiwa kuwa katika hali kama hiyo ( mara nyingi hii hutokea automatically) kwa maana ya ku "match" hali yake ya ndani. kiufupi yeye anakua "broadcasting station" wewe unakua "tuner" au "reciever". sasa utashindwa kumwelewa huyu mtu kwa ufanisi kama akili yako iki "warnder" kwenye condition zingine. (nashindwa kuyaweka haya maelezo kwa njia itakayoeleweka vyema). kiufupi hali yako ya ufahamu haitakiwi kubadilika na kuwa tofauti na hali iliyopo kwa wakati huo. yaani "attention" inatakiwa iwe kwenye huyo mtu na usiwe na wazo lolote linalokinzana ndani ya akili yako. kwa mfano ukiwa unazungumza na mtu, usiruhusu wazo lingine kuingia akilini. (hili linaitaji zoezi la kudhibiti mawazo yako)
 
Mbona wapo ? Na sio sayansi. Mzungu ndio anakuambia sayansi kumbe SIO. Tunatakiwa kufunguka akil waafrika.
Hii Mada ni ndefu kuielezea, na Mimi nmechoka kutype leo ila wapo na uwezo huo sio sayansi.
 
Mbona wapo ? Na sio sayansi. Mzungu ndio anakuambia sayansi kumbe SIO. Tunatakiwa kufunguka akil waafrika.
Hii Mada ni ndefu kuielezea, na Mimi nmechoka kutype leo ila wapo na uwezo huo sio sayansi.
ni kweli sio sayansi ila inaweza kuelezwa tu kwa mtazamo wa kisayansi
 
Nimekuelewa kwamba ukitaka kusoma akili ya mtu na anachokiwaza
Lazima u copy hali yake ya muda huo ili uweze kuhisi kile anachohisi

Inakulazimu kuunga frequency yako na yake ili signal isome na kupata taarifa pacha kati yangu na yeye

Kama nimeelewa niambie kuna sehemu sijaelewa niambie pia 🙏
 
Mbona wapo ? Na sio sayansi. Mzungu ndio anakuambia sayansi kumbe SIO. Tunatakiwa kufunguka akil waafrika.
Hii Mada ni ndefu kuielezea, na Mimi nmechoka kutype leo ila wapo na uwezo huo sio sayansi.
Kama huwezi kueelezea
Hii comment yako inakosa mantiki

Hakikisha ukiunga mkono hoja au
Ukipinga hoja isiwe ni juu juu

Weka bayana kile unachokifahamu ili watu wajifunze na wapate faida

Karibu ndani ya mada utuambie hiyo namna nyingine tofauti na sayansi ya mzungu mimi binafsi nipo hapa kupata experience mpya
 
Nimekuelewa kwamba ukitaka kusoma akili ya mtu na anachokiwaza
Lazima u copy hali yake ya muda huo ili uweze kuhisi kile anachohisi

Inakulazimu kuunga frequency yako na yake ili signal isome na kupata taarifa pacha kati yangu na yeye

Kama nimeelewa niambie kuna sehemu sijaelewa niambie pia 🙏
umenielewa kwa asilimia buku 1000%. fanya hilo zoezi kila mara na matokeo utayaona. kumbuka, akili inajifunza kutokana na marudio (repetitions). kitu cha muhimu, tawala akili yako usiruhusu akili yako ikutawale
 
Back
Top Bottom