Je, kuna Mungu? Kwanini aruhusu mateso makali duniani?

Kama cosmological argument inafosi, hebu nipe basi hoja yako mbadala ya jinsi ulimwengu ulivyofika hapa tulipo?
Historia ya ulimwengu ina eleza vizuri ni namna tumefika hapa tulipo.

Kama kila kitu kilichopo kitahitaji kuwa na MUANZILISHI hata muanzilishi wa kila kitu atahitaji kuwa na muanzilishi wake mwingine.

Pasiwepo kitu chochote kile kilicho EXIST chenyewe tu pasipo muanzilishi.

Hivyo kutakuwa na msururu mrefu usio na mwisho wa waumbaji wengi. Pasipo kukoma.
ulimwengu ulijiumba wenyewe bila sababu?
Na huyo Mungu alijiumba mwenyewe bila sababu?

Kwa nini unataka ulimwengu uwe uliumbwa?

Halafu unakubali tu, Huyo Mungu hakuumbwa?

Kama huyo Mungu unakubali aliexist mwenyewe tu bila sababu, Hata ulimwengu ume exist wenyewe tu, na hauhitaji sababu.

Lakini kama ulimwengu utahitaji sababu ya ku- exist kwake, Hata huyo Mungu atahitaji sababu ya ku-exist kwake.
au ulimwengu umekuwepo tangu milele kitu ambacho thermodynamics imeshathibitisha sio kweli? Ukikataa jibu lenye mantiki, inabidi ulete jibu bora zaidi, sio unalialia tu kwamba tunafosi.
Ikiwa mifumo tata inahitaji muumbaji, basi muumbaji naye anahitaji muumbaji aliye tata zaidi.

Hilo linapelekea msururu mrefu usio na mwisho wa waumbaji, ambapo kila mmoja anakuwa tata zaidi kuliko aliyemtangulia.

If complex systems require a creator then creator requires a more complex creator that imply an infinite chain of creators that get more and more complex.

Tatizo lenu nyie mnataka kufosi huyo Mungu wenu hana chanzo, halafu hapohapo unalazimisha ulimwengu uwe na chanzo.
 
Historia ya ulimwengu ina eleza vizuri ni namna tumefika hapa tulipo.

Kama kila kitu kilichopo kitahitaji kuwa na MUANZILISHI hata muanzilishi wa kila kitu atahitaji kuwa na muanzilishi wake mwingine.

Pasiwepo kitu chochote kile kilicho EXIST chenyewe tu pasipo muanzilishi.

Hivyo kutakuwa na msururu mrefu usio na mwisho wa waumbaji wengi. Pasipo kukoma.
Kama unadai pasiwepo kitu chochote kilicho exist chenyewe tu pasipo muanzilishi, basi niambie hiyo sheria yako unayoitumia sasa hivi ilianzia wapi? Kama kila kitu kina mwanzo bila kikomo, maana yake hakuna ukweli thabiti duniani. Kukubali uwepo wa uncaused first cause ndio suluhisho pekee la kiakili linalofanya ulimwengu na sayansi yako viwe na maana. Vinginevyo, unaamini ulimwengu umetokea from nothing jambo ambalo hata mtoto wa chekechea anajua haiwezekani!
Na huyo Mungu alijiumba mwenyewe bila sababu?

Kwa nini unataka ulimwengu uwe uliumbwa?

Halafu unakubali tu, Huyo Mungu hakuumbwa?

Kama huyo Mungu unakubali aliexist mwenyewe tu bila sababu, Hata ulimwengu ume exist wenyewe tu, na hauhitaji sababu.

Lakini kama ulimwengu utahitaji sababu ya ku- exist kwake, Hata huyo Mungu atahitaji sababu ya ku-exist kwake.
Nani kasema Mungu alijiumba mwenyewe? Kujiumba mwenyewe ni logically impossible, kwa sababu ili ujiumbe lazima uwe ulikuwepo kabla ya kuwepo kwako! Sisi hatusemi Mungu alijiumba,tunasema Mungu hajawahi kutokuwepo. Yeye ni wa milele. Yeye ndio asili ya nishati, muda, na nafasi. Kama kitu kiko nje ya mfumo wa muda neno mwanzo au kujiumba halina maana kwake!
Ikiwa mifumo tata inahitaji muumbaji, basi muumbaji naye anahitaji muumbaji aliye tata zaidi.

Hilo linapelekea msururu mrefu usio na mwisho wa waumbaji, ambapo kila mmoja anakuwa tata zaidi kuliko aliyemtangulia.

If complex systems require a creator then creator requires a more complex creator that imply an infinite chain of creators that get more and more complex.

