Je, kuna Mungu? Kwanini aruhusu mateso makali duniani?

Unakubali tu ili yaishe?

Au unatambua na kujua kwamba, Kuwepo kwa Mungu ambaye anadaiwa ni muweza wa vyote, mjuzi wa vyote, mwenye upendo na huruma kwenye Dunia iliyojaa uovu na mabaya kuna tengeneza utata?

Kwa sababu haiwezekani Mungu mwenye upendo na huruma, mjuzi wa vyote na muweza wa vyote awepo kwenye Dunia iliyojaa uovu.

Ni either Mungu huyo hana upendo na hawezi yote ndio maana Dunia ina mabaya.

Au Mungu huyo hayupo ndio maana Dunia ina mabaya.

Lakini mtu akisema Mungu anaweza yote na amejaa upendo na huruma. Wakati hapohapo Dunia imejaa Maovu ya kila aina. Kunatengeneza Utata.
Mungu huruhusu yote ili utukufu wake usibezwe shida mnataka kumuelewa Mungu kama unasoma notes za darasani
 
Sio kwamba natafuta sifa au nataka kubishana na mtu kuhusu imani. Lakini nikitazama yanayoendelea duniani vita, mauaji, watoto wanaoteseka, njaa, magonjwa na watu wasio na hatia kupoteza maisha naanza kujiuliza kwa dhati kama Mungu yupo na ana uwezo wote, kwa nini anaruhusu mateso haya yaendelee?

Huenda kuna majibu ambayo mimi siyajui. Lakini kwa sasa, swali hili limenifanya nianze kujiuliza kwa kina kuhusu uwepo wa Mungu.

Ningependa kusikia mawazo yenu Je, wewe unaamini Mungu yupo? Na kama ndiyo, unaelezaje uwepo wa mateso makubwa duniani?

NB: Bado nipo kwenye majonzi ya kumpoteza rafiki yangu, aliyeteseka kwa ugonjwa wa sickle cell. Na aliyeishi maisha ya maumivu mpaka kuondoka kwake. Kijana mdogo miaka 23.
Binadamu amepewa free will, lakini hiyo free will ndio inayomtesa. Mfano mdogo kwa yaliyotokea wakati wa uchaguzi je hapo mungu tutamuhusishaje wakati waliofanya maamuzi ni sisi binabadamu wenyewe.
 
Hili swali lilishanisumbua sana ila mwisho nikajaga ku conclude kuwa MUNGU yupo ila hana kujali mwanadam anachokipitia!

Ukiugua, ukiteseka kivyovyote, ukionewa/ mateso yoyote unavyopitia, yeye kwake ni mambo ya kawaida anachukulia kawaida tu! Yeye anachoangalia ukifa je utakua uko upande wake au upande wa mpinzani wake. Hata hao wanaougua wakamkimbilia huwa wanasota sana kupata uponyaji, kuna wanaofanikiwa na kuna ambao huishia kukata tamaa na kugail na kuishia kusema hamna Mungu!

Ki ufup maisha ya mwanadamu Mungu hayajali ndo maana hata mitume wake waliuawa vifo vya kikatili baadh yao lakn hakuleta msaada!

Fikiria Yesu aliambiwa na wanafunzi wake, "mwalim, kuna watu wameangukiwa na mnara, wakafa!" Yesu akajibu "na niny msipotubu mtaangamia kama hao!" Yaan kajb kirahs kabsa bila hata kustuka kwa kilichotokea!
Umeamdika kwa uchungu

Samahani.
Ila hapo kwenye mnara umepatoa wapi?
 
Mkuu kua sisi ambao unafika stage una transcend mitazamo na falsafa yaani unagundua vyote ni kuzunguka mbuyu tuu.

