Je, kuna Mungu? Kwanini aruhusu mateso makali duniani?

Je, kuna Mungu? Kwanini aruhusu mateso makali duniani?

Sun is Sun

JF-Expert Member
Joined
Mar 13, 2024
Posts
1,196
Reaction score
1,846
Sio kwamba natafuta sifa au nataka kubishana na mtu kuhusu imani. Lakini nikitazama yanayoendelea duniani vita, mauaji, watoto wanaoteseka, njaa, magonjwa na watu wasio na hatia kupoteza maisha naanza kujiuliza kwa dhati kama Mungu yupo na ana uwezo wote, kwa nini anaruhusu mateso haya yaendelee?

Huenda kuna majibu ambayo mimi siyajui. Lakini kwa sasa, swali hili limenifanya nianze kujiuliza kwa kina kuhusu uwepo wa Mungu.

Ningependa kusikia mawazo yenu Je, wewe unaamini Mungu yupo? Na kama ndiyo, unaelezaje uwepo wa mateso makubwa duniani?

NB: Bado nipo kwenye majonzi ya kumpoteza rafiki yangu, aliyeteseka kwa ugonjwa wa sickle cell. Na aliyeishi maisha ya maumivu mpaka kuondoka kwake. Kijana mdogo miaka 23.
 
NB: Bado nipo kwenye majonzi ya kumpoteza rafiki yangu, aliyeteseka kwa ugonjwa wa sickle cell. Na aliyeishi maisha ya maumivu mpaka kuondoka kwake. Kijana mdogo miaka 23.
Pole sana mkuu

Kuhusu Mungu.. Inabidi uishi kwa faith. Mungu si kitu wala mtu.. Mungu ana encompasate kila unacho kiona, kuhisi na kufikiri..

Ndiye muweza wa yote kama maandiko ya navyo sema.

Amini unacho amini lakini jua yupo na ndiye aliyesababisha wewe uwepo.

Ukifanya haya hautateseka sana..

Tatizo sio yeye, tatizo ni swali kuhusu uwepo wake.
 
Ukifanya haya hautateseka sana..😅😅😅😅😅
 
Back
Top Bottom