Je, kuna Mungu? Kwanini aruhusu mateso makali duniani?

Je, kuna Mungu? Kwanini aruhusu mateso makali duniani?

Kama unataka kulinganisha dini na vipimo vya muda, basi elewa hili, vipimo vya muda ) ni social constructs. Tunaweza kuamua kesho kuwa saa moja iwe na dakika 100 na maisha yakaenda. Lakini uwepo wa Mungu, maadili, na roho ya mwanadamu sio makubaliano ya kikao cha wanadamu, ni ukweli thabiti uliopo ndani ya nafsi ya kila binadamu tangu kuumbwa kwa ulimwengu.

Swali langu la mwisho kwako mtaalamu wa saa na sekunde, ukizima saa yako ya ukutani au simu yako ikazima chaji, muda utasimama au utaendelea?
Vipi kuhusu alphabet na namba? Zilitoka wapi.? Au nazo zilitoka kwa Mungu
 
Vipi kuhusu alphabet na namba? Zilitoka wapi.? Au nazo zilitoka kwa Mungu
Unarudia kosa lile lile la sekunde na masaa, wewe unachanganya alama na ukweli wenyewe, iko hivi aama za namba kama 1, 2, 3 na alfabeti A, B, C zilivumbuliwa na binadamu kama lugha ya mawasiliano.

Binadamu hajawahi kuvumbua hesabu, amegundua tu sheria za hesabu zilizowekwa na Mungu!
 
Mbona huu mfumo unautumia kila siku na huululizi maswali ya kishule? Kwenye soka , mshambuliaji huwa ana free will ya kufunga na kipa huwa ana free will ya kuokoa. Mshambuliaji akifunga, utasema free will ya kipa imeingiliwa kwa sababu amefungwa goli asilopenda?
Soka ni mchezo.

Kipa anajua kuna kufungwa na ana freewill ya kuokoa.

Mshambuliaji anajua kuna kuokoa na ana freewill ya kufunga.

Sasa kwenye mtu kuuwawa, freewill ya mtu huyu kutotaka kuuwawa inakuwa wapi?

Kwa sababu hakuna anayechagua kuuwawa. Lakini watu wana uwawa bila kuchagua, bila kuamua na bila kupenda.

Mtu A akiamua kumuua mtu B. Freewill ya "mtu B" ya kuepuka kuuwawa inakuwa wapi?
 
Fikiria hili kwa akili ya kawaida tu Mkuu, Kama kila mtu angekuwa na free will ya kiwango unachotaka wewe kwamba hakuna mtu anayeweza kukudhuru, kukuibia, au kukuua bila wewe kupenda maana yake kusingekuwa na makosa ya kimaadili duniani. Amri za Mungu kama usiue au usiibe zisingekuwa na maana, kwa sababu kusingekuwa na uwezekano wa kumuua au kumuibia mtu!

Thamani ya wema ipo kwa sababu mwanadamu ana uwezo halisi wa kuchagua kufanya ubaya na ukaleta madhara halisi kwa mwingine.
 
Unarudia kosa lile lile la sekunde na masaa, wewe unachanganya alama na ukweli wenyewe, iko hivi aama za namba kama 1, 2, 3 na alfabeti A, B, C zilivumbuliwa na binadamu kama lugha ya mawasiliano.

Binadamu hajawahi kuvumbua hesabu, amegundua tu sheria za hesabu zilizowekwa na Mungu!
Vipi kuhusu mipaka ya nchi ni nani aliiweka?
 
Fikiria hili kwa akili ya kawaida tu Mkuu, Kama kila mtu angekuwa na free will ya kiwango unachotaka wewe kwamba hakuna mtu anayeweza kukudhuru, kukuibia, au kukuua bila wewe kupenda maana yake kusingekuwa na makosa ya kimaadili duniani. Amri za Mungu kama usiue au usiibe zisingekuwa na maana, kwa sababu kusingekuwa na uwezekano wa kumuua au kumuibia mtu!

Thamani ya wema ipo kwa sababu mwanadamu ana uwezo halisi wa kuchagua kufanya ubaya na ukaleta madhara halisi kwa mwingine.
Kama mtu ana freewill ya kukuua na wewe huna freewill ya kuepuka kuuwawa, Utasemaje kila mtu ana freewill?