Na hapo ndo ule ukweli usio na pande huja.. Yaani unakuwa umevuka good and bad. Unabakia ukweli tu.. Na sio wa kuanza ku prove kwa watu
Upo sawa mkuu maana kila mtu katika imani yake anapaswa ajitetee amtetee Mungu wake,waganga nao wana miungu yao
 
Wewe unachopinga ni uwepo wake physically au?
Sio physically tu, Huyo Mungu hayupo kwa namna yoyote ile.

Kwa sababu, Angalau kitu kinaweza kuwepo kwa namna mojawapo ya kuonekana, kushikika, kuhisika na kupimika.

Huyo Mungu hayupo kwa namna yoyote ile.

Haonekani, Hashikiki, Haisiki na wala hapimiki.

Huyo Mungu hayupo kwa namna yoyote ile ya kuthibitishika yupo.
Maana kumbuka sio kila kitu kina onekana kwa macho ya nyama..
Upepo hauonekani kwa macho ya nyama, ila tuna tambua uwepo wake kwa kuupima na vifaa kama Anemometer na Windvane na kujua uwepo wake.

Pia upepo ukivuma tunaweza kuusikia ukivuma.

Joto na baridi, havionekani kwa macho ya nyama ila tunatambua vipo kwa kuvihisi na tunaweza kupima kiwango cha joto na baridi.

Kwa hiyo kuna vitu havipo physically, Lakini tunaweza kutambua uwepo wake kwa namna nyingine kama kupima, kuhisi na kusikia. Na tukajua vipo licha ya kwamba havionekani physically.

Lakini huyo Mungu hayupo kwa namna yoyote ile.

Let alone wewe mwenyewe haujui chanzo cha uhai...iweje uje uulize aliyekupa huo uhai ni nani.
Kama hujui chanzo cha uhai, Ulijuaje huo uhai tulipewa?

Kutokujua chanzo cha uhai sio conclusion kwamba tulipewa.

Na kama tulipewa uhai, Hata huyo aliyetupa uhai hawezi kuwepo tu from nowhere.

Na yeye atahitaji chanzo chake.

Ikiwa mifumo tata inahitaji muumbaji, basi muumbaji naye anahitaji muumbaji aliye tata zaidi. Hilo linapelekea msururu mrefu usio na mwisho wa waumbaji wengi, ambapo kila mmoja anakuwa tata zaidi kuliko aliyemtangulia.
When we use egoic flesh tunakosea sana. Ndo maana hata Buddhist wanaachana na flesh and mind kwanza..

Haya mambo na hizi stage utazivuka ukiwa consistent kufatilia hili jambo. Usibaki kwenye questionnaire.. Nenda kwenye practices pia itakusaidia zaidi.
Mungu hayupo.

Hakuna Mungu.
 
Hili swali lilishanisumbua sana ila mwisho nikajaga ku conclude kuwa MUNGU yupo ila hana kujali mwanadam anachokipitia!

Ukiugua, ukiteseka kivyovyote, ukionewa/ mateso yoyote unavyopitia, yeye kwake ni mambo ya kawaida anachukulia kawaida tu! Yeye anachoangalia ukifa je utakua uko upande wake au upande wa mpinzani wake. Hata hao wanaougua wakamkimbilia huwa wanasota sana kupata uponyaji, kuna wanaofanikiwa na kuna ambao huishia kukata tamaa na kugail na kuishia kusema hamna Mungu!

Ki ufup maisha ya mwanadamu Mungu hayajali ndo maana hata mitume wake waliuawa vifo vya kikatili baadh yao lakn hakuleta msaada!

Fikiria Yesu aliambiwa na wanafunzi wake, "mwalim, kuna watu wameangukiwa na mnara, wakafa!" Yesu akajibu "na niny msipotubu mtaangamia kama hao!" Yaan kajb kirahs kabsa bila hata kustuka kwa kilichotokea!
Mwanetu umeelezea vyema sana
 
Upo sawa mkuu maana kila mtu katika imani yake anapaswa ajitetee amtetee Mungu wake,waganga nao wana miungu yao
Yes uko sahihi. Ila waganga hutumia sayansi isiyo julikana tu.. Ni magicians wazoefu, na wengine hawajui the mechanics behind ila hasa hasa ni sayansi iliyo fichwa.

