Je, kuna Mungu? Kwanini aruhusu mateso makali duniani?

Je, kuna Mungu? Kwanini aruhusu mateso makali duniani?

Unaniuliza mimi kwani nimekuambia kama najua mungu yupo?
Sasa unabisha nini kama hujui..
Huwezi bishia kitu usicho kijua..

Unaweza kukiamini au usiamini..

Mimi binafsi ni najua experiencial wise, na ndo maana nimesema nilicho sema
 
Na kama unaamini Mungu hayupo kwa nini usitumie miujiza yako binafsi kumaliza hizo changamoto zote zinazokukabili maana wewe ulijiumba mwenyewe
 
Sio kwamba natafuta sifa au nataka kubishana na mtu kuhusu imani. Lakini nikitazama yanayoendelea duniani vita, mauaji, watoto wanaoteseka, njaa, magonjwa na watu wasio na hatia kupoteza maisha naanza kujiuliza kwa dhati kama Mungu yupo na ana uwezo wote, kwa nini anaruhusu mateso haya yaendelee?

Huenda kuna majibu ambayo mimi siyajui. Lakini kwa sasa, swali hili limenifanya nianze kujiuliza kwa kina kuhusu uwepo wa Mungu.

Ningependa kusikia mawazo yenu Je, wewe unaamini Mungu yupo? Na kama ndiyo, unaelezaje uwepo wa mateso makubwa duniani?

NB: Bado nipo kwenye majonzi ya kumpoteza rafiki yangu, aliyeteseka kwa ugonjwa wa sickle cell. Na aliyeishi maisha ya maumivu mpaka kuondoka kwake. Kijana mdogo miaka 23.
“Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu.
”
— Yohana 16:33 (Biblia Takatifu)
 
Sasa unabisha nini kama hujui..
Huwezi bishia kitu usicho kijua..

Unaweza kukiamini au uaiamini..

Mimi binafsi ni najua experiencial wise, na ndo maana nimesema nilicho sema
Experience gani hiyo unayoificha kama bangi ambayo hutaki kusema kabisa? Ulikamatwa na mkwe wa mtu ukaponea chupuchupu kupakwa mafuta?
 
Mkuu acha kunifanya mimi nikueleweshe kitu ambacho wewe mwenyewe hukitaki..

Umeshasema unataka logical consistency na mimi nilikwambia emotions hazipimwi kwa logic na hata AI haiwezi ku replicate ila bado unalazimisha..

Hapo siwezi, na kama unataka majibu sina.

Nimekupa ninacho kielewa ambacho Mungu amwruhusu kwangu thus kama utawiwa kufatilia utafanya
Hujathibitisha Mungu yupo, Unarukia kusema Mungu ameruhusu kwako.

Kwanza thibitisha Mungu yupo, kabla ya kusema ameruhusu kitu kwako.
 
Sio kwamba natafuta sifa au nataka kubishana na mtu kuhusu imani. Lakini nikitazama yanayoendelea duniani vita, mauaji, watoto wanaoteseka, njaa, magonjwa na watu wasio na hatia kupoteza maisha naanza kujiuliza kwa dhati kama Mungu yupo na ana uwezo wote, kwa nini anaruhusu mateso haya yaendelee?

Huenda kuna majibu ambayo mimi siyajui. Lakini kwa sasa, swali hili limenifanya nianze kujiuliza kwa kina kuhusu uwepo wa Mungu.

Ningependa kusikia mawazo yenu Je, wewe unaamini Mungu yupo? Na kama ndiyo, unaelezaje uwepo wa mateso makubwa duniani?

NB: Bado nipo kwenye majonzi ya kumpoteza rafiki yangu, aliyeteseka kwa ugonjwa wa sickle cell. Na aliyeishi maisha ya maumivu mpaka kuondoka kwake. Kijana mdogo miaka 23.
Unapoambiwa mshahara wa dhambi ni mauti unadhani dhambi ni keki au nanasi?
 
Personal experience isiyo na ushahidi?
Kuna mwingine huko mitandaoni anasema yeye ni Mungu, vipi inatupasa tujue ndio yeye?

Kuna wengine kule Kenya walipanda kwenye misitu sijui kilima shakahola na kustarve to death ili waende kwa Mungu, walikuwa sahihi?

Vipi kama upo delusional au upo hai baada ya kutumia madawa ya kulevya hasa bangi?

Hii ndio reference ya maana ulioiona uje nayo?
Sasa hayo mambo yako ya kijinga peleka unako jua wewe..
Am not down for that shit..

Hata Mungu hapendi
 
Kwa nini unapaswa umtetee mungu wako?
Kwa nini asijitetee yeye mwenyewe?
Kwani mahakamani jaji huwa anashuka kizimbani kujitetea mbele ya mtuhumiwa? Sisi wanadamu ndio tuko kwenye mtihani na majaribu ya haya maisha sio Mungu. Yeye alishaleta ushahidi wake kupitia the laws of nature. Kama wewe umechagua kuwa kipofu na kutoona huo ushahidi uliowazi, yeye hana cha kupoteza. He doesn't owe you a personal appearance just to satisfy your ego.
 
Hujathibitisha Mungu yupo, Unarukia kusema Mungu ameruhusu kwako.

Kwanza thibitisha Mungu yupo, kabla ya kusema ameruhusu kitu kwako.
Wewe kichwa chako kimashida gani?

Nimekwambia kila kitu na mwisho wa maelezo yangu, unataka nielezee kipo tena?
 