Kama mtu anaweza kutumia freewill yake kuua mtu mwingine, lakini huyo mtu mwingine hawezi kuepuka kuuwawa. Basi hana freewill.

Na freewill haipo.
 
Vipi kuhusu mipaka ya nchi ni nani aliiweka?
Kujibu swali lako la shule ya msingi, mipaka ya nchi kama ya Afrika iliyowekwa kwenye Berlin Conference ya mwaka 1884/1885 iliwekwa na binadamu, hivi ni vitu vya kufikirika vya kisiasa na kisheria.
 
Kujibu swali lako la shule ya msingi, mipaka ya nchi kama ya Afrika iliyowekwa kwenye Berlin Conference ya mwaka 1884/1885 iliwekwa na binadamu, hivi ni vitu vya kufikirika vya kisiasa na kisheria.
Nashukuru umenielewa. Vipi kuhusu utanzania wako mtu anaweza kukupokonya?
 
Kama mtu ana freewill ya kukuua na wewe huna freewill ya kuepuka kuuwawa, Utasemaje kila mtu ana freewill?

Kama mtu anaweza kutumia freewill yake kuua mtu mwingine, lakini huyo mtu mwingine hawezi kuepuka kuuwawa. Basi hana freewill.

Na freewill haipo.
Mbona unarudia swali lile lile neno kwa neno? Inaonekana yale maelezo niliyokupa kuhusu tofauti ya free Will na physical uutcome yamegonga ukuta kichwani kwako! Nani kakwambia Mtu B hana free will ya kukwepa? Ana free will ya kujitetea, kukimbia, au kupiga kelele. Akizidiwa nguvu na kuuawa basi, unatakiwa uelewe huko sio kukosa free ni kuzidiwa nguvu kifizikia!
 
Nashukuru umenielewa. Vipi kuhusu utanzania wako mtu anaweza kukupokonya?
Wewe sasa hauna hoja za msingi tena, kukujibu swali lako la somo la uraia, utanzania ni stakabadhi na makubaliano ya kisheria ya wanadamu.
 
Nimependa ulicho eleza, sasa hiyo changamoto ya ndani ya binadamu kutafuta maana ya maisha, haki, na Muumbaji inathibitisha nini? Kwa sababu huwezi kuwa na hamu ya kitu ambacho hakipo kabisa kwenye uhalisia.
Inathibitisha binadamu ndio mnyama mwenye ubongo mkubwa zaidi kwa uwiano wa mwili ndio maana ana lugha, ana hisia kali, anaweza kutengeneza nyenzo na machine, anawaza mambo dhahania na anajua kuna mwisho wake.
 
Utateseka sana kwa kuchanganya jinsi kitu kinavyofanya kazi na chanzo cha hicho kitu, ukieleza kuwa gari la Tesla lina kompyuta kubwa na betri zenye nguvu ndio maana linajiendesha lenyewe, hiyo inamaanisha Elon Musk hayupo au gari lilijitengeneza lenyewe?

Ni nani aliyeweka hiyo programu ya akili na utambuzi ndani ya huo ubongo?
 
Kama ungekuwa unajua kwa uhakika kabisa Mungu yupo, Swali la "Je kuna Mungu?" Lisingekuwepo.

Kwa sababu huwezi kuulizia kitu ambacho tayari unajua kipo.

Ni sawa sasa hivi uanze kuuliza, "Je Samia Suluhu Hassan ni Raisi wa Tanzania?" Wakati tayari unajua kabisa ni Raisi.
Kijana inaonekana una elimu ndogo sana kuhusu mambo ya lugha, kwenye lugha unaweza kuuliza jambo unajua kabisa lipo na matokeo yake yanajulikana.

Namna ya uulizaji huo ni kummakinisha mtu awe hadhiri na jambo husika.

Unaweza kuuliza hivi "Unajua kama usipo soma utafeli ?" Hili ni swali na hapa umeuliza.

Huu ni mfano mmoja tu katika mifano mingi.

Swali la Je kuna Mungu, lina fasiriwa au kuelezewa katika namna tofauti, na sio kila anae uliza swali hilo hajui kama Mola yupo.

Kingine uwepo wa Mungu uko wazi sana, kiasi ambacho hakuna kitu chepesi kuthibitisha kushinda uwepo wa Mungu.
 