Tatizo lenu nyie mnataka kufosi huyo Mungu wenu hana chanzo, halafu hapohapo unalazimisha ulimwengu uwe na chanzo.
We ndio unalazimisha vitu visivyo na mantiki bro. Laws of Nature, muda , na nafasi zilianza kuwepo baada ya ulimwengu kuumbwa. Mungu yuko nje ya ulimwengu na ndiye aliyezivumbua hizo sheria. Sasa iweje umtake Mungu afuate sheria za ulimwengu ulioumbwa?
 
Unataka Mungu amnyang'anye binadamu uhuru wa kuchagua? Maana thamani ya binadamu ipo kwenye uwezo wa kuchagua wema au ubaya, dhuluma ipo kwa sababu binadamu tunatumia vibaya huu uhuru wetu na tutakuja kuhukumiwa kwa hilo.
Ngoja nikupe mfano hapa.

Kuna "Mtu A" na "Mtu B"

"Mtu A" na "mtu B" wote wana freewill ya kuchagua.

Then "Mtu A" kaamua kutumia freewill yake kumuua "mtu B".

"Mtu B" kauwawa bila kuchagua, bila kutaka, bila kuamua na bila kupenda.

Freewill ya "Mtu B" itakuwa wapi ikiwa ameuliwa bila kuchagua?

Freewill ya "Mtu B" ya kuchagua kuishi badala ya kuuwawa itakuwa wapi?
 
We unataka ulimwengu ambao kila mtu anaishi kwenye ulimwengu wake peke yake ambapo hakuna mtu anayeweza kugusa maisha ya mwingine? Maisha ni mfumo wa kijamii unaotegemana. Uhuru wako wa kuchagua huwa unakuja na athari kwa wengine. Ukichagua kuendesha gari kwa kasi ukiwa umelewa na ukamgonga mtu, umemdhuru. Ubaya hautoki kwa Mungu, unatokana na wanadamu kutumia vibaya free will zao kudhuru wengine.
 
Kama unadai pasiwepo kitu chochote kilicho exist chenyewe tu pasipo muanzilishi, basi niambie hiyo sheria yako unayoitumia sasa hivi ilianzia wapi?
Ukitaka sheria hii iwe ilianzia sehemu fulani, Huoni kwamba hata hiyo sehemu itahitaji kuanzia sehemu nyingine tena?

Kutakuwa tena na msururu mrefu wa sehemu nyingi zinazoanza pasipo kukoma.

Kwa sababu kila sehemu inayoanza, itahitaji kuanzia sehemu nyingine tena. Kwa sheria zake.

Kama sheria lazima iwe ilianza, Hata huko ilipoanzia na huyo aliyeanzisha sheria hiyo, hawezi ku-exist tu pasipo kuanza. Na yeye atahitaji kuanzia sehemu nyingine tena.

Vinginevyo, Sheria hizi zimekuwepo kwenye ulimwengu ambao ndio MWANZO wenyewe.

Sheria hizi zimekuwepo kwenye ulimwengu ambao haukuanza.

Ulimwengu haujaumbwa wala hauja anza.

Hakuna wakati ambapo ulimwengu haukuwepo.

Ulimwengu umekuwepo milele.
Kama kila kitu kina mwanzo bila kikomo, maana yake hakuna ukweli thabiti duniani. Kukubali uwepo wa uncaused first cause ndio suluhisho pekee la kiakili linalofanya ulimwengu na sayansi yako viwe na maana. Vinginevyo, unaamini ulimwengu umetokea from nothing jambo ambalo hata mtoto wa chekechea anajua haiwezekani!
Hatuwezi kujua tusivyo vijua.

Tunachojua ni kwamba tuna exist kwenye ulimwengu ambao upo, unaonekana upo, una thibitishika upo na tumeukuta tayari upo.

Huyo Mungu hakuna mwenye uthibitisho kwamba yupo.

Habari za kwamba huyo Mungu ni uncaused first cause wala hazina UKWELI wala UTHIBITISHO. Kwa sababu kwanza, Huyo Mungu hajawahi kuthibitishwa kama yupo. Mnatetea kitu ambacho hata nyie wenyewe hamuwezi kuthibitisha uwepo wake.

Lakini Ulimwengu hata wewe unajua upo.

Na ulimwengu si lazima uwe ulianzishwa.

Tunaona jinsi ulimwengu unavyo jiendesha wenyewe pasipo kuongozwa na yeyote.

