Je, kuna Mungu? Kwanini aruhusu mateso makali duniani?

Je, kuna Mungu? Kwanini aruhusu mateso makali duniani?

Kwanza pole sana kuhusiana na rafiki yako.

Ndio Naamini Mungu yupo. Sisi watoto wake, wanadamu, espesheli wachaguzi wake - tumevunja matakwa na masharti yake tokea bustanini na hata baada ya ukombozi tokea utumwani Misri. Ukisoma Kumbukumbu la Torati kitabu cha 28 - utatambua matakwa na masharti yake na vile alitamka, tukiyafuata tutaishi bora, tusipoyafuata tutapelekwa utumwani tena na kuishi vibaya... hiki kitabu kwangu ni pia ushahidi waEbrania na wanaIsraeli wa ukweli ni kina nani...
Kwa nini mungu alimuumba shetani anayesababisha binadamu wavunje masharti yake??
 
Ndio maana mie huwa naona hata wenye kuona kwamba hakuna Mungu ni moja tu ya mitazamo au chaguzi zilizopo, wengi wasioamini Mungu na kusema hayupo walikuwa waumini wa dini na hata huyo Mungu wanayesema hayupo ni wa hizi dini mbili, lakini sio wote waliyoacha kuamini Mungu wa hizo dini basi alikana kabisa uwepo wa Mungu bali wapo waliyochagua kuamini Mungu tofauti na dini.
Kulingana na waamini wa dini za Abrahamic (Uislamu na Ukristo) hakuna mungu zaidi ya mungu wao mmoja. Kama humuamini huyo mungu ni sawa na huamini mungu kabisa.
 
Kulingana na waamini wa dini za Abrahamic (Uislamu na Ukristo) hakuna mungu zaidi ya mungu wao mmoja. Kama humuamini huyo mungu ni sawa na huamini mungu kabisa.
Mimi sizungumzii kulingana na imani ya ukristo na uislamu, nachozungumzia ni uamuzi wa kutokuamini kabisa Mungu kwamba ni moja ya chaguzi tu zilizopo. Wapo waliyoacha kuamini Mungu wa hizo dini na kuchagua kuamini mizimu au kuamini Mungu kwa namna tofauti na hizo dini zinavyomuelezea.

Mashambulizi mengi huelekezwa kwa Mungu wa hizo dini mbili ndiko kwenye ukosoaji hali inayowafanya waliyochagua kuamini nje ya Mungu wa hizo dini kujiona wanachoamini kiko sahihi nao huungana na wakana kabisa Mungu/miungu kukosoa Mungu wa hizo dini.
 
Sio chaguzi tu, ukisema ni uchaguzi tu ni kama vile wapiga kura ambapo leo wanaweza kuipigia kura CHADEMA na kesho wakaipigia CCM.
 
Sio chaguzi tu, ukisema ni uchaguzi tu ni kama vile wapiga kura ambapo leo wanaweza kuipigia kura CHADEMA na kesho wakaipigia CCM.
Watu walikuwa waumini wa dini fulani ya Mungu,wakaja kukana uwepo wa Mungu kabisa na mwishoni wanarudia kuamini Mungu kupitia dini nyengine ya Mungu, tunaona watu wakifanya hivyo kwahiyo ni uchaguzi tu katika machaguzi yaliyopo. Wengine wanachagua kuwa agnostic badala ya kuwa atheist.
 
Sio wajibu wa Sayansi kukanusha uwepo wa mungu ila ni wajibu wa waamini mungu kuthibitisha uwepo wake.
Waamini wanaweza kutoa hoja za kifalsafa kama;

1. Hoja ya chanzo cha ulimwengu
2. Hoja ya mpangilio/fine-tuning
3. Hoja ya maadili ya objektivu
4. Hoja kutoka kwenye uzoefu wa kidini.

Tatizo ni kwamba hoja hizo hazijafikia kiwango cha ushahidi unaokubalika kwa wote. Ndiyo maana mjadala unaendelea.

Na pia upande mwingine una mzigo mdogo zaidi mtu anayesema
“Mungu hayupo kabisa” naye anafanya dai kubwa, na akilitetea anahitaji sababu. Lakini kusema tu “sijaona ushahidi wa kutosha wa kuamini Mungu” si sawa na kusema “nimethibitisha Mungu hayupo.”
 
Kwa nini mungu alimuumba shetani anayesababisha binadamu wavunje masharti yake??
Biblia yasema aliumbwa kama Malaika mkuu, afu mbichwa ulivomkua alisaliti akitaka kuwa kama Mungu (kiongozi), alipofeli jaribio la mapinduzi, alitupwa duniani... kifungo cha nje, akingoja adhabu
 
Back
Top Bottom