Mkuu ngoja mi nikufafanulie sasa.
Kwanza anzia kwenye avatar. Kama ni ya kike kike hiyo ni hatua nzuri.
Baada ya hapo nenda kwenye profile yake. Kama una bahati itakuwa inaonyesha jinsia yake.
Kama hakuna avatar au profile yake haionyeshi jinsia basi fuatilia comments zake. Utajua tu kuwa huyu ni -me au -ke. Kwenye mada za mahaba utaona anavyotiririka. Kama ni dume hata ajifanye namna gani kuwa binti kuna siku atateleza tu na ukweli utajulikana. Instincts zako zitakuongoza.
Hatua nyingine ni kumuuliza mhusika point blank kuhusu jinsia yake. Hili unaweza kuuliza wazi wazi au unaweza kumuuliza private kupitia Private Message (PM).
Ukishaanzisha mazungumzo PM basi hiyo ni hatua nzuri. Mkielewana huko na urafiki ukakolea basi mnaweza hata kukutana physically na kufahamiana zaidi.
Yote kwa yote, huu ni mtandao na kusema kweli hakuna njia ya uhakika sana ya kuwa na uhakika kwa asilimia 100 kuwa unayewasiliana naye ni dume au ni binti. Hii si JF pekee bali hata dating sites na kwingineko. Uangalifu unatakiwa na kama alivyotuasa mtoto wa mjini kutoka Msoga always akili za kuambiwa changanya na zako.