Sometimes, imani pia humfanya mtu a manifest reality si unamkumbuka babu wa loriondo? Na kikombe chake, hapo utasema ni uchawi au placebo effect. Au labda huenda alikuwa na a great medicinal combination ya miti shamba who knows?
 
Mleta mada Mungu yupo anaitwa YHWH.
Kuhusu mambo mengi mabaya duniani ukitazama kwa asilimia kubwa yanaletwa na binadamu

Ndio maana Yesu alisema kuwa Amri Kubwa ni Upendo. Laiti kama kungekuwa na Upendo tusingeona mabaya haya

ILa....
 
Nashauri kasome the stori of job..
Au kaangalie video YouTube.. Inakusaidia kumwona Mungu katika zone zote za ubaya na uzuri... Akiwa na lengo la kukujenga kiimani
Huyo Mungu angekuwepo wala usingehitaji imani kuamini.

Ungejua kwa UHAKIKA Kabisa bila kutumia imani.

Mimi sihitaji imani.

Nahitaji facts zenye proofs and evidence.

I don't believe in believing.

Siamini kwenye kuamini na wala sitting kuamini.

Nahitaji kujua na nataka kujua kwa uhakika, ushahidi na uthibitisho.

Hizi story za Ayubu(Job) ni Hekaya za Biblia kama ilivyo stori za Abunuwasi kwenye Hekaya za Abunuwasi.
 
Sio kwamba natafuta sifa au nataka kubishana na mtu kuhusu imani. Lakini nikitazama yanayoendelea duniani vita, mauaji, watoto wanaoteseka, njaa, magonjwa na watu wasio na hatia kupoteza maisha naanza kujiuliza kwa dhati kama Mungu yupo na ana uwezo wote, kwa nini anaruhusu mateso haya yaendelee?

Huenda kuna majibu ambayo mimi siyajui. Lakini kwa sasa, swali hili limenifanya nianze kujiuliza kwa kina kuhusu uwepo wa Mungu.

Ningependa kusikia mawazo yenu Je, wewe unaamini Mungu yupo? Na kama ndiyo, unaelezaje uwepo wa mateso makubwa duniani?

NB: Bado nipo kwenye majonzi ya kumpoteza rafiki yangu, aliyeteseka kwa ugonjwa wa sickle cell. Na aliyeishi maisha ya maumivu mpaka kuondoka kwake. Kijana mdogo miaka 23.
Mungu yupo
 
siwezi kubishia unachokiamini, siwezi kubadilisha mtazamo wangu kwa sababu umesema lakini pia siwezi kukulazimisha usmini ninachokiamini
hivyo bado upo sahihi kwa mawazo yako
Mimi wala siamini.

Siamini kwenye kuamini.

Sina imani ya aina yoyote ile.

Kuna tofauti kati ya "kuamini" na "kujua".

Kuamini unaweza kuamini hata uongo.

Mimi sihitaji kuamini nahitaji kujua kwa uhakika, ukweli, ushahidi na uthibitisho.
 
Sio physically tu, Huyo Mungu hayupo kwa namna yoyote ile.

Kwa sababu, Angalau kitu kinaweza kuwepo kwa namna mojawapo ya kuonekana, kushikika, kuhisika na kupimika.

Huyo Mungu hayupo kwa namna yoyote ile.

Haonekani, Hashikiki, Haisiki na wala hapimiki.

Huyo Mungu hayupo kwa namna yoyote ile ya kuthibitishika yupo.
Sasa kama huwezi kudetect kwa macho, hisia na sauti mbona unatumia vitu hivyo ambavyo havina uwezo wa ku detect kuuliza?
Upepo hauonekani kwa macho ya nyama, ila tuna tambua uwepo wake kwa kuupima na vifaa kama Anemometer na Windvane na kujua uwepo wake.

