JamiiForums Usiku wa manane

JamiiForums Usiku wa manane

Mastory ya Bey

Uhusiano usio na afya ni ule ambao wahusika wapo kutoa shida zao au changamoto zao kupitia hisia zao,yani kila mtu ana shida zake,sasa wapi pakuzitolea ni kupitia kwa mwenzake,kwa maana nyingine kila mtu anamtafuta mtu wa kumbwagia shida zake

Kinyume na mahusiano yenye afya nzuri,mahusiano yenye afya nzuri kila mtu anajijua ana shida na changamoto,na yupo tayar kutatua shida zake mwenyewe au kwakusaidiwa na partner wake,hapa kila mtu anakuwa responsible na shida zake

Katika mahusiano yenye afya mbaya,mhusika mmoja anaamini na kutarajia kwamba mhusika mwingine anawajibika kutatua shida zake au changamoto zake,kinyume chake matarajio hayo yasipo timizwa basi ugomvu na shida zinaanzia hapa

Utasikia fulani anajua nina shida moja mbili tatu lakini mpaka sasa hajafanya juhudi zozote kuzitatua,yani yeye anajiweka mbali na utatuzi wa shida zake,badala ya yeye awe sehemu ya mchakato,anajiona kuna mtu anastahili kutatua shida zake

Mtu anatakiwa amsaidia partner wake pale anapojisikia kufanya hivyo,na sio afanye kwa kulazimishwa,unapofanya jambo kwa kulazimishwa hayo yanakuwa tena sio mapenzi,inakuwa ni kitu kingine

Na anayesaidia naye unakuta hasaidii kwa kuwa anajisikia kufanya hivyo kwa mapenzi,bali kwasababu ili apate mapenzi au upendo toka kwa partner wake,kwahiyo utaona kwamba kiuhalisia hakuna mapenzi hapo,ila ni kitu kingine kabisa kinacho waunganisha watu

Huyu asipotatulisha shida anaona hatendewi haki au ana dhulumiwa,na kwa upande wa pili huyu anayesaidia,anajiona kwamba ana paswa kutatua shida za mwenzake kwasababu inatakiwa iwe hivyo

Haya ni makosa makubwa sana,katika mahusiano yoyote yale kila mhusika anatakiwa ajue kwamba anawajibika kutatua shida na changamoto zake,na hata kama msaada unakuja basi ni sehemu ya msaada tu,na asifikiri kwamba anapaswa kusaidia kwa asilimia mia moja

Na kama akisaidiwa kwa asilimia mia hakuna ubaya,maadamu anajua kwamba hapo awali hayo yalikuwa majukumu yake hiyo imetokea kama zali tu

Lingine mahusiano yenye afya yana mipaka kwa kila mmoja,yani kila mhusika ana uhuru wa kufanya mambo fulani bila kupata kikwazo toka kwa mwingine,maadamu tu yanakuwa sio chanzo cha mfarakano katika mahusiano hayo

Mfano kama kila mmoja wao ana hobby fulani basi awe huru kufurahia hilo pasina kikwazo chochote,mfano kama mume anapenda mpira basi mke anatakiwa asiwe kikwazo juu ya hilo,maadamu haendi kuangalia sehemu ambazo zinaweza leta mtihani

Lakini mahusiano yasiyo na afya nzuri mara nyingi hakuna mipaka kwa wahusika,mathalani mume au mke anaweza kuwa na marafiki wema tu,lakini pasina sababu yoyote unakuta mmoja wao,anamtaka mwenzake asitishe urafiki huo

Kama kweli umeona marafiki wa mumeo au mkeo sio wazuri una haki ya kufanya hivyo,kwasababu mara nyingi watu huathirika na tabia za marafiki zao,ndio maana kuna ule msemo unasema,ukitaka kujua tabia ya mtu fulani basi angali tabia za marafiki zake

Kwahiyo kama hakuna ubaya wowote ambao umeuona toka kwa marafiki wa mwenza wako,basi heshimu mipaka ya mwenzio,na yeye vile vile,mpeane nafasi kila mtu awe huru kuwa na marafiki wema

Kwa kumalizia,mahusiano yenye afya ni yale ambayo kila mmoja atawajibika kwa changamoto zake na shida zake,msaada uje tu kama sehemu ye nyongeza

Pili huyu anayesaidia,asijisikie kwamba analazimishwa au analazimika kusaidia jambo flani,bali afanye kwa kuwa anataka kufanya hivyo bila shinikizo lolote lile,na hayo ndio mapenzi

Na asitoe msaada kwasababu ili apate jambo fulani,akifanya hivyo atakuwa amefanya kwa shinikizo ili apate jambo fulani

Mahusiano ya kweli yapo huru na wahusika wanajisikia wako huru ama kwa kufanya maamuzi fulani au wanakuwa pamoja bila masharti yoyote yale
 
Nukuu ya leo:

"Usikate tamaa kwa sababu ya safari ndefu; kila hatua unayopiga ni ushindi unaokukaribisha kwenye ndoto zako."
Methali ya motisha ya Kiswahili

Inakutia moyo kuwa kila hatua ya juhudi yako ina thamani, hata kama matokeo hayajaonekana bado.
 
Info:

Ubongo ni kiungo kikuu cha mfumo wa neva wa binadamu na viumbe wengi. Huu ndio "kompyuta kuu" ya mwili wako, unaosimamia kila kitu — kufikiri, kuhisi, kutenda, na hata kupumua.

