Je, kuna Mungu? Kwanini aruhusu mateso makali duniani?

Je, kuna Mungu? Kwanini aruhusu mateso makali duniani?

Hata kama hataki tumuone basi tuone hata ishara au dalili za Uwepo wake, zaidi ya maneno maneno ya bure bure kutoka kwa wahanga wa matatizo ya kidunia
kuna wana wa israel walikuwa kama nyie mm nawapa njia ya kumuona M-ngu kuwa safi kiroho mpaka kimwili atakuja kwako
 
Hata kama hataki tumuone basi tuone hata ishara au dalili za Uwepo wake, zaidi ya maneno maneno ya bure bure kutoka kwa wahanga wa matatizo ya kidunia
Ishara na dalili za uwepo wake ziko nyingi na ziko wazi sana.

Ushawahi kujiuliza katika umbile lako, kwanini jasho lina chumvi chumvi, au ute wa sikioni ni mchungu na mate ni kama hayana ladha ?

Angalia uwepo wa ulimwengu na vilivyomo, jinsi vilivyo pangwa na kupangika ? Hamtumii akili na moyo kufikiri ?

Uwepo wako kama ni mwenye kufikiria vizuri unaona wazi au ni ishara ya wazi kabisa ya kuwa Mola muumba yupo.
 
Sio kwamba natafuta sifa au nataka kubishana na mtu kuhusu imani. Lakini nikitazama yanayoendelea duniani vita, mauaji, watoto wanaoteseka, njaa, magonjwa na watu wasio na hatia kupoteza maisha naanza kujiuliza kwa dhati kama Mungu yupo na ana uwezo wote, kwa nini anaruhusu mateso haya yaendelee?

Huenda kuna majibu ambayo mimi siyajui. Lakini kwa sasa, swali hili limenifanya nianze kujiuliza kwa kina kuhusu uwepo wa Mungu.

Ningependa kusikia mawazo yenu Je, wewe unaamini Mungu yupo? Na kama ndiyo, unaelezaje uwepo wa mateso makubwa duniani?

NB: Bado nipo kwenye majonzi ya kumpoteza rafiki yangu, aliyeteseka kwa ugonjwa wa sickle cell. Na aliyeishi maisha ya maumivu mpaka kuondoka kwake. Kijana mdogo miaka 23.
Kwanini wengi hutafuta ithibati ya uwepo wa mungu kwa kutazama uwepo wa mateso na karaha mbalimbali tu na sio starehe na mambo yafurahishayo?

Hicho kitendo cha kuchukia na kuyakataa mateso manaake akili yako ipo vizuri, sasa badala ya kuanza kuuliza kwanini Mungu, basi zama deep kwenye akili yako uone namna gani unaweza kuzuia hayo.

Manaake kama akili imeona tatizo basi tatizo hilo hutatulika akili ikitulia.

Hicho kitendo cha kuwa na fikra au sensor ya matatizo tayari huo ni moja ya uwezo/uwezekano wa kuondoa hayo mateso.

Kwahiyo badala ya kusubiri Mungu akupikie ugali uondoe njaa au akuletee chakula, basi jua duniani zimewekwa nyenzo zote anazohitaji mtu ili njaa iishe.
 
Huyo Mungu angekuwepo, shida na misala visingekuwepo.

Mungu huyo ange epusha vyote.

Mungu huyo hayupo, Ndio maana Duniani kuna shida na misala ya kila aina.

Na HAKUNA YEYOTE wa kuepusha CHOCHOTE.
Sasa angeepusha vipi wakati yeye ndio ametaka viwe na vitokee na kama angeamua visiwe visinge kuwa.

Shida hutoi hoja za uhalisia zaidi ya falsafa ya kama mara ingekuwa mara vile.

Yaani unaleta Falsafa katika uhalisia.
 
