Kwanini huamini uwepo wa Mungu?

Kwanini huamini uwepo wa Mungu?

Mtu_Huru88

New Member
Joined
Aug 14, 2026
Posts
2
Reaction score
3
Tukiachana na masuala ya dini kwanza, kwasababu sio dini ndo zimeleta uwepo wa Mungu
Ukizingatia dini kuu zilizopo mfano Uislam umeanza baada ya uwepo wa Mohhamad S.A.W, mtume huyo alidai kashushiwa kitabu kutoka mbiguni (Kuran) na hapo ndio ukawa mwanzo wake kitu ambacho kabla ya Mohhamad kulikuwa na watu na maisha yaliendelea kama kawaida

Pia Ukristo ukristo vile vile baada ya masihi (Yesu) hata kama kuna watu walikuwepo before ila ulienea baada yake

Mods naomba msiunganishe uzi huu na mada zingine, Natumai sote ni wazima wa afya, nikupe pole kwa usumbufu huu kukuchosha na kukusumbua kwa andiko hili, lakini nakuomba twende pamoja kujadili hil, sina lengo la kukutoa kutokana na unachokiamini kwa imani yako hiyo

Karibu na wacha tujadili haya kwa pamoja

1: Je ni kweli Dunia imefanyika yenyewe tu bila kutokana na chochote, ilizuka tu from no where ikiwa na vitu vyake, udongo, hewa,viumbe nk tena vikiwa kwenye mpangilio

2:Je ipo vile vile toka ijiunde, inaendea kujiunda au unaisha inapunguza baadhi ya witu, udongo upo vile vile hauishi hata baada ya matumizi, vipi kuhusu viumbe wapo vile vile wanaongezea au wanapungua, kwamba samaki ziwani wapo vile vile, wanyama na viumbe wengine porini wapo vile vilw hawapungui, hakuna viumbe waliopotea ama kuadimika

Ripoti zinasema kuna baadhi ya viumbe wamepotea kabisa na wengine kuadimika maana ake kuna vitu vinaisha je kuna kuisha bila kuanza, huko kuanza kulianzaje

3:Vipi kuhusu mifumo yake na uendeshaji wake, mbona kama ipo kimpangilio na kwa hesabu kali
Utegemezi kwenye baadhi ya mambo, mfano mfumo wa jua (The Solar system) dunia na viumbe wake wote wanategemea

4:Sayansi na gunduzi zake, tukianza na sayansi ya fizikia ambayo inatokana na vitu vilivyopo kwenye mifumo ya Dunia
Mwanga, Sumaku na Mawimbi

Ni nini kilitokea kuwa na Dunia yenye mifumo au mfumo unaosomana kwa kiasi hiki, ni kweli imekuwepo tu hakuna nguvu au msukumo wa kitu nyuma yake?
 
Back
Top Bottom