🧠 Muundo wa Ubongo
1. Cerebrum (Ubongo mkubwa):
- Hushughulikia fikra, kumbukumbu, hisia, lugha, na harakati za hiari.
2. Cerebellum (Ubongo mdogo):
- Hudhibiti usawa, uratibu wa misuli, na harakati za mwili.
3. Brainstem:
- Dhibiti kazi za msingi kama kupumua, mapigo ya moyo, na shinikizo la damu.

🔄 Kazi Kuu za Ubongo
  • Kufikiri na kuelewa
  • Kudhibiti viungo
  • Kuhifadhi kumbukumbu
  • Kupokea na kutafsiri taarifa kutoka kwa milango ya fahamu (macho, masikio, n.k.)
  • Kuhisi na kudhibiti hisia (furaha, huzuni, hofu, nk.)

⚡ Uwezo wa Ajabu
  • Ubongo una takriban neva bilioni 86, zinazowasiliana kwa kasi ya ajabu.
  • Unaweza kuchakata taarifa kwa haraka kuliko kompyuta yoyote.

🧘‍♂️ Je, Unaweza Kuuboresha?
Ndiyo! Kwa kufanya:
  • Mazoezi ya mwili na akili
  • Kulala vizuri
  • Kula vyakula vyenye Omega-3, mboga na matunda
  • Kujiepusha na msongo wa mawazo na madawa ya kulevya

Ubongo ni kiungo kidogo kwa uzito (kama 1.4kg), lakini kinaongoza kila sekunde ya maisha yako.
 
LEO KATIKA HISTORIA:

Leo ni Mei 28. Hapa ni baadhi ya matukio muhimu yaliyotokea siku kama ya leo katika historia:

🌍 Matukio ya Kihistoria

- 1918 – Azerbaijan na Armenia zilitangaza uhuru wao kutoka kwa Urusi, na kuanzisha Jamhuri zao za kwanza. [1]

- 1937 – Kampuni ya magari ya Volkswagen ilianzishwa nchini Ujerumani, ikilenga kutengeneza magari ya bei nafuu kwa raia wa kawaida. [2]

- 1961 – Shirika la haki za binadamu la Amnesty International lilianzishwa mjini London, likiwa na lengo la kutetea haki za wafungwa wa kisiasa na haki za binadamu kwa ujumla. [3]

- 1998 – Pakistan ilifanya majaribio ya nyuklia kwa mara ya kwanza, ikijibu majaribio ya India, na kuadhimisha siku hii kama "Youm-e-Takbir". [1]

🎂 Watu Maarufu Waliozaliwa

- Ian Fleming (1908) – Mwandishi wa riwaya za James Bond. [3]

- Gladys Knight (1944) – Mwimbaji mashuhuri wa muziki wa soul. [4]

- John Fogerty (1945) – Mwimbaji na mtunzi wa nyimbo wa bendi ya Creedence Clearwater Revival. [4]

- Kylie Minogue (1968) – Mwimbaji na mwigizaji kutoka Australia. [4]

- Carey Mulligan (1985) – Mwigizaji wa filamu kutoka Uingereza. [4]
 
Ndani ya mavazi yangu rasmi... Alamsiki wangwanaa

1000027399.jpg
 
Chachandu special:

Wazaramo ni moja ya makabila ya asili ya Tanzania, hasa wanaopatikana katika mikoa ya Pwani, Dar es Salaam (Temeke), na sehemu za Bagamoyo. Hapa ni muhtasari wa utamaduni wao:

🌍 Asili na Lugha
  • Wazaramo ni sehemu ya jamii za Kibantu.
  • Lugha yao ni Kizaramo, lakini wengi huzungumza pia Kiswahili.

👪 Familia na Jamii
  • Familia zao ni za ukoo wa baba (patrilineal).
  • Hushirikiana katika kazi kama kilimo na harusi.
  • Wana heshima kubwa kwa wazee na vikao vya ukoo.

💍 Ndoa na Mila
  • Harusi za Kizaramo huambatana na ngoma, nyimbo na maandalizi ya muda mrefu.
  • Mahari hutolewa kwa wazazi wa bibi harusi kwa heshima na kuthibitisha ndoa.

🥁 Ngoma na Sanaa
  • Ngoma maarufu ni Mdundiko, ambayo huchezwa kwenye harusi na sherehe kubwa.
  • Pia wana mashairi na nyimbo za jadi zenye mafundisho na historia.

🌾 Maisha na Shughuli
  • Wanarithi ardhi ya ukoo na wengi ni wakulima wa mihogo, mahindi, mpunga na nazi.
  • Ufugaji na uvuvi ni sehemu ya maisha ya pwani.

🧙 Imani na Mila
  • Wengine huamini katika mizimu na waganga wa jadi.
  • Wengi sasa ni Waislamu, lakini mila za asili bado huonekana kwenye sherehe na tiba.

👗 Mavazi
  • Hupendelea kanga, kitenge, na mapambo ya asili hasa kwenye sherehe.
  • Wanawake huvalia kwa heshima, hasa kwenye vikao au mbele ya wazee.


Wazaramo wamechangia sana katika maendeleo ya Kiswahili na utamaduni wa Dar es Salaam.
 
Back
Top Bottom