JamiiForums Usiku wa manane
P_ mawenge

CORONA lyrics

Asubuhi natazama taarifa ya habari, wanatangaza kuna janga jipya la hatari.../

Tuokoe vizazi kwa kuvipa tahadhari, corona virus ukipita kaa mbali.../

Umeishaua sana watu elfu na mamia, kila taifa sasa ndugu zetu wanalia.../

Si marekani china hadi kwetu tanzania, tumuombe sana allah yesu na maria.../

Kirusi cha corona kikizama kwenye mwili, mpaka kugundua na kuanza kuona dalili.../

Imachukua siku mbili hadi wiki mbili, umakini uzingatiwe jamani tusikariri.../

Unasambaa kwa kukohoa na kugusana, hasa maeneo ambayo watu wana songamana.../

Kushika vitu bila kuzingatia usalama, na hata kwa nguo pia ikiwa tukivaliana.../

Dalili zake homa na pia kuumwa kichwa, maumivu makali ya koo na kitapika.../

Kikohozi kibichi na kuhema kwa tabu, ukiwa na sifa hizo unahitaji matibabu.../

Tujitahidi sana kuzifata tahadhari, ukijihisi ni muhimu kwenda hospitali.../

Ufanyiwe uchunguzi wa kina na daktari, na ukikutwa utibiwe kabla haijafika mbali.../

Tusalimie watu bila kushikwa mikono, tuepuke mabusu ya kugusisha midomo.../

Tukikohoa ni muhimu kuzima midomo, hadi janga la corona likishafika kikomo.../

Wanafunzi shuleni masomo yamesitishwa, hakuna matamasha wala semina kabisa.../

Masokoni vyakula na mavazi yameadimika, duniani sasa kila kitu kimevurugika.../

Shukrani sana kwa kila mtu anayepambana na corona kutunusuru afya zetu

Written by Scars

Good night
 
Dah! nilijiunga bando la youtube nikeshe usiku kucha ila limegoma, yaani nawasha data nazima hollaaaaa!

Leo tigo wameniweza sijalala mpaka saiz
 
Back
Top Bottom