Utateseka sana kwa kuchanganya jinsi kitu kinavyofanya kazi na chanzo cha hicho kitu, ukieleza kuwa gari la Tesla lina kompyuta kubwa na betri zenye nguvu ndio maana linajiendesha lenyewe, hiyo inamaanisha Elon Musk hayupo au gari lilijitengeneza lenyewe?

Ni nani aliyeweka hiyo programu ya akili na utambuzi ndani ya huo ubongo?
EVOLUTION
 
Sasa na kwa Mungu ni hivyo hivyo, Huyo Mungu angekuwepo kweli, Wala kusingehitajika kuulizia uwepo wake.

Kwa sababu tayari kila mtu angejua Mungu huyo yupo kwa uhakika kabisa bila hata kuamini na kuuliza.
Tatizo maswali yenu mnayajenga kwenye dhana na majibu mepesi ambayo muhusika hujafikiria uhalisia wa unachokiuliza.

Matumizi ya "..nge.." kwa maana ya "Angekuwepo ..." au kadha wa kadha ni dhana ambayo haina uhalisia.

Kusingehitajia vipi ? Umejuaje kama asingekuwepo kungekuwa na maswali haya ?

Hapa ndio kuna tatizo upande wenu.
 
Kwa nini mnahangaika kumtetea na kumuelezea huyo Mungu?

Kama yupo, Si ajitokeze mwenyewe ajidhihirishe na kujitetea, kama ana huo uwezo?

Kwa nini nyie muongee kwa niaba yake?

Kama yupo, AJE na AJITOKEZE Yeye mwenyewe.

Sio nyie mnahangaika kumtetea na kumuelezea.
Wewe kwanini unahangaika kukana kituambacho hukijui ?

Mola hafanyi mambo yake kama unavyo taka wewe, ndio maana kila kitu kinaenda kama alivyo panga yeye, sababu yeye ni mwenye nguvu mwenye kujua.

Tunaongea kwa niaba yake sababu yeye ametaka iwe hivyo, na huo ndio utaratibu wake, wala hautakuta katika taratibu za Allah ni zenye kubadilika.

Haji kwa kutaka wewe na hili halibadilishi juu ya uwepo wake.
 
Sio kwamba natafuta sifa au nataka kubishana na mtu kuhusu imani. Lakini nikitazama yanayoendelea duniani vita, mauaji, watoto wanaoteseka, njaa, magonjwa na watu wasio na hatia kupoteza maisha naanza kujiuliza kwa dhati kama Mungu yupo na ana uwezo wote, kwa nini anaruhusu mateso haya yaendelee?

Huenda kuna majibu ambayo mimi siyajui. Lakini kwa sasa, swali hili limenifanya nianze kujiuliza kwa kina kuhusu uwepo wa Mungu.

Ningependa kusikia mawazo yenu Je, wewe unaamini Mungu yupo? Na kama ndiyo, unaelezaje uwepo wa mateso makubwa duniani?

NB: Bado nipo kwenye majonzi ya kumpoteza rafiki yangu, aliyeteseka kwa ugonjwa wa sickle cell. Na aliyeishi maisha ya maumivu mpaka kuondoka kwake. Kijana mdogo miaka 23.
"Haikuwa hivyo tangu mwanzo, bali kwa ugumu wa mioyo yenu"

Mateso mengi si kwa sababu ya Mungu, ila kwa hila na ujanjaujanja wa wanadamu wenyewe. Mateso yalianza tangu mwanadamu alipoanza kukiuka maagizo.

Hata sahivi utakuwa shuhuda kwamba sio Mungu anayekutesa, labda unateseka kwa njia zako mwenyewe au kwa sababu ya watu wanaokuzunguka. Right?

Mtu anaambiwa husivute sigara, shisha, au pombe kali. Anajikuta mwamba. Akipata matatizo anamuona Mungu hafai.

Mtu anaambiwa acha umalaya,, akiibuka na kaswende, kisonono, au HIV anasema Mungu hafai.
 
Binadamu hajawahi kuvumbua hesabu, amegundua tu sheria za hesabu zilizowekwa na Mungu!
Physical laws za ulimwengu ni matokeo ya big bang na galaxies kujiunda kwa mabilioni ya miaka.
 
Back
Top Bottom