Je, kuna Mungu? Kwanini aruhusu mateso makali duniani?

Je, kuna Mungu? Kwanini aruhusu mateso makali duniani?

Kwanza freewill haipo.

Hatuna freewill ya kuchagua kuzaliwa ama kutokuzaliwa.

Hatuna freewill ya kuchagua kuishi milele.

Huna freewill ya kurudi mwaka 1990.

Hakuna freewill.

Hakuna Mungu.
Bro, rudi shule ukasome maana ya neno Free Will kwenye falsafa! Free Will maana yake ni uhuru wa akili yako kuchagua kati ya machaguo yaliyopo mbele yako.
 
Mungu anafundishwa kama alphabet, muda, namba, mipaka nk. Hivyo vyote vilivumbuliwa na mwanadamu ili kutengeneza jamii yenye utamaduni unaonendana.

Kwa mfano leo hii wewe unaamini kuhusu Mungu kupitia Yesu. Wapo wanaoamini kupitia mtume
Rudi ukasome sayansi ya sasa ya ubongo. Wanasayansi wasioamini Mungu wameshathibitisha kuwa mtoto mdogo akizaliwa na kukulia kisiwani peke yake bila kufundishwa alfabeti, namba, wala dini, akili yake kiasili bado itajua kuwa ulimwengu huu una Muumbaji mkuu.

Imani kwa Mungu imewekwa kiasili ndani ya DNA na ubongo wa mwanadamu, alfabeti na mipaka zikifutwa, ustaarabu unaweza kubadilika, lakini imani kwa Mungu haijawahi kufutika tangu kuumbwa kwa dunia.
 
Sio kweli hakuna kitu cha namna hiyo
 
Hahaha aisee, yani unatengeneza hoja dhaifu ya upande wa pili kisha unaishambulia! Nimeupenda huu mchezo.

Nani kakwambia kila anayeamini Mungu wa Abrahamu anaamini dunia au binadamu ana miaka 6,000 tu? Unatakiwa uelewe hiyo ni tafsiri ya kale ya kimapokeo tu ya baadhi ya vikundi.

Wasomi wote wakubwa wa kiteolojia wa sasa wa Kikristo na Kiislamu wanakubali kabisa ukweli wa kisayansi kuwa ulimwengu una miaka bilioni 13.8 na binadamu ana miaka mamilioni. Kupitia Mungu, sayansi na imani havipingani hata kidogo.
Bullshit,
Hakuna hata dhehebu moja la Ukristo linaloamini binadamu wamekuwepo duniani kwa zaidi ya miaka 6,000. Hiyo Quran ndio kituko zaidi kwa sababu ime copy mambo tu kiholela kwenye biblia ya agano la kale wala haileweki hata inaanza au kuishia wapi.
 
Nataka kujua kutoka kwako. Uzalendo wako upo kutoka ndani ya nafsi yako au kwenye makaratasi. Nimeanzia mbali ili ufahamu namna ubongo wako ulivyojengwa kwenye issue ya Mungu
Huo mtego wako wa kitoto wa kutumia uzalendo ili uje ulinganishe na Mungu nimeugundua mda tu, unajaribu kulinganisha uzalendo wa nchi ambao ni utambulisho wa kisiasa ulioundwa na binadamu na uwepo wa Muumbaji wa ulimwengu, huoni kama unafanya false analogy?
 
Mkuu umeruka madarasa mengi sana ya physics, physical laws sio matokeo ya Big Bang. Big Bang ndio matokeo ya sheria za physics zilizokuwepo from planck epoch! Ili mlipuko wowote utokee na vitu vitawanyike, lazima sheria za gavity), strong and weak nuclear forces na thermodynamics ziwepo tayari.

Huwezi kuwa na mechi ya mpira kabla ya sheria za mpira kuwepo! Shule bado inakusumbua kaka.
Screenshot_20260811-140950~2.jpg
 
Bullshit,
Hakuna hata dhehebu moja la Ukristo linaloamini binadamu wamekuwepo duniani kwa zaidi ya miaka 6,000. Hiyo Quran ndio kituko zaidi kwa sababu ime copy mambo tu kiholela kwenye biblia ya agano la kale wala haileweki hata inaanza au kuishia wapi.
Unajua kusoma vizuri kweli? ulicho kiandika hapa ni umethibitisha tu kwa uwazi huwa hausomi vitabu.

Na hujui maana ya continuity of divine revelation.
 
Ukipinga njoo na sababu kabisa ya kupinga ili nikuone una akili timamu.
Huwezi kujua uwepo wa Mungu kama hujafundishwa au hujakuta jamii inayokuzunguka ina utamaduni huo. Wewe unayebisha hili, zaa mtoto ukamuweke msituni huko na wanyama uone atakuja na kitu gani
 
Huo mtego wako wa kitoto wa kutumia uzalendo ili uje ulinganishe na Mungu nimeugundua mda tu, unajaribu kulinganisha uzalendo wa nchi ambao ni utambulisho wa kisiasa ulioundwa na binadamu na uwepo wa Muumbaji wa ulimwengu, huoni kama unafanya false analogy?
Aliyekuelekeza na kukuandikia kuhusu uwepo wa Mungu ndiye aliyekuandikia kila kitu kuhusu wewe. Huwezi kunielewa kwasababu tayari project yao imefanikiwa.

