FairPlayer
JF-Expert Member
- Feb 27, 2006
- 4,145
- 733
Mkuu FD,
I hope hapo juu una maana unalipa kidogo kidogo kulingana na masharti ya mikopo yako.
Kama una maana tofauti na hiyo, hilo ni jambo la hatari sana. Kukiuka masharti ya mkopo kwa sababu zozote zile si jambo la kujivunia na badala yake ni hatari mno.
Unapokuwa kiongozi wa siasa inakuwa hata hatari zaidi maana ukifilisiwa, kweli wewe unafaa hata kuongoza chama?
Ni kweli nchi haiwezi kuendelea bila wananchi wake kuweza kukopa na kuendesha biashara zao. Lakini inapotokea kwamba viongozi wanakopa sehemu kama NSSF ambako kuna nafuu kubwa na kuwaacha wananchi wanasota na mabank
ambako kuna interest rate zaidi ya 20%, kwa kweli haiwezi kuwa sawa. Matokeo yake viongozi huwa hawachukuia hatua kubadilisha sheria za mabank maana wanakuwa hawalipati hilo joto la jiwe ambalo linawakumba wananchi wa kawaida.
Wanasiasa waache kukimbilia sehemu kama NSSF na badala yake wakakope kwenye hayo mabank sawa na wananchi wengine.
Tupo pamoja mkuu. Deni langu nalipa kidogo kidogo kama tulivyokubaliana.
Ninachopinga ni watu kuongelea vitu visivyo na msingi kama kumiliki Vogue.
Pia rudi nyuma kidogo usome post ya Techmaro. Huu ni mkopo wa kibiashara, mabenki kukosa FOREX pia ni kigezo tosha cha kukaa meza moja kujadiliana na aliyekukopesha. Kuna mambo mengi hasa kama aliyekukopesha alijua nia yako ni nini, It is a business loan sio personal loan.
Mimi pia napinga Mbowe kutorejesha on time hela hizo.
Hili deni lina RIBA. Na riba compounded haifanani na simple interest rate.
EPA ni kitu kingine and Richmond ni kingine. Mbowe anatakiwa alipe deni alilokopa under terms and conditions. Hakuna mtu aliyesema Mbowe ni mwizi, noo. Bali Mbowe need to pay his Bills, that is how we suppose to conduct business. Alijua Riba ina Riba, alijua madhara ya kutolipa yanasababisha adjusted rate kutokana na Inflation aliyajua yote haya.
do you know the seriousness of these allegations you are making here?
Ben,Naona Chinga na kada wameamua kuuchuna.Kwa hiyo Mkullo ana walakini maanake dataz zinazomwagwa ni noma,wataanza kupiga ramli kuomba mjadala ufe na wameuanza wenyewe.
Na hizo hela za taasisi kubwa kama hiyo kama Mkullo alishindwa kuzisimamia na kuziweka kwenye mashaka hivyo,inakuaje kikwete amteue kuwa waziri wa fedha?
Je,katika utajiri alioupata Mkullo kama si wa halali,je ni nini uhusiano wa Mkullo na Kikwete,
Je,inawezekana mkullo alisaidia kampeni za kikwete kupitia hela za NSSF?
Je,kupatiwa uwaziri inawezekana kuna fadhila fulani zinalipwa?
Well,hapa kuna mashaka makubwa kama Mkullo hakua kiongozi makini kwenye taasisi hiyo na still akapewa wadhifa mkubwa kama huo.Tuanzie kule kwenye unaibu wa wizara hiyo nyeti.
Kidali po!
Ben,
kuna mtu mwenye data anipe connection ya NSSF(NPF) na SUKITA?
Nasikia kuna balaaa kubwa huko.
mkuki kwenda msituni haukupotea
Biashara yoyote kubwa ili iendelee inaitaji mkopo, kuna aina nyingi za mikopo. Short term debt and long term debt, sasa Mbowe alikopa kwa muda gani na kwa biashara gani? Hilo ni million dollar question. Kama alikopa kwa more than 10 years ili kufinance club yake that is fine, tatizo linakuja jee alikuwa anafanya month payments?
Na kama alikuwa hafanyi payments jee ni nani alikuwa anadefend collateral alizoweka zisiuzwe? Sababu kama unapiga kelele kwenye majukwaa kwamba CCM ni wezi, na wewe unatumia same strategy za CCM katika njia nyingine, then unakila haki ya kufananishwa na Gavana wa NY.
Nilishawai kusema natofautiana sana na Mboe sababu anaonyesha ni mbabaishaji. Mikopo yote ina rules and regulation, na dawa ya kukopa ni kulipa. Rejea maneno ya Mwalim " You borrow, you pay". Hakuna sijui nilikuwa sijui hili wala lile.
Ni mategemeo yangu wana CHADEMA wataomba explaination kutoka kwa kiongozi wao, jee haoni kama huko ni kufuja mali za umma? Jee yeye anajenga picha gani kama kiongozi? Jee ni kwa asilimia ngapi kuchelewa kwake kwa loan kuna adhiri viinua mgongo vya watu?
Sababu kumbuka kwamba pesa zile zinatumika kulipa pansion za baba na mama walio staff, sasa kama kuna mtu kwa njia moja au nyingine hataki kulipa kutokana na political power yake, then what is the different na mafisadi?
tehe....tehe...tehe......!!!maana nashangaa ! jiii imefutwa ! sasa tukisema JF ni pro-CHADEMA wanakataa na kusema tunaiponda JF, how ?
Ilinilazimu nitriple check kabla ya kuandika hii thread ndipo nikaona hamna kitu, nikashangaa !