Mtoa mada kwanza unatakiwa utambue kwamba Mungu yupo na ni mkuu na wa milele,halali wala hasinzii,hajazaa wala hajazaliwa na hakuna anaefanana nae/nacho.
Mungu yupo na anaonekana kwa wanaotumia akili zao sawa sawa kupitia alivyoviumba.
Mimi naomba nikupe njia moja tu ndogo ifanyie uchunguzi na kuanzia hapo utaona uwepo wake.
NJia yenyewe ni hii:
Tafuta somo/makala yoyote inayozungumzia MFUMO WA MMENG'ENYO WA CHAKULA KWA BINADAMU.
Kama hapa hujaelewa tafuta somo/makala ya REPRODUCTION SYSTEM YA BINADAMU
Soma au tazama video za makala hizi kwa UMAKINI MKUBWA....kama akili zako zimetulia hapo Mungu utamuona.
Ukijitoa akili tu kwamba hayupo utaishia kuona chenga tu na utaendelea kuungana na lile kundi la maiti zinazotembea zisizoamini uwepo wa aliyewaumba..... Yeye hujidhirihisha kwa wenye akili tu.
Mungu wa kweli ni jua kama sifa ya Mungu ni kufanya uhai
 
Wapumbavu hujisemea moyoni: Hakuna Mungu! Wote wamepotoka kabisa,
Wapumbavu hujisemea vichwani: Kuna Mungu! Wote wamepumbazwa na kukaririshwa.
Mtafuteni BWANA, maadamu anapatikana, Mwiteni, maadamu yu karibu; Mtu mbaya na aache njia yake, Na mtu asiye haki aache mawazo yake; Na amrudie BWANA, Naye atamrehemu; Na arejee kwa Mungu wetu, Naye atamsamehe kabisa.
Huyo BWANA alikwambia ana uhitaji wa kutafutwa?

Ana ni nyie mna kiherehere cha kumtafuta?

Huyo Bwana akitafutwa anafaidika nini?

Huyo Bwana asipotafutwa anapungukiwa nini?
 
Sio kwamba natafuta sifa au nataka kubishana na mtu kuhusu imani. Lakini nikitazama yanayoendelea duniani vita, mauaji, watoto wanaoteseka, njaa, magonjwa na watu wasio na hatia kupoteza maisha naanza kujiuliza kwa dhati kama Mungu yupo na ana uwezo wote, kwa nini anaruhusu mateso haya yaendelee?
Bro are you retarded? Mungu kawapa watu akili ya kujua baya na zuri. wanazitumia vibaya hizo akili halafu unamlamu Mungu tena?
 
Wewe unachopinga ni uwepo wake physically au?

Maana kumbuka sio kila kitu kina onekana kwa macho ya nyama..

Let alone wewe mwenyewe haujui chanzo cha uhai...iweje uje uulize aliyekupa huo uhai ni nani.

When we use egoic flesh tunakosea sana. Ndo maana hata Buddhist wanaachana na flesh and mind kwanza..

Haya mambo na hizi stage utazivuka ukiwa consistent kufatilia hili jambo. Usibaki kwenye questionnaire.. Nenda kwenye practices pia itakusaidia zaidi
Bila kufundishwa au kuelekezwa kuhusu uwepo wa huyo Mungu. Ni njia ipi inayoweza kumfanya mtu/binadamu aelewe/afahamu uwepo wa huyo Mungu?
 
Wapumbavu hujisemea vichwani: Kuna Mungu! Wote wamepumbazwa na kukaririshwa.

Huyo BWANA alikwambia ana uhitaji wa kutafutwa?

Ana ni nyie mna kiherehere cha kumtafuta?

Huyo Bwana akitafutwa anafaidika nini?

Huyo Bwana asipotafutwa anapungukiwa nini?
Hii kauli yako umeitoa kichwani kwako au umeinakili kwa makafiri wa mtandaoni? Wewe ndiye uliyekariri maana huna hoja yoyote ya maana uliyosimamia zaidi ya kashfa. Watu wanajadili cosmology, fine tuning, na moral laws, wewe unaleta mipasho Grow up!
 
Hili swali lilishanisumbua sana ila mwisho nikajaga ku conclude kuwa MUNGU yupo ila hana kujali mwanadam anachokipitia!

Ukiugua, ukiteseka kivyovyote, ukionewa/ mateso yoyote unavyopitia, yeye kwake ni mambo ya kawaida anachukulia kawaida tu! Yeye anachoangalia ukifa je utakua uko upande wake au upande wa mpinzani wake. Hata hao wanaougua wakamkimbilia huwa wanasota sana kupata uponyaji, kuna wanaofanikiwa na kuna ambao huishia kukata tamaa na kugail na kuishia kusema hamna Mungu!

Ki ufup maisha ya mwanadamu Mungu hayajali ndo maana hata mitume wake waliuawa vifo vya kikatili baadh yao lakn hakuleta msaada!

Fikiria Yesu aliambiwa na wanafunzi wake, "mwalim, kuna watu wameangukiwa na mnara, wakafa!" Yesu akajibu "na niny msipotubu mtaangamia kama hao!" Yaan kajb kirahs kabsa bila hata kustuka kwa kilichotokea!
Kwahiyo habari za Mungu umezijua kupitia bible?
 
Wewe kichwa chako kimashida gani?
kimashida❌️

Kina shida✅️

Wewe hata kuandika huwezi.

Rudi shule kwanza, ukafunzwe kuandika kwa usahihi.
Nimekwambia kila kitu na mwisho wa maelezo yangu, unataka nielezee kipo tena?
This is the futility of arguing with unreasonable people.

You are not mentally enough to argue with me.

Find someone of your league to parallel your mediocrity.

I'm done with you.
 
Back
Top Bottom