Ili uwe huru sio kazi rahisi
 
Rudi ukasome sayansi ya sasa ya ubongo. Wanasayansi wasioamini Mungu wameshathibitisha kuwa mtoto mdogo akizaliwa na kukulia kisiwani peke yake bila kufundishwa alfabeti, namba, wala dini, akili yake kiasili bado itajua kuwa ulimwengu huu una Muumbaji mkuu.

Imani kwa Mungu imewekwa kiasili ndani ya DNA na ubongo wa mwanadamu, alfabeti na mipaka zikifutwa, ustaarabu unaweza kubadilika, lakini imani kwa Mungu haijawahi kufutika tangu kuumbwa kwa dunia.
Acha kuwaambia watu warudi shule, walimu katika shule zote za Tanzania wanafundisha ulimwengu na viumbe waliopo unatokana na mungu wa Abraham, Hakuna hata mwanafunzi mmoja wa shule au chuo nchi hii amewahi kuingia kwenye academic debate ya chanzo cha ulimwengu na uhai. Wewe mwenyewe pseudo-intellectual yako haya mambo hujaitoa shule bali umeyasikia tu kwa Christian Apologists mtandaoni, wala hakuna shule uliyosoma au uliyowahi ku debate.
 
Huwezi kujua uwepo wa Mungu kama hujafundishwa au hujakuta jamii inayokuzunguka ina utamaduni huo. Wewe unayebisha hili, zaa mtoto ukamuweke msituni huko na wanyama uone atakuja na kitu gani
Waafrika wetu wa kale walikuwa na majina kama Mulungu, Ruwa, Lyuba kabla hata ya Ukoloni. Walifundishwa na nani kama sio ushuhuda uliopo ndani ya roho na akili zao kiasili?
 
Acha kuwaambia watu warudi shule, walimu katika shule zote za Tanzania wanafundisha ulimwengu na viumbe waliopo unatokana na mungu wa Abraham, Hakuna hata mwanafunzi mmoja wa shule au chuo nchi hii amewahi kuingia kwenye academic debate ya chanzo cha ulimwengu na uhai. Wewe mwenyewe pseudo-intellectual yako haya mambo hujaitoa shule bali umeyasikia tu kwa Christian Apologists mtandaoni, wala hakuna shule uliyosoma au uliyowahi ku debate.
Unazidi kujianika tu usivyoiitambua mitaala ya nchi yako! Kwenye masomo ya Geography form one na biology, mada za mwanzo kabisa ni the origin of the earth/solar system na cell evolution, wanafunzi Huwa wanafundishwa nadharia za kisayansi kama Big Bang na mabadiliko ya viumbe. Shule zinafundisha sayansi safi darasani, kama wewe ulikuwa unatoroka vipindi kwenda kucheza mdako hizo na shida zako.
 
Maisha ni mateso. Tunateseka si kwasababu Mungu yupo au hayupo, ni kwasababu hatupo tayari kupokea mabadiliko (mfano; kufiwa, kupoteza kazi, biashara, kuugua maradhi n.k) yanayo tutokea kwenye maisha yetu ya Kila siku. Ilihali mabadiliko ni sehemu ya maisha ya Kila mtu.

Ili kuepuka mateso ni kuifundisha Akili yako kuukubali ukweli. hii itakusaidia kuzuia mateso yasiyo na ulazima (majuto,hisia za maumivu, n.k) Kupingana na uhalisia ndio tunavyozidi kuzidisha mateso.
 
Inahitaji neema ya Mungu kujua hilo kama huna itakua ni ngumu kidogo kuelewa ni kama mbuzi anapigiwa gitaa
Ukishajua tu Kila chenye mwanzo kina mwisho wake. Iwe ni furaha, hisia za huzuni, ufukara, utajiri, na hata uhai wa kiumbe hai. Utakuwa na amani hasa wakati unapopitia nyakati ngumu. K
 
Acheni kumdogosha mungu wenu kumfanya awe na nguvu sawa na binadamu.

Mtoto anachomwa sindano kwa sababu ndio last option inayokuwepo kama binadamu tungekuwa na nguvu za kuamuru mtoto apone bila sindano, oparesheni au dawa zozote tungefanya hivyo ila hatuna huo uwezo, mungu wa Abraham anasemwa ana huo uwezo tena na wa zaidi hata kuzuia magonjwa kabisa.

Wewe ukienda hospitali halafu daktari akasema una cancer inabidi ukatwe mguu baadaye ukaja kugundua daktari alikuwa ana dawa au namna ya kukuponya bila mguu kukatwa na ukawa sawa kabisa utajisikiaje kuhusu huyo daktari??
Misingi ya hoja imebainisha kabisa kwamba uwezo wa Mungu sio sawa na binadamu.

Udhaifu wa hoja yenyewe ambao umegusia ni kwa nini huyo Mungu mwenye uwezo huo asizuie malaria au cancer ili matibabu yenye kuumiza au vifo visitokee?
Moja ya majibu ya hoja hii ni kwamba mabaya na mazuri ni mtazamo wa kibinadamu. Kwa Mungu matukio yote ni saahihi yana lengo analolifahamu yeye.
 
Shetani ni sahihi pia kwa mungu?
 
Back
Top Bottom