Sasa naamini UFISADI ni hadi katika uandishi, na kama chuki zenyewe ndio hivi SIDHANI KAMA WE WILL GET WHERE WE EXPECT TO GET ! Tutakuwa tunacreate vitu ambavyo tunakemea !
Maneno ni kweli mbowe kasema, sasa sijui wanafuta nini ! au alilazimishwa mbowe kusema hayo maneno ?
Mwafrica wa kike, Asha Abdala Rev Kishoka and so and so mimi naomba tuwaignore hawa watu
KADA MPINZANI
MAHESABU
CHINGA
Kwanza angalieni nick name zao
Kada mpinzani ni dhahiri amekuja humu kuleta upinzani usio na msingi na sometimes anabisha na kupost vitu ambavyo haviingii akilini na wala havina ushawishi kabisa.
Mahesabu:- Huyu amekuja JF na mahesabu ya kuvuruga watu as u know kuna watu wametumwa na (WAMENUNULIWA) kwa ajili ya kuchafua watu hapa JF
Chinga:- Ni nani asiyejua matatizo wanayokutana nayo hawa kina CHINGA??
KWA HIYO TUNAWEZA KUWA TUNAPOTEZA MUDA KUBISHANA NA WATU AMBAO WAMEATHIRIKA KUTOKANA NA NICK NAMES ZAO WALIZOZICHAGU MFANO MDOGO TU UNAAMUA KUJIITA DUDUBAYA WHAT DO U THINK?? KILA SIKU NI MATATIZO TU GROW UP GUYS WEKENI POST ZENYE USHAWISHI SI KUVURURUGA WATU HAPA JF.
Mbowe awaponda wenzake
*Asema wapo kwa maslahi ya tumbo
*Kuungana sawa na kufika mbinguni
Na Eliya Mbonea, Iramba
MGOMBEA urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bw. Freeman Mbowe (CHADEMA), amesema uwezekano wa viongozi wa kambi ya Upinzani nchini kuungana ni mgumu sawa na tajiri kuona ufalme wa Mbingu.
Alitoa kauli hiyo jana, alipokuwa akihutubia wakazi na wanafunzi wa chuo na sekondari ya Kinampanda mjini hapa, baada ya kuulizwa swali lililotaka kujua sababu ya wagombea urais wa kambi hiyo kutoungana na kuwa kitu kimoja.
Bw. Mbowe alisema chama chake kimekuwa cha kwanza katika historia ya upinzani nchini kuweka mbele dhana ya ushirikiano baina ya wapinzani.
"Vyama vichache vimepandikizwa na CCM kwa maslahi ya tumbo, CHADEMA mwaka 1995 haikusimamisha mgombea, badala yake iliungana na NCCR-Mageuzi, mwaka 2000 tukawaunga mkono CUF, jitihada zetu zote za kushirikiana zimekuwa hazizai matunda, hivyo mwaka huu tumesimamisha mgombea," alisema.
Aliongeza kuwa viongozi wengi wa Upinzani hawawezi kuungana kwa dhamira ya kuwatetea Watanzania, kwani wapo kwa ajili ya maslahi binafsi.
"Msifikirie kuwa kila mgombea urais au Mwenyekiti wa chama yupo kwa ajili ya kupigania mustakabali wa nchi, wamegeuza siasa kama biashara na wanaitumia kama vyanzo vya mapato," alisema mgombea huyo.
Alisema lazima CCM ikubali lawama za kulifikisha Taifa katika hali mbaya na ya kutisha, na kuwafanya wananchi wajione kuwa matatizo yao ni tofauti ya rangi za bendera badala ya kuwaeleza kuwa tatizo kubwa ni umasikini.
Akizungumzia nafsi yake, Bw. Mbowe aliwaeleza wananchi kuwa hakuingia kwenye siasa kwa ajili ya kutafuta ajira, kwani anachopigania si maslahi ya CHADEMA bali ya wananchi wote. "CHADEMA si mama yangu naweza kuiacha wakati wowote," alisisitiza msimamo wake.
Alisema kamwe hataacha kutumia busara na hekima za Mwalimu Nyerere katika kujenga utaifa, kwani kipindi chote cha miaka 44 bado misingi ya utaifa aliyoicha Mwalimu haijatekelezwa.
NAULIZA :
(1) Kama anajua fika kwamba vyama vya upinzani (ukiondo chadema) vimepandikizwa na ccm, iweje aungane nao wakati wamepandikiza na ccm ?
(2)Pili alisema kwamba wapinzani (chadema excluded)kwamba wapo kwa ajili ya matumbo yao, DOESNT THAT TECHNICALLY INCLUDE HIMSELF AS WELL kwa kuungana nao ??
(3) Je yupo tayari kueleza watanzania wakiwemo wapiga kura wake kwamba chama chake (CHADEMA) kimepandikizwa na CCM ?
(4) Na yeye binafsi kaungana na wenzake ili tumbo lake lipate rizki ?
(5)Kasema kwamba hayupo kwenye siasa kama ajira, ila hapo hapo alisema kwamba "wenzake"(wapinzani) DOESNT THIS EVEN RAISE MORE QUESTIONS THAN ANSWERS ?????????????
JAMANI NAOMBENI HII MUIACHE HAPA NA MSIIFUTE ! INAELEWEKA WAZEE WENYEWE NI PRO-CHADEMA, NA NAJUA YOU MIGHT BE GOING THRU A ROUGHT TIME, ACHENI TU IKAE HAPA !
Sasa kilichobaki ni kuungana na wazee wakuu kama muonavyo hapo chini !