Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,814
- 11,991
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiendelea na ziara yake ya kitaifa nchini India tarehe 10 Oktoba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Falsafa (Doctorate Honoris Causa) na Chuo Kikuu cha Jawaharlal Nehru kwenye hafla iliyofanyika New Delhi nchini India tarehe 10 Oktoba, 2023. Rais Samia ni Mwanamke wa Kwanza kutunukiwa Shahada hiyo ya Heshima na Chuo hicho Nchini India.
Ni Viongozi wawili tu ambao wametunukiwa Shahada hiyo ya Heshima akiwemo Rais wa Urusi, Vladmir Putin pamoja na Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Japan Hayati Shinzo Abe.
===
Amewashukuru wazazi wake kwa kuona umuhimu wa kuwekeza kwa mtoto wa kike, CCM, ndugu zake pamoja na watu wote waliomshika mkono kuhakikisha anafikia sehemu alipo hivi leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi pamoja na wageni mbalimbali mara baada ya kutunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Falsafa (Doctorate Honoris Causa) na Chuo Kikuu cha Jawaharlal Nehru kwenye hafla iliyofanyika New Delhi nchini India tarehe 10 Oktoba, 2023.
Tuzo hii ameitoa kwa watoto wa kike wa kitanzania wanaoishi kwenye mazingira magumu, amewatia moyo kuwa hakuna kisichowezekana.
Kwa Tanzania, India sio nchi tu bali ni sehemu ya familia iliyotenganishwa na mwambao wa bahari, pia ni rafiki wa majira yote. Urafiki huu ulianza zamani, tangu enzi za ukoloni ambapo wananchi wengi wa India wapo nchini Tanzania, hata baadhi ya vyakula vya kihindi vinapatikana Tanzania.
Sherehe ya diwali husherekewa pia Tanzania, pia mahekalu ya Kihindu yapo Tanzania na hata kwenye ziara hii imejumlisha Watanzania wenye asili ya Kihindi.
Chuo Kikuu cha Jawaharlal Nehru (Javāharalala Neharū Viśvavidyālaya) ni chuo kikuu cha utafiti wa umma kilichoko Kusini Magharibi mwa Delhi , India. Kilianzishwa mwaka 1969 na kupewa jina la Jawaharlal Nehru, Waziri Mkuu wa kwanza wa India.
Wanafunzi wa Vyuo Vikuu mbalimbali nchini India wakiwa kwenye hafla ambayo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan alitunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Falsafa (Doctorate Honoris Causa) na Chuo Kikuu cha Jawaharlal Nehru, New Delhi nchini humo tarehe 10 Oktoba, 2023.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye hafla ambayo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan alitunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Falsafa (Doctorate Honoris Causa) na Chuo Kikuu cha Jawaharlal Nehru, New Delhi nchini India tarehe 10 Oktoba, 2023.
PIA SOMA:
- Mama Samia Atunukiwa Udaktari wa Uchumi (Doctorate of Economics Degree) Uturuki
- Rais Samia atunukiwa Shahada ya Heshima ya Uzamivu ya Usimamizi ya Utalii na Masoko ya Chuo Kikuu cha Zanzibar (SUZA), leo Desemba 28, 2023
- Rais Samia ashiriki Mahafali ya 52 Duru ya 5 ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam. Atunukiwa Shahada ya Heshima
- Dkt. Jakaya Kikwete amtunuku Rais Samia Shahada ya Udaktari wa Heshima UDSM. Sasa ni Dkt. Samia
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Falsafa (Doctorate Honoris Causa) na Chuo Kikuu cha Jawaharlal Nehru kwenye hafla iliyofanyika New Delhi nchini India tarehe 10 Oktoba, 2023. Rais Samia ni Mwanamke wa Kwanza kutunukiwa Shahada hiyo ya Heshima na Chuo hicho Nchini India.
Ni Viongozi wawili tu ambao wametunukiwa Shahada hiyo ya Heshima akiwemo Rais wa Urusi, Vladmir Putin pamoja na Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Japan Hayati Shinzo Abe.
===
Rais Samia ameshukuru kwa heshima hii aliyopewa ya kutunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Falsafa (Doctorate Honoris Causa) kutoka chuo cha Jawaharlal Nehru, India, na amesema hii ni mara ya kwanza kwake kupatiwa heshima hii nje ya nchi baada ya kupatiwa na Chuo Kikuu cha Dar es salaam.Amewashukuru wazazi wake kwa kuona umuhimu wa kuwekeza kwa mtoto wa kike, CCM, ndugu zake pamoja na watu wote waliomshika mkono kuhakikisha anafikia sehemu alipo hivi leo.