JamiiForums Usiku wa manane

JamiiForums Usiku wa manane

Mastory ya Bey​


Hello My people

Mapenzi ndio yana run dunia kwahiyo hatuwezi ishi bila mapenzi au kuzungumzia mapenzi

Tuangalia namna ya kuponya majeraha ya kuumizwa kimapenzi,kama hujaumia leo basi tarajia kesho utaumizwa yan iko hivyo siku zote

Kwanza kubali hisia zako kwamba umeumizwa, jisikie vibaya na lia hata ukiweza,usijifanye upo okay wakati haupo okay,kubali maumivu ambayo umeyapata

Zungumza na mtu unayemwamini anaweza kuwa mshauri wa mapenzi,best yako wa ukweli na mwingine yoyote yule ambaye atakufanya uyaone mambo katika namna tofauti na kukufanya ujisikie gud

Jiepushe kumrudia ex wako kwa muda mfupi,wakati mwingine kutokana na mazoea waeza jikuta kama unataka kurudiana nae tena kwa haraka, kumbuka huyu ndio aliyekuumiza na kukupa machungu hivyo gangamala

Jipe kipaumbele katika nyakati hizi,fanya mambo ambayo unayafurahia,kama kusoma,michezo kutembea,kucheki movie,kutalii na kadhalika,give yourself a gud time

Epuka kujilaumu,mapenzi huvunjika kwasababu nyingi sana,na wakati mwingine sio makosa yako,kwahiyo usijilaumu kwa yaliyotokea

Jifunze kupitia maumivu ya mapenzi unayoyapata,jitathimini wapi unakosea,wapi unatakiwa uboreshe,je ni redflags gani uliziona toka awali lakini ulizichukulia poa na mambo kama hayo

Jipe muda kabla hujaingia kwenye mahusiano mapya,usikurupuke eti kumuonnyesha ex wako kwamba ukisema cha nini wenzio wanasema nitakipata lini, aisee hapo utajikomoa mwenyewe bila kujijua,baada ya muda si rmrefu utakuja kujua kwamba umefanya makosa makubwa sana

Toa msamaha au samehe yaliyo pita,kusamehe haimaanishi kwamba unarudiana nae laa! Ni kuponya moyo wako,unapokuwa na chuki dhidi ya mtu mwingine basi tambua unabeba mzigo mkubwa mgongoni mwako na utavunjika usipokuwa makini

Tambua unapotoa msamaha ni kwa ajili ya kuponya nafsi yako mwenyewe,kwahiyo fanya si kwa ajili ya aliyekukosea ila kwa ajili yako.

Bey
 

Mastory ya bey​


Hello my people

Leo tuzungumzie umuhimu wa personal reflection,,ile hali ya kujitathimini wewe binafsi,kujichunguza na kutathimini matendo yako ya siku nzima

Hii inakupa nafasi ya kujua kipi kilienda vibaya,kipi kiliharibika na kipi kilienda vizuri kwa siku nzima ya leo

Kwanza inabidi ufanye Journaling kwa maana chukua Kalamu na karatasi na jaribu kukumbuka matendo yako ya siku nzima ya leo,kuanzia kuamka kujitayarisha na kuendelea na shughuli zako au mambo yako mpaka usiku

Hii itakusaidia kukumbuka kila hatua na mwenendo wa siku yako,mathalani pamoja na mambo mengine leo uligombana na jirani yako,ukarushiana maneno machafu na mfanyakazi mwenzako,na kuna uzembe ulifanya kwenye shughuli yako

Kwa kufanya tathimini hii itakufanya kujua makosa yako ili kesho usiweze kuyarudia tena,hakuna ubaya katika kufanya makosa kwasababu makosa hutufundisha nakutuwezesha kuwa bora zaidi,kibaya ni kurudia makosa yale yale kila mara

Na kwanini tunarudia kila mara kwasababu hatujakaa chini na kuyatambua makosa yetu,lau ukitambua makosa yako na kuyatafakari kwa kina inakupa nafasi ya kurekebisha pale unapokosea

Mathalani ukijichunguza sababu iliyokufanya ugombane na jirani utaona ni ya kipuuzi sana,na saa nyingine unaweza kujiuliza hivi kama ningechagua kukaa kimya huenda ningeepusha mengi na huenda nisinge gombana na jirani yangu

Faida nyingine ya kujifanyia personal reflection ni kutambua yale mazuri uliyoyafanya kwako binafsi na kwa jamii inayokuzunguka,itakuwa ni chachu ya kukufanya uzidi kufanya mambo mazuri zaidi kwenye siku zijazo

Na kuandika sio lazima liwe gazeti bali inaweza kuwa summary yenye sentence fupi fupi lakini iliyokusanya taarifa zako kwa siku hiyo

Mwanzoni inaweza kuwa ngumu na kuonekana kama kitu cha ajabu lakini kadri unavyo endelea na utaratibu huu itabadilika na kuwa kitu unapenda kukifanya kila siku

Kumbuka lengo ni kutruck matukio yako ya siku nzima na kujitathimini na mwisho wa siku ujifahamu unaelekea wapi

Bey
 
Back
Top Bottom