Historia|Wasifu: Je, Benjamin William Mkapa ni nani hasa?

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,810
11,981
1595581893378.png

Benjamin William Mkapa alizaliwa mnamo 12 November 1938 huko Ndanda Wilayani Masasi Mkoani Mtwara. Alimaliza Shahada ya kwanza ya Lugha ya Kiingereza kutoka Chuo Kikuu cha Makerere nchini Uganda mwaka 1962

Mwaka 1963 alihitimu shahada ya Uzamili katika Mahusiano ya Kimataifa kutoka katika Chuo Kikuu cha Columbia

Aliwahi kuwa Afisa Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Waziri wa Sayansi na Teknolojia, alikuwa Balozi (Canada) 1982 na baadaye nchini Marekani 1983 - 1984

Aliwahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje, 1977 - 1980 na 1984 hadi 1990

Alichaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia 1995 - 2005

Alikuwa miongoni mwa viongozi walioshiriki kutatua Mgogoro wa Uchaguzi nchini Kenya mwaka 2007 - 2008

Aliteuliwa kuwa msuluhishi wa mgogoro wa nchi ya Burundi mwaka 2016 - 2019

SHAHADA ZA HESHIMA ALIZOWAHI KUTUNUKIWA BENJAMIN WILLIAM MKAPA:
Mwaka 1998 alitunukiwa Shahada ya Heshima na Chuo Kikuu cha Sōka University (Japan)

Mnamo mwaka 1999 alitunukiwa Shahada ya Heshima na Chuo Kikuu cha Morehouse College (Marekani)

Mwaka 2003 alitunukiwa Shahada ya Heshima na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania

Mwaka wa 2005 alitunukiwa Shahada ya Uzamivu katika Sheria na Chuo Kikuu cha National University of Lesotho (Lesotho)

Mwaka 2005 alitunukiwa Shahada ya Uzamivu katika Elimu na Chuo Kikuu cha Kenyatta (Kenya)

Mwaka 2006 alitunukiwa Shahada ya Heshima na Chuo Kikuu cha Dar es Slaam (Tanzania)

Mwaka 2007 alitunukiwa Shahada ya Uzamivu katika Sheria (Civil Law) na Chuo Kikuu cha Newcastle (England)

Mwaka 2008 alitunukiwa Shahada ya Juu katika Sheria na Chuo Kikuu cha Cape Coast (Ghana)

Mwaka 2009 alitunukiwa Shahada ya Uzamivu katika Sheria na Chuo Kikuu cha Makerere (Uganda)

MITAA, MAENEO NA MAJENGO YALIYOPEWA JINA KWA HESHIMA YA BENJAMIN WILLIAM MKAPA
Ukumbi wa Benjamini Mkapa uliopo Jijini Mbeya katika Mtaa wa Sokomatola

Barabara ya Benjamini Mkapa inayounganisha eneo la Mtoni Kidatu na Uwanja wa Ndege wa Abeid Aman Karume kupitia Daraja Bivu Zanzibar

Daraja la Mkapa ambalo ndilo daraja refu nchini (Tanzania) lenye urefu wa Mita 970

Jengo la Benjamin William Mkapa Pension Tower, ambalo ni miongoni mwa majengo marefu nchini (Tanzania) lipo Jijini Dar es Salaam

Eneo la Ukanda Maalum wa Uchumi wa Benjamin William Mkapa uliopo Jijini Dar es Salaam

Shule ya Sekondari ya Mererani Benjamin William Mkapa Secondary iliyopo Mkoani Manyara

Shule ya Sekondari ya Benjamin William Mkapa iliyopo Kariakoo Jijini Dar es Salaam

Hospitali ya Rufaa ya Benjamin Mkapa iliyopo Jijini Dodoma

Shule ya Msingi ya Benjamin Mkapa iliyopo Mtaa wa Makunguru Jijini Mbeya

Pumzika kwa amani Mzee Benjamini William Mkapa

PIA SOMA:
= > Breaking News: - TANZIA: Rais wa awamu ya 3, Benjamin William Mkapa afariki dunia
 
Binafsi namheshimu Sana Mkapa Ni Kati ya maraisi Bora sana waliopata kutokea Afrika.

Yafuatayo ni Mambo ambayo nayaona ni ya kipekee sana kwa MH hayati rais mstahafu wa awamu ya tatu Benjamin William Mkapa.

1.Kwa lugha ya Kiingereza alimzidi hata Mwl Nyerere.

2.Amekaa kwenye utumishi wa Umma katika nafasi mbalimbali muda mrefu kuliko maraisi wetu wote wa Tanzania alimzidi hata Mwalimu.

3.Alianzisha taasisi imara zinazofanyakazi mpaka Leo. Mfano.Takukuru.

4.Aliondoa Kodi ya kichwa na akaweka kodi ya VAT badala yake. Pia mtakumbuka Yale Mambo ya kukamata baiskeli mjini Kama hujailipia kibati fulani hivi kinafungwa kwenye baiskeli ukiilipia ushuru.

5.Alikuwa mahiri na bingwa wa siasa za kimataifaalikaa Mambo ya nje muda mrefu Sana kuliko mwanasiasa yoyote mkubwa Tanzania.

6.Ndie Alie mleta Dr Shein kwa watanzania.