Na hivyo hakuna sababu ya ulimwengu kuhitaji muumbaji wake.
Nani kasema Mungu alijiumba mwenyewe? Kujiumba mwenyewe ni logically impossible, kwa sababu ili ujiumbe lazima uwe ulikuwepo kabla ya kuwepo kwako! Sisi hatusemi Mungu alijiumba,tunasema Mungu hajawahi kutokuwepo. Yeye ni wa milele. Yeye ndio asili ya nishati, muda, na nafasi. Kama kitu kiko nje ya mfumo wa muda neno mwanzo au kujiumba halina maana kwake!
Hata Ulimwengu haujawahi kutokuwepo.

Kama unabisha, Sema ni lini ulimwengu haukuwepo?

Ulimwengu umekuwepo milele.

Hauja anzishwa na YEYOTE yuleee!!
We ndio unalazimisha vitu visivyo na mantiki bro. Laws of Nature, muda , na nafasi zilianza kuwepo baada ya ulimwengu kuumbwa. Mungu yuko nje ya ulimwengu na ndiye aliyezivumbua hizo sheria. Sasa iweje umtake Mungu afuate sheria za ulimwengu ulioumbwa?
Ulimwengu haujaumbwa.

Binadamu na viumbe wengine wote HATUUMBWI na wala HATUKUUMBWA.

Binadamu tunazaliwa kwa kuzaliana wenyewe kwa wenyewe. Wala hatuumbwi na hatukuumbwa na huyo Mungu.

Vivyo hivyo, Viumbe wengine wote hawakuumbwa na wala hawaumbwi.

Viumbe VINAZALIANA vyenyewe kwa vyenyewe. Haviumbwi.

Ulimwengu haujaumbwa na yeyote.

Ulimwengu umekuwepo milele.

Hakuna Mungu.

MUNGU HAYUPO.
 
We unataka ulimwengu ambao kila mtu anaishi kwenye ulimwengu wake peke yake ambapo hakuna mtu anayeweza kugusa maisha ya mwingine? Maisha ni mfumo wa kijamii unaotegemana. Uhuru wako wa kuchagua huwa unakuja na athari kwa wengine. Ukichagua kuendesha gari kwa kasi ukiwa umelewa na ukamgonga mtu, umemdhuru. Ubaya hautoki kwa Mungu, unatokana na wanadamu kutumia vibaya free will zao kudhuru wengine.
Kama kuna freewill ya mtu kuweza kudhuru wengine, Je freewill ya mtu kuweza kuepuka kudhuriwa inakuwa wapi?

Kama kila mtu ana freewill ya kuchagua chochote atakacho na apendacho,
Kwa nini freewill za watu wengine ziingilie freewill za wengine na kuwadhuru pasipo wao kuweza kuepuka?
 
Ahsante kwa kutetea hoja yangu bila wewe mwenyewe kujua, ulicho kieleza maana yake walikuwa na chanzo cha maarifa kisicho cha kawaida. Binadamu wa kawaida wa zama zile, wasio na teknolojia, walipata wapi akili ya kiwango hicho kama hawakuongozwa na Mungu aliyetengeneza hiyo akili ya mwanadamu?
Changamoto huleta maarifa. Huwezi jifunika blanket wakati wa joto kali. Hata huyo Mungu unayemtaja alileta na changamoto za wanadamu. Wakaamua kumuumba Mungu na kumpandikiza kwenye ubongo wako. Ndio maana huwezi kufahamu au kumjua Mungu bila kukulia kwenye jamii ambazo tayari virus Mungu yupo vichwani mwao
 
Sio kwamba natafuta sifa au nataka kubishana na mtu kuhusu imani. Lakini nikitazama yanayoendelea duniani vita, mauaji, watoto wanaoteseka, njaa, magonjwa na watu wasio na hatia kupoteza maisha naanza kujiuliza kwa dhati kama Mungu yupo na ana uwezo wote, kwa nini anaruhusu mateso haya yaendelee?

Huenda kuna majibu ambayo mimi siyajui. Lakini kwa sasa, swali hili limenifanya nianze kujiuliza kwa kina kuhusu uwepo wa Mungu.

Ningependa kusikia mawazo yenu Je, wewe unaamini Mungu yupo? Na kama ndiyo, unaelezaje uwepo wa mateso makubwa duniani?

NB: Bado nipo kwenye majonzi ya kumpoteza rafiki yangu, aliyeteseka kwa ugonjwa wa sickle cell. Na aliyeishi maisha ya maumivu mpaka kuondoka kwake. Kijana mdogo miaka 23.

Maisha yapo hivyo.
Unaishi kulingana na unavyotesa wengine. Ili uishi viumbe wengine lazima wafe.

