JamiiForums Usiku wa manane
2259hrs

 M
astory ya Bey

My people mmeshindaje,habar za kutwa nzima,hope mko poa kabisa,tunakutana tena kwenye kijiwe cha Mastory ya Bey

Guys leo bwana nataka kuzungumzia swala Zima la kupokea simu,kuna hii shu simu inapigwa halafu unaisikilizia weee kisha ndio unaipokea,hii sio poa kabisa,unawapotezea watu muda

Unajua mtu akikupigia simu ina maana ana shida ya chap,muongee mmalizane kisha aendelee na mishe nyingine,na sio wakati wa wewe kumsikilizisha muito wa simu muda mrefu

Simu ipo mkononi je kuna haja gani ya kuchelewesha kuipokea,unafanya hivyo ili uonekane uko busy au,sikia stop wasting people's time mtu akikupigia just pokea chap na msikilize kila mtu aendelee na mishe zake

Mimi bwana sina mambo mengi ,kwanza kile kitendo cha kuacha simu iite muda mrefu naona kero,yani imeita tu chap nareceive tunamalizana fasta

Kuna siku moja mzazi mwenzangu ile kapiga tu chap nikapokea,akasema duh simu ilikuwa mkononi nini? Nikamjibu si inaitwa simu ya mkononi au,akabaki anacheka tu

Kwahiyo ebu tuache zile mbanga za kupotezeana muda,simu imepigwa chap pokea msikilize anayekupigia chap tu mnamalizana,kusikiliziana ni nyie na baby wako lakini sio kila mtu unataka kumuweka pending kama una mmudu vile au kwasababu simu ni yako🤣🤣 ndio maana unaamua kuchelewa kupokea,tuache ujinga bwana!!!
 
LEO KATIKA HISTORIA

Hapa kuna baadhi ya matukio ya kihistoria yaliyotokea leo, tarehe 21 Septemba:


---

Matukio Makuu

1964 – Malta ilipata uhuru wake kutoka Uingereza.

1949 – Wana‐komunisti China walitangaza rasmi kuanzishwa kwa People’s Republic of China.

1921 – Maporomoko mkali katika kiwanda cha mbolea Oppau, Ujerumani; zaidi ya watu 500 waliuawa katika mlipuko.

1981 – Sandra Day O’Connor akapewa baraza la Seneti la Marekani kuwa Jaji wa kwanza mwanamke wa Mahakama Kuu ya Marekani.

1937 – Kitabu cha fantasía The Hobbit kilichokaliwa na J.R.R. Tolkien kilichapishwa kwa mara ya kwanza.



---

Kupaswa Kufahamika

Leo pia ni Siku ya Amani Duniani (International Day of Peace) inayoadhimishwa kila mwaka kwa ajili ya kusisitiza utulivu, usitishaji wa vurugu na uungaji mkono wa haki na usawa duniani.
 
Nukuu ya Leo

🌿 Nukuu ya Leo:


"Amani haimaanishi kutokuwepo kwa migogoro, bali ni uwezo wa kushughulikia tofauti kwa njia ya amani

 
Positive Affirmations

Hapa kuna positive affirmations za leo ambazo unaweza kuzirudia ili kukuimarisha kisaikolojia na kiroho:

✨ Nina nguvu na uwezo wa kukabiliana na changamoto zote zinazokuja mbele yangu.
✨ Kila siku ni fursa mpya ya kujifunza, kukua, na kufanikiwa.
✨ Moyo wangu umejaa shukrani, na shukrani huniletea baraka zaidi.
✨ Ninajiamini na najua thamani yangu.
✨ Amani na utulivu vipo ndani yangu, na navisambaza kwa wengine.
✨ Niko katika safari ya kuwa toleo bora zaidi la mimi mwenyewe.
 
My people hizi positive affirmations ndio zinazo badilisha mitazamo yeti katika maisha

Unajua mara nyingi sana huwa tunaambiwa maneno mabaya ya kutukatisha tamaa,kutuvunja nguvu na mwisho wa siku tunaathirika sana

Na sometime huwa tunajiammbia wenyewe maneno na kauli ambazo hututudisha sana nyuma

Hizi affirmations ndio dawa na suluhisho la kurewire upya ubongo wako,una update data mpya ambazo zitakufanya uwe unajiamini na kujifurahia mwenyewe,zifanyie kazi

Choose some lines na ishi nazo zisome kila wakati after some time u will be a new version of ur self
 
If you want to make big changes in ur life,then start with small ones,after sometime u will make it
 
Back
Top Bottom