Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,812
- 11,986
Benjamin William Mkapa alizaliwa mnamo 12 November 1938 huko Ndanda Wilayani Masasi Mkoani Mtwara. Alimaliza Shahada ya kwanza ya Lugha ya Kiingereza kutoka Chuo Kikuu cha Makerere nchini Uganda mwaka 1962
Mwaka 1963 alihitimu shahada ya Uzamili katika Mahusiano ya Kimataifa kutoka katika Chuo Kikuu cha Columbia
Aliwahi kuwa Afisa Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Waziri wa Sayansi na Teknolojia, alikuwa Balozi (Canada) 1982 na baadaye nchini Marekani 1983 - 1984
Aliwahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje, 1977 - 1980 na 1984 hadi 1990
Alichaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia 1995 - 2005
Alikuwa miongoni mwa viongozi walioshiriki kutatua Mgogoro wa Uchaguzi nchini Kenya mwaka 2007 - 2008
Aliteuliwa kuwa msuluhishi wa mgogoro wa nchi ya Burundi mwaka 2016 - 2019
SHAHADA ZA HESHIMA ALIZOWAHI KUTUNUKIWA BENJAMIN WILLIAM MKAPA:
Mwaka 1998 alitunukiwa Shahada ya Heshima na Chuo Kikuu cha Sōka University (Japan)
Mnamo mwaka 1999 alitunukiwa Shahada ya Heshima na Chuo Kikuu cha Morehouse College (Marekani)
Mwaka 2003 alitunukiwa Shahada ya Heshima na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania
Mwaka wa 2005 alitunukiwa Shahada ya Uzamivu katika Sheria na Chuo Kikuu cha National University of Lesotho (Lesotho)
Mwaka 2005 alitunukiwa Shahada ya Uzamivu katika Elimu na Chuo Kikuu cha Kenyatta (Kenya)
Mwaka 2006 alitunukiwa Shahada ya Heshima na Chuo Kikuu cha Dar es Slaam (Tanzania)
Mwaka 2007 alitunukiwa Shahada ya Uzamivu katika Sheria (Civil Law) na Chuo Kikuu cha Newcastle (England)
Mwaka 2008 alitunukiwa Shahada ya Juu katika Sheria na Chuo Kikuu cha Cape Coast (Ghana)
Mwaka 2009 alitunukiwa Shahada ya Uzamivu katika Sheria na Chuo Kikuu cha Makerere (Uganda)
MITAA, MAENEO NA MAJENGO YALIYOPEWA JINA KWA HESHIMA YA BENJAMIN WILLIAM MKAPA
Ukumbi wa Benjamini Mkapa uliopo Jijini Mbeya katika Mtaa wa Sokomatola
Barabara ya Benjamini Mkapa inayounganisha eneo la Mtoni Kidatu na Uwanja wa Ndege wa Abeid Aman Karume kupitia Daraja Bivu Zanzibar
Daraja la Mkapa ambalo ndilo daraja refu nchini (Tanzania) lenye urefu wa Mita 970
Jengo la Benjamin William Mkapa Pension Tower, ambalo ni miongoni mwa majengo marefu nchini (Tanzania) lipo Jijini Dar es Salaam
Eneo la Ukanda Maalum wa Uchumi wa Benjamin William Mkapa uliopo Jijini Dar es Salaam
Shule ya Sekondari ya Mererani Benjamin William Mkapa Secondary iliyopo Mkoani Manyara
Shule ya Sekondari ya Benjamin William Mkapa iliyopo Kariakoo Jijini Dar es Salaam
Hospitali ya Rufaa ya Benjamin Mkapa iliyopo Jijini Dodoma
Shule ya Msingi ya Benjamin Mkapa iliyopo Mtaa wa Makunguru Jijini Mbeya
Pumzika kwa amani Mzee Benjamini William Mkapa
PIA SOMA:
= > Breaking News: - TANZIA: Rais wa awamu ya 3, Benjamin William Mkapa afariki dunia