Nawe wapo viumbe wanaishi kwa kukutumia wewe na ipo siku kifo chako ni kutokana na ulaji wa kiumbe kingine
 
Sio kwamba natafuta sifa au nataka kubishana na mtu kuhusu imani. Lakini nikitazama yanayoendelea duniani vita, mauaji, watoto wanaoteseka, njaa, magonjwa na watu wasio na hatia kupoteza maisha naanza kujiuliza kwa dhati kama Mungu yupo na ana uwezo wote, kwa nini anaruhusu mateso haya yaendelee?

Huenda kuna majibu ambayo mimi siyajui. Lakini kwa sasa, swali hili limenifanya nianze kujiuliza kwa kina kuhusu uwepo wa Mungu.

Ningependa kusikia mawazo yenu Je, wewe unaamini Mungu yupo? Na kama ndiyo, unaelezaje uwepo wa mateso makubwa duniani?

NB: Bado nipo kwenye majonzi ya kumpoteza rafiki yangu, aliyeteseka kwa ugonjwa wa sickle cell. Na aliyeishi maisha ya maumivu mpaka kuondoka kwake. Kijana mdogo miaka 23.
usimsingizie Mungu kwa mateso ya binadamu.binadamu kajisababishia maumivu alipomuasi MUNGU pale edeni.
 
Kama kuna freewill ya mtu kuweza kudhuru wengine, Je freewill ya mtu kuweza kuepuka kudhuriwa inakuwa wapi?

Kama kila mtu ana freewill ya kuchagua chochote atakacho na apendacho,
Kwa nini freewill za watu wengine ziingilie freewill za wengine na kuwadhuru pasipo wao kuweza kuepuka?
Mbona huu mfumo unautumia kila siku na huululizi maswali ya kishule? Kwenye soka , mshambuliaji huwa ana free will ya kufunga na kipa huwa ana free will ya kuokoa. Mshambuliaji akifunga, utasema free will ya kipa imeingiliwa kwa sababu amefungwa goli asilopenda?
 
Changamoto huleta maarifa. Huwezi jifunika blanket wakati wa joto kali. Hata huyo Mungu unayemtaja alileta na changamoto za wanadamu. Wakaamua kumuumba Mungu na kumpandikiza kwenye ubongo wako. Ndio maana huwezi kufahamu au kumjua Mungu bila kukulia kwenye jamii ambazo tayari virus Mungu yupo vichwani mwao
Nimependa ulicho eleza, sasa hiyo changamoto ya ndani ya binadamu kutafuta maana ya maisha, haki, na Muumbaji inathibitisha nini? Kwa sababu huwezi kuwa na hamu ya kitu ambacho hakipo kabisa kwenye uhalisia.
 
Issue ya Mungu ni issue sensitive sana. Ndio maana kuna kujazana hofu huko na vitisho kibao. Lengo ni kuwafanya watu waishi tofauti na wanyama.

Ndio maana ukisoma amri za Mungu unaona kabisa zinatengeneza jamii iliyostaarabika. Kwahiyo Mungu ni issue ya akili tu kiuhalisia hayupo na hatakuwepo. Ndio maana nimesema aliumbwa na mwanadamu kwa lengo maalumu
 
Hoja yako ni kwamba binadamu alibuni Mungu wa kufikirika ili atengeneze jamii iliyostaarabika? That makes no sense!

Kwenye historia na saikolojia, huwezi kujenga mfumo thabiti na unaodumu kwa miaka maelfu juu ya msingi wa uongo na hofu ya kufikirika tu, mbona jamii zilizoamua kuacha dini na kufuata msimamo wako usioamini Mungu kama utawala wa kikomunisti wa soviet union au mao kule China ziliishia kuua mamilioni ya watu wao wenyewe kinyama?
 
Mkuu dakika ina sekunde ngapi? Vipi saa lina dkk ngapi? Siku je, ina masaa mangapi?

Unaamini kuwa muda umepangiliwa na mwanadamu ili kutusaidia kutunza kumbukumbu?
 
Kama unataka kulinganisha dini na vipimo vya muda, basi elewa hili, vipimo vya muda ) ni social constructs. Tunaweza kuamua kesho kuwa saa moja iwe na dakika 100 na maisha yakaenda. Lakini uwepo wa Mungu, maadili, na roho ya mwanadamu sio makubaliano ya kikao cha wanadamu, ni ukweli thabiti uliopo ndani ya nafsi ya kila binadamu tangu kuumbwa kwa ulimwengu.

Swali langu la mwisho kwako mtaalamu wa saa na sekunde, ukizima saa yako ya ukutani au simu yako ikazima chaji, muda utasimama au utaendelea?
 
Back
Top Bottom