Physical laws za ulimwengu ni matokeo ya big bang na galaxies kujiunda kwa mabilioni ya miaka.
Mkuu umeruka madarasa mengi sana ya physics, physical laws sio matokeo ya Big Bang. Big Bang ndio matokeo ya sheria za physics zilizokuwepo from planck epoch! Ili mlipuko wowote utokee na vitu vitawanyike, lazima sheria za gavity), strong and weak nuclear forces na thermodynamics ziwepo tayari.

Huwezi kuwa na mechi ya mpira kabla ya sheria za mpira kuwepo! Shule bado inakusumbua kaka.
 
Ushawahi kujiuliza katika umbile lako, kwanini jasho lina chumvi chumvi, au ute wa sikioni ni mchungu na mate ni kama hayana ladha ?
Kwa hiyo wewe ukiona Mawe yamejipanga moja juu ya kingine tayari unajua Mungu huyo Yupo hapo?
 
Mimi wala siamini.

Siamini kwenye kuamini.

Sina imani ya aina yoyote ile.

Kuna tofauti kati ya "kuamini" na "kujua".

Kuamini unaweza kuamini hata uongo.

Mimi sihitaji kuamini nahitaji kujua kwa uhakika, ukweli, ushahidi na uthibitisho.
Wewe unajua au unaamini ya kuwa imekwaje Ulimwengu ukawepo ?

Shids tamko Imani mnalichukulia katika muono finyu wa kustaajabisha. Imani kuna wakati hutanguliwa na kujua yaani kuwa na elimu ya yakini kabisa isiyo kuwa na shaka.

Sasa wewe mbona unashindwa kutupa ushahidi na uthibitisho ya kuwa Mungu hayupo, zaidi ya kucheza na maneno na falsafa.
 
The divine fallacy also known as the argument from incredulity—is a logical error. It happens when someone claims that a hard-to-understand event must be the work of God or magic simply because they cannot find another explanation.
Msingi wa logic ni nini, mpaka kwako iwe marejeo ?
 
Mimi nataka ukweli wenye logical consistency.

Sitaki imani zenye logical contradictions.

Kwanza una elewa maana ya logical consistency?

Ukweli hautakiwi kuwa na contradiction ya aia yoyote.

Nataka ukweli wenye logical consistency.

Una elewa maana ya logical consistency?
Unajua sababu ambazo huwa zinafanya Contradictions ziwepo ?

Sio kila jambo lina Contradictions, mfano la hili la uwepo wa Mungu. Bali ni ujinga wenu na matamanio yenu ya nafsi, ndio maaa si ajabu kuwaona mnabisha jambo na hamna hoja wala ithibati.
 
Ukisema Evolution, mbona inashindwa kueleza kwa nini binadamu ana sifa zinazozidi mahitaji ya kibaolojia ya kuishi tu?
Evolution inaelezea vizuri sana jinsi gani ubongo wa binadamu ulivyojiunda kwa zaidi ya miaka milioni 6 na jinsi gani ugunduzi wa moto wa kuwashwa na binadamu miaka 300,000 iliyopita ulivyochochea mabadiliko ya ubongo wake na mambo mengine yanayohitaji akili.

Hata hivyo haya ni mambo ambayo huwezi kuyaelewa kwa sababu kulingana na hadithi za mungu wa Abraham binadamu wana miaka kama 6,000 tu tangu wawepo duniani na waliumbwa wakiwa watu waliokamilika kwa kila kitu.
 
Mbona unarudia swali lile lile neno kwa neno? Inaonekana yale maelezo niliyokupa kuhusu tofauti ya free Will na physical uutcome yamegonga ukuta kichwani kwako! Nani kakwambia Mtu B hana free will ya kukwepa? Ana free will ya kujitetea, kukimbia, au kupiga kelele. Akizidiwa nguvu na kuuawa basi, unatakiwa uelewe huko sio kukosa free ni kuzidiwa nguvu kifizikia!
Kwanza freewill haipo.

Hatuna freewill ya kuchagua kuzaliwa ama kutokuzaliwa.

Hatuna freewill ya kuchagua kuishi milele.

Huna freewill ya kurudi mwaka 1990.

Hakuna freewill.