Pia upepo ukivuma tunaweza kuusikia ukivuma.

Joto na baridi, havionekani kwa macho ya nyama ila tunatambua vipo kwa kuvihisi na tunaweza kupima kiwango cha joto na baridi.

Kwa hiyo kuna vitu havipo physically, Lakini tunaweza kutambua uwepo wake kwa namna nyingine kama kupima, kuhisi na kusikia. Na tukajua vipo licha ya kwamba havionekani physically.

Lakini huyo Mungu hayupo kwa namna yoyote ile.
Yuo can not measure that which you can't see but feel.. Kuna jamaa aliyegundua micro chip kashasema kabisa we Cannot replicate a feeling... Because it is quantum.
Kama hujui chanzo cha uhai, Ulijuaje huo uhai tulipewa?

Kutokujua chanzo cha uhai sio conclusion kwamba tulipewa.

Na kama tulipewa uhai, Hata huyo aliyetupa uhai hawezi kuwepo tu from nowhere.

Na yeye atahitaji chanzo chake.

Ikiwa mifumo tata inahitaji muumbaji, basi muumbaji naye anahitaji muumbaji aliye tata zaidi. Hilo linapelekea msururu mrefu usio na mwisho wa waumbaji wengi, ambapo kila mmoja anakuwa tata zaidi kuliko aliyemtangulia.
Mkuu you're just playing with your mind. Hiyo ni neurosis
Mungu hayupo.

Hakuna Mungu
Amini unacho amini... It is whay "YOU" think not somebody else
 
Ni kwasababu umeuliza swali kwenye page yetu, huku tupo sisi😁
Au unataka Mungu awashe data aingie jf kukujibu hapa kwenye comment
Huyo Mungu wala hayupo popote.

Ni nyie tu mnahangaika kutetea illusions zenu za kidini na kiimani.
 
Huyo Mungu angekuwepo wala usingehitaji imani kuamini.

Ungejua kwa UHAKIKA Kabisa bila kutumia imani.

Mimi sihitaji imani.

Nahitaji facts zenye proofs and evidence.

I don't believe in believing.

Siamini kwenye kuamini na wala sitting kuamini.

Nahitaji kujua na nataka kujua kwa uhakika, ushahidi na uthibitisho.

Hizi story za Ayubu(Job) ni Hekaya za Biblia kama ilivyo stori za Abunuwasi kwenye Hekaya za Abunuwasi.
Actually, nilikosea kusema I believe...

I don't believe I know intuitively..

That surpasses any explanation because nitadogosha kile nafsi yangu inakijua

Nilikuwa kama wewe mpaka pale Mungu alipoamuwa kunifunza, na nina mshukuru kuniokoa maana ningekuwa mfano mbaya sana
 
Sasa kama huwezi kudetect kwa macho, hisia na sauti mbona unatumia vitu hivyo ambavyo havina uwezo wa ku detect kuuliza?

Yuo can not measure that which you can't see but feel.. Kuna jamaa aliyegundua micro chip kashasema kabisa we Cannot replicate a feeling... Because it is quantum.

Mkuu you're just playing with your mind. Hiyo ni neurosis

Amini unacho amini... It is whay "YOU" think not somebody else
Kutokuweza kitu fulani sio hitimisho la moja kwa moja kwamba jibu ni Mungu au kuna Mungu.

Maana wewe unataka kufanya Divine fallacy.

The divine fallacy also known as the argument from incredulity—is a logical error. It happens when someone claims that a hard-to-understand event must be the work of God or magic simply because they cannot find another explanation.

The divine fallacy can take various forms, but it generally has a structure similar to the following:

Premise 1: if I don’t know how to explain a certain phenomenon using science, then it must occur as a result of divine intervention(God)

Premise 2: I don’t know how to explain this phenomenon using science.

Conclusion: this phenomenon must occur as a result of divine intervention.
 
Back
Top Bottom