7.Alimleta Magufuli kwa Watanzania (hapa tumsamehe mzee wetu mkapa)

8.Ndie alimtengeneza Jakaya mpaka kuwa rais.

9.Ndie Alie muibua Frederik Tluway Sumaye. Ambaye ndie waziri mkuu aliekaa madarakani muda mrefu kuliko wote.

10. Alikuza uchumi na kudhibiti mfumuko wa Bei.Japo aliteleza kwenye ubinafsishaji.

Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.

Pumzika jembe.
 
superbug Namba moja hapana!!

Pia alikua hababaiki na ushindi wa wapinzani kwenye chaguzi ndogo ndogo ( by elections) yoyote atakaeshinda atangazwe hakusema eti" ole wake mkurugenzi atakaemtangaza mpinzani kashinda wakati namlipa huyo mkurugenzi mshahara na gari"

Hakuwahi kuingiza makada wasio na uelewa kwenye utumishi wa uma ndio maana wakati wake huwezi sikia DED kapigana na DC !!!!
Wakuu wa mikoa wa awamu yake hawakughushi vyeti vya taaluma
 
Kwa sababu ya sera za ubinafsishaji?
Siri nzito juu yake ambayo ni muda muafaka sasa kwa Watanzania kuijua,na kudai kuwa yeye si mtoto wa Julius Nyerere kama anavyopotosha Mkapa ila ni wa Josephat Nyerere.

Josephat na Julius ni mtu na Mdogo wake(kama hataki ajinyonge) huku akishangiliwa na umati mkubwa Sana uliohudhuria katika viwanja vya mkuytano uliofanyika Sing'si alimtaka Mkapa ajibu na aweke wazi juu ya Kifo cha baba wa Taifa aliyeondoka Butiama akiwa Mzima aliyekwenda tu kupima Afya na kurudi Mfu, huku umati ukipiga Mayowe kwa kushangilia, alitaka aweke wazi kilichomuua baba wa Taifa huku akimwaga Hadharani tofauti zilizojitokeza na Ugomvi kati yake na Mwalimu kilichopelekea Mkapa kuamua na kulazmisha mwalimu apelekwe London kutibiwa (kuuwawa) huku Nyuma akimyamazisha Daktari wa Mwalimu kwa kumpa Uwaziri ili asiseme kilichotokea.

Na alisema ilikuwaje Mkapa ataje Ugonjwa wa mwalimu ili hali Daktari wake yupo?alihoji, amemwaga vitu vingi ambavyo kwa kweli vitaleta Maswali Mengi juu ya wananchi wa Tanzania na dunia kwa ujumlaa.
 
Binafsi namheshimu Sana Mkapa Ni Kati ya maraisi Bora sana waliopata kutokea afrika.

Yafuatayo ni Mambo ambayo nayaona ni ya kipekee sana kwa MH hayati rais mstahafu wa awamu ya tatu Benjamin William Mkapa.

1.Kwa lugha ya Kiingereza alimzidi hata Mwl Nyerere.

2.Amekaa kwenye utumishi wa Umma katika nafasi mbalimbali muda mrefu kuliko maraisi wetu wote wa Tanzania alimzidi hata Mwalimu..

Namba nane sio kweli.
 
Siri nzito juu yake ambayo ni muda muafaka sasa kwa Watanzania kuijua,na kudai kuwa yeye si mtoto wa Julius Nyerere kama anavyopotosha Mkapa ila ni wa Josephat Nyerere.

Josephat na Julius ni mtu na Mdogo wake(kama hataki ajinyonge) huku akishangiliwa na umati mkubwa Sana uliohudhuria katika viwanja vya mkuytano uliofanyika Sing'si alimtaka Mkapa ajibu na aweke wazi juu ya Kifo cha baba wa Taifa aliyeondoka Butiama akiwa Mzima aliyekwenda tu kupima Afya na kurudi Mfu, huku umati ukipiga Mayowe kwa kushangilia, alitaka aweke wazi kilichomuua baba wa Taifa huku akimwaga Hadharani tofauti zilizojitokeza na Ugomvi kati yake na Mwalimu kilichopelekea Mkapa kuamua na kulazmisha mwalimu apelekwe London kutibiwa (kuuwawa) huku Nyuma akimyamazisha Daktari wa Mwalimu kwa kumpa Uwaziri ili asiseme kilichotokea.

Na alisema ilikuwaje Mkapa ataje Ugonjwa wa mwalimu ili hali Daktari wake yupo?alihoji, amemwaga vitu vingi ambavyo kwa kweli vitaleta Maswali Mengi juu ya wananchi wa Tanzania na dunia kwa ujumlaa.
Duniani kuna mengi,kwamba nyerere alipambana na beberu mweupe akasahau kuna beberu mweusi?
 
This is too cheap bro! Think harder, Hospital ya St. Fransis London ni hospitali yenye hadhi na jina kubwa, haiwezi kudanganya kuhusiana na sababu za kifo cha Baba wa Taifa, kama unazo tofauti zako na Mh. Ben uzitaje tuzifahamu kuliko kuzusha mambo yasiyo na msingi!
Ben ni moja wa maraisi bora kabisa kupata kutokea hapa Afrika
 
Back
Top Bottom