Hakuna Mungu.
 
Hakuna kitu cha bure bure hata hii Dunia ni mali ya Mungu haikutokea tu from no where. Naamini Mungu yupo
 
Wewe sasa hauna hoja za msingi tena, kukujibu swali lako la somo la uraia, utanzania ni stakabadhi na makubaliano ya kisheria ya wanadamu.
Nataka kujua kutoka kwako. Uzalendo wako upo kutoka ndani ya nafsi yako au kwenye makaratasi. Nimeanzia mbali ili ufahamu namna ubongo wako ulivyojengwa kwenye issue ya Mungu
 
Unajua sababu ambazo huwa zinafanya Contradictions ziwepo ?

Sio kila jambo lina Contradictions, mfano la hili la uwepo wa Mungu. Bali ni ujinga wenu na matamanio yenu ya nafsi, ndio maaa si ajabu kuwaona mnabisha jambo na hamna hoja wala ithibati.
Mungu mnayedai kwamba ni muweza wa vyote, mwenye upendo na huruma kwenye Dunia iliyojaa uovu na mabaya, Huoni contradictions hapo?

Ni either Mungu huyo hana upendo, hawezi yote na hayupo ndio maana Dunia ina mabaya.

Kuwepo kwa Mungu ambaye anadaiwa ni muweza wa vyote, mwenye upendo na huruma kwenye Dunia iliyojaa uovu, kuna tengeneza contradictions.

Huoni contradictions tu?
 
Wewe sasa hauna hoja za msingi tena, kukujibu swali lako la somo la uraia, utanzania ni stakabadhi na makubaliano ya kisheria ya wanadamu.
Mungu anafundishwa kama alphabet, muda, namba, mipaka nk. Hivyo vyote vilivumbuliwa na mwanadamu ili kutengeneza jamii yenye utamaduni unaonendana.

Kwa mfano leo hii wewe unaamini kuhusu Mungu kupitia Yesu. Wapo wanaoamini kupitia mtume
 
Wewe unajua au unaamini ya kuwa imekwaje Ulimwengu ukawepo ?
Hata kama hatujui ulimwengu umekuwepo vipi, bado jibu sio Mungu.
Shids tamko Imani mnalichukulia katika muono finyu wa kustaajabisha. Imani kuna wakati hutanguliwa na kujua yaani kuwa na elimu ya yakini kabisa isiyo kuwa na shaka.

Sasa wewe mbona unashindwa kutupa ushahidi na uthibitisho ya kuwa Mungu hayupo, zaidi ya kucheza na maneno na falsafa.
Unaelewa burden of proof philosophy?
 
Evolution inaelezea vizuri sana jinsi gani ubongo wa binadamu ulivyojiunda kwa zaidi ya miaka milioni 6 na jinsi gani ugunduzi wa moto wa kuwashwa na binadamu miaka 300,000 iliyopita ulivyochochea mabadiliko ya ubongo wake na mambo mengine yanayohitaji akili.

Hata hivyo haya ni mambo ambayo huwezi kuyaelewa kwa sababu kulingana na hadithi za mungu wa Abraham binadamu wana miaka kama 6,000 tu tangu wawepo duniani na waliumbwa wakiwa watu waliokamilika kwa kila kitu.
Hahaha aisee, yani unatengeneza hoja dhaifu ya upande wa pili kisha unaishambulia! Nimeupenda huu mchezo.

Nani kakwambia kila anayeamini Mungu wa Abrahamu anaamini dunia au binadamu ana miaka 6,000 tu? Unatakiwa uelewe hiyo ni tafsiri ya kale ya kimapokeo tu ya baadhi ya vikundi.

Wasomi wote wakubwa wa kiteolojia wa sasa wa Kikristo na Kiislamu wanakubali kabisa ukweli wa kisayansi kuwa ulimwengu una miaka bilioni 13.8 na binadamu ana miaka mamilioni. Kupitia Mungu, sayansi na imani havipingani hata kidogo.
 
Back
Top Bottom